TEST YA DNA
ILIVYOMPONZA BIBI MAMA MKWE
"Mama anaendeleaje?Anasemaje pia? Naomba msalimie mwambie nimampenda sana" Hii ilikua ni kauri yangu ya kila siku niliyomwambia mchumba wangu Jese. Wakati huo tupo University collage.
"Mama hajambo, anakupenda sana na pia anatamani siku moja akuome na akufurahie"Jese aliongea Kwa furaha Lugha tamu masikioni. Nilikua ni mwingi wa tabasamu Nilifurahia pia nilijiona kama Nina bahati ya kupata mchumba mzuri kama Jese. Basi mie nikasubiri sana siku njema ya kuonana na Mama yake Jese. Na ikawa kweli Jese akanikutanisha na mama yake aliyenipenda ghafla akanipokea Kwa mikono miwili na kunikaribisha chakula Cha usiku yaani Dinner na mara nyingine aliniomba nimsindikize Supermarket kununua bidhaa.
Uchumba wangu mie na Jese hatimaye ulikuja kuzaa harusi kubwa ya furaha ambayo baadaye harusi hiyo ikafanya ndoa ambayo ilikuja kuleta matokeo Lukasi wanangu wa kwanza alizaliwa. Ilikua ni furaha tele kwetu kumkaribisha Lukasi mbarikiwa wetu lakini ajabu ya furaha yetu Bibi mama Mkwe yaani Mamaye Jese hakufurahia ujio wa yule mtoto.
"Nina wasi wasi sana na ujio wa mtoto uliyemleta nyumbani."Bibi mama Mkwe aliongea Akimaanisha ana wasi wasi na ujio wa Mwanangu Lukasi.
"Wasi wasi Gani Mama?"Nilimuuliza Bibi mama mkwe ambaye Kwa kumsoma usoni alieonekana kutokuwa na furaha
"Mia ina maana kusoma hauwezi hata picha kutazama hautazami?"Sikuelewa swali lake lakini Kwa upole na Kwa busara Nilimjibu.
"Sijakuelewa mama tafadhali naomba ufafanue."
"Mia, Tazama kucha za Lukasi kucha za Lukasi hazifanani na kucha za Babaye Jese. Macho ya Lukasi Yana rangi ya Paka wakati Babaye ana macho rangi nyeusi Nywele za Lukasi ni nywele zenye Ualibinio yaani za Kaki wakati Babaye nywele zake ni nyeusi. Sasa unataka kuniaminisha Nini hapo?" Bibi mama Mkwe alitoa ya moyoni.
"Mama nawe" Nilicheka kidogo "Hayo ni majaliwa watoto wote ni Mali ya Mungu." Niliongea bila kujua kama nnamkasirisha.
"Tafadhali Mia naomba tuongee kama watu wazima, kila nikizitazama picha za mwanangu Jese na picha za mjukuu naona kama wawili Hawa hawaendani.Lukasi hajabeba appearance ya Jese Je unataka kuniambia Nini hapo?" Aliniuliza.
"Kha! Mama ya kale hayanuki na yalopita sindwele tuyangoje yajayo."Nilizidi kumfumba Bibi mama Mkwe. Moyoni nilijisemea 'Bibi anatania hili nalo ltapita'
Lakini kumbe nilijidanganya ikawa kila ikiwa Leo Bibi mama Mkwe lazima amkague mwanangu na kuanza kumkosoa Kwa nguvu ya ile Topic yake ya 'Lukasi hajafanana na Jese.' Uvumilivu ulianza kunipiku nikaingia wasiwasi juu ya kelele za Bibi mama Mkwe.
.........
"Au ulichepuka Kwa bahati mbaya Mia?Nina wasi wasi na mtoto huyu unayesema ni mtoto wa Jese mwanangu. Sura ya mtoto, meno na hata tabia yake sio vya Jese." Alimkosoa mwanangu mwenye umri wa MIAKA Miatano
"Mama tafadhali Topic ya kumjadili mwanangu naomba sana ife.'Jese Mume wangu alinitetea, tukiwa mezani twapata Dinner.
"Mia ndiye anayemjua Baba wa huyu mtoto na huyu mtoto ni wangu fullu stop!" Jese alimkemea Bibi mama Mkwe.
"Jese usimkemee Bibi Mama Mkwe."Nilimuonya Jese ambaye alikua akila chakula kilichokataa kupita kooni.
"Uzee ni dawa mwanangu Jese, ishi kwingi uyaone mengi. Nakwambia ipo siku utakuja kuniambia juu ya ukweli wa huyu mtoto unayedai ni mwanako."Bibi Mama Mkwe alipalia makaa.
"Ukweli Gani? Kitanda hakizai haramu Mama.Mimi ndiye ninaye lala na Mia na Mia analala na Mimi. Mia ananijua na Mimi ninamjua vizuri, hajawai kunisaliti sembuse kutamani kulala nje"Jese alinitetea Bibi mama Mkwe alikasirika akaacha kula chakula cha usiku ule akafanya kueleka chumbani kwake akajibwaga kitandani akiwa ni mwingi wa hasira. Mie na Jese Mume wangu tulimshangaa.
###
Siku ziliendelea kusogea Wala hazikukoma Bibi Mama mkwe aliendelea kupiga kelele juu ya mwonekano wa Mwanangu Lukasi Tena safari hii akaanza kufanya vitimbi na Mikasa ya hapa na pale. Nilipomwita Mezani akuje tujumuike pamoja chakulani lakini Mmh ! Bibi mpMama mkwe alinishangaza sio Kwa mgomo ule. hAKUTAKA KULA CHAKULA NILICHOPIKA ZAIDI YA YEYE KUINGIA JIKONI NA KUJIPIKIA. ZAMANI NILIKUWA NA KAWAIDA YA KUMFULIA NGUO LAKINI TANGU AMESHIKILIA TOPIC YAKE NA HISIA MBAYA JUU YA MWANANGU ALIGOMA MGOMO MZITO TENA HAKUTAKA NISHIKE NGUO ZAKE BAYA ZAIDI HAKUTAKA KUONGEA AU MIMI KUMUONGELESHA, KILA WAKATI ALINUNA.
"MAMA NAOMBA UKUJE SEBULENI TUANGALIE TAMTHILIA" NILIMWITA.
"NENDA MITAANI KAWAITE NA KUWAKUSANYA MAALIBINO MUANGALIE HIZO TAMTHILIA ZA KUCHEPUKA." Alinijibu Jeuri. Nilifadhaika nikawa ni mtu wa mawazo na kilio. Nikakonda na kudhoofika lakini Uzuri Mume wangu Jese hakunitupa mbali alinifariji pia alimuya mamaye juu ya kauli zake zinazoumiza na kuchoma MOYO."
"Nilikuwa nakuona kama Binti mmoja safi sana zamani lakini kumbe Malaya mchepuko. Umemzalia mwanangu damu haramu Kisha umeamua kumpumbaza na kumuaminisha kuwa huyo mtoto aso riziki ni wake Jese" Jesu! kauri za Bibi Mama mkwe zilifanya niague kilio kikuu kilio cha Mwendawazimu. Niliiona Dunia chungu Tena nilijuta na kutamani kuondoka pale nyumbani, lakini ningelienda wapi mie Mia mama Lukasi?
Bibi Mama Mkwe akaendeleza Libeneke akilalamika ati mtoto Lukasi kamwe hafanani na Babaye Jese Safari hii akaja na Topic mpya Lazima Lukasi afanyiwe Partenity Test Yaani DNA ili ijulikane kama mtoto Lukasi ni wa ile familia au la! Nilimsaliti mume wangu.
Wee! Nilikubali !?? Teh teh teh ππ€£π Niligoma na kukataa katakata nikamwonya Bibi mama Mkwe Kwa kumwambia kama yeye haniamini basi Mume wangu Jese ndiye wa kuniamini maana yeye ndiye aliyenioa na nyumbani kwetu sikutoroka nije kulazimisha kuishi na yule kikongwe.
Akatilia mkazo na usumbufu wake ukapamba moto hatimaye Jese akanibadilikia akageukia upande wa Bibi Mama Mkwe akamsikiliza mamaye, akazisikiliza kelele za Bibi mama Mkwe.
"Ina maana na wewe hauniamini Jese? Hauamini kama Lukasi ni mtoto wa damu yako?" Nilimuuliza Jese.
"Sio kwamba sikuamini Mia Nina kuamini sana Tena sana lakini makelele ya mama ndiyo yanayotunyima Raha ya usingizi wetu. Kwanini tusikubali kuichukua DNA test tumridhishe aridhike?"Jese aliongea.
"Tumridhishe mama yako kwani mama yako ndiye aliyekuzalia mtoto?" Niliuliza nikiwa na hasira shingoni
|"Mama yako alikuzaa wewe na wewe umemleta Lukasi hakuna different this is your blood kid, niamini tafadhali," Nikiambembeleza machozi yakinitoka.
"Kubali Mia" MUME WANGU ALINIBEMBELEZA PIA, MOYONI NILIWAZA kwanini Bibi mama Mkwe ananifanyia hivi? Je, haoni kama anataka kuibomoa ndoa yetu? Je, haoni kama anaweka nyufa juu ya penzi la Mimi na mwanaye Jese? Kwanini anaingilia MAPENZI yasiyomuhusu? Je, anafikiria Mimi ni sawa sawa na Wanawake wapumbavu wanaoishia KUCHEPUKA na kuharibu ndoa zao."Nililia, nikakonda na kudhoofu.
####
Jese alimwita Dakta wa familia, Dakta Ayubu. Dakta Ayubu akamchukua Jese pamoja na Lukasi kwenda Hospitali kuchukua Sampuli za damu pamoja na nywele zilizofanyiwa vipimo. Huku nyuma mie Mia nilikua katikati ya Depression, kukonda na mawazo kunisumbua. Kichwa kilikua na wazo Moja tu Kuomba talaka, sikupendezwa kuona Bibi Mama Mkwe anaingilia ndoa yangu. Sikupendezwa kuona Jese anafuata wazo ambalo sikuona umuhimu wake, Lakini Jese angelifanyaje? Alipaswa kuheshimu mawazo ya Mama yake.
"Hallow Mia!"Mchana wa siku ile Jese Alinipiga simu.
"Hallow! My Husband" Nilimwitikia.
"Majibu ya DNA test tayari yamekwishatoka
'Eh! Nakusikiliza" nilimwambia.
"Lukasi ni mwanangu na ni damu yangu kabisa,"Jese aliongea.
'Bila shaka umefurahia."Nilimwambia.
"Itisha kikao, tupo njiani kuja huko Mimi, mwanangu Lukasi pamoja na Dakta Ayubu. Mwambie Mama qkae mkao wa kula kuyapokea matokeo"Jese aliongea.
"Sawa" Nilimjibu. Kisha nikamwita Bibi Mama mkwe mwanamama anayeninunia na kunichukia, nikamweleza awe tayari kikaoni KUYAPOKEA majibu ya DNA test. Walengwa walifika kikaoni wakaketi SEBULENI, Mie Mia niliyekonda na kudhoofu Kwa kelele na gubu la Bibi Mama mkwe, Jese Mume wangu, Bibi Mama Mkwe, Lukasi mwanangu pamoja na Dakta Ayubu Dakta wa familia. Kisha Dakta akasimama kueleza matokeo ya DNA test.
"Vipimo vya DNA TEST VINAONESHA KUWA LUKASI NI MTOTO WA JESE yaani Original copy." Dakta aliongea.
"Damu ni ya Jese macho, pua, mikono, nywele na miguu ni ya Jese."Ayubu aliongea.
"What!? I cant believe it."Bibi Mama Mkwe alitokwa macho pima.
"Ndo hivyo Bibi hata tukijaribu kwenda Hospitali mia Bora za Dunia bado tu Lukasi atabaki kuwa damu ya Jese" Dakta alieleza
"Lakini mbona mtoto hafanani na Jese?Nywele za kialibino, pua, macho, mdomo, kucha na hata tabiaau matendo ya Lukasi ni tofauti na Jese mwanangu?" Bibi Mama Mkwe aliuliza.
"Swali lako zuri sana Bibi, Kuna matokeo ya pili baada ya kufanya uchunguzi wa DNA test. Tumeangalia Vinasaba yaani Heredity na Jeni upande wa mama mzazi wa Lukasi yaani Mia na upande wako Bibi Mama mkwe matokeo yetu yakaja kuonesha kuwa LUKASI ana Jeni nyingi kutoka upande wako wewe Bibi mama Mkwe" Dakta aliendelea kudadavua.
"Mjukuu wako Lukasi amechukua vitu vingi kutoka upande wako, mjukuu wako Lukasi amechukua vitu vingi kutoka kwa Babu aliyemza baba yako wewe Bibi mama Mkwe, nywele hizi za kialibino nywele ambazo hakuna mtu katika familia hii anazo ni nywele ambazo Babu yako wewe Bibi mama Mkwe alikua anazo. Sura kucha, midomo, pua na hata matendo anayoyatenda Lukasi yalitendwa na Babu yako wewe Bibi Mama mkwe. Yamkini hujapata kumuona au kuijua Historia ya Babu aliyemza baba yako "Dakta Ayubu alihitimisha. Bibi mama Mkwe alitazama chini Kwa Aibu.
"Mama "Jese alimwita Bibi Mama mkwe.
"Tafadhali naomba uingie chumbani kwako, ubebe kila kilago au kikolokolo na kikolombwezo chako Kisha uondoke nyumbani kwangu"Jese alimwambia mama yake.
"Jese my son!" Bibi Mama Mkwe alitoa macho kama Jusi lililobanwa mlangoni.
"Unanifukuza niende wapi mwanangu?Nirudi kijijini kulima? Kumbuka Mimi ni Mama yako." Bibi mama Mkwe aliteta.
"Tafadhali mama ninakupa dakika Tano tu uingie chumbani ubebe kila kilicho chako uondoke" Jese aliongea Kwa hasira mie Kimya Wala sikumtetea Bibi mama mkwe.
"Nisamehe Mia, Nisamehe Jese."Alitia huruma
"UMEMVUNJA MOYO MKE WANGU UMEMUACHIA DEPRESHENI, STRESS NA MAWAZO LUKUKI YAMEMNYIMA HAMU YA KULA AU KUNYWA. JE, ULITAKA AFE? Tafadhali beba kila kilicho chako Kisha uondoke"Jese hakutania Bibi Mama mkwe akatoka chozi Kwa Aibu na fedhea aliyoipata. Akaelekea chumbani kwake akabeba vilago vyake akatoka ndani ya nyumba. Kwani nilimsindikiza? We koma!π π€£πWacha aondoke na nyumba yetu ianze kutabasamu sio Kwa gubu na mnuno ule.
>>>>
"Nisamehe Mia, nisamehe mke wangu nilifanya vile kumridhisha mama yangu''Jese aliniomba msamaha.
"Nilivunjika moyo Jese, nilipoteza Imani na ilibaki kidogo NIOMBE talaka yangu" Nilimwambia ukweli Jese
"Naomba usiniache Mia niruhusu nitafute Mwanasaikolojia au msuruhishi wa ndoa atuweke sawa kiushauri"Jese aliongea.
"Wazo lako zuri" nilikubaliana na Jese Mume wangu Kisha nikamsamehe. Nilisamehe maana mawazo ya kutaka kuondoka ndani ya nyumba ile yalinisumbua.
<<<<<<<<<<
TCHAO
No comments:
Post a Comment