Tuesday, September 2, 2025

MTOTO ALIYETUPWA NDANI YA NDEGE

 





MTOTO ALIYETUPWA NDANI YA NDEGE.

  
SUBIRA



 (PART ONE)

    "No no no. Subira hiyo mimba sio yangu maana Mimi na wewe hatukupanga kuwa na mtoto au familia." Dickson Boyfriend wangu alipinga nilipompa taarifa juu ya mimba yangu.

    "Dick kitanda hakizai haramu, usiikatae hii Mimba ni Mimba yako namtoto atakayezaliwa ni mtoto wetu." Nilijaribu kumshawishi Dick Boyfriend wangu.


     "Narudia tena kusema Mimi sikua na tarajio la kuitwa Baba mapema namna hii, kama umefanya makusudi Subira naomba unieleze, sipo tayari kumpokea huyo kiumbe aliye tumboni kwako." Dick aliongea Kwa msistizo.


     "Tena kuanzia Leo naomba tuachane, siwezi kuishi na mwanamke anayefanya makusudi kuleta mtoto Duniani wakati mie sina tumaini hilo."Dick aliongea tayari kuondoka.

     "Dick mpenzi please usiniache na kumifanyia ubaya huu. Mbona tendo la ndoa tililishiriki pamoja na wakati tunashiriki mbona hsukuzikataa Raha ambazo zimeleta tokeo hili la kubeba mimba." Subira mie nililishika tumbo langu Kwa huzuni, machozi na kilio.


    "Usinijue na Wala nisikujue, shika njia yako mjaa tamaa wewe." Dick alikaza mwendo kuondoka aliniacha pale kwenye kijimvua nikiwa ninalia na tumbo langu. Nililia sana siku ile mvua ingali bado inanyesha Kwa hasira, nikatembea kutoka Kariakoo Hadi Nyumbani Malapa, mtaa wa Sharifu shamba pahali ambapo ninaishi na Baba yangu baada ya Mama kuaga Dunia.

      "Subira." Baba aliyekua akikota moto na kunywa kikombe cha kahawa aliniita.

      "Abee baba!" Nilijaribu kutafuta machozi ingawaje macho yangu yaliiva kama pilipili kichaa.

      "Keti karibu na moto." Kwa upole alinikabidhi kiti pamoja na kombe la kahawa. Nilipoketi na kunywa kombe la kahawa akaniuliza.

      "Naomba nieleze umepatwa na kadhia gani hata macho yako yaive kama damu ya mwanakondoo aliyechinjwa" Nilifuta chozi na kamasi👃🤧 zilizonitoka kama gundi nikaanza kusimulia Dady wangu mkasa wa mie kutemwa na Boyfriend wangu Dick kisa kikiwa ni kukamata ujauzito usiotarajiwa.


Baba hakuonesha furaha, alifura kwa hasira hasara, ile sura yake ya upole ikageuka na kuwa sura ya Mbogo 🐂🐃 aliyejeruhiwa. Akaniambia:


         "Nisikilize👂, umenitia aibu kubwa sana Subira,😱😳 nitaificha wapi sura yangu?🙈 Matarajio yangu yalikua ni wewe kuolewa na mwanaume safi ambaye angelikukuta bikra, huna tumbo hilo👉🤰" Aliendelea kunena.

       "Sasa ninakuambia jambo moja nenda kautoe huo ujauzito wako ili heshima yangu irejee."

      "No, Dady no🙅🔇, siwezi kuutoa huu ujauzito" Niliongea Kwa uchungu hata kahawa ile ya kiafrika aliyonipa niinywe iliniongezea uchungu moyoni." Dady akasimama na kubwata.🔊

     "Huna adabu siku hizi Subira! Sasa nakwambia neno moja usipoutoa huo ujauzito wako Leo naomba nisikukute hapa nyumbani, uondoke, usinijue wala nisikujue." Dingi alitoa kiapo.

     "Please Dady naomba usinifukize naomba unifikirie. Nimeumizwa na boyfriend aliyenikataa alafu na wewe Baba yangu unanishauri nikautoe ujauzito, unaniweka katika hatari' ya kupoteza maisha au kuvurugwa kisaikolojia." Nilitegemea Dady angelielewa na kuonesha huruma.

       " I don't care, nikisema nimesema. Usipoitoa hiyo mimba Leo hii usilale nyumbani kwangu. Aliongea na kutoweka na kuniacha nikilia na kumchukia Dickson umbwa 🐶🦴yule aliyeniharibia maisha.

       'Sintakuwa tayari kuitoa au kuharibu hii Mimba, bora tu niondoke nyumbani.' Nilijisemea. Nikaingia chumbani kwangu na kuanza kuvipakia vikorokoro vyangu pamoja na pesa  kiasi nilizozitunza kwenye kibubu kisha nikaondoka nyumbani na kuelekea kigogo ya Mburahati nilikopanga chumba na sasa kuanzisha maisha.
      
       Maisha yangu hayakuwa rahisi, nilipaswa kudamka Alfajiri sana kuelekea Posta soko la ferry ⛴️  nikanunue dagaa na mafungu ya Samaki 🎣🎏🦈Kisha ningeliwakaanga na kuwauza Kwa wakina mama wenye familia na vijana wakaao Singo wakajipikia dagaa na ugali wakawale na kushiba. Ilipofika mida ya jioni nilikimbilia kituo cha Manzese huko niliweka kijimeza changu nikauza supu ya Pweza na kachori,🐙🦑 hapo kidogo niliweza kumudu gharama za maisha.

      Basi mimba yangu ikawa kubwa kama mzigo, sikuzile sikutaka kuwasiliana na Baba yangu aliyenitaka niondoke nyumbani kwake, kisa tu nina ujauzito uliokataliwa na boyfriend wangu Dickson ambaye nilimtoa moyoni wala siku sikumtamani tena.

Ninakumbuka miezi Tisa kutimua mvua kubwa ilianza kunyesha mida ya jioni kila mtu alikimbilia nyumbani kwake kujilinda na kadhia ya mvua za Dar. Mie bila hofu nilijibanza ubandani kwangu nikisubiria wateja wangu wamalize kujinywea supu ya Pweza 🥣🍜waondoe ubaridi wa ile mvua.

        Ghafra tumbo lilianza kunikata, uchungu mkali ukanishika, kelele za kuomba msaada zilianza kunitoka. Nilikua pekee yangu wakati huo wateja walikwisha kukimbilia majumbani kwao. Nikaanza kupiga 🔊🔉kelele za kuomba msaada, kilio kikuu, lakini wapi! Sikuziona darili za kupata msaada. Mvua ilipamba moto. Niliona hapa naweza kupoteza maisha Bora niondoke pale ubandani, nijisogeze karibu na nyumba za watu huko niombe msaada.

Taratibu na kwa maumivu ya uchungu nilijitembeza na kujikokota kuelekea kule nyumba za watu zilipo, sikuweza kuendelea. Uchungu mkali ulinizidi nikaanguka chini na kuendelea kulia Kwa uchungu ajabu mvua nayo ilizidi kelele za kilio changu. ⛈️🌧️

       Ashukuriwe Mungu anayejibu maombi haraka, 🛐nikiwa nimejibwaga pale chini ya tope lilipita Gari 🚘zuri aina ya Prado likatua pembeni ya miguu yangu mie niliyekua nikijigaragaza kwa maumivu. 

Aliteremeka mwanamke mtu mzima akiwa ameushikiria mwamvuli☔ wake, aliponiona tu moyo wake ukaingia huruma akaninyanyua pale aliponilaza kwa kuukosa msaada. Akanifariji Kwa maneno ya huruma na upole, ❤️ taratibu akafanya kuniongoza nyuma ya Gari yake akanipakia na kunikimbiza Hospitali.

Nilijifungia salama mwanangu wa kiume niliyembatiza jina Clinton Dickson, yule Mama aliyenichukua na kunipekeka Amana Hospital 🏥 aliichukua na kunirudisha nyumbani kwangu. Hapo tayari siku tatu zishapita tangu tukio la mvua kubwa kunyesha na mie kukimbizwa Leba.

Ah! Mambo niliyoyakuta pale nilipokua naishi kabla sijamzaa Clinton yalinifanya ninwage chozi la kukata tamaa. 

Ilisemekana ile mvua kubwa ilikua ni mvua ya mafuriko, mvua iliyobomoa vijumba na nyumba, ukitegemea mie nilikua naishi kwenye lijumba Cha ubavu wa Umbwa kila kitu niliconunua nakuweka nyumbani kwangu kilisombwa na mafuriko kikatupwa mbali na mto msimbazi. Kwahiyo miesikuwa na hata Safuria au kijiko kunyweshea uji Clinton wangu.

     Tamari, yule Mama aliyenionea huruma, mama mwenye huruma kwangu, akaniomba niende nikaishi nyumbani kwake lakini mie niliyejaa stress na uchungu wa kupoteza kila kitu kutokana na majanga ya mvua za Dar nikikataa nikimuomba naurianisaidie niondoke Jiji la Dar nielekee Arusha popote pale nikaanze upya. Tamari aliendelea kunisihi na kunibembeleza lakini mie nilikata tamaa ya kuendelea kuishi Bongo.

      Basi Tamari mama mwema akanipatia shilingi million Moja ya kuanzia maisha niwapo ndani ya Jiji la watalii Arusha. Uzuri wa kukutana na Tamari ni mwanamke anayejiweza pia anapesa zake. Akafanya kunikatia Tiketi 📜 ya ndege🛩️ mie niliyedanganyankuwa nenda kuishi Kwa BIbi yangu feki aliyepo Arusha.

Nikakatiwa ticketi ya Ndege daraja la kwanza, safari  ya kwenda Arusha ilinoga, ingawaje bado sikufahamu ni wapi nitafikia. Nikiwa ndani ya Ndege nikaingia mawazo yaliyoutesa sana moyo wangu, niliwaza:  

'Nitamlea vipi mtoto huyu ikiwa sina maisha bora'

'MToto Clinton Dickson anahitaji maisha Bora na Mimi mama yake nisingeliweza kumpatia.  Oh! Njia panda nifanye Nini mie Subira?! Nikapata wazo la KIJINGA ambalo hadi Leo hii nikilikumbuka ninajuta kwa upumbavu nilioufanya, Niliichukua kalamu na karatasi Kisha nikaandika ujumbe.



TAFADHALI MCHUKUE MTOTO HUYU UMTUNZE AWE WAKO ANAITWA CLINTON DICKSON. NISINGELIWEZA KUMLEA SABABU NINA MAISHA MAGUMU, NAKUOMBA UMTUNZE, MILIMA HAIKUTANI LAKINI BINADAMU TUNAKUTANA. NI IMANI YANGU KWAMBA IPO SIKU TUTAKUTANA TENA AJAPOKUA MTU MZIMA MWAMBIE NINAMPENDA NA PIA ANISAMEHE KWA UAMUZI HUU MGUMU.


    Niliandika machozi yakinibubujika kama maji ya chemichemi, niliumia kwa ule uamuzi wangu mbaya, Nmekataa uamuzi wa kumtoa tumboni, amekaa tumboni mwangu zaidi ya miezi tisa alafu bila huruma ninamtelekeza? Mama gani mimi, nililia kilio cha kwikwi.🥲


     Ndege ilipotua Arusha lnternational Airport, nilihakikisha kuwa abiria wote wametoka nikabaki mie na mwanangu pamoja na mhudumu mmoja ambaye hakuniona Bali mie ndie nilimuona vizuri, akipanga na kupangilia vitu vilivyo ndani ya ile ndege.


     Nikambusu 😘😚mwanangu shavuni na juu ya komwe lake, nikamkumbatia sana machozi yakinibubujika, nikalia na kumwambia mwanangu 'KWAHERI CLINTON, KWAHERI BABA UISHI SALAMA KWENYE MIKONO ILIYOJAA UPENDO NA AMANI. BABA MOLA AKIPENDA TUTAONANA MAJALIWA.'😭

 Nikabeba kijibegi changu na kumuacha mwanangu Clinton pale juu ya kiti cha Ndege nikafanya kumpita yule mhudumu ambaye beji yake ilisomeka 'ESELINA BOAZI' Mie nikatabasamu😊

               🛬😊


PART TWO


ESELINA BOAZI


Ninakumbuka siku ya jumapili tarehe kumi nane mwezi October tulirusha Ndege ya Air Tanzania.  Iliyofanya Safari zake kutoka Dar es saalam kwenda Arusha. Mimi ni Fry attendant yaani mhudumu wa Ndege kazi yangu ni kutoa huduma kwa abiria.

 Basi Ndege ilipotua Arusha lnternational Airport mie Eselina Boazi nilikua bize nikijishuhulisha na usafi ndani ya ndege, si mnajua tena usafi kitu muhimu na cha lazima,usafi ndio afya ya wasafiri.


     Moyoni nilitingwa tingwa mawazo yaliyokitibua kichwa changu, maana nyumbani Arusha mawifi wenye gubu haweshi kulalamika ati si bora niachie ngazi kuliko kujiketisha nyumbani nikibugia ugali na kujaza choo pale kwa mume wangu wakati nashindwa hata kumletea mtoto wa kusingizia.



     Kusema kweli ndoa yangu yenye miaka sita sasa inachangamoto na jinamizi linaloitwa GUBU, mawifi hawanipendi yaani ni Bora ya mume wangu anayenipenda na kunithamini.


 Kwa wataalamu tumeenda sana mahospitalini nako wanadai hatuna ubaya, kizazi kipo saaafi salama, mbegu za mwenzangu zimeshiba afya tele, sijui tatizo nini jamani sie tukose mtoto 🥲😭 lakini ya Mungu mengi ya binadamu machache.


     Siku hiyo stress ziliusumbua mtima wangu, mawazo yalininyanyasa sana lakini ghafla nilikuja kushituliwa na sauti ya kilio cha mtoto mchanga 'ng'aaa ng'aaa ng'aa' 😿Mola we! Mapigo ya moyo yalinienda kasi. Mtoto!? Nilijiuliza⁉️ Nikamsogelea na kumkuta mtoto mchanga akiwa amelala juu ya kiti cha Ndege.


Nikaangaza macho yangu huku na huko yamkini ninaweza kumuona Mama au Baba wa mtoto lakini wapi! Sikuona mtu. Nikamnyanyua yule mtoto ili nimbebe hapo ndipo nilipokutana na kikaratasi chenye ujumbe kilichodondoka miguuni kwangu. Nikakiokota na kukisoma, kilisomeka hivi:



TAFADHALI MCHUKUE MTOTO HUYU UMTUNZE AWE WAKO ANAITWA CLINTON DICKSON. NISINGELIWEZA KUMLEA SABABU NINA MAISHA MAGUMU, NAKUOMBA UMTUNZE, MILIMA HAIKUTANI LAKINI BINADAMU TUNAKUTANA. NI IMANI YANGU KWAMBA IPO SIKU TUTAKUTANA TENA AJAPOKUA MTU MZIMA MWAMBIE NINAMPENDA NA PIA ANISAMEHE KWA UAMUZI HUU MGUMU.


Nilipomaliza kuusoma ule ujumbe mikono yangu ilitetemeka, macho yalikosa amani moyoni nililaani tendo la mwanamke mwenzangu kumtelekeza mtoto mchanga ndani ya ndege. Wakati sie wenzie tunahangaika kwa waganga na wataalam kutafuta watoto Bado tu magubu ya mawifi yakituandama.


     Any way silaumu wakunga kizazi kingalipo. Nikamchukua mtoto Clinton  Dickson, nikaelekea nyumbani kwangu Buza huko nilikutana na mume wangu niliyemueleza Kila kitu kuhusu mtoto niliyemuokota ndani ya ndege pamoja na kukisoma kipande cha barua kilichoachwa karibu na yule mtoto.


Mume wangu ni mtu mwelewa, alikubali tumtunze  Clinton Dickson. Basi mtoto Clinton akawa wetu, tukamlea kwa furaha na baraka tele.


    Niwaambie ndugu zangu kulea yatima ni baraka tosha sababu tulikua tumepanga kijumba pale Buza mwaka moja baadae tulikuja kushangaa shirika la Ndege likituzawadia nyumba Moja nzuri yenye Kila kitu NDANI, bahati nzuri NDANI ya mwaka ule ule mume wangu' alipandishwa cheo akawa ni mtu wa maana kazini, mwenye mshahara mnono wenye marupurupu. Sio jambo la kushangaza leo tukiwaambia tuna Gari mbili za kutembelea wakati zamani tulikua tukinyunda chini ya Jua lililotubananga.

         ######

Miaka kumi na tano baadae mwanangu Clintoni alikua akiingia kidato Cha kwanza ndani ya miaka hii kumi na mitano bahati nyingine ilitutembelea Mola alijibu maombi yetu nyumba ikajaliwa furaha ya kuwakaribisha wanetu wawili Lea na Andrea. Basi siku moja nikajawa tafakari kwa sasa kijana amekua na anaelekea utu uzima sio vizuri kumkalia kibubu lazima aijue historia yake, ni wapii ametoka? Wapi anaelekea? Nikamwita na kumketisha chini tukanywa kikombe cha kahawa kisha nikamweleza.


       "Nilikuokota mwanangu, nilikuokota ukiwa ndani ya ndege unalia kwa uchungu wa kutelekezwa. Uzuri Mama yako hakukutupa wala kukubwaga makusudi sema changamoto za kimaisha ndizo zilimpelekea afanye maamuzi ya kumuumiza moyo. nina imani Mama yako anajutia kitendo alichokifanya"



      "Mwanangu Mama Yako anakupenda kama kijikaratasi hiki chenye ujumbe kinavyoeleza, anakupenda na alitoa ahadi ipo siku isiyo na jina atajitokeza mfurahi pamoja, tafadhali ajapojitokeza. msamehe na muishi kwa amani" nikaendelea kusimulia.


      "Ishi ukijua mimi kwako ni Godmother, Mama mlezi ninakupenda sana mwanangu na pia ninahitaji UISHI pasina kukumbatia majuto au wasiwasi juu ya historia ya maisha Yako" Nilihitimisha na chozi lilimtoka, akasimama pale alipoketi akanifuata pale nilipoketi kisha akanikumbatia chozi na kilio cha uchungu vilimbubujika.😭


*********
 
Basi baada ya mwanangu kuijua historia ya maisha yake kwa ufupi akawa ni mtu ambaye hajatulia kila siku akiperuzi mitandaoni au kuuliza watu kuhusu pahali alipo Mamaye mzazi. Sikuchukia wala kumkataa sababu ile ilikua ni haki yake, haki ya kuwajua wazazi wake, haki ya kuijua historia yake.

 Baada ya kupita miaka miwili siku Moja nikiwa sebuleni ninapakaza dawa viatu vya mwanangu (Shoe shine )nilikuja kushituliwa na mlio wa simu, nilipoipokea maongezi yetu sikuyapendelea japo nilitarajia ipo siku maongezi yale yatakuja kuniamsha kutoka usingizi wa mawazo ya miaka mingi.

       "Hallow! Nani mwenzangu?" Nilimuuliza mara baada ya kupokea simu.

        "Mrs BOAZI mimi ni Subira Mama mzazi wa Clinton samahani ninaomba tuonane tuongee mengi juu ya suala la Clinton, binafsi ninaumia na kujuta."


        "Ebo! 🥴Miaka yote hii kumi na misaba mwanamke Leo ndio umemkumbuka mwanao, nadhani UNAMATATIZO wewe? Nilikasrika nikakata simu na kuitupia juu ya sofa.


PART THREE.


SUBIRA
 
SUBIRA mie baada ya kumtelekeza mwanangu Clinton Dickson ndani ya Air Tanzania kule Arusha Airport moyo wangu uliniuma sana nikawa ni mtu wa kulia na kujutia uamuzi wangu lakini moyo huo huo ukanipooza kwa kuniambia niondoe wasiwasi kwani mwanangu yupo katika mikono salama. 

     Nikaingia ndani ya Jiji la Arusha na kutafuta ubanda wangu ambao niliulipia kodi ya miezi sita baada ya hapo nkaadhimu kusaka kazi ambayo ingeniweka Mjini kidogo nisake ugali na tembele. Nilipata kazi ya kuosha vyombo na kupuguta deki ndani ya Hoteli Arusha Moja ya Hoteli zenye hadhi ya nyota tano,✨✨ kazi yangu ilinilipa vizuri na kula nilkula vizuri lakini Bado nilijiona nimepungukiwa mtu muhimu maishani mwangu ambaye ni mwanangu Clinton.


          Miaka kumi na misaba kupita bila aibu nikafanya kumtafuta yule mhudumu niliyeamini atanitunzia mwanangu niliyemtelekeza ndani ya ndege. Eselina BOAZI. Niliitafuta nambari yake ya simu ndani ya shirika la Ndege Nikampigia japokua mwanzo alikua ni mkali wa moto binafsi nilitakiwa kujishusha na kunyenyekea maana nilijua kosa na udhaifu wangu.


        "Ninaomba unipe ruhusa ya kuongea na mwanangu Clinton, Sina Raha, Sina furaha nazidi kukonda na kudhoofika kila siku kwa ajili yake. Historia yangu iliniumiza hata nifikirie kumtelekeza ndani ya ndege. Tafadhali nihurumie Nina Mpenda sana mwanangu, Niliongea kwenye simu pamoja na Eselina Boazi.


       "Kwendraaa👌, mwanamke mchafu wewe hufai kuitwa Mama sababu Mama mwema hawezi kumtelekeza mwanaye Kisha aende Duniani kufanya starehe." Eselina Boazi alinijibu kwa hasira.


    "Please Mrs BOAZI.... Please" Sikumaliza kuongea alinikatia simu. Bado tu sikukata tamaa hata zilipopita wiki tatu nilimbembeleza Mama mlezi wa Mwanangu kama wazungu wanavyosema Never give up. Siku Moja Eselina alinipgia simu akanitaka tukutane Royal Arusha Hoteli nilifurahia maana mwanamke huyu ana roho ya huruma na upole.

*******


PART FOUR

CLINTON.

"Wewe ni shetani tena shetani asiye na huruma."Clinton alinipigia kelele tukiwa ndani ya Royal Arusha Hoteli.


     "Huna maana ya kuitwa Mama, Mama gani amtelekezaye mwanaye? Je, ulipenda niwe mtoto chokoraa au nikalelewe kwenye vituo vya watoto yatima?" Aliniuliza wakati huo mie chozi la uchungu lilinitoka.


    "Naomba unisamehe mwanangu, nisamehe damu ni nzito kuliko maji, changamoto za Dunia zilinikatisha tamaa."Nilijitetea.


        "Kukusamehe nimekusamehe lakini usidhani nitakuita Mama, Mama yangu ni mmoja tu ambaye ni Eselina Boazi sio wewe Subira." Mwanangu aliongea ukweli kutoka moyoni.


        "Ninakubali Clinton, ninakubali fanya utakavyo lakini unisamehe tena usinitenge kama nilivyokosea mimi ." Nililia sana siku ile nililia nisiamini kama kweli mie na Mwana tuliyepotezana miaka kumi na misaba Leo angelionesha huruma na upendo kwake nisiyefaa kuitwa Mama.


      "Ninaomba wikiendi niwatembelee nyumbani kwenu mwanangu." Niliomba tu nianzishe undugu mwema.


      "Utakavyo." Nilimwambia Mwana yule mpole mwenye macho yangu na sauti inayofanana na yangu

**********

      Nilipofikisha miaka ishirini na tatu nilielekea Chuo kusoma mambo ya ustawi wa jamii na maendeleo. Umri wangu ulienda sana nikawa ni mtu mzima Sasa ninaye jielewa.


SUBIRA mama aliyenitelekeza hakuacha kumshukuru Mama yangu Eselina Boazi kwa wema na uvumilivu wake kunitunza mie ambaye alinikatia tamaa ya kunilea. Kila siku alikua akimtaja Tamari kama Mama ambaye alimsaidia sana nauri ya ndege ambayo mimi nilitelekezewa humo, Subira Kila siku ananiambia popote alipo Tamari Mungu ambariki sababu Hana cha kumlipa zaidi ya maombi na baraka tele.
________________________

Ngriiiiii ngriiiiii Kengere ya mlango wa nyumba ya  Bi. Eselina Boazi iliita. Dakika tatu badaye nilijitokeza mie Clinton nikamkaribisha na kumpokea Mama yangu mzazi alikua amebeba zawadi alizoniletea. Viatu vya michezo, boksa nzuri, kofia ya kapero na socks ndefu kwa ajiri ya michezo.



       "Asante Clinton, Asante niumekaribia."SUBIRA alinishukuru kwa kumkaribisha akaingia ndani alikomkuta Mama yangu Bi. Boazi na Babaangu Bwana Boazi wameketi wakinywa Wine ya mzabibu kwa furaha. Mama AKATABASAM.


__________________

TCHAO 💖 
________________


Let love 💞 lead.





No comments:

Post a Comment

BEKA

 SURAYA TATU                        “AKIPITA ATAJIPITISHA.” Beka akawa member wa kampuni ya SIGA, akipelekwa hapa na pale kulinda mali za ma...