Monday, September 16, 2024

KUKU WA KIZUNGU ๐Ÿ“ Sehemu ya tano

 


KUKU WA KIZUNGUu


Sehemu ya tano

Tulipoishia

        "Here you go, take this.” Islama alimpatia Laizer ile Pisi ya Sigareti, Laizer kaipokea.

“Vuta mafunda mawili matatu hifadhi mdomoni mwako, kisha nitakuelekeza….” Laizer akaizamisha mdomoni ile pisi ya Sigareti akaivuta funda moja kubwa akisubiri maelekezo mengine kutoka kwa boss wake.

“Utoe moshi wa Sigareti Puani kama mimi nilivyotoa funda la kwanza.” Laizer alibaki akipepesa pepesa macho yake hata asijue anapaswa kufanya nini, dakika tatu kupita bado tu Laizer hakujua anapaswa kufanya nini.

Tuendelee hapa๐Ÿ‘‡๐Ÿ’ž

    “Fanya hivyo Now” Laizer hakujua anapaswa kufanyanini, akalimeza lile funda. 'Koh! Koh! Oh!' Sauti ya makohozi ya Laizer ilimuacha hoi Islama Laizer aliona aibu kwa kile kitendo cha kushindwa kwake.

“Oh! No, I can’t  do it againa Madame,” Laizer alimrudisha Islama ile pisi ya sigareti ya kizungu.

Aaah aah aah๐Ÿคฃ๐Ÿคฃ” I slama alicheka tena kwa mapozi, uzuri wake ulionekana wazi, meno yake mawili ya juu marefu Yale menu ya kizungu yalionekana, nywele zake ndefu za kizungu zilimpendeza kwa kifupi English figure amejaliwa uzuri wa kimalaika.

“Mwanzo mgumu eeh!? Yataka moyo mwenyewe utapenda ukiisha kuzoea.”  Islama alimtuliza Laizer akaichukua ile Pisi ya Sigareti akaivuta kwa mapozi zaidi akiujaza moshi wa ile sigareti mdomoni mwake, akiutoa ule moshi kupitia chemba za pua yake. Moshi ule ulisambaa  pale sitting room na uzuri wa sigara  za kizungu moshi wake unanukia marashi ya Pemba na Unguja.

“It’s simple,” Islama aliongea.

“Je tuendele?” Alimuuliza Laizer.

“Kufanya nini?”Laizer alimuuliza Madame

  “kushindana,”

“No, Madame, I say no!” Laizer aliongea kwa woga, ameaibishwa na ile sigareti ya kizungu, yamkini kaanza kuiogopa.

'Teeh teeh teeh๐Ÿ˜น’ Islama alicheka kizungu.

“We have another new precious game mbele yetu,” Islama aliongea.  Akizitazama Bottle za vilevii vikali, vilivyosambaa pale  juu ya meza. Akavifungua vifuniko (vizibo) akamimina   kwenye glass  moja nzuri yenye mguu mmoja, akaigugumia ile John walker na baada ya ya kufanya hivyo akamsogelea Laizer pale alipoketi, akaupitisha mkono wake wa mashoto kunako mabega ya Lazier mapenzi yalimjaa Islama kila dakika kila sekunde anamtamani kijana wa kimaasai. Islama akatwaa ile glass yenye kilevi akamnywesha Laizer.

“Meza tafadhari,” Laizer akajaribu kuimeza.

“Aaaahsh!” Uchungu na ugwadu ulimwandama zaidi mdomoni mwake.

“How do you feel about it?” Islama alimtazama Laizer, alimtazama yale macho mazuri yampendezayo yeye, macho yenye mboni Nyeusi, wakati Islama ana macho yenye mboni za Blue Bahari.

“Uchungu……. Ni kali sana,” Laizer alimjibu Islama.

“Sio tamu,”

“Yes, Madame,”Laizer alilikunja paji la uso wake, kuashiria kuwa bado anahisi uchungu mkali wa kilevi cha kizungu.

“Ninataka tunywe wote tufanye kujaribu tena na tena,” Islama alimshawishi Laizer, Lazier hakuwa na pingamizi, mkono wa Islama ukatua kiunoni kwake Laizer, kiuno ambacho kilikuwa wazi kimefunikwa kwa Lubega, akampapasa kimahaba. Laizer alikuwa kama NDONDOCHA LA KIMAASAI hajui ae wala bae.

“Hivi Lazier nikuulize swali,” Islama aliongea angali anampapasa papasa  Laizer Kifua chake kikubwa, angali anaupitisha pitisha mkono wake mlaini mweupe peeeeee kwenye kiuno cha Laizer.

“Uliza tu Madame,”

“Kwanini hauna hisia na mimi?” Laizer hakulijibu lile swali kwa pupa bali alimuuliza Islama.

“Hisia gani Madame?”

“Laizer, wewe ni mwanaume umeoa tayari, una mke na mtoto, usijifanye haunielewi nielewe tafadhai.” Leo Islama alidhamiria kuyatoa yale yote ya moyoni mwake, amevumilia sana, mwezi mzima wa kuishi na Laizer haukua kidogo, alitamani yule Mmaasai amtongoze lakini mmmh! ‘Mume wa mtu sumu’ walisema Wamaasai.

“Nakuelewa Madame,”

“Haunielewi Laizer,”Safari hii Islama akabadilisha sauti, kutoka ile ya kawaida sasa akaanza kuongea ile ya kimahaba niue, mahaba nipumzishe, mahaba nipende,  mahaba nakutamani, mahaba nikuibe, mahaba, nikupeleke Ulaya. Lakini akumbuke walisema Wamaasai  'cha mtu mavi.’

     B“Je unanielewa nini?” Laizer hakuweza kujibu lile swali.Islama  akakitwaa kidole chake kimoja mkononi, akakiweka nje ya midomo ya Laizer, akafanya kukitembeza kwa mtindo wa kuupapasa mdomo wa Laizer.

“Ni hivi Laizer, ninaomba unielewe, mie ninakupenda pendo la kupendeka, pendo langu pendo la dhati,naomba unielewe. Upweke nilionao unaniudhi na pia unanichosha, ninahitaji kuwa karibu karibu na wewe. Sijali kama umekwisha Oa au la! Mie nimekupenda,  nielewe tafadhali.” 

Islama hakuwa na jinsi, leo aliona bora kuyavulia maji nguo na tena alijipanga kuyaoga.

“Mapenzi uanzia moyoni, mie nimetokea kukupenda wewe, sijali hata kama wewe ni mali ya mtu, ninachoomba tuufungue ukurasa mpya wa kupendana, ukinipenda kama nilivyo kupenda nitazidi kukupenda tena tutapenda ‘More than love’ zaidi ya upendo.

“Madame,”

“No, no, no, no,no, usiniite Madame. Kuanzia leo ninaomba uniite, majina mazuri ninayoyapenda ni kama vile: Love, Sweet Love, Mpenzi Hamour, My  quuen, My Dear na  majina mengine matamu yenye mahaba. Nielewe Sweet Laizer, hakuna mwingine ambaye  atatutibua.” Islama  alimwanga Sera zake Moyoni alijisemea, 'Huyu ndege simuachi, kufa kupona lazima nimteke.'

“Nitakupenda, amini usiamini hata sasa ninakupenda kuliko kitu chochote kile duniani, wewe haujajua kuhusu hilo, naomba unielewe, itakuwa ni siri yetu, asijue mtu wala asitwingilie mtu. Wawili tukipendana mapenzi moto moto ni yetu, tena mapenzi yetu Mubashallah!” Islama akaendelea kumpapasa Laizer akimtia hamasa ya kufanya mahaba, akachukua  kile klevi  kikali ch kizungu akamnywesha Laizer, taaratibu, taaratibu na yeye akanywa, dakika ziliendelea kukatika, mahaba yalimpanda  English figure, akamsogelea Laizer, akajipweteka kiunoni kwake, (kwenye kiuno cha Laizer) akaketi juu ya kiuno cha yule mwanaume Mashine, akamsogelea usoni wakatazamana, wawili waliendelea kupapasana, maana pombe ilianza kitibua bichwa vyao.

Islama akautwaa mdomo wake, ulimi nje nje, akaupitisha kwenye mdomo wa Laizer, jambo geni sana kwa Lazier, hajawahi pewa ulimi, ndivyo walivyo wamaasai kutoa Ulimi mabahiri kweli. Basi wapenzi wasomaji, mambo kunoga, mate kubadirishana, hisia na hisi, joto na pumzi, presha sio presha, mmmh!  Watoto wasisome sehemu hii, makubwa jamani!      

                ####################lll#######

Mapenzi kunoga, mapenzi kunogela, ndio hayo tena, mapenzi kati ya Islama na mtumishi wake Laizer yakanoga nakunogela. Ni miezi miwili sasa wanayaendeleza matamu yao kwa siri kubwa mno. Nakwambieni jinsi mwanamke wa kizungu anavyompagawisha Laizer kwa zile Style za sita kwa sita, haki! Mapenzi anayewaza na uzuri wa kuyaweza Laizer anamwaga chozi akijilaumu kwanini alizubaa?  kwanini alichelewa kumkimbiza kuku wa kizungu? Kwanini alikuwa Ndondocha wa kimaasai? Mmh! Mzungu anavyojua kupenda na huduma zote anatoa, simchezo! Kapenda boga, kapenda na ua lake, hakamatiki wala hashikiki, kaoza kama lote, kaoza kwa huyu kijana wa kimaasai kaoza na kunuka kwa huyu Mtumi wake, kaziba masiko yake asitake kusikia wala kuambiwa chochote kile juu ya huyu Shamba boy wake, na uzuri wa Mtumi (Mtumishi) huyu , mapenzi anayatoa kila siku hadi Islama najisemea moyoni “NABAKI AFRIKA”

Siri pekee ndiyo inayoyadumisha mapenzi yao, asijue mtu yeyote yule, asijue BaloziOle wala asijue Mkewe Laizer, Siri juu ya Siri. Yamkini sasa upweke Ushampungua Islama, amekuwa akicheka cheka kwa furaha, muda wote yupo karibu na Mtumi wake asitake kumwona Mtumi wake akifanya kazi nzito yupo radhi kujitolea apate kumsaidia. Angalieni jamani mapenzi haya, kweli mahaba nichanganye, mahaba nitie presha, mahaba  nife na nizikwe pamoja na wewe.

 Islama kamuongeza Laizer mshahara, kamuongeza mara tatu ya ule anaompaga kila mwezi, chakula ampacho ni kingi tena kingine kinabaki anampelekea mkewe na mwanae. mavazi anayo mnunulia ni mavazi mapya tena uzuri wa hayo mavazi anaagiza kutoka England, kweli Islama kaoza kwa huyu Mwanaume aliye uteka moyo wake.

.............๐Ÿ’ž

Ni miezi mitatu sasa tangu Islama ameingia ndani ya kijiji cha Maasai Land Balozi Ole bado anatamani kumla kuku wa Kizungu ndo maana na leo tena Kafungasha Safari yake, kabisha Hodi lango la Islama, kafunguliwa na Laizer, Balozi kajaa tele,  Hapunguki Zawadi za kumletea Islama, ndio maana leo kamletea, Mbuzi BEBERU mzima mkubwa haswa, zawadi ya Islama.  Japokuwa kapungua Afya yake, mmh! Ana nini? Tunashangaa, embu ngoja tumsome:


Tukutane kesho sehemu ya sita.

Wakaribishe rafiki zako kuisoma.

No comments:

Post a Comment

ZEE LA ZAMANI

  SEHEMU YA KWANZA. HOTELINI Ndani ya Hoteli Paradiso katikati ya Jiji la Mzizima (Dar es salaam) ZEE LAZAMANI akiwa na Mwanagenzi wake JAN...