KWENYE PENZI MWANAGENZI.
Mimi kwako mwangenzi, ndani ya lako penzi,
Zumbukuku mwanafunzi, mbumbumbu wa ujuzi,
Nijulishe niyahenzi, matamu yatoa chozi,
Unizidishie pumzi, nipate ishi azizi.
Ati mapenzi ni nini? Na yanafaida gani?
Hasara zake ni zipi? Matunda yake ni yapi?
kwanini yapo duniani? Kwanini yapo mbinguni?
Au mapenzi utumishi? Au mapenzi utumwa?
nieleze e kigori ๐ฉ๐ค, sinifiche banati,๐ฉ❤️๐จ
Nipate kujua ukweli, niifurahie bahati,
Kuyauliuza maswali, si ujinga si jeuri,
Gizani natafakari, naomba tuyajadili.
Watu walia mapenzi, je, mapenzi ni kilio?
watu wawaza mapenzi, je, mapenzi mawazio?
Watu wafia mapenzi, je, mapenzi matangio?
Watu watafuta mapenzi, haya mapenzi ufunguo?
Haya mapenzi tamanio, haya mapenzi kusudio,
Dhamiraye marudio, mazoea tarajio,
Mabayaye ufagio, memaye mazalio,
Je, penzi linapofusha? Je, mapenzi yanachosha.
Kwanini wanachinjana, waburundi na wakongo?
Kwanini wanatengana, amani yao kisogo?
Kwanini wafarakana?mapatano ni kinyongo?
Ajabu ya makafara, hawayajuyi mapenzi?
No comments:
Post a Comment