SURA YA TATU
DIMBWI LA MAWAZO.
Usiku wa leo mara baada ya Bwana Cheppe kutoka Hospitali anamwacha mkewe Cheusi yu mgonjwa hajiwezi tena hawezi. Mawazo mengi yanatibua mtima wake, anawaza na kushindwa kuwazua, anajaribu kutafuta suluhisho la juu zaidi namna gani ataweza kukabiliana na changamoto hii kubwa iliyombele yake. Mganga wa jadi anajaribu kumuaminisha kwamba mkewe amerogwa, amelaaniwa na kutupiwa mkosi. Wakati huo huo Dakta wa hospitali ya Mkuranga amemwambia asiamini sana maneno yanayozungumzia ushirikina. Oooh! Cheppe Yupo njia panda angali hajui afanye nini au aanzie wapi kukabiliana na hili zigo zito linaloumiza kichwa chake..
Je afanye kuzikata nyeti za mtoto mwenye tatizo la ngozi(Albino)? Duh! Huu ni mtihani, hajui ataanzaje anzaje, ukitegemea huu mtihani una mambo mawili yanayomchanganya, kwanza hajawai kukifanya kitendo hicho. Kitendo anachotarajia kukifanya kina madhara yake, kubwa kuliko yote ni pale atakaposhuhudia kifo cha huyo mlemavu wa ngozi. Anaiogopa zambi hii, ni kosa ni hatia na ni uvunjifu wa sheria. Na iwapo akigundulika kuwa ameua kifo cha kunyongwa chamsubiria, hatia na kufungwa jera maisha ni adhabu kubwa sana.
Anayapenda sana maisha yake, maisha yake yameharibiwa na matendo ya mkewe, anampenda sana mkewe, anatamani kumuona akiwa amepona na ni mwenye uzima tele, anapenda sana kumwona mtoto wake wa pekee James anaishi maisha ya raha na starehe, aishi mikononi mwa babaye na mamaye, lakini James ataishije? Ikiwa mama na baba ndio hivyo tena, wangali wmeathirika kwa ugonjwa wa UKIMWI, wangali wankufa na kumuacha James akiwa yatima. Machozi yalimtoka yule dereva kijana.
Akiwa angali bado anawaza mara akapata huruma juu ya kiumbe aitwaye Albino (mlemavu wangozi) moyo wake ukamwambia ‘je unafahamu kwamba Albino nayeye ni mtu, mtu kama watu wengine?’ je unayo furaha kumuona mlemavu wa ngozi akiwa ndani ya mateso mara baada ya kukatwa kiungo chake muhimu kinachomsaidia katika kuyaendeleza maisha? Kwa mfano ujapokatwa wewe moja ya viungo vilivyo ndani ya mwili wako utajisikiaje?
Furaha ipo wapi iwapo utamuona Albino akitumia mirija au mabomba ambayo yatamsaidia katika kuitoa haja ndogo? Hivi cheppe huoni jinsi gani huyo mja wa Mwenyezi Mungu atakavyo teseka? Ingiwa na huruma usifanye hivyo, mpende Albino usifanye hivyo tambua kwamba Albino naye ni mtu tena ana haki ya kuishi kama wanavyoishi watu wengine duniani.
Mawazo yalimtibua Bwana Cheppe, akikumbuka kwamba amepewa siku tatu za kutimiza hayo yote ambayo anapaswa kufanya ili ayaokoe maisha ya mkewe, yeye binafsi na ya mwanaye mpenzi James. Je atende au asitende? Maswali ambyo Cheppe alikosa majawabu yake.
Ooooh! Masikini anapenda kuishi lakini je ataishije katika dhiki hiyo? Je atende au asitende? Roho ikamwambia tenda nyingine ikamwambia usitende. oooh! Wakati ni mgumu hatimaye akafanya maamuzi, maamuzi ya moyo wake hana budi kutenda na tena anapaswa kutenda haraka iwezekanavyo.
Itaendelea
No comments:
Post a Comment