KUKU WA KIZUNGU
Sehemu ya 9
ENGLAND
Nyumbani kwa Islama Tino ameketi mezani kuna vyakula vya kila aina juu ya Meza lakini Tino hali chakula machozi yamtoka. Kuna televisheni Screen Moja kubwa imetundikwa kutani, Channel Moja kutoka Afrika Mashariki yaonesha picha za Wanyama wa aina mbali mbali wanaopatikana Tanzania, Milima mirefu iliyopo Tanzania pamoja na watu waishio Vijijini.
Islama aliingia ndani ya Jumba lake la kifahari ameongozana na Davidi mpenziwe wa zamani gari yao ilipaki pahali moja kwa moja Islama na Davidi walipitiliza faranga (Sebuleni) huko walimkuta Tino analia akimwanga machozi.
“Tino!” Islama alimsogelea Tino, akaketi karibu na mwanaye akakitwaa kitamba chake binafsi akamfuta machozi yule Chotara wake.
“Stop crying, usilie mwanangu.” Islama alimfuta machozi Tino David akaketi pembeni ya Tino.
“Hapana Mama I must cry, lazima nilie sababu hautaki kunipeleka kwa Baba yangu Afrika. Kila siku rafiki zangu wanicheka wakinidhihaki kwa kusema sina baba mimi ni yatima, nataka kumuona Baba.” Tino alilia.
“Utamuona Tino, utamuona Babayo Laizer wiki kesho tumepanga kwenda Afrika nimetuma Barua na uzuri wa Barua hiyo Babayo ameahidi kutopokea.” ISLAMA ALIMPOOZA Tino mwanaye maana kila siku Mtoto asumbua amtaka Baba yake wa Kiafrika.
“Its true Mama…… Ni kweli.” Tino alianza kufarijika. Mtoto sasa amekuwa mkubwa ana miaka minane amekopi kila kitu kutoka kwa Laizer BABAYE LABDA Nywele zake ndefu zinazojiviringa hizo amerithi kutoka kwa Mamaye.
“Mama asemayo ni kweli tupu Tino. Tukifika Afrika twaenda kutembelea Mbuga za Wanyama tutapanda Mlima Kilimanjaro na pia tutatembelea maeneo mengi ya Kihistoria David mpenzi wa Islama alichangia hoja.
“Uhakika! Au ni ndoto za mchana.”Tino hakuamini maana amekua akilia kia siku ataka kumuona Babaye Laizer.
“Surely, Uhakika upo.”Islama aliongea tena.
“Chukua hii picha niliificha ajili yako.” Islama aliitoa Mchoro mzuri wa Tembo akampatia mwanaye.
“Umeipata wapi Mama.”Tino alimuuliza Mamaye akaendelea kuitizama ndani ya fremu.
“Babayo alinipa miaka 8 iliyopita lakini sijawai kukuonesha, bahati nzuri unapenda kuchora ukiisha kula nenda ukachore. “Tino alipendezwa na ile zawadi machozi hayakumtoka tena alienda mezani kula akala kwa furaha. Islama na David waliketi mezani wakapakua vyakula vyao wakaanza kula taratibu wakimtizama Tino aliyebadilika kutoka huzuni hadi furaha.
“Tutaketi kwa kipindi cha Mwaka mmoja Maasai Land.” Islama alimwambia David wakaendelea kula.“
" It will be good, ok. Ilimradi Tino apewe ruhusa Shuleni.” Davidi aliongea akauliza.“Vipi kuhusu Pamera Mdogo wako ameipenda Safari ya kwenda Afrika?"
"Binafsi nimemshangaa kilio cha Tino kwenda Africa kimekua ni kilio cha Pamera kwenda Africa kwa pamoja wana hamu ya kwenda Maasai land.
“Rudi nyuma miaka nane iliyopita ulimsimulia Pamera uzuri wa Tanzania nchi yenye amani, upendo, furaha , raha yenye wema na ukarimu.” Davidi alimkumbusha Islama.
“Mazuri haya yamemvuta Pamera kuelekea Afrika.” Islama aliongeza neno.
“Vema tuachane na hayo tuongee yetu, yetu mapenzi.” David aliketi vizuri pale mezani akaongea.
“Ni muda mrefu sasa tangu nikuvishe pete mpenzi kwanini hauniambii ni lini twaweza kufunga ndoa tuishi kama mke na mume.”Davidi alimkumbusha Islama.
“Nitakwambia mpenzi wacha twende Afrika tujapomaliza tour yetu mambo yote yatanoga.” Davidi hakupendezwa na lile jibu lake Islama.
“Wamaanisha harusi yetu itafanyika baada ya kuketi mwaka mmoja Afrika?” David alichukia.
“I dont mean so.Simaanishi hivyo. Lakini Yawezekana tukafunga ndoa tukiwa Afrika.” Islama alibadili nia.
‘No, Islama siwezi kuruhusu harusi yetu ifanyike sehemu wanazoishi watu masikini kama Afrika. Ninataka harusi yetu iwe ni harusi ya gharama na fahari. Mimi binafsi sijapenda kwenda Afrika nafanya kukuunga mkono na kiukusindikiza.”
“David sijaipenda kauli uliyonena.” Islama aliwacha kula akamtizama David kwa hasira kidogo.
“Mapenzi hayatazamii umasikini au utajiri. Mapenzi yapo popote duniani, kwani waafrika sio watu hata tufikie hatua ya kuyakataa mazingira yao.” Islama alimkosoa Davidi.
“Kama haupendi kwenda Afrika sikulazimishi baki England niache mie na Tino tuenende Afrika,”
“Aaah! No, David alitweta akainama chini kwa aibu japokuwa alikuwa na maumivu tele moyoni sababu mpenzi wake wa kweli amezaa na mwanaume wa kiafrika. Ni muda mrefu sasa na ubaya wa wa kuletewa motto wa kiafrika anamtia wasi wasi David iwapo Islama atataka kwenda pekee Afrika.
“Ninakupenda Islama” David mpenzi wa Islama aliongea.
“Ilove you too David.”Islama alimjibu David waliendelea kula.
..............
(MAASAI LAND- TANZANIA)
Asubuhi Laizer alidamka kimyakimya pasina kumweleza mkewe pahali anapokwea . Swije Mama mwenye watoto wawili bado alikuwa usingizini, Laizer alipotoka chumbani mkuki wake mkononi, sime kiunoni, moja kwa moja akaelekea pahali miaka minane iliyopita, pale penzi lake na Islama lilipozaliwa. Pale Laizer alipokuwa mtumi Maasai,Pale Islama alipomzaa Tino, pale Islama aliishi kwa zaidi ya mwaka mmoja na nusu. Laizer akatabasamu moyoni akajisemea.
“Uje tena Mpenzi wangu uje na mwanangu, uje nyumbani.”
Nyumba aliyoiacha Islama iliota nyasi ndefu kama kichaka japo milango na madilisha yalikuwa salama, hayakuliwa na mchwa, Laizer alihitaji kuifanyia usafi pamoja na kuikarabati ili iwe bora zaidi lakini je, angeliikarabati kivipi ikiwa idhini lazima itolewe na Balozi, Kibali cha ukarabati kipo mikononi mwa Balozi hata funguo za hiyo nyumba ya wageni wajao kutalii Maasai Land, ili Laizer apewe idhini ya kuingia ndani ya ile nyumba alipaswa kwenda moja kwa moja hadi nyumbani kwa Balozi.
######
“Wahitaji Ufunguo wa Nyumba ya kulala wageni?” Balozi alimuuliza Laizer moyoni atabasamu ajuafika kuwa kuna mazuri yatafuata pale Masai land.
“Ndio Balozi ninahitaji kuifanyia ile nyumba usafi.”
“kawaida ya kuja kuuchukua ufunguo wa nyumba ya wageni wajao kutalii hapa Maasai land. Embu nidodose kwa ufupi nini kilichokufanya ufanye maamuzi ya kuja kuuchukua ufunguo wa nyumba ya wageni?" Balozi aliuliza.
“Kuna wageni waja kutembelea Maasai land.”Laizer alijibu kwa ufupi. Balozi alifurahia moyoni uchunguzi wake ni uchunguzi wenye faida kwake.
“Nitakupatia ufunguo utaenda pamoja na Yiaro Mtumi wangu mkasaidiane kufany usafi. BADO UJANIJIBU SWALI LANGU embu nieleze ni nani hao wajao kijijini?” Laizer aliona haina haja ya kuuficha ukweli sababu Wahenga walisem mficha Jipu usaha umuumbua. Balozi alitabasamu kisha Laizer Akaongea.
“Wamkumbuka Islama?”
Itaendelea
No comments:
Post a Comment