KUKU WA KIZUNGU
Sehemu ya sita.
Basi siku moja yapata mchana wa saa nane, Swinje yupo dukani kwake, banda la mahitaji ya kila siku, mahitaji ya nyumbani. Anauza hapo Sukari, chumvi, majani ya chai, Mafuta kula, Mayai, Bisckuti, unga, mchele, harage mafuta taa pipi na vitu vingine vingi ambavyo wanakijiji wanafurahia sababu hudum a yake ni nzuri na ipo ‘Very good’ Laizer amefanya juu chini kumfungulia mkewe Duka hapo kijijini na Laizer mwenyewe kawezeshwa kamtaji kanono kutoka kwa nyumba ndogo, English Figure. Swinje akiwa hana hili wala lile mara Islama akalivaa lile Duka, ameja tele, hayupo single yupo yeye pamoja na mwanye TINO, mtoto amekopi kila kitu kutoka kwa mume wa mtu. Leo Islama amekuja ndani ya Duka la Swinje kuchukua mahitaji ya nyumbani na uzuri wa siku ya leo Islama ameona heri anyoshe nyoshe miguu kidogo, sababu hana kawaida ya kutembea tembea hapo Maasai Land, siku zote amekuwa Bize akifurahia mapendo apewayo na Mtumi Laizer.
Sio kwamba Mtumi Laizer ameanza tabia ya uvivu, La! Hasha, ndivyo mapenzi yalivyo, mapenzi ni kupendana ukipenda boga penda na Ua lake, mapenzi ni kusaidiana au sio? Kusema kweli Swinje hamjui wala hajapata kumuona huyu English figure. Hamjui Modo aliyezaa na mumewe, bali amekuwa akizisikia sifa na wema wa English Figure, sifa na wema huo anahadithiwa na mumewe, Mumewe amekuwa akimsifu sana Mzungu kwa kudai kuwa ni mtu mwema na pia ni mtu mwenye roho ya huruma. Kama ilivyo kwa bibie Swinje, Ndivyo ilivyo kwa Islama, Islama hamjui mke wa Laizer bali anazisikia tu habari kwamba Laizer ana mke mwenye watoto wawili. Tuseme kwa kifupi, wake wa Laize Hawajuani wala hawajawahi onana laivu.
“Hallow mama Yoyo.” Islama alimwita Swinje.
“Hallow Mzungu, karibu sana.” Swinje alimkaribisha Islama Dukan kwake.
“ Asante sana, mie nipo na shida, ninahitaji maziwa ya kopo, Sukari na mkate.”Islama aliagiza mahitaji yake yote mara baada ya kutoa salamu.“Sawa Mzungu.” Swinje akafanya kama alivyo agizwa lakini macho yake yote yalitua mbele ya sura ya TINO mwana wa Islama, akimshangaa shangaa yule mtoto kwa jinsi alivyofanana na mumewe Laizer. Macho ya Swinje hayakukoma kumwangalia Tino kila alipotoa huduma na bidhaa alimtazama yule mtoto. Uvumilivu ulipomshida Swinje mkewe Laizer akajikuta anauliza.
“Samahani Mzungu, hivi huyu mtoto ni mwanao?”
“Yes, he is my son. My precious my every thing lslama alijibu kwa furaha, Swinje angali bado anashangaa.
"Mwanao kabisa…. Mwana wa kumzaa? Swinje alidadisi.
'NDIO, MWANA WANGU WA KUMZA, DAMU YANGU, PACHA WANGU.” Islama alijibu bila hofu.
"Kulikoni, mbona umetamani sana kujua?” Islama alimuuliza Swinje Swinje hakua na pupa ya kujibu.
"Aah! Mmmh! Nimependa tu kujua maana mwanao anafanana sana na sura ya baba wa watoto wangu.”
“ Baba wa watoto wako?”
“Ndio, yaani mwanao amechukulia kila kitu kutoka kwa mume wangu.” Swinje aliongea moyoni amejaa mashaka juu ya uwepo wa yule mtoto, anahisi kitu moyoni, anahisi labda ndio hivyo tena, anawaza labda yale maneno aliyoyanena Balozi juu ya kumchunguza Mumewe hapo yamefikia.”
“Mumeo! Mumeo jina lake nani? Islama alitaka kujua.
“Anaitwa Laizer.” Swinje alitoboa. Islama alipolisikia jina la Laizer alihisi hatari mbele yake, moyo wake, ukamwenda mapigo, alitetemeka. Alipona hatari mbele yake sababu yeye binafsi anajua fika kuwa ‘Fahari wawili hawalali Zizi moja.’ Yasije yakamkuta yale asiyo yataka, yasije yakamkuta makubwa ya dunia. Mume wa mtu sumu, hayo tena anayaogopa.
"Aaah! Duniani wawili wawili,” Islama alijibu kwa kifupi.
" Ya mungu mengi, Mungu ndiye aliyepanga mwanao, afanane na mumeo.” Islama alijitetea, ingawaje alijua fika kuwa siku za mwizi Harobaini, yasije yakamwagika nani atayazoa.Ghafla Islama akatoka mbele ya yale Mahadhari pasina kuaga, amejaa hofu ajabu, hajapata kuwa na hofu ile, ‘One by one’ akaelekea nyumbani kwake ni mwingi wa mawazo, asijue itakuwaje iwapo itagundulika kuwa amemuibia mume mwanamke wa kimaasai. Kwa jinsi anavyowajua wanawake wa kimaasai huwaga hawataki mchezo, wana hasira hasara, wakipandisha Mori wamepandisha. Wakitaka kumfanyia ubaya mwanamke huyu watamfanyia tu, iwe isiwe, kwa udi na kwa uvumba. Iwe kwa gharama au isiwe kwa gharama atajuta Islama, maji shingoni, bado kutapatapa. Islama akatia hofu moyoni mwake.
...........................
“Love.” Islama alimwita Mtumi Laizer.
“Yeah, Sweet Amour.” Laizer aliitikia Sauti ya Bossi wake, wakati huo wote pamoja wmeketi bustanini wakifurahi pamoja na mwana wao Tino.
“I have some thing to tell you,” (kuna jambo nataka kukuambia) Islama alimwmbia Mpenzi wake. Ni wiki ya tatu sasa tangu akumbane uso kwa uso na mkewe Laizer bibie Swinje, Islama bado anaogopa sana.
“What is all about?” (Yahusi nini?) Laizer alihitaji kujua nini Islama anataka kumweleza. Islama hakuwa na pupa ya kumueleza Laizer yale yaliyo moyoni mwake. Alihitaji kuyapanga mawazo yake balabala, mbinu na ujanja wa kumweleza Laizer ili apate ujanja wa kuyatoroka mazingira ya Maasai Land.
“Unajua Love, Mimi wako wa rohoni nimekuwepo ndani ya kijiji cha Maasai Land kwa muda wa mwaka Mmoja na nusu sasa, Islama aliongea.”
“Yes najua kuhusu hilo.”
“Tena tumebahatika kuwa na mtoto mzuri wa kiume.”
“Ni mapenzi ya Mungu.” Laizer aliongea.
“Yeah! Mungu ni pendo.” Islama alijibu kwa ufupi kisha akaendelea kuongea.
“ Laizer bado ninakupenda , nakupenda sana sweet.”
“Na mimi pia,Ilove you so much”
“Sitaki kukuacha.”
“Uniache uende wapi?” Laizer aliongea kwa tabasmu anamchezea chezea Tino mtoto wao ,mtoto anacheka cheka kwa fura ya kitoto.
“Siend popote, lakini ninataka nirudi nyumbani England.”
“ENGLAND.!!?” Laizer alishituka kidogo,
“England kufanya nini?” Laizer alihitaji kujua.
“Kusalimia baba na mama yangu, wametuma E-mail wanasema wamenimiss sana wanataka kuniona.”
“Kwa hiyo unataka kuondoka moja kwa moja?”
“Sio kwamba ninataka kuondoka moja kwa moja, Love nitarudi ni short time , ‘Just for warm greetings’.” Islama alijitetea ingawaje moyoni mwake akijua fika kwamba hana mpango wa kurudi Afrika. Anataka kuondoka moja kwa moja anatambua fika kuwa kitu cha mtu mavi, kisije kikamtokea puani. Kama ni suala la kuishi Afrika tayari ameishi, mkataba wake wa mwaka mmoja na nusu tayari umefikia tamati. Anapaswa kurudisha ile gari aliyoazima, anapaswa kukabidhi ile nyumba aliyofikia tena anapaswa kuondoka kurudi England. Kama angelipenda kuendelea kuishi Tanzania yupo free kuongeza mkataba, Lakini moyo wake hautaki tena kuendelea kuwepo Afrika japokua bado anapapenda sana Maasai Land, anampenda sana Laizer anampenda yaani hadi machozi yanambubujika.
“Hapana usiondoke Love,”Laizer alimuomba Islama.
“Bado ninakuhitaji, najua ukiondoka hauwezi kurudi tena Tanzania,” Laizer alijaribu kuipinga Safari amabayo Islama aliipanga.
“Sikudanganyi Love, nitarudi, nitarudi haraka ili tuliendeleze Penzi letu, kama ujuavyo tena ‘Home is best and a better place,’ nimepamiss home, nimepamiss so much.” Islama alijitetea, machozi yamejaa machoni bado kidogo kudondoka.
“ Kwa hiyo ndio unataka kuondoka, vipi kuhusu mwanetu Tino unaondoka naye.?”
“Yes ninaondoka naye, muda si mrefu ni bada ya wiki mbili zijazo.”
“What? Unaondoka na tino?!!”Laizer alipigwa naa mshangao.
“Mbona umeshituka sana Love? Je wewe unataka Tino abaki Afrika?”
“Yes, that’s all.” Laizer aliongea.
“No, haiwezakani, kwanini niende pekee yangu Euorope? Wakati tayari nimekwisha waeleza wazazi wangu kwamba ninaye mjukuu wao, ninakuja naye England, isitoshe hapa Afrika Tino atakaa na nani? Bado kifaranga wa kunyonya. Kama ujuavyo tena mapenzi yetu yalikua ni ya siri kubwa mno.”
“Nitabaki naye mie.”Laizer alijaribu kumtetea mwanaye.
“ How? Kivipi ? Mpenzi je huogopi mkeo? Huogopi vurugu, ugomvi na kuvunjika kwa ndoa yako?”
“Sijali sana kuhusu uwepo wa mke wangu, ninajali uwepo wako wewe na mwanetu Tino.” Laizer aliongea kisha akaendelea.
“Sio lazima nimpeleke Tino nyumbani kwa mke wangu Swinje naweza kumchukua na kumtunza nyumbani kwa Balozi Ole hadi hapo utakaporejea Sweet Amour.”
“Sipingani na maamuzi yako mpenzi,” Islama aliongea.
“Ninajua ni kwa jinsi gani unavyonipenda na pia unavyompenda mwanetu Tino, hata hivyo ninataka nikuambie kwamba usimwamini sana Balozi Ole, hii ni kwa sababu anakuchukia wewe lakini wewe binafsi haujui kuhusu hilo. Ana wivu sana yule Balozi, alinitamani na kuniambia kuwa ananihitaji lakini moyo wangu ulimkataa, tizama sasa haujafahamu kuwa yaliyo moyoni mwake yana matokeo. Na hayo matokeo ni mazito ni sawa na jambo usilolijua usiku wa giza.”
“Au twaweza kwenda wote England?” Laizer alikuwa kin’ang’anizi, lengo lake asimpoteze Tino mwanawe anajua fika kwamba Islama akiondoka kuna asilimia ndogo ya yeye kurejea, haamini kama Islama anaweza kurudi, anajua fika kuwa Wazungu wengi sana wametembelea Maasai Land, na wengi wa hao wazungu hawajapata kurudi tena labda wachache wenye moyo wa kurejea Afrika.
“Sipingani na ombi lako la kwenda pamoja na mie, lakini mpenzi acha niseme hivi, uniruhusu nitangulie kwanza, niende nikakuandalie mazingira, nikaweke mambo yote sawa na baada ya hapo nikirudi tutapanga Safari ya pamoja ya kwenda England. Islama aliongea,moyoni mwake anajua fika kuwa anazingua ili apate chance ya kumtoroka handsome wake.
“Ooh! Love,” Laizer aliongea anasura ya huruma, hana imani juu ya Safari ya Sweet love wake, Armour wa moyo wake. Anawaza sana, je itakuwaje iwapo Tino wake akitoweka machoni kwake?”
“ Usiende Love.” Laizer aliongea kwa sauti ya upole na msistizo.
“Acha niende Love.” Islama alibembeleza. Moyoni akijisemea; ‘Ipo siku nitarudi tena Afrika.’
“Please love…. Please Islama, I still love you, Istill need you.” Kwa mara ya kwanza tangu Laizer amjue Islama leo alilitamka jina lake. Islama akadondosha machozi, hakua na jinsi moyo wake ulimwambia ‘Rudi England’ akamkumbatia Laizer, akambusu Shavuni, Machozi yakamdondoka, yakatua kifuani kwa Laizer pale ulipo moyo wa Laizer.
#################
‘Teeh teeh teeh teeh🤣.’ Balozi Ole alicheka kwa sauti kuu alicheka mbele ya Laizer ambaye alionekana wazi kufura kwa Hasira hasara, kidogo angempandishia MORI lakini hacha tu, alimheshimu Balozi, alimheshimu Mwanasiasa wa kijiji.
“Kiko wapi!? Kizuri hujiuza, kibaya je? Uliona vyaelea hukujua kwamba vimeundwa.” Balozi alimkebehi Laizer.
“Ni miezi misita sasa tangu Islama ameondoka, kijana usitarajie kama atarudi tena, amekuzingua yule, amekudanganya , ati angechukua wiki mbili tatu za kuwasabahi wazazi wake, ndugu, jamaa na marafiki huko alikokwenda England '
"Teeh teeh teeh…😹😹..Ai, ndivyo walivyo Kuku wa kizungu wakiyachoka mazingira magumu ni lazima wayatoroke.
”Balozi aliongea, angarau ndani ya miezi hii misita afya yake imerudi, imerejea, sababu hapo awali alikua hali, hanywi, anakonda na kudhoofika kwa sababu ya KUKU wa kizungu, Kuku ambaye hajamla wala hajamwonja, hajayagusa hata mabawa yake, sembuse supu ya huyo kuku anaisikia tu japo hajawahi kuinywa. Afadhali kwa sasa angarau afya ya Balozi imerudi, kipindi yupo Islama machoni pa watu alionekana mifupa mitupu, lakini heri na afadhali kwa sasa ameshiba hadi kile kitambi chake kimeanza kutabasamu.
“ Nifanye nini Balozi?" Chozi la mapenzi lilitaka kumdondoka Laizer, amekuwa akilia kila siku, picha ya Islama na mwanaye Tino inapomjia kumbukumbu, amekonda na kudhoofika kwa sababu ya mapenzi, ama kweli kufa kufaana, leo kwangu kesho kwako. Yaliyomkuta Balozi yamehamia kwa Laizer. Lo! Asipoangalia atakwenda na maji. Asipoangalia ataisha na kupurukutika.
“Ufanye nini?” Teeh teeh teeh teh🤣🤣🤣😹’ Balozi aliendelea kucheka kwa dharau.
“Eti ufanye nini? Nenda England,ukamtafute English figure, kama huwezi basi baki na mkeo Swinje, kula bata furahia maisha ya Kijiji.”
“Na mwanangu Tino je?”
“Walisema waswahili, kiendacho kwa Sangoma(Mganga) hakirudi, kikirudi ni bahati na miujiza, tena kama ujuavyo, bahati haijagi mara mbili mbili, usingeliichezea hiyo bahati.” Balozi aliongea kimafumbo.
“Hapo hadi Mungu na Mizimu ya Maasai land ipende, la sivyo basi utangoja mwenzetu, utangoja hadi mwisho wa dunia. Ndivyo walivyo Kuku wa kizungu (Balozi alianza kulaumu) Keisha timiza matamanio yake na sasa anaendelea na maisha yake.”
“Balozi!” Laizer alidondosha chozi.
“Nisaidie,”
“Nikusaidiaje,umekula Kuku umeshiba, mimi hujaniacha hata mifupa, sembuse utumbo au miguu saizi unaniambia nikusaidie… nikusaidiaje? Kama unataka nikusaidie basi nakushauri tafuta kuku wa kienyeji utapata vifaranga wengi .” Balozi Ole alitabasamu, moyoni mwake akijisemea;
“Ona, uliringa sana, sasa umerudi tena kwenye ufukara, japokuwa mie sikubahatika Kumla kuku, nyakati nyingine lazima niwe ‘Attention,’ kuku akija hapa Maasai, mie nitakuwa wa kwanza kumla. Kuku akihitaji Mtumi mie nitajitolea niwe Mtumi wake, ‘teeh teeh teh' Balozi alicheka kimoyo moyo, anamtizama Laizer akimwaga chozi, chozi la mahaba yake kwa Islama.
Itaendelea.
No comments:
Post a Comment