Saturday, September 14, 2024

WAMEZIDI Sehemu ya 06

 


WAMEZIDI

Sehemu ya sita


Kuondoka kwa mke wa Waziri Beni kuliambatana na kuingia kwa Secretary Rose ndani ya nyumba ya Waziri Beni. Rose kwa sasa akawa ni mke mpya wa WazirI Beni, Waziri wa Fedha ndani ya nchi ya Tanzania. Japo kwa Siri na kwa kificho Rose alitembea pamoja na Max wakipanga mipango na mikakati ya kumchuna yule Buzi anayechunika.

        “Keisha nielewa,” Rose alimwambia Max, siku moja wapo Hotelini wanapata mlo wa jioni. Rose amemuaga Waziri Beni kuwa anakwenda Mwananyamala kuwasalimia wazazi wake kumbe hana jipya, yupo ndani ya Serena Hoteli anakula Bata pamoja na Mpenzi wake Max.

          “Wacha we! Tayari umekwisha mregeza.”  Max aliongea akaligugumia funda moja la Bia.

            “Mie tena nishindwe? Nishindweje kwa mfano? Maneno mawili matatu ya mahaba na mabembelezo yashamtia ndege tunduni.” Rose alichekelea.

            “Waoo! Wewe ni mwanamke bora duniani.” Max alimwagia sifa Rose

            “Tena ni jasiri na shupavu.” Rose  aligamba. 

             “Hivyo basi?” Max aliuliza.

            “Ndo’ hivyo tena tushakuwa matajiri, wacha tumsubirie yule Boya aende Bank akazichote hizo Billion mbili kwisha kutupatia tu tayari tutakuwa matajiri.” Rose aliongea.

             “Cha mlevi kiliwe na mgema.” Max alichombeza.

            “Izidi kuwa siri au sio.” Rose alisistiza.

              “Nani ajuaye zaidi ya mimi na wewe? Si Viva si Mimi si Joe wala Dino ajuaye kuhusu huu mpango wetu, huu ni mpango wetu na mpango wetu ukiisha  ‘Hit’ tunaihama Dunia.” Rose aliongea wawili wale wakaendelea kunywa kwa mapozi moto moto.

                             #####################

      Sio kweli kusema ati Bi. Mkubwa mke wa Waziri Beni alifunga Safari na kuelekea Kijijini. Wala hakuelekea Kijijini alichofanya yeye ni kujichimbia ndani ya nyumba yake yeye mwenyewe aliyoijenga huko Mbezi Beach, ameijenga hiyo Nyumba miaka kumi iliyopita, asijue mtu kama amejenga Nyumba ni siri ya yeye na wanawe watatu. Mumewe hajui kuhusu hilo sababu mume mwenyewe ni  Mume asiye na maarifa. Mume huyu ni tegemezi tena ni mtegemea cha nduguye afe masikini, hataki kujenga nyumba yake mwenyewe. Anaishi ndani ya Nyumba aliyopewa na Serikali, Miaka nenda miaka rudi anategemea ati akiisha kustaafu Uwaziri wake wacha ajijengee Nyumba yake safi kwa pesa za Serikali.

              Mara baaada ya mke wa Waziri kujipweteka ndani ya Nyumba yake  huko Mbezi Beach, Roho yake haikuridhika alihitaji kumchunguza mumewe, alihitaji kujua sababu ya mumewe kumlazimisha ati aende kijijini kwao akapumzike pumziko la Long time hadi pale Waziri  Beni atakapotoa neno la kuruhusu Mkewe arejee Nyumbani.

            Basi ikawa hivyo tena mke wa Waziri akaanza kumchunguza mume, kumperuzi na kumtizama kwa jicho la wizi ili ajue kunanini huko nyumbani kwake? Uzuri wa yule Mwalimu alikuja kugundua kuwa kumbe yote hayo yanasababishwa na Mumewe kutekwa kimapenzi na huyo Secretary wake aitwaye Rose. Hapo ndipo mke wa  Waziri alihitaji kujua mwisho wa ubaya aibu.

               “Leo ameyasikia vizuri yale maongezi ambayo Max pamoja na Rose wameyaongea ndani ya Serena Hoteli. Anamfuatilia sana huyu Rose pasina Rose kujua kuhusu hilo, mbona hata hili dili la Bilioni mbili Bi. Mkubwa tayari Keisha linyaka na sasa anataka kulitumbua.

"""""""""""''____

         “Unajua mie nina mimba?” Rose aliongea.

           “Oh! Kweli !?” Max alitoa mshangao macho pima kidogo glasi aliyoikamata idondoke chini  paaaaa

            “Yes, mbona umeshangaa hivyo Bebi?” Rose alimuuliza Max ingawaje moyoni Rose yupo njia panda hajui hiyo mimba ni ya nani kati ya Max na Waziri Beni amejikuta anene tu pasina kutarajia.     
                                          
             “Vizuri basi tutarajie kuwa na Malaika wetu.” Max aliongea kwa kifupi Moyoni hana imani kama huo ujauzito ni wa yeye au ni wa mume mwenzie Waziri Beni.

            'Mmmh! Tungoje, labda ndio hivyo tena nitauziwa Mbuzi kwenye gunia.' Max aliwaza, anasubiri hicho kitoto kitakacho zaliwa, moja kwa moja kikiisha kuzaliwa ni lazima kipimwe DNA ili kuangalia uthibitisho iwapo hicho kitoto ni cha kwake Max au la! Maana hapa  Mjini ni shidaa!  Utafiti umefanyika  watafiti wanasema asilimia 44 ya wanawake wenye watoto watoto hao sio watoto waliozaa na waume zao, bali watoto hao ni kutokana na Michepuko, mahawara na wapenda starehe za haraka haraka. Max alitia Shaka

(Tukutane sehemu ya Saba)

No comments:

Post a Comment

I promise you

   I PROMISE YOU. (NINAKUAHIDI.) SURA  YA KWANZA. UBAYA WA POMBE. “Umenizingua job, umenizingua kwa muda mrefu sana mpenzi wangu…….kwanini l...