Sehemu ya pili
BEATUSI.
Mara baada ya kuanuwa matanga Shaabani na Nela waliwekwa chini ya mikono ya baba yao mdogo Beatusi watoto wale walindwe, wakuzwe wapewe mahitaji yao yote ya kibinadamu, hapo mwanzo Beatusi alijifanya kuwa ni baba bora kwa hawa watoto Shaabani na Nela. Mlevi huyu asiye na kazi maalumu ya kufanya alijaribu kuwadekeza ili kuwapendeza wale watoto wa Msubisi na Naomi watoto wakiwa ni wenye majonzi sasa majonzi yao yalianza kufutika taratibu, sababu Beatusi ali ‘act’(alitenda) kama baba bora kwao. Mara taapu baada ya miaka miwili ya madekezo na mapendeleo kwa wale pacha, hali ya upepo ilianza kubaadirika kwa kasi ya ajabu hii ilitokana na ujio wa Neema aliye olewa na bwana Beatusi.
Neema hakuonesha upendo, mahaba na mapenzi yake kwa wale watoto tuseme aliwachukia chuki iso na kipimo, huyu binti wa Kikurya kuolewa na Mnyakyusa kwa sasa yeye ndiye mama mwenye nyumba na ukitegemea mama mwenye nyumba ni mtawala, hataki mchezo akisema amesma, akitenda ametenda, akikaripia amekaripia, Neema akajiona amefika. Kutoka mara kuja Dar es saalam sio pafupi ni parefu, ajabu ati mama wa kambo awakute watoto wa mzazi mwingine, mbona palichimbika, kutwa kuchwa Neema alipitisha bakora, Stick na mboko kwenye miili ya wale watoto pacha. kutwa kuchwa akiwatusi matukano mazito, makubwa yasiyo faa kwa wale watoto wadogo kuyasikia.
Nakwambieni ni matukano ya nguoni matukano ambayo Shaabani na Nela hawapaswi kuyasikia sembuse kuyasikiliza. Vipigo havikukoma, njaa ilizidia watoto wakakonda na kukondeana. Ajabu kila siku afya zao zilidorola na Neema hakukoma aliendeleza mateso makuu aliendelea kuwapiga kwa maboko na mastick, watoto walilia wakawakumbuka baba na mama yao.
Siku walipomweleza baba yao kipenzi Beatusi, Beatusi aliwasikiliza na kumuonya mkewe asiendelee kuwatesa watoto wake, Kuona aaah! Kumbe mumewe anawatetea sana wale pacha Neema akayapunguza mapenzi yake kwa mumewe, akawa hamjari wala hamthamini mumewe, kutwa kuchwa akimtajia visababu vya kuwanyima raha wale watoto pacha. Hakukomea hapo, Neema alizidisha maringo akilalama ati hawezi kuishi pale nyumbani pamoja na wale pacha na kama mumewe anampenda basi afanye kuwaondoa pale nyumbani haraka iwezekanavyo.
Beatusi hakumsikiliza mkewe bado alikuwa bega kwa bega na watoto wa kaka yake Msubisi, hakutaka asikie habari za kuwafukuza watoto wa kaka yake, roho ilimuuma, roho ilimchoma, roho ilimsuta na kumkosoa, alikuwa na huruma sana kwa wale watoto aliumia kwa ajiri ya watoto wake, aliumia na kulia machozi pale alipowakuta wamepigwa na kuumizwa ni wagonjwa pia. Aliwapa chakula, aliwaogesha na kuwajari hali ambayo ilizidisha wivu, chuki na hasira kwa mkewe Neema.
Sawa Beatusi ana moyo wa huruma, tatizo lake ni ulevi, tena ulevi wa kupindukia, ulevi ambao kwa bahati mbaya umemnyima kazi nzuri ya kuyaboresha maisha yake, kuwekeza na kukumbuka juu ya maisha ya baadaye (future life) anazitegemea zile pesa ambazo Msubisi na Naomi waliwekeza kwa ajiri ya watoto wao anategemea kuyauza yale magari ambayo Msubisi na Naomi waliyatunza kwa ajiri ya watoto wao anategemea kuzipiga bei hizi nyumba mbili pamoja na horofa ambayo Msubisi na Naomi wameacha kwa ajiri ya watoto wao pacha Shaabani na Nela
Beatusi hafanyi hivyo ati kwa sababu moyo wake unamshurutisha kufanya (kuuza nyumba na magari ambayo ni urithi ulioachwa kwa ajiri ya shaabani na Nela) bali anafanya hivyo kwa sababu ya kushurutishwa na mkewe mpenzi Neema.
Itaendelea
No comments:
Post a Comment