Tuesday, September 17, 2024

KUKU WA KIZUNGU .🐓SEHEMU ya sita



Kuku wa kizungu

SEHEMU ya 6

Tulipoishia Jana

         miezi mitatu sasa tangu Islama ameingia ndani ya kijiji cha Masai Land Balozi Ole bado anatamani kumla kuku wa Kizungu ndo maana na leo tena Kafungasha Safari yake, kabisha Hodi lango la Islama, kafunguliwa na Laizer, Balozi kajaa tele,  Hapunguki Zawadi za kumletea Islama, ndio maana leo kamletea, Mbuzi BEBERU mzima mkubwa haswa, zawadi ya Islama.  Japokuwa kapungua Afya yake, mmh! Ana nini? Tunashangaa, embu ngoja tumsome:


Leo tuendelee hapa

“Ninaona maisha ya kijijini yamekupenda sana mwanadada.” Balozi Ole alianza kuongea. 

“Sana, yaani kwa kifupi nitabaki Afrika,  Afrika yanitosha, upepo mwanana, mvua zisizo na gharika, amani tele,” Islama aliongea, wakati huo Laizer alikuwa Mekoni anamkaanga kuku mnono, maalumu kwa ajili ya Balozi Ole. Mgeni njoo wenyeji wapone.

“Ubakie milele ndani ya kisiwa cha amani, tena kama ungelijua fika kuwa nilikuwa ninataka kukushauri  kuanzia sasa usikae tu nyumbani, fanya kutembelea sehemu mbali mbali za Tanzania, enenda kutalii Tanga, Dar es salaam, Zanzibar, Pemba, Unguja, Mbeya,Iringa na Tabora. Ujapo rizika kwa hayo matembezi usichoke endelea kuzunguka sehemu nyingine nyingi za Afrika fanya kwenda Mombasa na Nairobi Kenya, miji hiyo ni miji yenye mvuto sana Afrika. Balozi kwa porojo mbona hajambo, ni muongeaji mzuri, Islama mwenyewe aliupenda uongeaji wake.

“Ushaurii wako ni mzuri lakini nisikufiche Balozi, moyo wangu umetua ndani ya kijiji cha Maasai Land, hapa ndipo penye tulizo la moyo wangu, sioni haja ya kwenda kwingineko. Kwanini nitoke Maasai Land niende kwingineko? Kitu hiyo haitatokea ‘never ever’.” Islam aliongea kama Mwenyeji.

       “ Ushakuwa mzalendo bibie, ndivyo inavyopendeza, uzalendo huanzia nyumbani, nyumbani ndio kila kitu, ukicheza nyumbani utatunzwa ukiipenda asili utakuwa mjasili. Balozi aliongea.

“Sure,”

         "Yes.” Laizer aliingia pale farangani amekwisha mwandaa kuku lost na wingi wa chips kavu ili mgeni na mheshimiwa Balozi ale ashibe ajisikie yupo nyumbani.

“Namwona Mtumi Laizer siku hizi  amekuwa na afya bora zaidi, ananenepa na kupendeza kwa kunawili.” Balozi alimsifu Mtumi Laizer ambaye hakuketi sana pale Sebuleni alitoka nje kumwogesha Umbwa🐕 mdogo anayependwa na Islama.

“Nimchapakazi, Mashine kweli kweli,”

“Teeh teeh teeh,🤣” Balozi aliagua kicheko kikuu.

“Mie ninakonda kwa mawazo mengi juu yako weye Islama kumbe kidume mwenzangu ananenepa na kupendeza,” Balozi alitania. Islama aliagua kicheko kikuu.😂😆

“Kawaida bwana, muhimu kuheshimiu kanuni za fya, kula vyakula bora na kufanya mazoezi ya mara kwa mara au kufanya shughuri chache za nyumbani pamoja na kujipumzisha.”Islama alimjibu Balozi.

“Aright, tuachane na hayo bibie, ungelijua fika kuwa nimefungasha Safari yangu yote hii mguu huu ni wa kwako,  usishangae kuniona nipo Suprisngly” Balozi alichanganya sentensi.

“Nimekuja kuchukua jawabu la mahaba yangu, 🌷🥰 nina wingi wa imani kusema kuwa bibie umenifikiria, mie nipoe na nipoozwe mtima wangu,” Balozi aliendelea kubugia vipande vya chipsi kuku na ile Juisi aipendayo juisi ya Zabibu,

“Oooh!  Hilo bado unalo moyoni Balozi wangu.”

         “Niliweke wapi mpenzi wangu? Sina pa kuliweka zaidi ya moyoni mwako, ujue fika kuwa moyo wangu umetua kwako kama kipepeo,”

“Ooosh!” 😤 Islama akatua pumzi Tabasamu dogo usoni kwake👧

“Nini mbona wapumua kwa nguvu ‘Ooossh!’ Wanitia hofu mwenzio, ujue mie sipendi mizinguo”

“Usijali Balozi lakini mie nataka nikuambie tayari nimekwisha mpenda mtu…… Na yeye amenipenda ajabu.” Islama hakutaka kuuficha ukweli.

“Eeeh! Umesema…….? Umekwisha pendwa tayari au nimesikia vibaya” Balozi aliacha kutafuna vile vipande vya Chips kuku akabaki mdomo wazi anashangaa.🤭

“Ndio Balozi wangu, Moyo ndio unaoanza kupenda, mwili upokea upendo uliopendwa, Bahati ni kitu nasibu kukubali ni heri, uvumilivu una kikomo chake, Pia kila lenye ncha ufikia ukingoni, mie tayari nimo mapenzini nimependa pale nilipopapenda, nadhani na pia nafikiri kuwa pale nilipopapenda napenyewe pamenipenda.” Islama aliongea.

“We Islama, wasema kweli au wanizingua….. Mbona sikuelewi?”

“Ukweli ndio huo na uthibitisho wa hili jambo ninataka nikuambie kuwa Ninao UJAUZITO wa miezi miwili, kwanini nipende pengine tena?”

“Islama!!!!!😱😱😨😷” Balozi alipigwa na butwaa mikono yake ilitetemeka tetemeka, alimanusula glass yenye juisi ya Zabibu imwagike, macho aliyoyatoa nikama vile Mjusi amebanwa mlangoni.

“Tayari umekamata ujauzito mara hii, Ooooh! Ama kweli wanaume wa Maasai Land hawachelewi kuoa, walisema wahenga Ngoja ngoja  utakuta mwana si wako. Sasa umependwa na nani? Na huo ujauzito ulio nao ni nani alie kupatia?” Balozi alihitaji kujua maana amevunjika sana moyo💔 wake kwa yale maneno aliyoyatamka Islama,

“Niliyempenda ni siri yangu, aliyenipenda ni siri yake, yanini kuumwaga mtama mbele ya kuku wengi, siri ya mimi nayeye itabaki kuwa siri milele.”

“Usinifiche Islama  ama je umempenda LAIZER, maana kwa mazuri umtendeayo  sio haba kijiji kizima kinashangaa jinsi anavyo iendesha ile TAX yako ya fahari, kwa sasa amenawili na kupendeza,anaihudumia vizuri familia yake.  Je ni Laizer au…..….?”

“Hiyo ni siri yangu mimi Balozi, siwezi kuropoka na kusema ni Laizer wakati mie binafs najua fika wanaume wako wengi, sio Laizer pekee hata nyumbani England kuna wanaume wananipenda na mie ninawapenda sana.” Islama alijitetea, akijaribu kuuficha ukweli.

“ Mmmh!🤭 “ Balozi aliguna kimoyo  moyo ni mnyonge wa ghafla na ni mwenye huzuni inayokondesha🙁

“Duh! Bibie nitakonda kwa ajili yako mwaka huu”

“Usijali Balozii, maisha kutafuta, endelea kutafuta nawe utapata, hupaswi kufa moyo.” Islama alimjibu Balozi.

###################

  Ikawa hivyo tena, Balozi Ole alimkosa Islama Kuku🐔 wa kizungu, Kuku aliyemtamani ajabu, kuku huyu hajalipenda JOGOO ZEE, Jogoo babu. Ndiposa Kuku wa kizungu amekimbilia kwa vijogoo vijana, any way Balozi Ole aliapa kufanya uchunguzi ili ajue ni mwanaume gani kijana anayemsumbua Kuku wa kizungu tena aliapa iwapo angelikuwa ni Laizer basi atafanya juu chini ili amchongee kwa mkewe ili ndoa yao iingie tufani.  

                        #

Miezi tisa ilipotimu, Islama alijifungua mtoto wa kiume, ni mweusi wa rangi rangi ya kiafrika, hana tofauti na uzuri alionao Laizer. Amekopi kila kitu kutoka kwa babaye Laizer. Furaha ilizidi kuongezeka kwa wale wawili waliopendana sababu mapenzi yao yameleta majibu na matokeo ya majibu. Mtoto akatunzwa na kutunzika.

Miezi saba mingine mbeleni hali ya Balozi Ole kiafya ilizidi kuzorota na kuwa mbaya zaidi, alizidi kukonda kwa sababu ya kukosa kumla kuku wa kizungu, ile anamwona machoni kwake tu lazima augue na kudhoofika, ile anamwona  yule Kuku akifurahi pamoja na mtoto aliyezaa na Laizer wivu na roho mbaya havikukoma kumwandama.

“Why me? Kwanini mimi?” Balozi alijiuliza moyoni mwake.

“Je mimi sio mwanaume…….. hapana mimi ni dume na dume lililokamilika sharti limpende mwanamke. Mimi ndiye niliyeanza kumpenda Islama kwanini Laizer amenipiku na kunishusha cheo? Oooh! No, haiwezekani hata kidogo, Laizer ni Mtumi na Mtumi hawezi kunizidi mimi Mwanasiasa mwenye cheo kikubwa hapa Kijijini.” Balozi aliwaza. Anazidi kukonda na kudhoofika, leo amelala juu ya keka moja kuukuu chakavu halitamaniki yupo nyumbani kwake  ni mwingi wa mawazo na masikitiko, wakeze wawili hawajui nini kinachomsumbua baba watoto, kama ni kula chakula hataki kula, kama ni kunywa maji hataki kunywa, yaani hataki hata kwenda kazini, kutwa kuchwa anashika tama, mawazo yasiyo na kikomo yamemfunika, anawaza kwanini amemkosa kuku? Kwanini hajamla kuku? Kwanini kuku amependwa na Mtumi wakati yeye ni Mwanasiasa, yeye ni mwenye cheo pale kijijini, yeye ndiye aliyempokea Islama nayeye ndiye anayempelekea Islama zawadi nyingi ikiwemo yule mbuzi Beberu mkubwa.

“Mwenda bure sio mkaa bure uenda akaokota kitu,” Balozi alijipa matumaini.

“Wacha niyatibue maji yachafuke, wacha jipu lililoiva lipasuliwe ni bora wote tukose haiwezekani mie niendelee kuugua kidonda cha mapenzi wakati huo huo namwona adui yangu anaendelea kuboreka, afya tele, kitambi kule, bukheri mwenye uzima, Mmmh! Laizer anaendesha Gari wakati mie hata pikipiki siiwezi.  Amemjengea mkewe duka la kijiji wakati mie hata kibanda cha M-pesa sina, mmmh! Ni shidaa.” 

“Lazima niyamwage maji yasizoleke, mapenzi kidudu mtu, sina shida ni bora tuyakose wote, ili moyo wangu uwe na amani, jamani sina amani! Wahenga walisema ‘amani bila ncha ya upanga hiyo sio amani.”Balozi akadamka pale  alipolala akayavaa Malapa yake, Lubega mabegani, Sime kiunoni, fimbo kubwa anayoitumia kuwaswaga ng’ombe aliishika mkononi, hakuwa na haja ya kuwaaga wakeze, moja kwa moja  akatoka pale nyumbani kwake akaelekea nyumbani kwa Mtumi Laizer.

Ilikuwa ni majira ya asubuhi, saa nne muda ambao Laizer alikuwa kwa nyumba ndogo (Islama) anawajibikia kazi zake za kila siku. Balozi Ole alipokelewa vizuri ndani ya  nyumba aliyoijenga Laizer, nyumba nzuri pale Maasai land, tofauti na nyumba nyingi za wanakijiji, nyumba zenye makuti na mbavu za umbwa. Nyumba ya Laizer ilikuwa ni nyumba Bora Sababu Islama aliiboresha kwa tofali na bati pamoja na milango safi. Ndio maana hata ukiiona nyumba ya Balozi Ole mwenyewe utacheka sababu bado ni ile ile ya udongo , ya makuti na ya  mbavu za umbwa, ama kweli bahati imempita Balozi wa watu.

Balozi alipokelewa vizuri ndani ya nyumba aliyojenga Laizer kwa msaada wa Madame Islama, watoto wawili wa Laizer hawakuwepo nyumbani walikuwa malishoni wanalisha mifugo ya baba yao.

“Ndio maana nimekwambieni siri ya mtungi aijuaye kata,” Balozi aliongea kwa mafumbo.

“Bado nashindwa kukuelewa Balozi , kwani mume wangu amfanya kosa gani tena hata uniambie maneno yenye mafumbo?” Swinje mkewe Laizer aliongea.

         "Sikiliza Mama Yoyo, nyie wanawake ni viumbe dhaifu, daima mmekuwa wategemezi mnategemea kila kitu kutoka kwa waume zenu, sijui huu udhaifu wenu ni lini utafikia kikomo? Haupaswi kuwa mama wa nyumbani tu bali pia unapaswa kumlinda mumeo kumchunguza mumeo na pia kumtega mumeo. Ujue ya kwamba dunia ya sasa imefikia kikomo, magonjwa siku hizi ni mengi tena mengi hayo yanatafuna jamii kama Nzige atafunavyo mazao shambani. 🪳 Angalia Mama Yoyo usije ukapukutika wewe na mumeo hatimaye leo na kesho muwaache watoto wenu yatima.” Balozi alichonga kwa hasira.

“ Eeh! Kwa mana hiyo Balozi unamaanisha kuwa mume wangu anachepuka, au? Maana sielewi.”

“Uelewe au usielewe kazi kwako mie uwaga sipendi kesi za kijinga, ili mradi tayari ujumbe nimekugea.” Balozi akaondoka kwa hasira, amemuacha mke wa Laizer mwingi wa maswali yaso na majibu.

“Yallah! Toba, mume wangu jamani bado ni kijana,kwanini Michepuko waingilie ndoa yangu nasema sikubali acheni nifanye juu chini kulizuia Jahazi lisije likazama.” Swinje Mama Yoyo mkewe Laizer aliongea yeye na moyo wake. Japokuwa hamjui huyo amzuzuaye mumewe, lisemwalo lipo kama halipo langojewa, wacha swinje apeleleze peleleze kisha hapo baadaye afanye maamuzi sahihi.

#################



Tukutane kesho

Kizuri tafuna na mwenzio

Karibisha ndugu wajiunge wasap group +255744225388

No comments:

Post a Comment

I promise you

   I PROMISE YOU. (NINAKUAHIDI.) SURA  YA KWANZA. UBAYA WA POMBE. “Umenizingua job, umenizingua kwa muda mrefu sana mpenzi wangu…….kwanini l...