Ben akiwa anajiandaa kucheza mpira pamoja na rafiki zake wawili Kijiko na Kichungu, mara ghafla Kijiko alianzisha maongezi.
KIJIKO: Oya! Ben, ninasikia siku hizi unatembea na mtoto Amina.
BEN: (Kwa aibu Fulani). Mmmh! Ni nani kakwambia?
KICHUNGU: Mzee, mapenzi hayana siri, mapenzi ni kikohozi, usilolijua litakusumbua, shule nzima wanafunzi wote wanajua kuwa wewe una mahusiano na Amina. (Anaongea kwa utani).
BEN: (Anashangaa na kuguna). Mmmh! Ishakuwa balaa, yaani mimi na Amina hatuna hata mwezi mmoja katika mahusiano yetu, nashangaa haya yamevuma kama upepo wa baharini.
KIJIKO: Ndio hivyo mkuu, sisi tumezinyaka tetesi kutoka kwa madenti wa darasa analosoma Amina, wanadai kuwa Amina anawaambia kuwa wewe ni wa kwake, hakutemi wala hakutupi.
BEN: Duh! Nilijua itakuwa siri, sasa naamini kama dunia haina siri, hapana siri ya watu wawili.
KICHUNGU: Yanini kuficha ficha Ben, eeh! Mficha uchi hazai, kula vitu bwana, ondoa aibu inayokutafuna, mchinje yule kuku, ule umtakavyo.
BEN: (Anacheka kwa aibu).
KIJIKO: Vipi huyo kuku ushamla au unasubiria hadi apoe(Anajaribu kucheza mpira wa danadana).
BEN: Wallah! Bado kabisa.
KICHUNGU: Unasubiri nini sasa?
BEN: Mmmh! (Anaguna). Aaah! (Anashindwa kuongea).
KIJIKO: Wakati ndio huu mzee, kula ujana uzee safari ndefu.
BEN: (Anajaribu kucheka).
KIJIKO: Lakini pia ukumbuke kuvaa mpira, si unajua tena zigo likituna tumboni inakuwa kesi, utaiacha shule pasina kupenda, utawakwaza wazazi wanaokusomesha, na baya zaidi utapoteza ndoto zako. (Kijiko alitoa mashauri).
BEN: Poa washikaji, nimewageti, nitafanya kama mnavyonishauri. (Ben, Kijiko, na Kichungu walianza kucheza mpira).
****************************
BEN:(Ameketi pamoja na Amina wakiwa Canteen, wanapata chai na mihogo, maongezi yao yanaendelea). Vipi masomo yako yanasemaje?
AMINA: Hata siyapendi.
BEN: (Anashangaa kidogo Amina). Kivipi, mbona sikuelewi mpenzi wangu?
AMINA: (Anarembua rembua macho). Mie sielewi kitu chochote wanachofundisha walimu.
BEN: Hilo sio tatizo kubwa sana Amina, mie nipo radhi kukusaidia somo lolote lile ambalo linakushinda.
AMINA: Ooooh! Jamani Ben. (Anakanyaga mguu wake Ben).Asante sana, nitashukuru.
BEN: (Anajaribu kujiondoa pale alipokanyagwa). Shaka ondoa, binadamu kusaidiana, leo kwangu, kesho kwako, mbona wahenga walisema, ‘Wema hauozi’, tenda wema uende zako, nifae la mvua, nikufae la jua, maisha ni kusaidiana’.
AMINA: (Mwingi wa fahari, japokuwa anachukia masomo yake). Leo nataka uanze kunisaidia somo la Kiswahili, au hauna muda huo.
BEN: Anawaza moyoni mwake). Mmmh! Hadi Kiswahili kinamshinda…au!? Mmmh! Anajua kukiongea, kukiandika hawezi. (Anamjibu Amina). Ninao muda mwingi wa kutosha.
AMINA: Vizuri, basi mie nitakuja geto kwako, si uliniambia umepanga huko Buguruni?
BEN: (Anaingiwa na wasi wasi). Aaah! Ndio…Ka…Ka. Karibu sana, utakuja saa ngapi vile?
AMINA: Usiku ndio mzuri, saa mbili hivi nitamdanganya mama yangu, nitamwambia leo naenda kujisiomea kwa Shoga yangu Anna, nitalala huko huko. (Amina aliongea bila wasi wasi).
BEN: Hapana Amina, usifanye hivyo, basi mie nitakufundisha muda wa mchana tutokapo shule, ili usiku uwahi kurejea nyumbani. (Ben alitia wasiwasi).
AMINA: Hapana Bwana, jua kuwa mie nakupenda, nikubalie ili leo nije nyumbani kwako. (Amina alimlazimisha Ben, Ben hakuwa na jinsi, alijikuta anakubali.)
##
ANNA: (Wakiwa darasani Siku liyofuata). Eeh! wacha we! Unasema kuwa ulilala kitanda kimoja na yule handsome aitwaye Ben?
AMINA: Sikufichi, nakwambia ilinibidi nimlazimishe ku do naye, yaani kijana alionekana mgeni haswa, mara nimshike hapa, utakuta anatetemeka, mara nimpapapse pale, angelitoa mikono yangu, lakini yote tisa kumi nilimuweka pale alipopaswa kuwekwa.
ANNA: Teh! Teh! Teh! Teh! (Anacheka) kuku mgeni hakosi kamba, huyo keishaingia kiulaini laini, na kwa jinsi nijuavyo mie atakulilia huyo, hakuachi ng’o, atakuwaza iwe usiku iwe mchana, hawezi kula kulala, wala kusoma juu yako.
AMINA: ( Anakomboa mafuta ya kujipaka midomoni kunako kopo dogo alilobeba kisha anajipaka paka midomo yake). Swala keishaingia mitegoni.
Itaendelea
No comments:
Post a Comment