Friday, October 4, 2024

Ndoto ya kutisha.. sehemu ya nne

 

4


Ndoto ya kutisha

SEHEMU YA NNE

 Nilippozinduka nilijikuta ndani ya andaki, nimelazwa kitandani, nikiwa nimevalishwa mavazi na maumivu yakiwa yamepungua kwa uchache wake, kwani nilikuwa kama mtu aliyepewaa huduma ya kwanza. Niliangaza huku na kule nikaiona miale, miale miwili ya moto inanijia, miale ile ilileta mwanga, nikagundua nipo mapangoni. Miale ile ya moto  ni mwenge uliyoshikwa na wanaume wawili wakimwangazia njia mwanamke  mmoja aliyeonekana kupewa heshima zote.

             Kundi lile la watu watatu lilimfikia kiumbe mtukufu yule aliyekuwa akimulikiwa njia, ni yule mwanamke katiri aliye ghairisha kifo changu. Wanaume wale vijakazi hwakuwa Wangunjwasi niliowatambua kwa mionekano yao haswa idadi ya makovu waliyo nayo na  mavazi waliyoyavaa hawakuwa na alama za makovu maalumu ya kingunjwasi na walivalia mavazi sare na mimi. Lakini na wao walikuwa na ulemavu mbali mbali.

  Yule mnwanamke aliniaangalia kwa hasira ksha akaniambia;

“Piseletigo kweila   pwiyageropitoku –swa,  pyekeriso

Lukanelolukaku   pgi-pgo-pswairezimu, pumpu

Pumnpyaswilahegi   pgoti-pommkwiranyizapi ppesai”

( Nimekuokoa usibanikwe jikoni, kwa kusudi mojatu, uungane na hawa wenzako kunitengenezea jeshi, ninahitaji kuwapindua wazee wote wa hapa niwe kiongozi wao). Alipoweka nukta nilikuwa nimelowa tepe tepe kwa mate yake yanukayo.

               Nilimjibu kwa kumuomba animalizie kuniua kwani hapa nilipo nipo mguu mmoja hauaini mwingine umautini siwezi kujipigania mwenyewe nitampiganiaje mtu? Nilimwambia “Nashukuru kwa kuniongezea masaa ya kuishi naomba uniue.”


                Aliniita kwa jina jipyaJigani kisha akaiambia kwa kinjwasi ya kuwa bado nino uwezo, bado ninayo nafasi ya kujisimamia na kuishi tena kwa furaha, nikamkatalia kwanza siitwi Jigani safari hii nikiwa na mzuka hadi nikafanikiwa kukaa kitandani kwa sekunde kadhaa alafu nikadondoka, aliita kwa nguvu Powenzeo (jeshi) ghafla mamia kwa mamia ya wanajeshi wake wakamkusanyikia, wakatoa heshima zao wakamsujudia wakanyamaza kimya kusikiliza. Akaendelea kwa kusema “leo tumempata Jigan tuliyekuwa tunamsubiri sasa tayari kwa vita alinyamaza akaninyoshea kidole akawaambia wale wanajeshi “Jigan!!” wote walipig kelele za shangwe


 akaja pale kitandani kwangu akasema “ Umechaguliwa na Miungu yangu kuwa Jigani yaani mwanaume baada ya Malkia mimi kwenye serikali yangu ijayo lakini ni lazima ushiriki vita ya kuwaangusha wale wangunjwasi wazee ninao uwezo wa ajabu nitakurudishia viungo vyako vyote huwa nafanya hivyo nikiwahitaji wanajeshi wangu waende vitani ila wewwe Jigani nitakupatia milele.


                   Alipomaliza kuongea hivyo, nilikuwa na moyo mwepesi kumkubalia kwani viungo vyangu vyote vilivyopotea vilinirudi kasoro nywele, nilisimama kijasiri nikaonesha kichwani kama mtu anayeuliza huku vipi? Nywele zikaanza kuchomoza toka kushoto kwenda kulioa zikiwa kati kati ya kichwa kwenda kulia mamia ya wanajeshi walitenganishwa kulia na kushoto tena Joka likapita juu yao. Moja kwa moja likatujia mimi na yule mwanamke kwa hasira kuu likatuangalia.


                 Na hapo ndipo niliposhtuka toka usingizini na kupiga ukelele hadi msimamizi wa mtihani akashtuka na wanafunzi wenzangu wakaniangalia. Kamwe sitoisahau ndoto hii ya kutisha niliyoiota ndani ya chumba cha mtihani wa kidato cha nne kwennye somo la Hisabati

Mwisho.


No comments:

Post a Comment

ZEE LA ZAMANI

  SEHEMU YA KWANZA. HOTELINI Ndani ya Hoteli Paradiso katikati ya Jiji la Mzizima (Dar es salaam) ZEE LAZAMANI akiwa na Mwanagenzi wake JAN...