SURA YA PILI
CHOTARA WA KIAFRIKA NA KIARABUSikio la kufa halisikii dawa, za mwizi harobaini, Baba alimwambia, Beka Kiburi sio maungwana, mkataa pema pabaya panamwita, Beka alikamatwa na wananchi wenye hasira akapigwa vibaya, akachanwa chanwa kwa visu na nyembe, alimanusura achomwe moto wapetrol, alikamatwa na wizi wa piki piki aliyopora usiku wa kuamkia jana, kipigo alichopewa amsalie mtume, Kama sio Polisi waliofanya juu chini leo hii Beka angelikuwa ni marehemu.
Kesi yake ilipita mahakamani, akatupea jera miaka miwili sababu aligundulika ametenda kosa . maisha ya jera yakampa changamoto, akatamani qaridhi ipasuke aingie humo. Maisha ya jera yakawa magumu kwake, kula yake ikawa ni ya shida, kunywa shida, uhuru hauopo tena, kutumikishwa kjazi kama mtumwa, kupigwa pigwa na kutakanwa ovyo hatimaye alipoyazoea maisha ya jera aakajifunza Heshima, adabu na utii.
Aloitumikia jera kama fundi seremala, akiranda randa mbao, akichonga chonga vitu vya aina mbali mbali, vitu muhimu n yumbani; Meza, viti, vitanda, na vinu, baada ya kutoka jera alitamani angeliendelea na kazi ya kuchonga lakini moyo wake ulibadiri nia akapenda sana awe mlinzi, mlinzi awalindie watu binafsi, taasisis, mashirika na makampuni.
Mzee Armour babaye Beka akafanya juu chini mwanaye aende kujiunga na kikosi cha wanamgambo ambao mara baada ya mafunzo kuisha Beka alichukuliwa na kampuni ya SIGA aende akalinde pale alipopangiwa.
Beka akawa sasa ni kijana aliyevalia magwanda ya Askari Mgambo analinda hapa na pale alipopangiwa,Keisha iacha ile tabia yake ya kupora, kunyang’anya na kuvamia watu nyakati za usiku, kwa sasa yeye ni kijana mwenye utu na mwenye heshima hana yale matendo ya kuitia hasira jamii. Zile nywele zake zizo jaa Mba, chawa na viroboto hana tena nywele hizo ametakata na kuwa ni kijana mwenye mvuto hata hivyo ile tabia yake ya kuvuta sigara bado hajaiacha, anaupenda huo moshi usio shibisha mdomo bali unaburudisha rohoni.
Beka ana sura Fulani yenye mvuto mashallah, kijana ni mweupe wa uchotara na huo uchotara ameurithi kutoka kwa babaye ambaye ni chotara wa kiarabu na kiafrika, ananywele funi ziazokua kwa kasi na kujiviringa viringa azikate asizikate bado tu zitakuwa nyingi zimwjiviringa viringa.
Chotara huyu ni mrefu kiasi,so mnene sana, hana kifua cha mazoezi sababu yeye bnafsi hana tabia ya kufanya mazoezi, ngozi yake laini kama ya motto, sura yake laini kama ya motto, uzuri alionao Beka sio wake pekee, wadogoze Aisha na Tunu hawapunguki kwa ubora wa kusifika.
Baleghe yake ilimfanya abadirike vizuri na kuingia ukubwani na huko ukubwani Beka alikutana na mabadiriko mengine mwngi ya kimwili, kisaikolojia nay ale yatokanayo na mazingira yanayomzunguka.
Baleghe yake ilimfanya asumbuliwe na wanawake watu wazima, vigori na vijori, sura yake peke iliatamanisha wengi wapendao sura, ndevu zake kidevuni zilionesha mvuto wa hali ya juu alipendeza na kuwapendeza hao wanawake wapendao Sura, meno yake meupe, macho yake meupe, midomo yake minene na laini, ngozi yake ni ngozi yenye rangi ya chungwa umbo zuri amerithi kutoka kwa babaye mzee Armour na uzuri wa mzee Armour Mungu hakumtupa alibarikiwa sana ujanani alibarikiwa kwa uzuri na mvuto
Kwa sasa mzeeArmour amekula chumvi nyingi, ujana umempita, uzee umempokea, hana jinsi, anakubaliana na matokeo ya mungu mengi ya binadamu machache ayapangayo Mungu mwanadamu hapangui, ujana na uzee ni mal ya Mungu ni vitu visivyo epukika.

No comments:
Post a Comment