Sehemu ya pili:
Safari ilipamba moto, ilikua ni Safari moja ya Raha na starehe, Safari ya kwenda kujifurahisha nje ya nchi Yao Tanzania Uzuri wa ile Safari wapambe wa Bosi Beni walikua na uhuru wa kuomba, au kulilia kitu chochote walichotamani.
Viva akadeka "Bosi mie nashauri next week tufunge Safari ya South Africa"
Bosi Beni akamjibu Viva "Hapana, next week Nina Safari ya kwenda Namibia kuhudhuria mkutano mkuu wa SADC, Bwana Raisi ameniteua niwe mwakilishi kule.
Mimi akaongea "😋Wacha we usitumegue mkuu tunahitaji kukusindikiza"
Viva alihitaji kujibiwa ombi lake "Lakini Bado sijapewa ufumbuzi wa Safari niliyoichagua 🙃"
Mimi akamkosoa Viva. "Waziri amesema wiki ijayo atakua ana Safari ya kwenda Namibia, Sasa unaforce Nini?🥴"
Bosi akahitimisha ugomvi wa majibizano yaliyoibuka kati ya mimi na Viva."Msifarakane, Sherehe za Noeli na Mwaka mpya zipo karibu, Wacha tupange Safari ya Viva tukale Bata na kuinjoi life huko South Africa."🔥
Viva akatia neno. "Kitu kama icho."🏋️ Furaha ilichomoza moyoni mwao, kusikia wataenda Afrika kusini Kufurahia Christmas na Mwaka mpya. Walijipanga wamchune Bosi Beni, aandae mabunda ya pesa ili wayatumbue na kiyachezea.
Ndivyo alivyo Bosi Beni wapambe wanamuendesha kama mtoto mdogo, jambo lolote like lazima wamg'ate sikio wamdai watakavyo. Wamdai kama vile wanachodai chatoka mikononi mwao. Si wanamjua huyu Bwana mpole kama kondoo😂 akiombwa hatoi kwa choyo, anatoa kwa moyo mkunjufu
Waziri Beni kwake safari ni kitu Cha kawaida amekua akisafiri safari nyingi sana, Ubaya wa Safari zake ni mtumizi mbaya wa pesa za Serikali. Yeye si ni Kiongozi wa Serikali! Wacha azichezee pesa za Serikali atakavyo. Hana shida anazichota hizo pesa atakavyo na ubaya wa kuzichota hizo pesa anazichota too much, anazidisha kipimo haoni kama Kuna mtu wa kumshtua au kumshitukiza kwa sababu pesa zipo mikononi mwake Wacha azichezee atakavyo.
Rose secretary akapaza sauti " Waziri Beni unaonaje sherehe za Noeli tuwepo sisi kama sisi private" Sijui kwanini Rose aliongea wazo hili maana 🌹 yupo hapo kumchuna Waziri Beni.
"Waziri aliachia mguno Kisha akanena " Mmh! Kwanini umewaza hivyo Dear 🌹?"
Rose hakuwa na haraka kujibu, ila Max akamsaidia kujibu: "Rose anataka uwe na furaha zaidi."
Beni akamjibu Max. "Kwani nikiwa na mke wangu siwezi pata furaha?
Max akajibu. " Unajua Bosi Rose anakupenda sana, tena mshukuru Mungu kumpata Mtoto Rose, Mtoto mrembo mdatishaji. Mkeo Keisha choka na kuchakaa, hatamaniki." Kebehi zile zikawafanya Max, Viva, Mimi na Rose waague vicheko vilivyomwambukiza Waziri alijikuta na yeye hoi taabani kwa cheko.
"That's true.Dino alitua neno Kisha akaendelea.
"Waziri unahitaji kutoka out na watoto wazuri hapa town.." Dino akazidisha kauri "Mkeo ameishapitwa na wakati, embu fikiria wewe una miaka 60 mkeo 50 lakini ukipita mitaani watu wanahisi wewe ni mdogo wake.
Viva akapaza sauti 🔊" Mkuu wewe ni Baba lao, Bado kijana unaepaswa kula ujana" Wote wakaagua kicheko🤣😂 kikuu kilichopasua miamba ya sayari.
"Unahitaji KAMPANI ya Mtoto Rose" maneno yale yalimuingia kichwani Waziri, Kila Lecture aliyoambiwa aliikubali .
Ghafla akayakumbuka maneno ya mkewe yalivyomwingia
"Mume wangu punguza Safari za mara kwa marakwa mara ujapozidisha hizo Safari haunipi nafasi ya kuwa na wewe katika familia!"
"Mke wangu Safari hizi za mara kwa mara ni Safari za kikazi, kazi ninayoifanya waijua lengo ni kulinufasisha taifa. Jana nilienda China na kuongea na Raisi wa china kuipa kipaumbele Tanzania ipate mikopo isiyo na riba. Juzi nilikwenda Mexico nikaongea na Waziri mkuu wa Mexico tukaandikiana mikataba ya kiuchumi kesho tena ninategemea kwenda Norway." Beni alijitetea.
"Lakini Mume wangu Safari zote hizo ni wewe tu? Je serikali haiwezi kumchagua mtu mwingine wa kwenda?" Mke wa Waziri aliuliza.
Waziri Beni alibadirika akaongea kwa hasira hadi mkewe alianza kuogopa "Mwanamke mpumbavu wewe, wataka aende nani zaidi ya mimi?"👿👺
Waziri akaongea tena "Mimi ndiye ninayeaminika Serikalini Wacha niende popote pale duniani kulitafutia maendeleo taifa langu, Sipangwingwi"
Mke wa Waziri akaongea kwa woga na kutetemeka " Nimekuelewa Mume wangu lakini kumbuka miaka miwili iliyopita ulilitia hasara taifa kwa maamuzi Yako mabaya ya kwenda kuomba misaada nje ya nchi"
Beni akamkaripia mkewe." Wanikumbusha Nini we mwanamke!?🥴🥺 Yaliyopita si ndwele tuyagage yajayo. Mimi ndiye ninayeijua Siasa sio wewe Mwalimu wa shule ya msingi." Beni alizidi kumkwaza mkewe.
"Kwenye siasa Kuna kupanda na kushuka, kwenye siasa Kuna kuzuka na kutoweka, kwenye siasa Kuna kukumbuka na kusahau. Mimi ndiye mjuzi wa siasa sio wewe."Waziri alijigamba🦾
(Itaendelea sehemu ya tatu.)
No comments:
Post a Comment