Tuesday, September 17, 2024

LOVE AGAIN LOVE ๐Ÿ’

 Mapenzi utamaduni.




Nayo mapenzi huliwa, chakula bora ni dawa,


Nayo mapenzi uvaliwa, mavazi yano heshimiwa,


Mapenzi uchezewa, ngoma zinazosisimua,


Mapenzi yanatamka Lugha bora za dunia.




 

Mapenzi utungiwa nyimbo bora Mashairi,


Mapenzi udaliziwa, Maua yenye Hariri,


Mapenzi ushonewa, vitambaa vya Johari,


Mapenzi upambiwa, vito vilivyo saburi.


 



Mapenzi tamu zabibu, ni dawa ilo ajabu,


Uungwana ustarabu, siwepo wa kuharibu,


Hadithi zao mababu,thamani yake dhahabu,


Ngoma za taratibu, asili yake tarabu.







No comments:

Post a Comment

 love is all Given and found,๐ŸŒน It's all around,๐Ÿฅฐ It's hard to tell about,๐Ÿ˜ Easy to show,๐Ÿคฉ One sure thing when you feel it You kn...