KUKU WA KIZUNGU
Sehemu ya Saba
BARUA KUTOKA ENGLAND.
Baada ya miaka Saba kupita
Ni siku nyingine tena, Miaka saba kipindi kirefu tangu Islama aondoke Maasai Land na kurudi ENGLAND, siku ya leo Balozi Ole ameketi kwenye Kijumba nyasi chake, yupo yeye na wakeze wawili, wamemwandalia Nyama ya mbuzi aliye chomwa, kuna maziwa mengi ndani ya kibuyu kikubwa kama mkongojo wa tembo. Anakula na kunywa taratibu, siku hizi hana mawazo mengi kama kipindi kile English figure alivyomkondesha kwa kumpenda Laizer, kupungua kwa mawazo yake kumemfanya Balozi Ole anenepe vizuri sana, Mvi juu ya kichwa chake zimeanza kumtamania. Mkewe mkubwa alikuwa akiwajibika kazi ya kujenga Nyumba yao. Balozi anataka awe na nyumba mpya pale Maasai Land, sababu ya wivu na kijicho chake kwa Laizer mwenye nyumba ya Bati na milango saafi ya mbao na chuma kisichoshika kutu wala kisicho liwa na mchwa. Anamwonea wivu Laizer sababu amependelewa, amejengewa nyumba bomba pale kijijini, amejengewa kwa pesa za English figure, amefanyiwa mazuri ya mengi kipindi kile. Ndo’ sababu Balozi ameona heri ajichange change kidogo haba na haba akauza mbuzi na ng’ombe wake wengi pale kijijini akanunua sementi, tofali na mabati ya kuekeza Kofia ya nyumba. Basi kazi ya kujenga ile nyumba akawaachia wakeze wawili wajenge kama mila za wamaasai zinavyowataka wanawake wajenge nyumba. Lakini leo mkewe mkubwa amechukua jukumu la kujenga akiwa pekee, mke mdogo ambaye bado ni kijana kijana anafanya kukamua maziwa ya ng’ombe na mbuzi akiisha kumaliza kazi hizo budi aende Kisimani kuteka maji au Porini kuokota kuni.
“Hodi hod hodi Mheshimiwa Balozi.” Ilikuuwa ni sauti ya YIARO Mtumi wake Balozi Ole, alitumwa aende Posta, Arusha mjini kuchukua Barua Za wanakijiji , kijiji cha Maasai Land. Leo amepokea Barua moja tu, siku zingine huja na barua tatu au tano, leo amekuja na Barua moja tu.
“Ingia Yiaro Mtumi wangu.” Yiaro aliingia Mkuki wake mkononi, sime yake kiunoni, vumbi miguuni kama ugolo wa kimaasai. Alimsabahi Balozi na baada ya Kumsabahi Yiaro alinena.
“Leo Posta nimeikuta Barua moja tu, hii barua ni maalumu kwa Ole Laizer, Yiaro aliongea akitegemea Balozi angeli ichukua ile Barua aifungue apate kusoma nini kiklichoandikwa ndani. Ndio kawaida ya Balozi siku zote Barua za wanakijiji zikiwasili uzifungua na kusoma soma nini kilichoandikwa ndani na kwa sababu Balozi ni Mbea tena ni Mwizi siku hizi, Barua za wanakijiji zikiwasili lazima aibe pesa kidogo zilizotumwa ndani ya hizo Barua, iwapo tu hizo Barua zimeambatanishwa na Fedha.
‘Mfyuuuuuuuu,’ Balozi aliachia mfyonyo wa nguvu, uliomshitua hadi Bi. mkubwa, mkewe wa kwanza aliyekuwa bize akichanganya changanya mchanga na sementi ili aendelee kuijenga nyumba yao.
“Embu mpelekee mjinga huyo barua nyumbani kwake, sitaki hata kusikia habari za Laizer.” Balozi alinena mara baada ya kusikia kuwa ile ni barua ya Laizer adui yake.
“Balozi kwa hiyo leo hatuifungui Barua ya Laizer kama tunavyozifunguaga Barua za watu wengine, ili tuusome umbea ulioandikwa ndani.”
“Bull shit! Yiaro usitake nipandishe Mori sasa hivi, embu mpelekee Laizer mali yake, sipendi kabisa kusikia habari za Laizer.” Balozi aliongea Yiaro alitii amri ya mkubwa wake moyoni mwake Yiaro amesikitika sana sababu mfuko wa ile Barua ya kaki ulituna balaa, kama sio pesa zile basi ni vitu vya bei gharama.Yiaro aliondoka, Balozi maneno yanamtoka balaa, anamchukia na kumlaani adui yake.
“Miaka misaba iliyopita Laizer alikulaga kuku wa Kizungu pekee yake na ubaya wa yeye kumla Kuku wa kizungu amesababisha kuku wengine wasije hapa maasai Land, huu ni mkosi, tena huu mkosi ufagiliwe mbali.” Balozi aliongea maneno ambayo wakeze hawakumwelewa neno baada ya neno.
“Jamani oneni wazungu walikuwa wakimiminika hapa Maasai Land kama mvua ya gharika, ajabu kama maajabu miaka hii saba ya mkosi hajaonekana Mzungu au chotara wa kizungu hapa Maasi Land.” Balozi alikuwa ndani ya mawazo.
“Eeh!” Mara akashituka.
“Hivi ile Barua ya Laizer imetoka wapi? Mungu na Miungu ya Maasai Land nilisahau kumuuliza Yiaro, au nimkimbilie ili nijue ile Barua imetoka wapi?........ mmmh! Ngoja arudi.” Wasi wasi na shaka kidogo vilimwingia Balozi.
“We mume, kula nyama, kunywa maziwa hayo, acha kuongea vitu usivyovijua, ujue muda unakimbia, vikao vya wazee vinakungoja.” Bi. Mkubwa alimpigia kelele Balozi ambaye mawazo yalianza kumtinga na kumsumbua kichwani.
“Alafu mume wangu tabia uifanyayo siku hizi sio nzuri na tena haipendezi katika jamii.” Bi. Mkubwa aliacha kujenga nyumba yao akiwa amesimama hapo anapojenga aliongea.
“Tabia gani we mwanamke? Unaacha kufanya kazi zako unaingilia mambo ya wanaume, haipendezi katika Maasai Land.”
“Hata kama haipendezi katika Maasai Land mume wangu sio vizuri kufungua barua za wanakijiji, unavunja heshima zao unaharibu siri zao, unaiba pesa zao.”
“ Achana na mimi wewe, wewe ni mwanamke tu, hupaswi kujua siri za wanaume, mambo haya hayakuhusu, kwanza wajibu wako wewe ni kuzaa na kulea watoto tu.”
“Sababu hujaelimika ndio maana unanijibu hovyo, lakini ipo siku utakuja kulifungua Jini ndani ya hizo barua za wanakijiji.” Bi. Mkubwa alilalama.
“Kweli kabisa, kweli usemalo Bi. Mkubwa.” Bi . Mdogo aliaacha kukamua ng’ombe maziwa akamuunga mkono Bi. Mkubwa.
“Wanawake nyie mna nini ? mbona mna umoja wa kunishutumu, mimi ni kiongozi na kiongozi lazima ajue mienendo ya wanakijiji wake, je iwapo watu wabaya wamepanga njama ya kufanya ugaidi hapa Maasai Land? Itakuwaje sasa?”
“Ugaidi kwa kupitia barua.”Bi. mkubwa na Bi. Mmdogo walimjibu Balozi kwa pamoja. Balozi hakuendelea kuongea aliuchunia maana alitambua kuwa tayari ameaibika.
##########
Itaendelea.
No comments:
Post a Comment