Monday, September 16, 2024

BABA NYERERE


 


1


Tukiwa chini mkoloni, siku zile tukatawaliwa,

Akatunyonya nchini, sie kunyanyapaliwa,

Tuligandamizwa chini, mapenzi yalipokonywa.

2

MAPENZI tulipokonywa, tukawa wake watumwa,

Tulifanywa kusukumwa, TENA tulilazimishwa,

Yale alopendezewa, mabavu yakatumiwa.

3

MAPENZI yalilazimishwa, MAPENZI yalitumikishwa,

MAPENZI yalidharauliwa, MAPENZI yalidhurumiwa,

MAPENZI yaliteswa, MAPENZI yalinyonywa.

4

MPENZI BABA NYERERE, mwenye WINGI wa MAPENZI

Akaja kutupigania, akaja kituokoa,

Sasa twajivunia, kuwa ametukomboa,

5

Ni MAPENZI yake Mola, sisi kutuweka huru,

MAPENZI tuliyoporwa Sasa yamejaa nuru,

Twaishi Kwa kusifiwa, sababu umefauru,


6,Tulikua masikini, masikini wa MAPENZI,

Tulitekwa mashakani, MAPENZI yalitumainzi,

Likua elimu duni, elimu ya mapenzi,


7, Akaja baba NYERERE, akaja kutuinua

Akaja baba nyerere, akaja kutuinua,

Akaja baba nyerere, akaja tuunganisha,


8Leo hii Tanzania na Dunia Kwa ujimla,

MAPENZI twafurahia, chereko shamra-mra,

Maumivu umefagia, MPENZI BABA NYERERE 


9 Baba Mola akulaze, huko kwema Peponi,

Ili tuje tukujuze, amani duniani,

Huko uliko tutangaze, MAPENZI YAKO mema.






No comments:

Post a Comment

ZEE LA ZAMANI

  SEHEMU YA KWANZA. HOTELINI Ndani ya Hoteli Paradiso katikati ya Jiji la Mzizima (Dar es salaam) ZEE LAZAMANI akiwa na Mwanagenzi wake JAN...