Sunday, October 13, 2024

Hadithi FUPI YA 4G










📱. HADITHI FUPI YA 4G

Kama kawaida Bi. Harusi aliamka alfajiri kuendelea na kazi ndogo ndogo za nyumbani, alijisindikiza taratibu kwa sauti yake ya Kasuku;

“Wanaume tumeumbwa,

Matesosoo, matesoo,

Kuhangaika…..”

Mzee Kapita humkatisha akitokea usingizini, leo tena hivyo hivyo alifoka;

“Kaimbie nje! Unatamani wanaume eh!? Ichukue basi! Chukua basi!” Bi.Harusi alimjibiza;

“Nimechoka kuwa na kidume wa nyumba hii, fedha nilete, chakula nilete, nyumba nilinde, polisi niwatoe, na safari hii huyo kidume suruali mwenzio ataozea ndani.”

 Marumbano haya endelevu yalikatishwa na mlio wa simu ya mkononi ya Nasra iliyoita mara kadhaa bila majibu, ndipo sasa Bi. Harusi alikata shauri la kumuangali Nasra kwanin I hapokei simu. Kumbe Nasra bado yu fofofo, mamaye akajisogeza mpaka kitandani kwake, akaichukua simu iliyoonesha simu zisizopokelewa tatu za jina la ‘My Boo Love’.

Taratibu mapigo ya moyo yalipanda, akapoteza fahamu chini puu!, Kishindo chake kiliwainua Nasra na babaye vitandani, Mzee Kapita pasi na maulizo aliwasilisha malaumu kede kede kwa bintiye;

“Umemfanya nini mke wangu?”

` “Fedhuli weye!! Uchawi gani asubuhi yote hii?”

“Simu yako imemuua, kidato cha aa simu ya nini?”Sauti za malaumu
 ziliwasafirisha wawili na nusu wale hadi kwenye kituo cha afya, familia ilichotwa wakagawana majengo ya serikali, mama Hospitali, kaka sero, baba na dada wakizurura zurura kuisaka riziki, wawapelekee wapendwa wao chakula. Kila kukicha ilikuwa ni afadhali ya jana, kwani mama na kaka ni wawezeshaji wakuu wa familia, japokuwa Bi. Harusi ni mzoefu wa hakli, alicheza michezo mara vikoba, mara mikopo ili familia ipeleke mikono vinywani, pia Mika alifanya juu chini kuitunza familia yake kwa heri ama kwa shari kwani hana ujuzi, kipaji ama elimu yoyote, hali inayomsukuma kwenye ‘U-chorichori’ akisahau cha mntu mavi, vituo vya polisi ni nyumba zake za ibada, mamaye ilimtoka rushwa kila juma.
Upande mwingine mzee Kapita ni Koala Mzee hodari wa mdomo na michezo ya ubashiri. Hubeti na kupiga bhodi milioni moja lakini mara nyingi baada ya ushindi mnono hupotea nyumbani.

Nasra kitinda mimba wa Bi.Harusi, kigori, kaidi na mateka wa 4G, hulishughulisha Gumbale usiku usiku kucha, hivyo huwahi shule kipindi cha mapumziko siku tano za juma. Ilimpasa ahitimu miaka mitano iliyopita kama kusingalikuwepo mchujo wa kidato cha pili.
Utafiti wa Kidaktari ulibainisha Bi.Harusi alikumbwa na kisukari. Daktari alisema.

“Hii blood pressure plus Diabetes itamgharimu hadi five days kitandani, inawezekana akazinduka kesho ila sio kuamka.” Nasra alibubujikwa na machori ingawaje sio ishara ya macungu bali jinsi.

Ghafla baba akawa baba, aliingia hapa akatokea pale kutyasaka malipo ya matibabu na kumtunza mgonjwa na wanawe. Nasra hakuhudhuria shule kabisa, alipika akajigawanya kupeleka milo asubuhi, mchana na jioni hospitalini na kituo cha polisi. Maisha yao yakawa mtihani, mpaka Bi.Harusi alipotoka hospitalini baada ya majuma mawili, na baada ya juma moja alimtoa mwanawe mahabusu alipokuwepo, akabakiwa na deni la elfu kumi kwa afande Jabali na umeme ukakatika wote, tulilazimika kulala tukiwa na kiu ya kujua muendelezo wa Tamthiliya ya 4G.

Ngriiii!! Te, te, teee! Zuuu! Zuuu! Ni kelele za simu za mkononi, zilizotuamsha kila mtu alijiandaa haraka haraka, kina kaka walitafuta usafiri wa kutupeleka uwanja wa ndege, saa moja juju ya alama tulianza safari ya kuelekea South Afrika. Baba, mama, kaka Sele, kaka Stan, Da, Edna na mimi (Emele) ambapo shangazi alitualika tukalie sikukuu ya Noeli kwake, Pretoria. Tulifurahishwa sana na huduma za shirika la ndege Tanzania, pia tulisikitishwa kwa vile hatutoangalia tena 4G. Na kwa vile Bi Harusi alipona na alimtoa mwanawe kifungoni, mama alizidi kutusisitizia ju ya ushupavu wa mwanamke, aliendeleza kampeni;

“Si mmejionea wenyewe! Hembu ngoja kwanza.” Alitoa Sumu, akafungua program ya Biblia kisha aligamba;

“Mwanzo 2:18 Biblia inasema; Bwana Mungu akasema, si vema huyo mtu awe peke yake, nitamfanyia msaidizi, msaidizi wa kufanana naye.”Akatugeukia akaendelea;

“Mwanangu, mtu akiushindwa mzigo aletewe mwenye nguvu au dhaifu zaidi yake?” Mimi na dada tulijibuy;

“Mwenye nguvu zaidi yake.”Baba akasafisha koo, wote tukakaa tayari kumsikiliza, akajibu mapigo;

“Waefeeso 5:22, inasema, Enyi wake watiini waume zenu.” Alitia Nukta mjadala japokuwa minong’ono iliendelea kusikika toka kwenye ndege, alijua kwamba tu familia.

Ikawa tuliposhuka uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Nelson Mandera, Johannesburg, kila mtu yupo na lake, tuliwakuta shangazi na mjomba wanatusubiria, tulitumia saa chache kufia Pretoria waqnapoishi kwa kutumia Treni la umeme. Tulipofika kwenye jengo wanaloishi tulitumia ‘lift’ kufika kwao mpaka tunaingia ndani hat5ukukutana na jirani yoyote.
Ilikuwa ni siku ya furaha sana, mjomba na shangazi walisahau upweke wao wa kukosa mtoto, wao waliishi na njiwa wengin waliowafuga juu kabisa ya ghorofa ili wawafariji. Tukiwa kwenye chakula cha jioni da Edna alianzisha mazungumzo;
DA EDNA;Huku vitu vyote vya Tanzania tunavipata kasoro…

KA STAN;Tamthiliya ya 4G.

KA SELE; Ndiyo! Yan daah!

MAMA;Huku kuna Tamthiliya nyingi nzuri zaidi ya 4G.

BABA; Mmmh! Sidhani.

MJOMBA;Tamthiliya nyingine zipo ila 4G ipo pia.

BABA;Ile familia yam zee Kapita?

SHANGAZI;Ndiyo ila hairuhusiwi runingani, ni kwenye kumbi za sinema, wanaongea Kiswahili, kuna ‘subtitle’ ya Kizulu.

MIMI;Tunipenda sana.

BABA;Si runingani hivyo ni rahisi kuiona?

SHANGAZI;Kakaa! Tutawal;ipia watoto wafurahi.

MAMA;Na mimi mtoto mkubwa.

WOTE;Hahahahh! Teh! Teh! Teh! Uuuhuhuhuhu!

DA EDNA;Kitu kingine tunachokikosa huku niiii, Ushindani wa baba na mama.
Wote tulicheka ikawa ndio sasa tuklitawanyika vitandani mwetu.
Kabla sijalala, nilibembelezwa na sauti za magari, pia niliamshwa na sauti za magari, usiku wa kwanza nje ya nchi uliokuwa mrefu, asubuhi jua lilichomoza mithili ya mwenge angavu, nilijihisi ni wa kwanza kuamka, lakini kila mtu alikuwa macho.

Nilitoka kitandani nikajisafisha nikaelekea ukumbini ambapo niliwakuta ndugu zangu na sura mbili mpya za kizungu, niliwasalimia wote nikaketi.
Baada ya dakika kadhaa tukapata chakula cha asubuhi, hapo ndipo nilipogundua kwamba wale Wazungu ni Madaktari bingwa wa masuala ya uzazi, na leo wapo kwenye huduma ya Home Clinic and Councelling kweani mjomba na shangazi ni wateja wao waliochanganya mbegu zao miezi miwili iliyopita ili kumtengeneza mtoto kupitia In vitro fertilization katikati yam lo tukiendelea kustaajabu uwepo wa Tamthiliya ya 4G nchini Afrika ya Kusini, wale Madaktari walituelez mambo chungu mzima tunayoshiriki nchini Tanzania na nchi nyingine au dunia kiujumla, wakitueleza jimsi maendeleo ya Sayansi na Teknolojia yalivyoifanya dunia kuwa kitongoni, baadhi ya vitu vinavyoshiriki dunia nzima ni pamoja na dhana ya soko la dunia na bei zake kiujumla ambazo zinaongoza manunuzi na mauzo ya bidhaa na huduma zote duniani, pia kwenye muunganisho wa (Internet) yaani International Network, ambayo hutuunganisha watu wa Mabara yote kupitia mitandao ya kijamii kama Instagram, Facebook, Skype na You tube pamojan na matumizi mwengine ya Data.

Baada ya kutuvua Ujinga, tulinyanyuka kuelekea ukumbi wa Winnie Mandela kuangalia Ratiba ya jumla ya Sinema.

Ukumbi wa Winnie Mandela ni ukumbi mkubwa wenye maduka na kumbi mbali mbali, Mjomba, baba, mama na sisi tulinyoosha moja kwa moja hadi kwenye jumba la Sinema, Tulipoiona ratiba ya Tamthiliya ya 4G ni saa tatu usiku kila siku tukiwa tumewaacha shangazi na Madaktari nje. Baada ya kujua Ratiba, tulitembelea maduka mbali mbali, bidhaa tofauti tofauti zinauzwa zikiongozwa na bidhaa za Kielectronic na bidhaa za kifedha, tulishangaa kujua fedha tulizozitunza mabenki ya nyumbani (Tanzania) Tungewweza kutoa tukiwa kule (Afrika ya kusini) zikiwa shilingi za Kitanzania, Dollar au Randi. Baada ya kuzunguka sana tulitoka nje turudi nyumbani tusiwakute Madaktari ila shangazi pekee. Tukaongozana kwa pamoja kurudi nyumbani ili kujiandaa kwa baadaye usiku.

Muda haukuganda, saa mbili uiku tulishakata tiketi, tukaingia ndani tulipopewa miwani ya 3Dtayari kwa ajiri ya 4G.

4G inazidi kuchachamaa, siku ilianza, Bi.Harusi akiwa kwenye chumba cha uangalizi wa hali ya juu (ICU) Familia ikiwa katika hali ya sintofahamu wanapewa taarifa za kifo cha Bi.Harusi, jumba zima lilijawa na huzuni, karibia watizamaji wote tulikuwa tukipambana na machozi, mama alishindwa kujizuia na Edna ambaye alilia kwa sauti kubwa kulingana na ukimya wa mule ndani. Da Edna aliniomba nimsindikize bafuni kunawa uso kwa sababu ya ugeni wetu, sote, shangazi alinipokea jukumu hilo.

Kwenye kioo ni vilio na majonzi, majamvi yametandikwa, ndugu, jamaa na marafiki wakimlilia marehemu.

Baada ya Da Edna kuingia Maliwatoni, shangazi alisikika akiongea na simu.
“What!!! You can’t be serious. I have to get a baby this year, I’m at Winnie Mandela Hall ok.” Da Edna alipotoka, shangazi alimuomba wasubiri kidogo, nje kuna rafiki yake, angekuja ndani ya muda mfupi ujao, wakafanya hivyo, kukiwa na mwanga hafifu, gari lilichuna breki mbele yao kinguvu, shangazio na mtu asiyefahamika walimziba dada mdomo, wakasaidiana kumpandisha kwenye gari na likaanza kuondoka, shangazi akafunga mlango puuh!

“Puuh! Puuh! Puuh! Vijana walianza kazi ya kufukia kaburi, kaburi la Bi. Harusi bega kwa bega, watu walilia, Nasra naye alilia.

Baada ya kukawia sana, shangazi alirudi kama mtu aliyechanganyikiwa akiuliza maswali mfululizo kama Da Edna amerejea ndani? Mjadala wetu ulizua makelele, istoshe tulikanyaga nyaya, hali iliyopelekea watu wa nyuma walalame,ikabidi tutoke nje ya jumba la sinema tukiiacha 4G ianendelea.

Maswali ya shangazi juu ya uwepo wa Da Edna yalizidi kutuweka njia panda, na maswali yalipomnuelekea yeye alishindwa kujibu, kwani alikuwa analia sana, mama alikata shauri la kuanza kumtafuta Da Edna, kwani shangazi alikuwa haeleweki, tulijigawanya tukaanza kumtafuta, tuliingia kwenye migahawa,maduka, vyooni hadi kumbi za starehe tusimuone, lakini hatukufa moyo, tulitafuta na kutafuta lakini wapi! Mwishowe tukatafutana, mama alikuwa wa mweisho kuonekana, ilitupasa tutoke nje, kwani muda wa kubakio kwenye jengo ulikuwa umeisha.

Tulivyotoka nje tuliendelea kumchunguza haswa kwenye magari ya watu waliokuwa wanaondoka, kubwa nililoambulia ni mmazungumzo ya familia iliyokuwa ikiendea gari lao walipomlaumu mzee Kapila kwa kujiua akidai amemfuata kipenzi chake, roho iliniuma, taswira ya Da Edna na Nasra zilinifanya nilie kilio kilichonisafirisha mpaka kesho yake asubuhi nilipoamka mapajani mwa shangazi, alinipa pole, akaniletea chai pale pale nilipoamka, nikiwa nakunywa chai alinieleza wifi yake na kaka zangu walienda kituo cha polisi kutoa taarifa, mjomba na baba wameenda kuendelea kumtafuta Edna, kisha akatoa maoni yake.
“Sidhani kama watampata, mji huu ni mkubwa.” Maneno yaliyonifanya niache kunywa chain a fikra zihame hadi kwenye sehemu mojawapo ya TMTHILIYA YA 4G, ambapoNasra alipotea kwa mwezim mzima wakimtafuta bila ya mafanikio hadi pale aliporudi mwenyewe, nikajisemea moyoni;

“Atarudi.”Nikaenda kuoga, niiporudi mnikamfuata shangazi alipoenda, juu kabisa ya ghorofa nilikaa pembeni yake nikamuegamia begani, kisha tukaanza kuongea;

MIMI;Nimemkumbuka sana dada yangu.

SHANGAZI; Mmmh! Ila.

MIMI;Ila nini?

SHANGAZI;Nilimuona anaangaliana na kijana wa kizungu siku ile, inawezekana.

MIMI;Ajkaswa ameondoka naye? Hapana, da Edna si mteremko hivyo,
 namjua!Nilijiinua toka begani mwake, nikakumbuka Nasra alipouliza alikuwa wapi mwezi mzima, ilifahamika alikuwa kwa mwanaume.
“Inawezekanaje da Edna akawa na mwanaume?”Nilijiuliza, nikachukua kopo la mtama, nikaanza kuwarushia njiwa, ghafla nikajikuta ninaimba;

“Ewe njiwa ewe njiwa, peleka salamuu,
Kwa yule kwa yulee, wamngu wa muhimuu,
Njwa peleka salamu,
Oh kwa yule wangu muhimu,
Umuelezee,
Afahamuu,
Kwamba nibnapata taabu,
Oh umuelezee,
Afahamu,
Kwamba ninapata taabu.

Nilikatishwa na simu ya shangazi, ilipoita aliiangalia kisha akakata. Mata ya pili simu iliita, aliipokea, alikuwa ni kaka Sele aliyetuomba twende ndani, kwani wao wamesharejea, kauli zake zikionesha hahitaji maneno mwengi. Ikabidi mimi na Shangazi twende nda ni, nilichokiona sikuamini macho yangu, niliwaona kaka zangu kwenye hali ambayo sikuwahi kuwaona, hivyo kabla.
Sikuwa na maswali mengi, nilijitupa alipo mama ambaye alipoteza fahamu, nikaanza kulia huku nikijmuamsha kwa nikimpepea.

Kauli zake zisizohitaji maswali zilituinua haraka tukiwa na kihoro kama wamempata au la, na niaje mbona ka.Sele alikuwa vile, aliongea tofauti na nilivyomzoea. Haraka zangu za kushuka kwenye ngazi, zlinifanya nikwae kwenye ngazi nikachanika kidogo mkononi na nikachunika mguuni, kwa bahatuimmbaya au nzuri sikumuona shangazi, inamaanisha yeye alikuwa anakuja taratibu.Nilisimama kijasiri, nikaelekea kwenye chumba chetu, nilipofungua mlango, niliwakuta kaka zangu wamenyong’onyea zaidi yangu, njikakumbuka walipewa mwanamke (mimi) awe msaidizi kwao wanaposhindwa. Nikatazama chini nikamuona mama amelazwa, nikapiga moyo konde, nikachukua hatua.
Niliendelea mpaka mama alipozinduka.

“Mama, kaka kwani vipi?”Niliwauliza mbele ya shangazi, Ka.Stan alianza kuhadithia;

“Tulipofika kituoni kutoa taarifa tuliulizwa kwamba tulimtafuta kwenye hospitali zozote, wakimaanisha Mochwari kwenye kitengo cha miili iliyopatikana kwenye ajali? Tulimuona.”Tulishtushwa, Ka Stan akaendelea;

“Tumehakikisha ni yeye, yeye kabisa.” Mama akasema;

“Hayupo, hayupo tena.” Huku akitokwa na machozi. Ka Sele akasema;

“Huwezi kuchukua mwili ulioopatikana kwenye ajali bila kibali cha polisi, tulipofata kiba;li kituo cha piolisi tulishtushwa kumuona baba akiingizwa kituoni akiwa amechakazwa kwa kipigo hata asiweze kuongea vizuri.”MNama kwa sauti ya majonzi alisema;

“Tulipojaribu kumuulizia kosa lake hatukujibiwa, ila tulimsikia askari akimuambia mqwenzake kuwa huyu jamaa ni mwizi Mtanzania, yani bora wageni wa Kizungu, hawa ngozi nyeusi wenzetu ni matatizo tu.Hili nimelikamata huko chini, alikuwa anajaribu kuiba kwenbye lile duka la yule mtaalamu.” Ka Sele akaendelea;

“Na kiloa tulipomueleza yule baba yetu, ndugu yetu, mtu safi, si mwizi, hawakutuelewa, hivyo baba aliingizwa rumande akuiwa hoi, tukiwa hatujui mjomba yuko wapi, tukaamua kurudi kwanza nyumbani, njiani hali ya mama ilizidi kutetereka,m hata tulipowasili hapa alizimia.”Kimya kilitawala, hata angelikatuiza mende angeweza kusikika.”

Ghafla Mjomba anaingia akiwa amefungwa bandeji nusu ya jmwili wake wote, tukiwa tumechanganywa na muonekano wake, hali ya mama ikaanza kuwa mbaya, poresha kama ile ya Bi.Harusi ilianza kumpanda kwa haraka akazima tena huku akitokwa na mapovu mdomoni.

Shangazi aliponyanyua mdomo amjibu, mlango ulifunguliwa ni baba, ka.Sele, Ka.Stan, wale Madaktari na Da Edna.Midomo yetu ikawa wazi kama lango la Maktaba, macho yakatutoka kama vile peremende iliyopulizwa, tumeganda kama barafu, hatuna hili wala lile juu ya kinachoendelea, yule Dakta mwana mama alianza kuhadithia;

“Kwa takribani miaka miwili tubahangaika, wateja wetu bwana na bibi Denis waweze kupata watoto, hatuna historia ya kushindwa kwenye kazi yetu, ila kwa wao historia ilianza kubadirika, tumetumia vyakula, madawa na upasuaji wa aina mbali mbali kwa zaidi ya m,ara saba bila ya majibu chanya, hali ambayo sio ya kawaida, ila tulichofanikiwa kukijua ni kwamba mke wa Dennis, Maria hawezi kupata mtoto, iwe ndani au nje nya mwili wake. Hivyo basi, mimi Dakta Queen nilimshauri Dakta John tutumie alternative nyingine.

Hakujali hali yake ilivyo, bali aliwasamuru kaka zangu wakatafute gari la wagonjwa wampeleke mama hospitali, kwani mama aliendelea kutoa mapovu yaliyoandamana na damu.Tulisubiri kwa kitambo kidogo, kina kaka hawakurudi, tulizidi kuchanganyikiwa, mama alitokwa na mapovu wee, mjpaka mjomba alipoingia chumbani na kutoka na kikop[o kidogo cha dawa akamnywesha.
Dawa ambayo kiukweli ilifanya kazi kwa haraka ajabu, mapovu yalikata kutoka, na baada tya muda dakika kadhaa, mama alizinduka akionekana mwenye kumbu kumbu vizuri, aliuliza. “Na wanangu Stan na Sele wako wapi?”Mjomba alimjibu swali kwa swali;

“Unajisikiaje?”Mama aliuliza tena kihasira na uchungu.

“Wengine waache waende, wapo wapi wanangu?”

“Tuligundua mbegu za Dennis zitarutubisha kwa haraka na kuzalisha kiumbe kizuri zaidi kama zitakutana na yai la kigori, wapo Wazungu wanaouza mayai yao, lakini alihitajika mtoto awe mweusi.Tuliwaeleza wanandoa hawa hali halisi wakasema wapo tayari kwa lolote lile.Wakituachia kazi ya kumtafuta Kigori atakayetupatia mayai yake, tu8m,lipe mdada mmoja wa Kiafrika atupatie mayai yake tusifanikiwe tena.

Siku ile nilipokuwa ukumbi wa Winnie Mandela, Daakta Johnm alimpigia simu Maria kumjuza kwamba zoezi lile pia halikufanikiwa, Maria kwa jaziba alituambia tuje ukumbi wa Winnie Mandela ili atupatie kigori mwingine twende tukajaribu tena, tulifika akatupatia kigori ambaye tulishindwa kumtambua kutokana na giza..

Mimi na Daktari mwebnzangu tulishauriana kwamba, inawezekana awali hatukufanikiwa kwa sababu tulichukua mayai ya siku za kawaida, badala yake huyu wa awamu hii tungechukua mayai yale ya siku za hatari kwenye mzunguko wake wa hedhi, hivyo basi, tulimtuza specimen wetu hadi angefikia siku za hatari ambapo tungechukua mayai yake kwa kutumia mashine.

Leo tukiwa kwenye duka letu la madawa kule chini ambako tumemhifadhi Edna kwenye stoo, baba yenu na bwana Dennis walikuja, baba yenu akiwa mwenye hamu ya kukagua kila sehemu ya duka letu, tukaona huyu atatuharibia mambo, tulimtengenezea kesi ya wizi, tukamuitia polisi akakamatwa.
Saa moja lililopita, duka letu liliwaka moto mahali ambapo tuliweka hazina zetu zote, mimi na mume wangu, tukafanya juhudi zote kuwapigia zima moto, hatukuwapata, ilibidi tuanze kuuzima moto kwa juhudi zetu binafsi, Stan na Sele, walikuwa wakipita njia, waliungana nasi tukawa watu wanne tunaozima moto kwenye duka lililojaa madawa na lenye mtu ndani. Sisi hatukuweza kuwatambua kina Stan kwa sababu moshi, tulizima moto mpaka moto wote ulipokoma, Edna akiwa bado yupo ndani, kwani mlango wa Stoo ulikuwa….. Tulipogundua kuwa ni Sele na Stan nbdio waliotusaidia, mioyo yetu ikatusuta, ilibidi…Edna, walikuwa wanashgangaa baba yenu…dukani akitokea kituo cha polisi, walipomuachia huru baada ya kumuona hana hela ya kuwahonga.

Japokuwa …ana hasira ya kutengenezewa kesi alipobahartika kumuona Edna. Tuliwaopmba msamaha, tukawaomba tuongozane nao hapa ili tuwaombe msamaha na ninyi. Tunaomba mtusamehe.”

Hakuna aliyekuwa na kinyongo.
“Wewe, wewe Emele, hembu kalale ndani.”Da Edna aliniamsha akakatisha ndoto yangu, Da Edna akasema;

“Unalala tu, Tamthiliya ya 4G imeisha, Nasra amepata Stashahada yake, Mika ameoa, Bi.Harusi na mumewe wamesafiri kwenda Dubai.”Nilinyanyuka kwenye kiti nikaenda kulala chumbani.







No comments:

Post a Comment

I promise you

   I PROMISE YOU. (NINAKUAHIDI.) SURA  YA KWANZA. UBAYA WA POMBE. “Umenizingua job, umenizingua kwa muda mrefu sana mpenzi wangu…….kwanini l...