KENYA YENYE MAPENZI.
Mapenzi yasiyopofuka, mapenzi yanayooneka,
Mapenzi yasiyozimika, mapenzi yanayoishikika,
Mapenzi yanotafutika,mapenzi yanoneemeka,
Mapenzi yaliyopo Kenya, Kenya ni yenye Mapenzi
Mapenzi yasiyokwisha, mapenzi ya kutamanika,
Mapenzi yanayotosha, mapenzi ya kiafrika,
Mapenzi yasiyochosha, mapenzi kama nafaka,
Mito inayofurika, mabonde yanayoinuka.
Mapenzi yaliyopo Kenya, Kenya yenye mapenzi,
Mapenzi yasotaka vita,Mapenzi Democrasia,
Haki pasina Tabaka, wajibu wa kila raia
Kazi nazo kufanyika, maendeleo kutujia.
Mapenzi yaliyopo Kenya, Kenya Yenye Mapenzi,
Ulinzi kwa kila kaya,ni mwanga wa mbalamwezi,
Yasijetokea mabaya, tukachinjana kama wezi,
Amani kama Ulaya, Kenya iso ubaguzi.
Mapenzi yasomeguka,mapenzi yasodondoka,
Mapenzi yalositawika, mapenzi yaloboreka,
Mapenzi yanayomwagika,mapenzi matamu hakika,
Mapenzi yaliyopo Kenya, Kenya yenye mapenzi.
Pasiwepo vita Vita,kwani vita yaua mapenzi,
Pasiwepo tata tata, utata uleta mapinduzi,
Pasiwepo shaka shaka,mashaka uleta uchochezi,
Pasiwepo andamano, andamano uvunja amani.
Mapenziyalofurika, mapenzi kama gharika,
Milima isotikisika, bahari isochafuka,
Aridhi isotetemeka, mashamba yanovunika.
Mapenzi yaliyopo, Kenya, Kenya yenye mapenzi.
No comments:
Post a Comment