MBOSSO
SEHEMU YA PILI.
“Kamata mwizi huyo……. kamata hilo…… kamata.” Zilikuwa ni sauti za Wananchi wenye hasira wakiitana kila pande ya mji wa Kariakoo ili wamtie kibindoni mwizi aliyemkwapua pesa mkobani Mwanamama mmoja hivi mnene kiasi, mwenye pesa zake.
“Amekimbilia wapi jamani?” Wananchi wenye hasira walipiga kelele.
“Kaenda huku, tafuta huyo……… kapita kichochoro hiki.” Wananchi walizidi kumtafuta Mbosso aliyekwisha pita mtaa wa Muhenza, naye akajichomeka ndani ya mtaa wa Karume akipita ile barabara ya Uhuru ili aingie kwenye vichochoro vilivyo hapo Karume karibu karibu na kiwanda cha Bia (TBL). Haikuwa rahisi kumkamata sababu Mbosso aliwapiga chenga na kuingia kwenye kundi la watu wengi waliokuwa bize pale soko la Karume akajichanganya changanya na kutoweka kimiujiza.
“Yallah! Toba jamani mwe! Mkoba wangu una million mbili, saa na mikufu yangu ya Dhahabu, simu yangu Samsung Touch screen, nguo zangu nzuri za bei gharama pamoja na vikorokoro vyangu vimeenda.” Alilia yule mama aliyeibiwa na Mbosso.
“Pole sana mama, ipo siku tutakuja kulikamata hilo jizi, dawa yake ndogo, siku za mwizi ni harobaini." Wale waliomsaidia yule mama aliyeibiwa walimtia moyo. Ingawaje walijawa na wivu pamoja na tamaa waliposikia wingi wa fedha zilizoibiwa, vidani pamoja na vikorokoro mbali mbali vilivyoibiwa.
****
“Eeeh! Mpenzi, mbona hivyo? Mbona unaonekana umekimbia sana, umechoka, mwili wako wote umejaa jasho jingi ajabu?” Diva alimuuliza Mbosso. Mbosso macho yalimtoka kumwona Diva amekuja Geto kwake maeneo ya Kigogo ya Mburahati, hata asijue amefuata nini mrembo yule? Hata asijue kwamba mwenzie amebanwa na mapenzi, anampenda ndio maana wakati wote yupo karibu karibu akimfuatilia ili ayapunguze mawazo yanayomuandama juu ya mapenzi.
“Mbona hupo nje?” Mbosso alimuuliza Diva hata asikumbuke kwamba lango la Geto lake lishafungwa na mfungaji si mwingine bali ni yeye mwenyewe Mbosso.
“Fungua mlango basi,” Diva aliongea kimahaba zaidi. Mbosso aliyekuwa hoi kwa kukimbia akiogopa kukamatwa na wale wananchi wenye hasira, wale wananchi wasiopenda uovu ule uitwao wizi. Aliufungua mlango, tena aliufungua kwa kuurudisha tu nao ukafunguka, mandhari machafu ya kile kijumba kilichoezekwa dari yenye mbavu za Umbwa yalionekana. Chumba cha Mbosso kilikuwa na vitu vingi vya zamani, hapakuwa na mali yenye ubora na uthamani.
Kitanda kikuukuu chenye godoro kuukuu pamoja na chupa tupu, chupa ambazo Mbosso alizitumia kujifurahisha kwa ulevi wake, ulevi wa pombe haramu, haramu ya gongo. Vipisi kibao vya Bangi na sigara, sindano kibao za kudungia madawa ya kulevya, hivyo ndivyo vitu ambavyo kwake Mbosso aliviona ni vyenye thamani kubwa yaani kwa kifupi Mbosso hakuwa na future, yote aliyotenda kwake ilikuwa ni starehe, mambo ya kupita machoni.
“Nieleze mpenzi, niambie kilichokufanya ulowe jasho, ajabu mkononi mwako umeshikilia koba la Mwanamke.” Diva alimuongelesha Mbosso ambaye mara baada ya kufika chumbani kwake alijibwaga kitandani kwa uchovu aliokuwa nao.
“Aaah! Kazi za Wanaume bwana ni nzito.” Njemba alimwambia Diva.
“Najua ila niweke wazi huu mkoba ni wa nani na kwanini upo mikononi mwako?" Diva alimuuliza Mbosso ambaye hata hivyo hakulijibu lile swali la Diva. Alimuacha Diva anapekuwa pekuwa ndani ya ule mkoba, alimuacha Diva anatoa zile pesa mingi, vitambulisho vya Benki, cheni za Dhahabu pamoja na nguo mpya za mwanamke, ajabu mbele ya macho ya Diva zilikuwa ni chupi za mwanamke, Diva akashangaa kidogo.
“Nini hiki?” Diva aliingiwa na shauku ya kutaka kujua.
“Usijali mpenzi, nitakwambia.” Mbosso aliongea, huku ameketi juu ya kitanda chake kichakavu kilichojaa wadudu wapendao kufyonza damu, kunguni, chawa na viroboto.
“Nimeiba vitu hivi vyote.” Mbosso aliongea kwa kujiamini. Diva alimtizama sana Mbosso wake machozi yakamlenga, kisha akaongea huku akiendela kumtizama Mbosso.
“Ninakupenda, lakini kwanini unanifanyia hivyo?”
“Nimezoea mpenzi, siwezi kuacha tabia yangu.” Mbosso alijibu.
“Unaweza mpenzi, tena unaweza pale tu utakapokuwa karibu karibu na mimi. Mimi nataka nifanye uache kabisa tabia yako ya wizi ili hapo baadaye tuje kuishi wote kwa furaha, raha na amani, ili hapo baadaye jamii yote isikuchukie, ikupende, ikuthamini na ikuchukulie kama mtu anayefaa kuigwa.” Diva aliongea huku amejilaza juu ya kifua cha Mbosso machozi yakimdondoka.
“Nashindwa Diva, nashindwa kwa sababu macho yangu yajapoona kitu cha thamani hutamani sana, siwezi kuona kinanipita na kuniacha, sijaanza tabia hii leo, nina miaka kumi na miwili ningali bado napora watu, nakaba watu na kuwatisha kwa kutumia Zana za moto na zile zenye ncha kali.” Mbosso alijitetea.
“Niamini mpenzi, utabadilika tu, kwanza achana na wizi, acha kuanzia leo, hata ikiwezekana kama unamnjua huyo mtu uliyempora huu mkoba umrudishie, ninakupenda sana Mbosso, ninatamani uishi pamoja na mimi lakini sio ati kwa kukubali utende mambo yanayochukiza na kuwaumiza wengine.” Diva aliongea.
“Je, haujui kuwa kuiba ni kosa kisheria? Kuiba ni dhambi, tena dhambi hiyo ina adhabu kali kwa mhusika, mbali na kupigwa, kuchomwa moto, kukatwa katwa viungo, pia mhusika anaweza kufungwa.” Diva aliongea kisha akaendelea.
“Ninakupenda Mbosso, usiendelea kufanya hayo mambo yanayoumiza moyo. Unajua kuwa unapaswa kuwa baba bora na mzuri kwa wanao watarajiwa basi usiendelee kufanya haya mambo yanayoumiza. Elewa na tambua kwamba mimi ni mjamzito, hakuna mtu anayejua zaidi ya mimi na wewe leo ninakwambia.”Diva aliongea akiutazama uso wa Mbosso uliochanua ghafla na kupendeza kama Maua.
“Unasema kweli!?”mbosso alimuuliza Diva kwa mshangao.
“Yes, I speak the truth, I’m pregnancy. Nina ujauzito tena ni ujauzito wa miezi miwili sasa.” Diva aliushtua tena moyo wa Mbosso
“Waoooh! My Love.” Mbosso alimkumbatia Diva pale juu ya kitanda walicholala. Akambusu tumboni, mapenzi yakawatawala, hawakuwa na haja ya kuongea mengi, tayari walikwisha kuelewana, muda si mrefu Diva alichukua ufagio uliokuwa pembeni ya lile Geto la mpenzi wake MBOSSO Diva akafanya kufagia kile chumba cha Mbosso wake.
Mara baada ya dakika tano akazoa takataka zote, akayakusanya mashuka machafu kitandani, akaelekea bomba lililo nyuma ya Geto lake Mbosso akafanya kujaza ndoo tatu za maji, moja kwa ajiri ya kuoga mpenziwe, ya pili kufulia yale mashuka machafu ya Mbosso na ndoo ya tatu kwa matumizi ya jikoni.
“Nenda kaoge baba kijacho wangu.” Diva alimtania Mbosso.
“Nataka twende tukaoge wote mama Mbosso journiour”
“Tangulia my Love, si unajua kwamba natakiwa kufua mashuka yawe safi?”
“Ok. Love, sijui leo tutakula nini Baby?” Mbosso alimuuliza Diva.
“Wewe unapenda tule nini Love?”
“Upendacho wewe Diva.”
“Ok. Mie natamani wangu wa mapenzi ndio uanze kunena.” Diva aliongea.
“Ok. Ungependa twende Hoteli?”
"La, hasha! Sipendi. Mkeo nipo kwa ajiri yako, nitakwenda soko kununua Samaki, mchele, matunda na viungo kidogo.” Diva aliongea wakati huo Mbosso tayari kashavua nguo zake naye anaelekea bafu kusafisha mwili wake. ****
Itaendelea kesho.
Usikose
No comments:
Post a Comment