Friday, October 4, 2024

KUCHEPUKA SIO dili.. sehemu ya nne




Sehemu ya nne


SIKIO LA KUFA.  

   

                                                                                                  

                   Kawaida ni kama sheria, mwonja asali  haonji mara moja, huchonga mzinga, hivyo ndivyo bwana Mawe alikua na masikio makubwa yaliyozidi kichwa, hakusikia la mwadhini au la mkwea nazi, alikua ni mgumu kuelewa, alikua sawasawa na sikio la kufa  halisikii dawa kila alipotoka nyumbani kwke alipitia Buzi Bar kuvinjari na  kimada wake Rehema wakati Bosi anamfuatilia ili ajue mwenendo wake nyumbani kwake Mawe hakuacha pesa za kutoshelezea huduma za kifamilia.

                  “Eeeh! Niambie hivi unataka nikununulie kitu gani muda huu?” Mawe alimbembeleza Rehema.

                  “Ninataka chips kuku mzima na mayai.” Rehema alideka zaidi.

                  “Hilo tu au kuna jingine?”

                  “Hapana baby ninataka bia na konyagi mzinga  mkubwa.”

                  “Ok. Babya mwite mhudumu akuhudumie.” Rehema alimwita mhudumu akaagiza vyote alivyo vitaka na hata walipo maliza kula wawili hawa walielekea nyumba moja ya kulala wageni iliyo karibu na ile bar ya Buzi ilikua yapata saa tano usiku, simu ya mkewe iliita.

                  “Ni nani huyo anayepiga simu nyakati hizi Baby tukiwa tumelala?” Rehema alimuuliza Mawe

                  “Ni mke wangu, sijui ana shida gani embu ngoja nipokee.”

                  “Achana nae huyo bwana.” Rehema alionekana dhariri, shairi amelewa. Mawe aliongea.

                  “Acha nipokee ili nisikilize ana semaje.” Akaiweka ile simu mkononi mwake.

                  “Hallow!!”

                  “Hallow, mume wangu, uko wapi wanitia wasi wasi usiku wote huu,”

                  “Nipo njiani ninakuja kuna foleni kubwa sana my wife Mawe alimdanganya mkewe.

                  “Lakini mume wangu, toka saa nane mchana hadi saa hizi inaelekea saa sita usiku wa manane bado ujafika nyumbani.”

                  “Mkewe alikata simu, ilihali moyoni mwake, hana amani anamuwaza mumewe.    Bwana  mawe alipokata simu yake alianza kuongea na mchepuko wake Rehema

                  “Mke wangu ana shida huyo.”

                  “Wala usingelipokea simu yenyewe” Mchepuko aliongea.

                  “Acha nirudi nyumbani”

                 “lakini Baby haujalipia kile chakula nilichokula  pale  Buzi bar”

                 “Aaah! chukua hii elf Hamsini ukalipe alafu chenji inayo baki iweke mfukoni iwe kwa matumizi yako binafsi sawa.”

                 “Sawa Baby wangu mwaaa!” Rehema alimchumu bwana Mawe

                 “Una mambo wewe.” Mawe aliongea kwa furaha

            ###############################

Saa nane usiku, Mawe alirejea nyumbani kwake na kugonga mlango wa nyumba yake.

                 “Hodi! …hodi!…. Hodi! Mke wangu” Mawe alikua  amelewa na kupepesuka, mkewe alishituka kutoka usingizini akagutuka apate kwenda kumfungulia  mumewe.

                 “Mke wangu eeh!” Mawe alimwita mkewe “ Abee mume wangu, ninakuja” mke wa mawe aliitika kivivu vivu na kutoka usingizini akaenda kufungua mlango  

                 “Jamani baba watoto mbona umelewa hivyo, ajabu umekua ukichelewa kuja nyumbani kila ikiwa leo tizama sasa ni saa nane na nusu usiku, ulikuwa wapi mume wangu.” Mke wa Mawe aliuliza kwa upole.

                 “Embu niache nikapumzike, suala la kulewa na kuchelewa vina mahusiano gani hapo.”  Mawe alijibu kwa ukari.

                 “Sio hivyo Mume wangu, kazi gani unayonyafa ikufanye kila siku unachelewa kurudi nyumbani, baya zaidi sina furaha ya ndoa, sipati haki yangu ya ndoa au kuna mwana…….” Mume akamkatisha mkewe kwa kuogea

                 “Nilikwambia foleni bwana eeh, niache nikalale.” Mawe aliiingia chumbani kwake, akajitupa kitandani  kwake puu, pasina kuoga pasina kula akapitiwa na usingizi.

                 “Looh! Mume huyu! Nguo zake zote zinanukia marashi ya mwanamke, au atakuwa na kimada huko njee? Lakini ngoja nimfuatilie taratibu, taratibu pole pole ndio mwendo, maneno mengi hula vitendo niwe makini kwa hilo.” Aliongea mke wa Mawe yeye na moyo wake, akijaribu kumtomasa tomasa mumewe aliyelala fofofo usingizi wa pono, haelewi wala hajielewi.

             ####################################

Kama kawaida  asubuhi jogoo aliwika mkewe alifanya juhudi kumuamsha mumewe aliye lala fofofo

                  “Naomba uniambie jana ulikuwa wapi mume wangu hata ukachelewa namna ile?”

                  “Hayakuhusu embu niache mie nielekee kazini.”

                  “Hayanihusu kivipi? Jana umeondoka nyumbani pasipo kuacha ela za matumizi madogo madogo alafu leo unasema hayanihusu, haujui watoto wamekula nini? Haujui watoto anavyo endelea lakini kusema hayanihusu hapo ndipo unapo pajua eeh!” mkewe alibwata lakini Mawe hakujali kilio cha mkewe,

                  “Chukua hii shilingi elf tano iwatoshelezee kwenye mahitaji ya leo”

                  “Mume wangu umepandwa na wazimu nini? Yaanii badala ya ya kunipatia shilingi elfu  ishirini unanipa elfu tano hivi je shilingi elfu tano itatoshelezea mahitaji ya nyumbani pamoja na kulipa madeni tunayodaiwa kila siku, kwanini wanitesa hivyo mume wangu?”

Mawe hakumjibu mkewe alichofanya yeye ni kuondoka na kurejea kazini.


No comments:

Post a Comment

I promise you

   I PROMISE YOU. (NINAKUAHIDI.) SURA  YA KWANZA. UBAYA WA POMBE. “Umenizingua job, umenizingua kwa muda mrefu sana mpenzi wangu…….kwanini l...