MUME WANGU ALINILAZIMISHA NITAFUTE KAZI YA PILI LAKINI NILICHOKUJA KUGUNDUA KILINIFANYA NIOMBE TARAKA.
Nilipopokea mshahara wangu wa mwezi October nilijipongeza na kumshukuru Mola sababu niliona mpango wangu wa kujinunulia gari π ulibisha hodi.
"Nitachukua mshahara wa mwezi October na miezi mingine ilopita nitaichanganya nikajizawadie Prado nyeupe au Rolly Royce." Nilijitania ingawaje uwezo wa kununua Rolly Royce sikua nao mie Mwalimu Husna.
"Nikiisha keti mbele ya siti ya Dereva nitampungia mkono Mume wangu Jodi, 'Hallow Baby Jodi... By by lm now driving my beautifully Car' " Mbwembwembwe zilinisumbua.
"Lakini mmh! Kumbe nimepuunguki washilingi Million Tano Ili kukamilisha ununuzi wa Gari yangu" Nilikumbuka kuwa Salio halitoshi. Furaha yangu ilianza kuyeyuka taratibu kama barafu Juani.
"Oh! Mola wangu nihurumie!," Nilihuzunika.
"Ok. Nitamwambia Mume wangu Jodi aniongezee Millioni tano ililiyobaki" Nilijipa matumaini, wazo langu lilikua faraja kwangu. Huzuni ilinipungua maana nilijua Jodi hawezi kuninyima Salio lililopelea. Jodi anapesa nyingi za kumwaga, kazi yake inalipa maana yeye ni Injinia, Fundi msanifu wa majengo makubwa.
Jioni ilipowasili niliingia Mekoni kuandaa chakula kitamu ambacho Mume wangu hakika angelinisifia. Ninajua kupika na mapishi ninayaweza. Mara baada ya mapishi niliingia bafu kukosha mwili na kujipulizia uturi wa kipemba Ili babu akisikia harufu ya karafuu na tende anipende zaidi. Na nijuavyo mie Wapemba na waunguja mambo tunayaweza.
Aliporejea nyumbani nilimpokea Kwa wingi wa mabusu π₯°na matabasamu☺️ akaeleka kukosha mwili bafu mie nikaandika meza tule na kulishana mahanjumanti hapo ndipo nikapata mwanya wa kumueleza Jodi juu ya shida yangu.
"Muda si mrefu na mie Ua la MOYO wako nitapendeza nikiwa na ndinga langu mwenyewe" Niliongea taratibu nikamega tonge la ugali nikalichovya na mchuzi rojorojo Kisha nikamlisha wangu nimpendae Jodi.
"Waoo! Hongera Sweet heart❤️ UNATAKA kuniambia Ndo ndo ndo imekua chururu na kibubu kimetick." Jodi Mume wangu mwenye masharubu yake na na tumbole kubwa kama kabeba mapacha aliniambia.
"Kibubu kimetick Dear ila bado ninashida Moja ndogo ingawa nzito SEMA ninatumaini KUPITIA wewe wangu wa MAPENZI nitafanikiwa mafanikio mengi kama mchanga wa bahari" Nilimkonyezea JIcho nikarembuka na kudeka.
"Shida Gani Mamie, ongea nikusaidie " Jodi alinipa nafasi ya kueleza dukuduku langu.
"PESA yakununulia gari niipendayo haijakamilika, hapanilipo Nina kiasi Cha shilingi Millioni hamsini na Tano mfukoni imesalia millioni Tano Ili shuhuli ikamilike, Tafadhali naomba uniwezeshe kiasi cha pesa iliyosalia." Niliwasilisha ombi langu nikasubiri kumsikiliza Nini atasajest.
"Mmh! Ombi lako kwangu Mlima Daring" Sikuielewa kauri ya Jodi.
"Una maanisha Nini Daring?" Nilihitaji kujua.
"Sina pesa hizo Kwa Sasa lakini kama utafuata ushauri wangu lazima utapata hitaji la MOYO wako." Jodi aliongea.
"Jodi usiniambie hauna pesa nilizoomba kumbuka mshahara wako ni mara nne ya mshahara wangu." Niliropokwa.
"Mamy usikurupuke, bado sijamaliza kukueleza Nini unapaswa kufanya. Unapaswa kufanya kazi ya pili mbali na kazi yako ya Ualimu"
"Jodi sintakuelewa unanishauri nifanye kazi ya pili wakati Nina kazi yangu ya kwanza. Aya niambie ni kazi Gani hiyo ya pili." Nilisubiri jibu lake.
"Kama nilivyosema Sina Millioni tano ya kukuongeza ununue gari, tafuta kazi yoyote ile ya pili ikuwezeshe upate pesa." Jordan alinichanganya
"Kazi Gani Sasa? Nilibadirika furaha yangu ilianza kuchuja.
"Yoyote ile nzuri" Alisistiza
"Hapana Jodi siwezi, ningali Nina majukumu shuleni kama MWALIMU na Nyumbani kama Mkeo kupika, kufua. Kulisha mifugo, kwenda soko, usafi nakadharika."
"Tafuta kazi nyingine Bana."
"Siwezi Jodi, kama unashindwa kunisaidia hiyo Million Tano basi niruhisu niuze Moja ya magari YAKO Yale SITA Ili na Mimi nifurahie kumiliki gari yangu mwenyewe." Nililitetea wazo langu.
"Kamwe usithubutu kuigusa gari yangu ukaiuza," Alininyoshea dole. Akadamka pale alipoketi mara baada ya kukosha mikono yake haraka haraka akaelekea chumbani kulala. Niliogopa kidogo moyoni nilihisi yamkini nimemuudhi Mume wangu, yamkini hajapendezwa ombi langu, nikaacha kula nikanawa mikono na kumfuata chumbani nimbembeleze.
................
"Ombi la Mumeo lashangaza" Mama yangu Bi. Subira alishangaa mara baada ya kumweleza maudhi ya mume wangu. Leo nimemtembelea Mama kumuomba ushauri na kumueleza juu ya mabadiliko' ya mume wangu Jodi.
"Usitake kuniambia kuwa mkwe wangu Jodi hakupi kila kitu nyumbani" Mama alionesha wasi wasi.
"Kila kitu ninapata Mama lakini hili la kuambiwa NITAFUTE KAZI nyingine Ili nijichange kununua ndinga langu limeniumiza. Jodi ananitwisha zigo zito la majukumu." Nilimwambia mama
"Kipenda roho ula nyama mbichi Husna" Mama aliendelea kunipa mawaidha.
"Mke mwema uheshimu na kutii mawazo ya mumewe, tafadhali sikiliza sauti yake labda Kuna MAZURI utayapata kutokana na mawazo yake." Mama alimuunga mkono Jodi.
"Hapana Mama nahitaji huruma kwa hiyo natakiwa kufanya kazi ya kufundisha watoto Shule na pia kuhangaikia mambo mengine? Ina maana siku Tano niwepo Shule na siku mbili ambazo ni jumamosi na jumapili niwepo kwenye kazi ya pili.
"Kama unania ya kulipata gari liupedezalo MOYO wako basi fanya lakini kama hauna nia achana na matamanio yako." Mama aliongea. Nilirejea nyumbani kwangu nikiwa mnyonge mnyong'onyevu Sina Raha moyoni zaidi ya HASIRA nilijiuliza kwanini Jodi akatae kunisaidia shilingi millioni Tano tu? Ukitegemea Kwa uwezo alionao angeliweza kunisaidia hata Millioni kumi ya zawadi.
.............
Wiki mbili zilipita lakini kila nikimbembeleza Jodi kuhusu Salio la Gari alitia msistizo nifanye kazi yoyote ile ya pili itakayoniwezesha kudunduliza dunduliza vijipesa. Ndani ya wiki hizo mbili MOYO wangu uKAANZA kuregea taratibu nikairegeza kamba na msimamo wangu wa kutokufanya kazi ya pili ilihali kazi ya kwanza ninayo. Nikamwambia Jodi nipo tayari kufanya kazi ya pili sababu mwenzangu amekuwa mchoyo hataki kunisaidia pesa ndogo ndoago kama kinyesi Cha lnzi.π€£π€£π€£π€£
Jodi aliposikia kwamba nipo tayari kufanya kazi ya pili alifurahi sana na kunipa baraka zake akasema lazima nitafanikiwa Tena akaongeza madoido yakeq eti akasema mwanamke mpenda maendeleo hamtegemei mumewe Bali hutumia nguvuze kujipigania. Nikamnunia sana hata unyumba nikatamani nisimpe.
Katikati ya fikra zangu niliwaza ni aina Gani ya kazi itakua fiti Ili nifanikiwe zaidi. 'Je, nifanye shuhuli ya kuuza Duka la mahitaji ya nyumbani?' ' Hapana sikuwa tayari kupoteza akiba yangu kuanzisha biashara ukitegemea damu yangu haipatani na biashara. Je, nifanye kazi za ndani Yaani kazi ya u house geli? Teh teh tehπππ€£ nilicheka yaani mie Mwalimu Husna mke wa bosi nikafanye kazi ya kupuguta deki, kukosha vyombo au kulisha umbwa na nyau π
.
Ghafra nikapata wazo nitahudumu Bar, πΊ Tena Bar ambayo Mume wangu Jodi upendelea kuketi pamoja na marafiki zake akinywa na kulewa. Nikalifurahia wazo langu sababu huku kwetu Mbezi beach Groceries na Bar zinalipa mno. Haraka nikatoka nyumbani kwangu na kueleka Bar 'KWETU BAR' Baada ya kufika na kupokelewa na Meneja Nilimweleza shida yangu, kuhudumu Bar. Meneja yule mwenye roho ya kilokole hakuwa na pingamo alikubali ombi langu akanitaka siku ya kesho yaani Jumamosi niwepo kazini nikihudumia walevi.
"Kumbuka haupaswi kuja kazini ukiwa umesuka hizo twende kilioni na kuvaa magauni ya twende Kwa Mwamposa." Alinichekesha
"Vaa kimini Bibi, vaa sketi FUPI yenye mpasuo utakaoonesha Chupi na mapaja yako manono." Aliniambia mie nilipigwa butwaa π§π§ nikishanga kanuni zile
"Pakaza midomo yako lips π rangi nyekundu inayonata nata na kuita wateja, kitopu chako kiwe kinabana na pia kioneshe tundu la kitovu chako kizuriπ€£ uhakika uwe umevaa shanga za kutosha kiunoni ilikuvuta wateja sababu wanawake warembo kama wewe ni kivutio Cha walevi. " Alimaliza somo lake, nikamuelewa nakukubaliana na kauri zake nikampa ahadi ya kuwai kazini. Wakati naondoka alinisindikiza Kwa jicho la ngono, matamanio yalimjaa Kisha akatamka.
"Mteja yeyote yule akikutaka kingono mkubali, nikisikia umemkatalia uwe tayari kumwaga unga." Mtume! Nilishangaa mie Hussna kazi za Bar kumbe zinachagamoto. Hapana, ninalitaka gari Millioni tano ni pesa Gani!? Nitazipata tu maana Meneja amenihakikishia kila mwisho wa mwezi nitaondoka na shilingi laki tano. Kwa kadirio la miezi michache tu mambo yangu yatakuwa 'Mwaaππ₯°π'
..............
"Tayari nshapata kazi Babu we!" Nilimjuza Jodi Rafiki yangu, Mume wangu na Huba langu.
.
"Woooo! Usiniambie Daring! Hongera sana," Alinipongeza Wala sikutaka kumwambia aina ya kazi niliyotegemea kufanya zaidi ya kumwambia usiku ndio muda mzuri Kwa mie wake wa Huba kuanza kazi.
"Ushawini Love π " Alinipongeza.
"Kabisa Daring." Niliongea Kwa tabasamu. Jioni Jodi aliniaga anakwenda 'KWETU BAR' kuinjoy yeye na rafiki zake Moja moto Moja baridi πΊπΎπ» PASINA yeye kujua kuwa huko 'KWETU. BAR mie pia nitakuwepo kuhudumia walevi.
"Ungekunywa supu kwanza kabla ya kwenda Ulevini." Nilimtania
"UNATAKA nitapike eeh! NIWE kichekesho? Au nijinyee huko." Alinichekesha akasepa na Prado yake nyeusi PASINA huruma kunihurumia mie mtembea miguu, mkung'utwa Jua la saa SITA.. Ah! Jamani Constructor wanguπΏ.
...............
"Husna Dear hongera sana Kuwai kufika kazini." Sauti ya mrembo nisiyemfahamu ilinikaribisha mie niliyejimwagia mapodali usoni ilibaki kidogo nifanane na Zombi. Nikamtazama mrembo aliyenipokea. Kabla sijanena neno akanena
"Niite Preda Meneja amenielekeza KWAKO, ameniambia nikusaidie iwapo walevi watakuletea fujo." Preda msichana mrembo na mzuri aliniambia mie mgeni niliyevaa kimini, kitopu na skuna zilizosheeni vikuku miguuni.
"Asante Preda nimefurahi kukujua twaweza kusaidiana" Mimi na Preda tukaanza kazi ya kuhudumia walevi, tukawapa pombe na Spirit. Macho yangu yalitua pahali nikamuona Jodi akiwa anakunywa na kuelewa pamoja na rafiki zake, sikujali lakini macho hayana pazia na yeye pia aliniona. Hakuyaamini macho yake alinitzama mara mbili mbili kama vile ameona kiumbe kipya. Mie nikaendelea kuhudumia walevi.
Ghafra nilihisi Kuna mtu amenishika mkono. wangu wa kulia kwa nguvu almanusura nidondoshe Chupa za bia.
"Husna unaafanya nini hapa? kwanini umevaa mavazi yasiyo na sitara Kwa Binti wa kiisalamu?" Jodi alijaribu kuishusha sauti yake isipenye kuwafikia walevi wengine.
"Nipo kazini Babu ninawajibika Tena naomba ondoa mkono wako niendelee kuwajibika." Nilimjibu Mume wangu Jodi
"Husna una akili wewe? Hivi hizi ndio kazi za kufanya mwanamke mtulivu kama wewe?π₯Άπ‘" Aliongea Kwa hasira.
"Sasa kumbe!π‘ Au alitaka nifanye kazi Gani!? Nikaokote makopo jalalani." Nilimjibu.
"Niwache Babu we, walevi wengine wanaitaji huduma yangu." Nikajiepusha na mikono ya Jodi Mume wangu aloyesimama amepigwa butwaa. Nikaendelea na shuhuli yangu ya kuhudumia walevi. Moyoni nikijichamba na kujisemea ' Leo kitanuka nikirejea maskani' ' Atanilazimisha niache hii kazi ya kuhudumia walevi' 'Teh teh teh πππ€© akitaka niache hii kazi basi awe tayari kuniongezea Millioni tano ya kununulia gari niipendayo. La sivyo tutakuwa tukiongozana kuja Bar.' niliwaza Kisha nikaendelea kuhudumia walevi.
...........
Baada ya kuhudumia walevi nilirudi kaunta pale nilipomuacha Preda, Preda aliponiona tu akanisogelea na kuniuliza.
" Shogangu hivi yule Bwana anakutaka!" Aliniuliza akinyosha mkono pahali.
"Yupi tena Shogangu." Nilimtazama Preda Kisha nikageuza geuza shingo kumuona huyo Bwana anayenitaka.
"Si yule pale anayekuangalia sana, yule aliyevaa Form six mwenye tumbole kama pipa."Alimaanisha Jodi.
"Aka! Kwanini umesema hivyo Preda." Nikajifanya kulinogesha gumzo
"Nilimwona alivyokufata akakushika mkono na Kwa jinsi anavyokutazama nahisi hisia zake zote zipo juu yako."
Teh teh tehπ
π nilicheka kishambenga.
"Wamjua Shogangu. " Nikaukoleza ushoga.
"Nisimjue tena yule Bwana mchafu mchafukoge, mchafu na chukizo Kwa wanawaie. Yaani mjaa laana. Kila akimuona Bar maid mpya lazima akamchape huko Guest bubu huwezi kuamini ashatembea na mabar medi karibia wote hapa 'KWETU BAR'.Preda alinishitua Mtima wangu.
"Unamjua vizuri Preda?" Nilihisi macho YANGU yanaanza kutetemeka.
"Nakwambia Jibaba linayaweza matunzo Hilo. Wanaliita Sponsa la Bar. Mimi mwenyewe nishalala nalo Kwa kila mlalo mmoja liliniachia laki tatu." Toba! Preda alikua akimwaga Siri za Mume wangu Jodi PASINA kujua kuwa mwenye Mali naumizwa na habari zile.
"Baya zaidi." Preda aliendelea kunitonesha donda la wivu.
"Kulikuwa na Bar maid mmoja jina lake Mwanaisha. Hilo Sponsa lilipomwona bila kuchelewa lilimjaza Mwaisha mimba. Lilipokujagundua Mwanaisha amebeba mimba yake likamruka kimanga likakimbilia mitini likagoma kulea mimba ya Mwanaisha. Mwaisha alipojifungua akalikamata na kulifosi waende wakapime DNA. kitanda hakizai haramu mtoto aliyezaliwa alikua kopyraiti .
Basi Mwanaisha akaona hapa Dili dilisha akaanza kudai matunzo makubwa makubwa juu ya mtoto aliyezaliwa.Lile jibaba lilipogoma Mwanaisha akalitishia kwenda kuwaona wansheria au kumpa taarifa mkewe" Preda alinipa ubuyu wa kipemba, ubuyu wenye pilipili kumbe mie mwenzie nawashwa ulimi, natetemeka macho, napata mashaka na kuugua mtimani"
"Kwahiyo Hilo Jibaba linatoa matunzo Kwa Mtoto wa Mwanaisha?"
"Sasa kumbe! We haliogopi!!? Linaogopa liapelekwa mbele ya Mwanasheria au mkewe kupewa taarifa Hadi liseme, na taraka juu"
"Mmh!" Nikaguna Kwa hasira. Yaani Jodi hataki kunipatia Millioni tano nikajinunulie gari niinjoi na kujisikia kumbe Kuna kimada amezaa nacho, kimada hicho kinammalizia pesa na mshara wake?
Nikamuacha Preda aliyekua akizipanga panga Chupa tupu za bia pale kaunta nikamwendea Jodi alieonekana Hana amani siku hile
"Kwahiyo kelele zote zile za kunitaka nifanye kazi ya pili kumbe mwenzangu Ulitaka pesa nitakayolipwa upeleke Kwa kimada wako Mwanaisha kimada uliyezaa nae?" Niliongea Kwa hasira na sauti kubwa karibia walevi wote walioshituka wasikie.
"Hapana babyπ§ hapana. I will explain..... Nitaeleza baby" Jodi akitetemeka sana.
"Utaeleza Nini Malaya nyoko wewe? Utaeleza Kwa Mwanasheria. Nakwambia Jodi NATAKA taraka yangu." Nilipiga Tena kelele zilizowashangaza wale walevi. Sikutaka kumpa nafasi Jodi hasira zilinikaba kila pande ya shingo yangu nikaondoka pale 'KWETU BAR' nimefura mahasira sitaki tena kulisikia jina la Jodi.
..........TCHAO....
No comments:
Post a Comment