KUKU WA KIZUNGU
Sehemu ya nne
################################
Ni wiki moja sasa tangu Laizer aingie ndani ya nyumba ya Islama kama kawaida Laizer huja asubuhi na mapema, huja kufanya kazi zote za pale nyumbani, kusafisha mazingira, kufua, kupika, au kutumwa hapa na pale, kufanya hiki na kile na hatimaye muda wa jioni Laizer urejea kwa mkewe ni mwingi wa furaha kwa sababu Islama anafanya kazi kubwa ya kumuondolea uzuzu wa kiiafrika na asasa anampeleka kwenye upya wa kizungu.
Embu mtizame leo, Laizer yupo kupika wali kuku kwenye hilo jiko la umeme, sijui linaitwa Oveni๐, mmmh! Sie tusiojua kimomboo (kizungu) mbona tunashida, Laizer yeye alitegemea labda ipo siku angelimpikiia yule Bi. Dada kwenye jiko la mafiga matatu. Embu mwone Laizer akiichezea chezea Remote ya Televisheni Screen, wacha we! Anajifunza mambo mapya ambayo hata hivyo hayajui maishani mwake. Vipi kuhusu matumizi ya Jokofu, pangaboy, na pasi ya umeme, ni mshamba wa matumizi ya hizo zana, lakini uzuri wake, Islama anamfunda Laizer, anafundika.
Upendo wake Islama kwa huyu Handsome, unazidi kadri siku zinavyozidi kusonga mbele, chakula alacho Laizer ni kingi sana na uzuri wa hicho chakula kingi Lazier ufungashiwa kingine ili akampatie mkewe mpenzi Bibie Swinje. Mavazi anayonunuliwa Laizer ni mavazi mazuri na tena ni yabei gharama, kwa ufupi Laizer anapendwa tena anapendwa pendo lakupendeka yeye binafsi anafurahia kupendwa na mzungu mwenye roho safi.
Siku hazigandi Jua uchomoza jua uzama siku mpya uzaliwa Sifa ya Mwanagenzi (mwanafunzi) kujifunza tena kujifunza yale mapya na kuyakumbuka yale ya zamani Laizer alijifunza na katika kujifunza kwake alikuwaa ni mtiifu kwa yale aliyojifunza.
“ Laizer,” islama aliita.
“ Year Madame,” Laizer aliitikia.
“Chukua Gari kimbiza ufike sokoni,” Laizer Keisha zoeshwa kuiendesha Gari.
“Ok, Madame,” Laizer anafanya hima hima kutimiza maagizo ya bosi wake.
“Laizer,”Islama anaita,
“Year Madame,”Laizer anaitikia.
“Mchukue yule Kuku mkaange kwenye Oven,” Islama anamwagiza Mtumi wake.
“Ok Madame,” Laizer anachangamkia shuhuli.
“Laizer,”Islama anaita.
“Year Madame,”Laizer anaitika kwa utiifu.
“Zitwae nguo zangu chafu uzifue kwa kutumia ile Mashine ya kufulia nguo ukimaliza uzipige Pasi.”Laizer anafanya kama alivyo agizwa. Walah! Maisha ndani ya nyumba ya Islama yamekuwa Simple kweli kweli, muda wote Laizer anatumia Mashine za utandawazi, japo hakuzoea lakini tumwache ajizoeze kwa nguvu na kwa akili zake zote na uzuri wa Islama anayazidisha mapendo kwa huyu Mtumi Maasai.
#############################
Kuna ili jambo moja lina muumiza Islama bado anajiona upweke, fahari ya yeye kuzunguka hapa na pale ndani ya Tanzania haimtoshi, raha na furaha ya kupata vyote avitakavyo haimtoshi bado anajiona mpweke, nyakati za usiku, sababu asubuhi na mchana yupo pamoja na Mtumi wake Handsome wake,Laizer .
Kutokana na upweke mwingi kumwandama Islama hujikuta anajipooza kwa kuikumbatia moja ya picha kubwa aliyopiga pamoja na Laizer, wakati wote Laizer umwingia akilini mwake, wakati wote Islama ufikiria jinsi gani aanze kumwingiza Laizer ndani ya akili zake. Subira pekee humtosha, hana haraka haraka sababu anajua fika kuwa haraka haraka haina Baraka, pole pole ndio mwendo, tunda bora uchumwa mtini, Haliokotwi kwenye Vumbi.
Mwezi mmoja kuisha Balozi alimtembelea Islama, amejaa tele haachi kuja na zawadi nyingi kwa ajili ya mgeni wake, Islama. Leo kamletea buyu limejaa maziwa ya mgando (mtindi), kuna buyu limejaa asali mbichi, kuna Mayai ya mbuni, shangaa kibao za kuvaa kiunoni, kamlete malapa ya kimaasai (Makatambuga) pamoja na vikorokoro vingine kibao ili tu amfurahishe yule mgeni.
“Matumaini yangu Laizer anawajibika ipasavyo.” Balozi Ole aliongea, wameketi sebuleni yeye pamoja na Islama wanapiga story mbili tatu kwa furaha, “ Nakwambia sio haba, kijana ni mchapa kazi pia ana uelewa wa hali ya juu,” Islama alimwaga sifa nyingi kwa ajili ya Laizer “Nilisema mimi hapa mwenyewe umefika na mwenyewe utapapenda sio bure, hautatamani kurejea ulaya, hapa kuna amani tele furaha na utulivu kibao, wamaasai wana umoja upendo na ushirikiano.” Balozi alitia neno.
“Mie mwenyewe nimejione kwa macho, sitegemei kusikia nijaporudi nyumbani Europe sintakoma kuisifia Tanzani kwamba ni Nchi moja bora Duniani, waweza kuishi miaka elfu bila kufa kwa sababu ya amani upendo na utuliuvu.” Islama alitania.
Teeh teeh teeh. Balozi alicheka. “ Ndio maana DOCTOR LEAKEY na mkewe MARRY waligundua fuvu la mtu wa kwanza kuishi Duniani alipatikana Tanzania, tizama ni jambo jema lenye Baraka tele, Maisha yapo Tanzania, hapa ndio Paradise ndogo, hapa ndio penye kisiwa cha uzima na umilele,”
Leo Balozi alikuwa ni muongeaji sana, sijui kwanini amefurahi namna hiyo au ndio anazitanguliza swagga?Anaipenda sana hiyo Juisi ya Zabibu, mara chache sana utamwona akitafuna tafuna ugoro na kupiga chafya kama mwendawazimu.
“Upo kimya sana mpenzi,” Balozi alianza kumwaga Swagga.
“ Leo ni leo msema kesho ni muongo, nimeona bora nije nichukue jibu la moyo wako, kama ujuavyo tena nimekupenda pendo la hapa moyoni. Balozi aliugusa moyo wake amejaa tabasamu yale mapengo yake juu ya ufizi yanaonekana yapo wazi .
“Tangu siku yangu ya kwanza nilipokuona moyo wangu ulikufa ganzi, mikono yangu ikatetemeka, magoti yaliishiwa nguvu za kutembea, mapigo ya moyo yalinienda kasi na kusi, nilikutamani sana ila kwa sababu nilikuheshimu sikuhitaji kufanya pupa, kama waswahili wanavyosema, haraka haraka upokonya Baraka, nikawa kimya muda wote japo nilikuomba offa ya kuwa pamoja na wewe pia nilihitaji uwe huru na wazi kunieleza lini upo free mie mahabuba wako nije niingie moyoni mwako tuufungue ukurasa mpya wa mahaba.”
Leo balozi aliona wacha ayanene yale yatokayo moyoni mwake anamtamani sana huyu kuku wa kizungu, hajawahi kumla kuku wa kizungu maishani mwake mwote, amechoka kula kuku wa kienyeji, basi acheni ajaribu bahati yake.
.....
“Aaaah, aaah, aaaah!” Islama alicheka sana, maongezi yao yakapamba moto.
“Balozi Bwana, mie najiona ningali bado mgeni ndani ya Afrika, tena zaidi ya hilo ningali bado ninajifunza kuhusu mazingira ya Kiafrika, wacha nikwambie kwa kifupi, mie bado sijafikiria. Kwa hiyo nipe muda mrefu kidogo nikikaa vizuri nitakupa jibu la moyo wangu.” Islama aliongea kumbe hajamtamani huyu Balozi mtu mzima sawa sawa na baba yake wa kumzaa.
“Ah! Mpenzi usininyime mapenzi, moyo wangu unawashwa kwa sababu ya mapenzi yako, nahitaji uingie moyoni mwangu unikune ili nipoe na kupona kabisa.” Balozi alichombeza ingawaje yeye binafsi anajijua fika kuwa hanaga uhusiano wowote ule wa kimapenzi pamoja na Islama
“Usijali Balozi, mie siko hivyo, mie ni mtoto wa kizungu kawida sie wazungu sio wachoyo wa mapenzi, ninayapenda sana mapenzi, natambua na pia nafahamu kuwa mapenzi ni uhai kukunyima siwezi, nipe muda mrefu kidogo nitakupatia jibu la moyo wangu,” Islama alimzingua Balozi.
“That’s Beautiful.” Balozi alitabasamu tabasamu pana kama mwanga wa Jua, moyoni mwake anacheka cheka kwa mapozi.
“ Lini nitegemee my Love,” “I will tell you , Worry it off. Usijali” Islama hakumjibu ipasavyo yule Balozi.
“I’m a man, mimi ni mwanaume, mwanaume wa kiafrika anapaswa kuwa msubirivu kwa mwanamke. Sawa bibie, ninayaheshimu mawazo yako, mie nitasubiria hadi pale utakapofanya maamuzi yako mpenzi.” Balozi aliongea usoni tabasamu lakini kumbe moyoni mnyonge wakati wote ana waza kumpata kuku wa kizungu, amchinje kwa hasira, amtupie ndani ya maji ya moto, amnyonyoe manyoya yote, ambanike juu ya moto, akiisha kuiva lazima amle mzima mzima bila kubakisha mifupa, maana yeye binafsi kasika kuwa kuku wa kizungu walivyo watamu, asikwambie binadamu, ngozi laini mifupa laini na uzuri wa yule kuku mwenye ENGLISH FIGURE bado ni MODO
. ############################
“Nataka tujaribu,” Islama alimwambia Laizer Mtumi Maasai. Wameketi kwenye chumba maalumu kilichotengwa wao kupumzika wajapochoka kwa uchovu wa kazi za hapa na pale.
“Sijawahi Madame,” Laizer alimwambia Islama katikati yao kuna chupa kibao zenye vilevi vya kizungu vimeandikwaJOHN WALKER, QUUEN ELIZABETH,TEACHER, SHIRAZY, HANSON CHOICE, K-VANT na vinginevyo kibao vikali balaa.
“Usiogope leo nataka ujaribu sawa,” Islama akaingiza mkono wake wa kuume kwenye mkoba wake uliokuwa pembeni ya siti aliyoketi akatoa paketi moja la sigara pamoja na kibiriti chake , kibiriti cha gesi.
“umewahi vuta.”Islama tayari kaichomoa pisi ya sigareti kaiwasha na kuvuta funda moja refu lililosambaaa ndani ya kile chumba cha kupumzikia (sitting room)
“No sijawahi.”
"Ok. Here you go, take this.” Islama alimpatia Laizer ile Pisi ya Sigareti, Laizer kaipokea.
“Vuta mafunda mawili matatu hifadhi mdomoni mwako, kisha nitakuelekeza….” Laizer akaizamisha mdomoni ile pisi ya Sigareti akaivuta funda moja kubwa akisubiri maelekezo mengine kutoka kwa Boss wake.
“ Utoe moshi wa Sigareti Puani kama mimi nilivyotoa funda la kwanza.” Laizer alibaki akipepesa pepesa macho yake hata asijue anapaswa kufanya nini, dakika tatu kupita bado tu Laizer hakujua anapaswa kufanya nin.
Itaendelea kesho.
Comment please.and put your Like๐๐
No comments:
Post a Comment