Friday, October 4, 2024

KUCHEPUKA SIO dili...sehemu ya pili


               


Sehemu ya pili

TAHADHARI.

Juma tatu ya leo Bwana Mawe alimuaga mkewe, akamwambia asingelichelew kurejea kutoka kazini lakini yote tisa kumi, bwana Mawe alikua  akimvisha kilemba cha ukoka mkewe, alimficha ilihali akijua fika kuwa yeye sio mkweli wala yeye sio mwaminifu.

               “Kwa heri mke wangu mimi ndio naelekea kazini, ninakutakia mchana mwema wenye mafanikio, “ Akilegeza regeza tai aliyo jifunga ili ipate kukaa vema.

               “Sawa mume wangu ninaomba usichelewe kurejea, mpenzi ukumbuke kuwahi kurejea nyumbani ujumuike na familia.”

              “Ok my wife, I love you all, ninawapenda wote. Ilove you so much, ninakupenda sana, ninakuahidi jambo moja zuri la kupendza sintachelewa kurejea, nitawaletea watoto zawadi wazipendazo.” Akalibeba begi lake mkononi huyo tayari kuondoka.

              “vipi mume wangu mbona unaondoka pasina kuacha pesa za matumizi ya  hapa nyumbani Bi. Neema alimkumbusha mumewe.

              “Pesa  za matumizi zipo ndani ya lile kabati letu la nguo, tafadhari uzitumie vizuri, ujuwe namna ya kuzigawa kwa ajiri ya matumizi ya nyumbani.” Mawe alimpiga mabusu mawili matatu mkewe kisha akaondoka.

Mkewe alijua fika kwamba ile shilingi elf tano aliyo kabidhiwa isingelitosha kwa ajili ya matumizi ya pale nyumbani hata hivyo bwana Mawe aliweka kiasi cha shilingi elfu hamsini kibindoni kwa ajili ya starehe zake.

 Kwa vile aliondoka nyumbani kwake Sinza kijiweni yapata saa mbili  aubuhi, aliweza kuwasili kazini kwake yapata saa tatu na nusu kwa sababu ya foleni na msongamano wa magari. Alipofika kazini kwake, Secretary alihitaji kuongea na yeye mawili matatu.

              “ Habari za asubuhi, bwana Mawe.”

              “Nzuri tu secretary wangu, je hawajambo wote waliopo kazini?”

              “Sio kwema sana bwana Mawe.”  Asha Secretary alimjibu bwana Mawe kwa ufupi.

              “Una maana gani kusema hivyo bibie?!” Bwana mawe alidadisi kidogo.

               “Bosi amenipa ujumbe nikufikishie.”

               “Oooh! Ujumbe ni ujumbe gani ten huo? Bwana mawe alikua na shauku ya kutaka kujua juu ya huo ujumbe.

               “Labda ungeliketi hpo chini kwenye kiti ili nikutupie ujumbe wako.” Asha aliongea.

               “Ok. It’s not bad.” Bwana mawe aliketi kwenye moja ya viti viwili vitatu vilivyo mbele ya ile ofisi akisubiri kusikia  maneno mawili matatu kutoka kwa Secretay.

               “Bosi amesema hapendezwi natabia zako, nadhani kufika hapo umenielewa.”Asha aliongea kama vile anamjua kwa undani zaidi yule Bwanamkubwa.  

               “Tabia, eeh! Tabia gani haswa.?” Mawe alihitaji kuambiwa.

               “Nisingependa kukufunulia jungu, nikitambua kuwa mwenye macho ahambiwi tazma.”

                  “Kwa kifupi Habari yenyewe ni hii,” Asha alianza kumweleza bwana Mawe.      “Bosi anayajua machimbo yako yote, angependa kusikia umejirekebisha kabla maji hayajamwagika, kabla maji hayajazidi unga.” Asha aliongea kwa mafumbo.

                   
                  “Asha una manisha nini haswa, sipati picha na uhalisia wa maneno uyanenayo.” Mawe alihoji

                  “Mimi binafsi bosi hajanieleza kwa undani zaidi, hata hivyo kama una maswali zaidi ingelikuwa vema kama utamuona bosi mwenyewe anaweza kukusaidia.” Aliongea Asha akaendelea kuchapisha chapisha kazi za kiofisi.

                   “Bosi yupo Ofisini?” Mawe alihitaji kujua.

                  “Hapana bosi hayupo ofisini, amekwenda Kipepeo Hoteli kuonana na mwekezaji, kuna mambo ya kusaini mikataba.

                    “Je alisema atarejea Ofisini au atapitia nyumbani kwake?”

                    “ Alisema atarejea jioni ya leo.”

                    “Sawa ninashukuru kwa taarifa.”

                    “Ok. Have a nice job.” Asha yule binti mmoja mrefu, mwembamba, mrembo, chotara wa kiarabu na kipemba aliongea. Mawe ni mwanaume mwenye umi wa miaka 35 mtu mzima mwenye masharubu, ana umbo la miraba minne aliingia Ofisini kwake akaendelea na kazi zake, kichwani alikua akifikiria  kwa kina yale maneno aliyo nena Asha.

                     Saa nane mchana ni muda wa kumaliza kazi za kiofisi mara baada ya kumaliza kazi za kiofisi Mawe hakuitaji kurejea nyumbani kwake mapema aliamua kumsubiri Bosi wake anene  pamoja naye mara akirejea, bosi hakurejea.

                     “Sijui atarudi huyu bosi, mmmh! Ngoja ngoja yaumiza matumbo Mawe aliendelea kumsubiri bosi pasina darili za kumuona. Ilipotimu saa mbili usiku Mawe alikata shauri la kurejea nyumbani kwake, akajipa matumaini kwamba kesho angelimwona mkubwa wake.

Alirejea nyumbani kwake ni mwingi wa mawazo, amenuna kweli, mashavu yake yalionekana kutuna kama vile yameunguzwa  kwa amfuta ya kula, hana salamu, hana neno, moja kwa moja alipitiliza na kuingia chumbani kwake, kufika huko akajibwaga na kujitupa kama gunia lenye mpunga.

                    “Habari za kazi mume wangu? Pole na majukumu ya leo.” Bwana Mawe kimya.

                    “Mume wangu kwanini haunijibu salamu yangu tena?” Mama alimshangaa baba alivyoganda kama barafu mara ile bwana Mawe alishituka na kugutuka kutoka kwenye dimbwi la mawazo.

                    “Eeeh! Aaah! Unasemaje mke wangu?” aliongea na kumtizama mkewe kwa mshituko

                    “Mume wangu nina kusalimu, ninakuuliza habari za kazi?

                     “Nzuri tu mama watoto.”

                     “Pole na majukumu  mbali mbali ya huko kazini,”

                      “Asante sana mke wangu.”

                      “Mbona ninakuona kama haupo sawa kifkra mume wangu umekumbwa na nini?”

                      “Nipo sawa mke wangu.” Mara ile Bwana mawe alitoka na kwenda bafuni kukoga na baada ya kukoga alirejea chumbani kwake akalala, mkeweaijishika tama kutokana na kuona mabadiriko makubwa kutoka kwa mumewe.

                      “Ana nini mume wangu siku ya leo, mbona anaongea kama yupo ndani ya mawazo mazito, hajala, hajanywa siku nzima ya leo, oooh jamani! A mepatwa na kadhi gani mume wangu? Mmmh! Makubwa haya madogo yana naafu.”

Hata hivyo kesho yake bwana Mawe alichelewa sana kuamka apate kwenda kazini kwake. Kama sio kuamshwa na mkewe basi angeliendelea kuuchapa usingizi mzito hata ufike mchana wa siku ile.

                   “Mme wangu, mme wangu” mkewe alimuamsha mumewe aliyelala usingizi wa Fofofo.

                   “Eeeh! Nini tena mie niko bize nimelala bwana.” Mawe alijipangusa tongo tongo machoni.

                   “Mme wangu tizama leo umechelewa sana kuamka, sasa ni saa tatu yaelekea saa nne, sijui utamjibu nini bosi ajapo kukemea kwa uchelewaji huu.”

                   Bwana Mawe akakurupuka pale kitandani. “Mungu wangu we! Ama kweli usingizi mtamu na mnono.” Shagalabaga, hakuoga wala hakupiga  mswaki moja kwa moja alivaa ovyo ovyo  akazichana nywele zake ovyo ovyo na kukimbilia kazini kwake, huku nyuma akimuacha mkewe anaishangaa hali ya mumewe, hali ambayo ajapata kuiona tangu wafunge ndoa ya kanisa.





No comments:

Post a Comment

I promise you

   I PROMISE YOU. (NINAKUAHIDI.) SURA  YA KWANZA. UBAYA WA POMBE. “Umenizingua job, umenizingua kwa muda mrefu sana mpenzi wangu…….kwanini l...