Sunday, September 22, 2024

KIGUU NA NJIA.. sehemu ya nne



 KIGUU NA NJIA

#

Nyumbani


MAMAYE AMINA: Eeh! Na hii barua nayo inahusu nini tena, au ndio umesamehewa na hao walimu wako? (Anaifungua barua mara baada ya kuweka vifuko vya karanga pembeni).

AMINA: Hata sijui inahusu nini, yanini kuandikia mate wino ukiwepo, hembu funua wewe mwenyewe nawe uridhie kilichoandikwa humo.

MAMAYE AMINA: (Anayakodolea macho yale maandishi). Mmh! Hembu muamshe babayo aje atusomee hii barua, mie mwenyewe sijui kusoma, nakodolea hii barua macho kama mwenda wazimu vile, ni heri na mwenzangu yeye amesoma soma hadi darasa la sita kuliko h mimi ambaye hata darasa la kwanza silijui vizuri.

AMINA: (Anamwamsha Babaye aliyelala usingizi wa fofofo kama samaki aina ya pono). Baba, Baba, Babaeeeh! (Anamtingisha). 

MZEE KIPUTA: Nini nawe mwana, usimwamshe aliyelala, ukimwamsha utalala wewe (Anaamka pale kwenye mkeka alolalia fofofo). Shida nini haswa. (Ananyanyua chupa ya matapu tapu na kuimiminia mdomoni mwake mafunda mawili matatu).

AMINA: Kuna barua kutoka Shuleni mama anakuomba uisome (Anamkabidhi ile Barua).

MZEE KIPUTA: Mimi mwenyewe nina matatizo ya macho siwezi kusoma vizuri. Tafadhali soma mwenyewe. (Anajitupa juu ya keka lake na kufunga macho yake).

AMINA: (Anaisoma ile barua aliyopewa Shuleni). Jamani baba na mama, Barua inasema kuwa nimefukuzwa Shule kwa sababu nina…”

MZEE KIPUTA: (Anagutuka). Nini? Umefukuzwa shule kwa sababu gani?

AMINA: (Analia na kushindwa kuisoma ile Barua, anakimbilia chumbani na anajifungia huko analia kilio cha Kwi! Kwi!

MAMAYE AMINA: Mtoto amefukuzwa shule kwa sababu ya ujauzito aliopewa na wanafunzi wenzake. (Anaongea kwa masikitiko).

MZEE KIPUTA: What!? Wala siwezi kuamini hayo maneno. Hiyo mimba ni nani amempatia na kwanini ameipata akiwa shuleni? Nakuuliza ewe mwanamke.

MAMAYE AMINA: Mume wangu, nitajibu nini mie daima nilijisemea moyoni mwangu kuwa Amina atakuja kutukomboa katika umasikini na ujinga, lakini jambo la kushangaza yaliyozuka ndio hayo  yanayoumiza mioyo na kutukatisha tamaa.

MZEE KIPUTA: Lawama zote nakutupia wewe mke wangu, wewe ndiye unayemharibu mtoto, kutwa kuchwa kumfanyisha kazi za kuuza ubuyu na karanga, anajikuta hana muda wa kujisomea zaidi ya kufanya biashara inayomkutanisah na wanaume waharibifu. (Anaongea kwa hasira).

MAMAYE AMINA: (Anaongea kwa hisia na uchungu) Usiseme hivyo mume wangu, kumbuka kuwa huyu ni mwanetu, na jukumu la kumlea kimaadili sio la kwangu mimi pekee bali ni la kwetu sote. Tulipaswa kukumbuka usemi wa wahenga waliposema, Samaki mkunje angali mbichi. Hata hivyo mume wangu na wewe umezidi haujali maendeleo ya mtoto kielimu, hautaki kusikia kama anaendelea vizuri, haujui kama anadaiwa ada, sare mpya za shule, michango mbali mbali ya shule, nauli, na hata pesa kidogo za kula shule. Vyote hivyo ninagharamia mimi, wewe kutwa kucha unashinda virabuni, kunywa na kupiga kelele za wendawazimu.

MZEE KIPUTA: Hilo halinihusu, ninachotazama ni kama mwanangu  anasoma na kufaulu  mitihani yake tu. Ajabu umemharibu mwanangu, na sasa utetezi wako unanitupia kombora ati sigharamii huduma zake..

MAMA AMINA: Usimlaumu dobi, kaniki ndio rangi yake, maji tayari yamemwagika, wala hayazoleki, hatujuii hatima ya mwenetu.

MZEE KIPUTA: (Anacharuka kama mvuta bangi). Nasema hivi muondoke haraka sana hapa nyumbani kwangu, siwezi nikawa nawalinda binadamu kumbe nawalinda mapaka na majibwa yasiyo na faida, mmenitia hasara isiyohesabika.

MAMAYE AMINA: Tuondoke twende wapi? Labda uondoke wewe na hiyo hasara ni wewe unayetutia hapa nyumbani, kutwa kuchwa kushinda virabuni na ukirudi unabweka kama Jimbwa ati nikuwekee chakula, unadhani chakula hicho kinaokotwa?! Kinatafutwa babu we! Elewa wajibu wako kama Baba katika familia, elewa unapaswa kufanya nini wewe kama kichwa cha familia.

MZEE KIPUTA: (Ananyanyuka ili kwenbda kukabiliana na mkewe). Nadhani umekwisha iamsha mizimu ya akili zangu. Sasa chokoza nyuki ulambe asali. (Wakati huo mamaye Amina anakimbilia ndani  alikojificha mwanaye).

****************

AMINA ANAMTEMBELEA ZEE LA PUTAPUTA.

Amina amekutana nna Zee la Putaputa pale pale wanapokutanaga siku zote. Amina hakumficha zee la PutaPuta, alimweleza kinagaubaga juu ya suala la yeye kugundulika kuwa na ujauzito na kufukuzwa shule lakini jambo la kushangaza zee la putaputa hakutaka kabisa kusikia kilio cha Amina.

ZEE LA PUTAPUTA: Huo ni uzembe wako wewe mwenyewe Amina, unajua kuwa wewe ni mwanafunzi tena mwanafunzi wa Sekondari, unaamua kujiingiza katika suala la mapenzi kwenye umri huu mdogo ulionao. (Anaendelea kumfokea) Na huo ujauzito sio wangu, kawapelekee hao hao wahuni wenzako, sio mimi. Sipendi kesi za kubambikiziwa, mimi ninayo familia yangu, nina mke na watoto wengi tu, isitoshe kunipakazia ujauziuto huo siwezi kukubaliana na wewe.

AMINA: Lakini Zee la PutaPuta wewe ndiye uliyenisonga twende kufanya zinaa huko kwenye magest na mahoteli, kumbuka wewe ndiye uliyenizoesha tabia hiyo.

ZEE LA PUTA PUTA: Nimekwambia nisingelipenda kuendelea kusikiliza kero zako, Mbwa wewe, na ukiendelea kunifuatilia nitatumia pesa zangu kukutia matatani. Kama sio kwenda jela basi ni ahera, Pusi wewe! Mbwa kabisa. (Zee la Putaputa, akawasha gari yake na kuondoka). Ndio ujue kuwa mimi ndio Zee la PutaPuta, sitaki  michezo ya kitoto na vitoto kama nyie, pesa kwangu zinaongea na kuogelea.

Amina alilia siku ile, alilia akijua kuwa yule mzee aliyemchezea mwili wake na kumuachia kidonda chenye hasara. Amina akajishauri  labda aende Buguruni kumwona Ben ampakazie ile kesi, kwa bahati nzuri, Ben siku ile alikuwa ameketi kwenye Geto lake, yeye pamoja na rafiki zake Kijiko na Kichungu wanapiga stori mbili tatu juu ya matatizo yaliyomkumba Bwana Ben.

KIJIKO: (Ameketi juu ya kitanda chake Ben). Hembu tustorishe mshikaji wetu,. Ilikuwaje hata ticha Mbigi akataka kukurostisha Skuli.

BEN: Mmmh! Kweli mapenzi na elimu ni sumu moja kali sana, tena sumu inayoua haraka sana, yaani wazee nilipoitwa pale Ofisini kwa Master nikasomewa shitaka la kumpa mimba Amina yule Demu aliyenipenda balaa.

KICHUNGU: Eeeh! Ikawaje? Ulikubali hilo shitaka au ulikataa? ( Kichungu ameketi kwenye kiti kilicho karibu karibu na meza ambayo Ben anaitumia kwa ajili ya kujisomea.

BEN: Ningekubalije ikiwa habari hizo ni mpya kwangu na tena ni za kushitukiza, ilibidi nikatae, hapo ndipo panga kali la maneno ya Headmaster lilianza kunirarua mwili wangu wote.

KIJIKO: Duh! Hatari.

BEN: Headmaster alinisema mbele ya Madam Grace, alinisema vibaya mno, alisema ati nimechoka kusoma ndio maana nimeona nijihusishe na mapenzi katika umri mdogo wa miaka kumi na minane, maneno…Maneno…Maneno… yalimtoka Headmaster, mwisho si aliafiki kuwa ni lazima nifukuzwe Shuleni.

KICHUNGU:Mbona hatari!

BEN: Nililia kama mtoto mdogo, nililia kweli. Nililia kama vile nimefiwa na mtu wangu wa karibu. Hatimaye nikapewa leta ya  kuwaita wazazi wangu waje skonga. (Ben alipumzika kunena).

BEN: Faza na Maza walikuja skuli,  wakasomewa shitaka langu, maongezi marefu yakashika Pahali pake, baba na mama walikesha wakiniombea msamaha ukitegemea imebaki miezi miwili tu ili nimalize kidato cha nne, hata hivyo roho ya mkuu wa shule ilikuwa ngumu kama jiwe. (Ben akaendelea kusimulia). Korapsheni  ndio iliyosovu tatizo lile, bila corruption  basi bandugu leo hii msingeliniona nikija skuli kuendelea na makamuzi.

KICHUNGU: Lakini hata hivyo tulikuambia unapotaka kugongana na yule demu ungelitumia Salama, Kwanini sasa haukufanya hivyo?

BEN: Duh! Unajua mwanangu nilikuwa new comer kitandani, Hivyo mambo yote nilimuachia yule Demu ayashughulikie,  hata suala la kukumbuka matumizi ya mpira wa salama nilikwisha yasahau kitambo.

KIJIKO: Huo ndio uzembe lakini ushukuru hongo limetumika, bila hongo leo hii hicho cheti cha form four ungelikisikia tu  midomoni mwa watu. (Mara walisikia mlango ukigongwa, alikuwa ni Amina, naye akakaribishwa, mara baada ya kukaribishwa, Ben aliwaomba Kijiko na Kichugnu wawapishe wapate kunena yao ya moyoni).

AMINA: Pole sana kwa yote yaliyokukuta mpenzi wangu. (Anamtizama Ben kwa masikitiko makubwa).

BEN: Pole nyingi zikuendee wewe mwenzangu, mimi mwenyewe nimenusurika kidogo tu mara baada ya wazazi wangu kutoa rushwa iliyoniwezesha kupita hivyo hivyo kwa taabu na mashaka. (Ben yungali mwenye sononeko na huzuniko).

...... Sorry karatasi  Moja ilipotea hapa👇....

AMINA: (Analishika shika tumbo lake). Usiniche Ben, hata kama mie nimefukuzwa shule mpenzi bado ninakupenda, tena bado nakutegemea sana mpenzi, nipe nafasi niendelee kuwa wa kwako moyoni.

BEN: Lakini  nikuulize swali Amina, Hivi huo ujauzito wako ni mimi niliyekupa au una mwingine pembeni.

AMINA: (Anasita sita kulijibu lile swali lakini anaona heri nusu shari kuliko shari kamili). Kwanini uwe wa mwingine Ben wangu? Mie ndiye nitakayekuzalia mtoto mzuri, sijui atakuwa wa kike? Sijui atakuwa wa kiume? (Akawaza kimoyo moyo). Lakini nitashukuru mwenyezi Mungu kama huyu Mtoto atakuwa wa kike aliyechukulia kila kitu kutoka kwangu. Kikubwa ni kwamba soma sana  ili hapo baadaye tuje tumtunze mwanetu.

AMINA: Ben, niamini mpenzi, tazama baba amenifukuza nyumbani, sina pahali pa kwenda, hapa nilipo nimekuja kuomb hifadhi kwako, tafadhali Ben, please.

BEN: Sina neno, waweza kwenda popote pale unapoona panafaa kwenda. (Ben alijiandaa kutoka ndani ya chumba chake).

AMINA: Tafadhali Ben, Please Ben!!! (Amina alilia kilio cha Kwi! Kwi! Kwi!).


Mwisho


OMBI:  kurasa mbili zilipotea, Mola Jalia nitaandika tena.

No comments:

Post a Comment

OBIMO CHETA

  OBIMO CHETA REMEMBER MY LOVE 💕  Sehemu ya nne Hakuwa na pahali pazuri pa kulala, hakuwa na maji, hakuwa na chakula, alilala kwenye majeng...