MISS YOU LUPITA.
Nimeishikila picha ambayo mie na Lupita tulipiga yapata mwaka 2014 kwenye harusi yetu, picha ile nzuri ilituonesha sisi wawili tuliopendana, tukiwa ndani ya furaha kuu, furaha ya ndoa yetu, ndoa iliyobarikiwa na Mwenyezi Mungu. Japo ilivunjika kutokana na wivu pamoja na tamaa. Wivu wa RAISI ANTONIO wivu uliotokana na TAMAA YA MPENZI WANGU LUPITA. kuondoka kwake moyoni kwangu kulinifanya niwe na upweke mzito ulionifuata.
Harusi yetu haikuwa harusi kubwa sana, ilikuwa ni harusi ya kawaida, Simple Marriage, hatukuhitaji kutumia gharama nyingi ili kuifanya harusi yetu inoge, na kupendeza. Gharama zile za haba na haba zilifanikisha harusi yetu, ukitegemea hali za wazazi wetu kiuchumi hazikuwa nzuri.
Mie MIKA pamoja na mpenzi wangu LUPITA tulikutana chuo kikuu cha DAR ES SAALAM, MLIMANI, tukapendana moyoni, tukayajenga mahusiano bora na yenye malengo ya kuwa pamoja mbele ya safari yetu ya maisha. Hata baada ya kuhitimu elimu yetu ya chuo hatukuhitaji kupoteza muda tulihitaji kuishi pamoja kama mke na mume na hatimaye lengo letu lilikuja kutimia siku ile siku moja tamu siku tuliyovishana pete mie na Lupita, tukaandika cheti cha ndoa mara baada ya kula kiapo kitakatifu.
Lupita akawa wangu na mie nikawa wake, wawili tukapendana, tukapendana kweli, tukapendana mapenzi moto moto na uzuri wake, hatimaye ndoa yetu ikaleta majibu, Lupita akashika ujauzito akajifungua mtoto wetu wa kwanza wa kiume tuliye mpa jina MALIKI –SHUA.
Upendo ukaongezeka ndani ya nyumba yetu,furaha ikazidia, ndani ya familia yetu, wakati wote mie na Lupita tulikuwa ni watu wenye furaha na Bashasha na vicheko, tena mapenzi yetu yakaongezeka. Hakuna mfano, nilimpenda Lupita na yeye alinipenda pia hakuna siku ambayo sie tulikosa raha furaha na amani.
##############################
Naitwa MIKA, jina nililopewa na wazazi wangu wapenzi walionileta hapa duniani,nina umri wa miaka 27 (ishirini na misaba) wakati Lupita mke wangu mpenzi ni mwenye umri wa miaka 23 (ishirini na mitatu, tumepishana miaka minne tu. Nimesomea uinjinia wa vifaa vya Usafiri wa anga, yaani Ndege nilitarajia kuwa Injinia mkubwa ndani na nchi ya BARA.
Kipindi mie mika nasomea ulubani Mpenzi wngu Lupita alikuwa ana akichukulia Udakta naye akitegemea kuwa Dakta mkubwa ndani na nje ya nchi ya Bara. Kwa Mungu yote yanawezekana. Hatimaye mie na Lupita wangu tulitimiza matamanio ya mioyo yetu Lupita akawa ni Dakta mkubwa ndani ya nchi ya BARA wakati mie nikawa Lubani wa kutegemewa ndani ya nchi ya bara.
Mwaka 2018 ndoa yetu ilikuwa na miaka mitano ya Baraka, ndani ya miaka hiyo hiyo mitano ya mapenzi Lupita wangu akapandishwa cheo cheo kikubwa cha Udakta mbali na kupandishwa cheo lupita alipewa barua ya kumtaka awe nmtumishi wa IKULU, wakati huo alipaswa kuwa Dakta wa kumtibia Raisi Antonio, raisi wa nchi ya BARA.
Cheo cha mke wangu kiliifanya nyumba yetu iwe ni nyumba yenye wingi wa amani na furaha tele, kwa mke wangu kupewa cheo kikubwa kama kile ilimaanisha kuwa malipo ya kazi zake zote yataongezeka na kuongezeka kwa hayo malipo kutatufanya sie wanafamilia tuwe na maisha ya kifahari , maisha bora zaidi, maisha matamu kama pipi, maisha yenye nyingi heri na Baraka.
Tulianza kuyaona hayo maisha matamu, nyumba yetu tuliyo anza kuijenga ilikamilika kwa muda mfupi sana mara baada ya Lupita mke wangu kupandishwa cheo. Tuliweza kununua mashamba makubwa mawili matatu, tukawaweka wakulima watulimie mazao ya chakula. Mwanetu Maliki –shua tulimpeleka moja ya shule bora zinazotoa elimu kwa kutumia lugha ya kizungu (English Medium School) uzuri wake miaka ilivyoendelea kukatika tukanunua magari mawili matatu ya kifahari.
Haki! Maisha mazuri ni lazima uwe na elimu, kadri tunavyozidi kujituma ndivyo tunavyozidi kuyaona matunda yatokanayo na juhudi zetu, malengo yetu pamoja na matarajio yetu yanatimia kidogo kidogo. Binafsi ninawashauri vijana wenzangu waishike sana elimu,elimu ni ukombozi, elimu ni ufunguo wa maisha magumu yenye shida, tabu , dhiki, machungu na maumivu.
MAISHA yetu yakawa bora zaidi, na uzuri wa hayo maisha ni kwamba Lupita mpenzi mke wangu alikuwa akilipwa mshahara, marupu rupu na posho zingine vizuri sana kwa muda na kwa wakati maalumu pasina kikwazo chochote.
Nyumba yetu haikupata kuwa na kiu, njaa au shida za ulimwengu, Sio jambo dogo kwa Lupita kupewa cheo kikubwa kama kile, cheo cha kumtibu mkuu wan chi, nchi nzuri ya BARA, Raisi Antonio, kiongozi mkuu wanchi, kiongozi aliyedumu madarakani kwa zaidi ya miaka 30 angali bado ana hamu na uchu pamoja na tamaa ya kuwa Raisi wa milele katika nchi ya BARA
Mwaka wa sita, mwaka wando ya mimi na Lupita ni mwaka mmoja baada ya Lupita kupandishwa cheo na kuwa Dakta wa kumtibu Raisi Antonio, mwaka huu niliuona ukianza vibaya ndani ya ndoa yetu, lupita mke wangu alianza kubadirika badirika na kuonesha tofauti ndogo ndogo ndani ya nyumba yetu., upendo wake kwangu ulianza kupungua, mapenzi yake kwangu yalianza kuwa hafifu.
Zamani, kabla Lupita hajapandishwa cheo, alikuwa ni mwanamke wangu mcheshi sana, mwenye tabasamu na furaha kila wakati, akicheka cheka pamoja na mimi, ajabu ndani ya huu mwaka wa sita, hacheki pamoja na mimi wala hawi karibu na mimi. Zamani Lupita alikuwa na kawaida ya kuwahi kurejea nyumbani, alikuwa akirejea mapema sana, siku hizi anachelewa sana tena akirejea lazima anieleze kuwa kazi zimekuwa nyingi ofisini kwake, ameongezewa majukumu, zamani alikuwa akimtibia Raisi Antonio pekee lakini siku hizi amekuwa akiwatibia watoto wa Raisi, mke wa Raisi pamoja na wafanyakazi wengine wa Ikulu.
Sijui kweli alikuw na hayo majukumu, binafsi sifahamu sababu sikuwa na ruhusa ya kwenda Ikulu, mie pia sio mtumishi wa Ikulu, sio rahisi kujua mengi yanayohusu ile Ikulu, nilikubaliana na mke wangu Lupita kadri alivyonena.
Kwanini nimtilie mashaka mke na mpenzi wangu? Sikuona kama itakua ni jambo la Busara kumtilia mashaka yule nimpendaye, yule ninaye mwamini, yule wangu wa moyoni, yule tuliyeandikiana cheti kwa pamoja, yule tuliyefunga pingu za Maisha. Nilimpenda Lupita sikutaka kumuumiza kwa wingi wa maswali yanayochosha japokuwa mwenendo wake kwa sasa unaniumiza, unaninyima raha na furaha, sijisikii amani ninaumia sana.
Mke wa Raisi Antonio anaumwa! Yes, mkewa Raisi Antonio ni mgonjwa habari Hizo nilizipata ndani ya vyombo mbali mbali vya Habari ndani ya nchi ya BARA, amepatwa na ugonjwa wa KANSA YA KOO, hawezi kula, hawezi kunywa yu mahututi juu ya kitanda chake ni miezi mingi sasa.
Lupita mke wangu amechukua jukumu la kumuhudumia, Lupita anaporejea nyumbani kwangu uniambia machache juu ya afya na uzima wahuyu bibi, mke wa Raisi
“Afya yake imetetereka, afya yake imeyumba, afya yake haileti matumaini……..” Haya ni baadhi ya maneno ambayo Lupita afya yake imeyumba, afya yake haileti matumaini……..” Haya ni baadhi ya maneno ambayo Lupita mke wangu aliniambia juu ya maendeleo ya afya ya GRACE First lady, mke wa Raisi Antonio,
“Muhimu kumuombea kwa mungu mke wangu, kwa sababu mbele za Mungu hakuna jambo linaloshindikana, atapona tu, atapona kwa imani.”Niliongea na kumtia faraja Lupita mke wangu aliyekuwa na kazi kubwa ya kumtibia Rais Antonio.
“Sawa ninakubaliana na wewe mpenzi lakini mimi ni Dakta, ninajua fika kuwa mke waRaisi HATOPONA ATAKUFA TU, kwa sababu ugonjwa wake ni uugonjwa unaokatisha tamaa, amedhoofika sana, hawezi na tena………” Lupita alishindwa kumalizia kauri yake alikuwa ni mwingi wa mawazo.
“Natena nini tena?” Nilimuuliza Lupita mke wangu tukiwa sebuleni tunatizama Televisheni.
“Hali, hanywi, hapati usingizi, amekonda na kudhoofika.”
“Duh!” Nilisikitika.
“Chakula chake ni uji uji hata kama angelipikiwa ugali, ugali huo lazima usagwe na kuwa uji uji.” Lupita alinieleza nilisikitika.
“ Tumuombee kwa mwenyezi Mungu, Mungu ndiye mpangaji wa mambo,, Mungu ndiye mpanguaji wa mambo, Sisi wandamu ni mali yake, Sisi wanadamu ni kondoo wake, kondoo wa malisho yake, Sisi wanadamu ni mapenzi yake Mungu, Mungu ni mwingi wa heri huruma na mapenzi, Acha Mungu aitwe Mungu.” nilichangia hoja. Mie n a Lupita tukawa ni wenye shaka juu ya Afya ya Raisi Antonio.
Miezi misita baadaye taarifa juu ya kifo cha Grace, FIRST LADY na mke wa Raisi Antonio zilisambaa ndani na nje ya nchi ya BARA, vilio majonzi na machungu, vilisikika ndani na nje ya nchi ya BARA, wengi waliomjua Grace walilia sana, sababu Grace alisifika kwa upole, huruma ukarimu na moyo wenye upendo. Nchi ilikuwa ndani ya Simanzi la kuondokewa na mtu muhimu ndani ya BARA
Mimi pamoja na mke wangu lupita tuliudhuria msiba wa First lady Grace, Viongozi wa Serikali, wananchi pamoja na watu wenye hadhi na vyeo vyao Serikalini walihudhuria msiba wa First Lady. Tukashirikii kwenye Maziko ya mke wa Raisi Antonio na baada ya siku chache kila mtu alishika majukumu yake. Mie Mika nikashika jukumu langu la kuiongoza ndege, Mke wangu Lupita akashika jukumu lake la kiutabibu wakati mwanetu Maliki –Shua aliendelea na masomo yake darasani, uzuri wa mwanetu alikuwa na bidii na juhudi darasani.
Inaendelea
No comments:
Post a Comment