Tuesday, September 17, 2024

BEAUTINESS OF ZANZIBAR lSLAND

 UTURI WA ZANZIBARI






Yapendeza mahandhari, ya ndege na vipepeo,

Yanayonukia uturi, uturi wa Zanzibari,

Upepo ukiwa shwari mapenzi  yawe Johari

Upepo ukiwa shwari mapenzi  yawe Johari

 



Mapenzi ni kama kito, cha johari maishani,

Yana mwili wenye joto, na burudisha moyoni,

Penzi lenye manukato uturi wake maanani.

 



Moyo una burudiko kwa uturi wako mama,

Ningalipo na sisimuko kwa yako mandhari mema

Nataka niwe kwako, niishi katika usalama,

 

 


Uturi wa hali pevu, uturi wa Zanzibari,

Ningali bado mwenye nguvu, nikae kwako mwanamwari

Unipe maarufu, nakupenda Zanzibar.

 


Ewe binti Sultani, Uzuri wangu mbinguni,

Unipe matumaini, niwe nawe maishani,

Na makuli unilishe ni nenepe ni bukheri

 


Niliyasaka sana, mandhari yenye mapezi,

Lakini sikuyaona, mazuri yalo azizi,

Yaliyo na uungwana, kama yako eh! mapenzi



 

No comments:

Post a Comment

I promise you

   I PROMISE YOU. (NINAKUAHIDI.) SURA  YA KWANZA. UBAYA WA POMBE. “Umenizingua job, umenizingua kwa muda mrefu sana mpenzi wangu…….kwanini l...