Monday, October 14, 2024

3 Michelle Obama's Prayers (Maombi ya Michelle)

 


MGAHAWANI.”

 

Jumamosi moja yapata muda wa saa sita mchana, jua lingali linawaka, ni jua kali la utosini, muda huo mzuri ulikuwa ni muda muafaka kwa familia ya Barrack Obama kuketi mezani na kuanza kuyashambulia mapocho pocho, huo ni muda wqa kula chakula ndani ya ile familia, Muda mzuri wa kusali pamoja na kumshukuru mwenyezi Mungu kwa maandalizi mazuri ya chakula kiwapacho afya na uhai.

            Lakini jumamosi ya siku ya leo ilikluwa tofauti na jumamosi zingine zote ambayo familia ya Barrack Obama ilizoea kuketi kwa pamoja ili ipate kujumuika ufahari wa vyakula bora vya utamaduni wao wenyewe.Ilikuwa ni Obama aliyetoa wazo, wazo la kutoka ‘out’ yeye na mkewe pamoja na wanawe wawili Sasha na Maria. Lengo la kutoka Out halikuwa lingine zxaidi ya kwenda kupata Lunch au kujumuika pamoja na watu wengine wa daraja la chini (Lower Class) katioka mahoteli au katika mabanda yao ya vyaklula vya bei poa (mabanda ya mama ntilie).

            Sio kwamba Obama’s Family  hawakuwa na uwezo wa kwendsa kwenye mandhari  ya hoteli za bei gharama, hoteli za watu wanaoitwa Higher class, hapana, mbona hata hivyo Obama’s Family ni familia ya hali ya juu sana zaidi duniani, baba akiwa ni Raisi wa 44 wa Marekani, mama akiwa ni first Lady, mwana mama anayeheshimiwa sana duniani. Uwezo wa kufanya hivyo wanao na pia wamefanya hivyo mara million zaidi. Basi leo Obama alitoa wazo na pendekezo la kwenda kubadirisha mazingira nje ya White House.

            Ombi au wazo la huyu kichwa cha familia hakupingwa, liolipokelewa kwa mikono miwili mbele ya mkewe na mbele ya wanawe wawili Saha na Maria.Safari iliandaliwa, polisi wote wa,lindao Raisi (Board guards) wana usalama wote, wapelelezi wa FIB, na wengineo muhimu kwa ajiri ya kumlinda Raisi familia yake walimtangulia mkubwa wao mbele wangali wamevaa mavazi yao ya kawaida, hawajioneshi kama ni wanausalama, tena wapelelezi wa Shirika la Upelelezi Marekani (FIB).

            Obama na familiaa yake, walihitaji kula ndani ya hoteli moja tulivu ya watu wa hali ya chini na bahati nzuri mbona walipata kuingia ndani ya mgahawa (Restaurant) mmoja usio na jina kubwa ndani ya  Jiji LA New York. Basi wakaagiza malaji pamoja na manywaji yao, wakiwa tayari wameketi kunako meza yao wao binafsi, yaani watu wane; Obama, Michelle Sasha na Maria nao wakaagiza lunch yao pamoja na manywaji yao.

            Mgahawa ule ulikuwa ni mgahawa uliomilikiwa na jamaa mmoja ambaye kwa kiasi fulani alikuwa ni masikini japo si wa kutupwa kivile, pesa zake zilimsumbua ili kuboresha mgahawa wake, ndio maana aliona bora awapatie ajira mabinti wawili waliohudumu vema upande wa kusambaza vyakula, wakati huo huo upande wa vinywaji yule jamaa alishika usukani.

            Kazi nzito kweli kweli, mabinti walijiweka bize kuuza vyakula vya aina mbali mbali, sio vyakula tu, bali pia kupika na kupakua, jamaa naye alijibidisha katika ugawaji wa vinywaji mbali mbali mchana hadi jioni, kazi nzito kweli kweli, japo uvumilivu pekee ulimtosha kumsukuma sukuma asonge mbele.

            Alex alisogelea Meza waliyoketi Obama, Michelle, Sasha na Maria akawakaribisha kwa heshima na adhama ya biashara kama tujuavyo tena ‘Mteja ni mfalme’, anapaswa kuhudumiwa kwa ufasaha mkubwa.

            "Loverly, you are almost welcome.”(Wapendwa karibuni sana) Alianza kuongea Alex akiwatizama wale watu weanne asiowajua.

            “Thanks so much.” (Tunashukuru sana). Kwa pamoja wale wanafamilia walimwitikia Alex.

            “Good afternoon All of you.”(Habari za mchana).

            “Good afternoon, how are you?”(Habari na wewe, U hali gani?”)

            “I’m good!”(Mimi ni mzima).Alex aliwajibu wale wateja wake akiwa amevalia mavazi ya watoa huduma migahawani, kofia moja kubwa ile wanayovaa Mabakery (Waoka mikate) pamoja na kivazi kingine kilichozunguka shingo na kiuno chake, rangi ya viwalo hivyo kwa kawaida ni nyeupe ya kupendeza, mavazi haya daima huwakilisha muhusika kama nani katika hoteli, anafanya nini (Anatoa huduma gani) katika ile hoteli.

            Mara baada ya salamu, Alex alihitaji kujua hitaji la hao wageni waliomtembelea, lakini ghafla, macho yake yaliganda kunako first Lady Michelle, hata asijue ni nani huyu, kama vile anamkumbuka, ama walionana sehemu fulani, ama kwa bahati tu. Mmmh! Alex hakupata jibu sahihi.

            Obama, Michelle, Sasha na Maria walikwisha  agiza malaji na vinywwaji vyao, baso malaji (vyakula) yakaletwa na hao wadada wawili warembo, wakati huo huo manywaji (vinywaji) vililetwa na mwenye huo Mgahawa Alex.

            Lakini bado tu Alex alikuwa akimtazama sana Michelle, moyoni mwake asitake kuamini kama amepata kumuona pahali fulani huyo mwanadada. Hata hivyo akiwa tayari amekwisha kuwa sevia yale manywaji yao, uvumilivu ulimshinda, alihitaji kuuliza, yawezekana labda amepata kumuona pahali huyo mwana dada ambaye leo anamtizama sana.

            “Samahani dada.” Alex alianza kuongea akiwa akiowa anamtizama Michelle, huku amesimama wima kama Mlingoti, Hoteli imetulia tuli, kila mteja anafurahuia malaji ya pale mgahawani.

            “Bila samnahani, waweza kuongea.”Michelle alimpa ruhusa na uhuru huyu mmiliki wa hii hoteli kuongea.

            “Nimekutizama sana dada yangu, na katika kukutizama tizama ni kama vile hisia zangu zinaniambia nimepata kukuona pahali fulani.” Alex aliongea akiwa angali anawaza, wakati huo huo wale wana familia  wakimtizama mwenyeji wao.

            “Yawezekana ndio tumepata kuonana, yote kwa sababu Waswahili wanasema ‘’Milima haikutani, bali binadamu hukutana.” Michelle aliongea kwa ufupi.

            “Mmh! Sura yako sio ngeni machoni mwangu, kial nikivuta picha nahisi kama bado ninakufahamu…Je, wewe ni Michelle?”Alex alimuuliza First Lady, ingawaje moyoni mwake alisita sita kuamini kwamba yule ni Michelle, sio mtu mdogo duniani, Michelle ni jina kubwa sana duniani, ni mwanamke anayeheshimiwa sana duniani, yawezekana leo watu wenye pesa zao (Higher Class kwenda kwenye kihoteli cha watu wa Lower Class kula na kufurahia?

            Alex anaamini kuwa watu wa madaraja ya juu siku zote wanapendele vitu vya anasa na vya fahari, hawawezi kamwe ati kufurahia pishi la ugali wa mihogo kwa kisamvu, mchicha, mrenda au Bamia walizoagiza wale wanafamilia. Alex anaamini kuwa watu wa daraja la juu ni watu wanaopendeleq kuwa ndani ya mahoteli makubwa makubwa duniani, huko wanatawanya pesa watakavyo, huko wanafuja mali watakavyo, huko wanafanya kila ubaya na uzuri kwa kutumia pesa. Pesa ni sabuni ya roho, pesa nzuri machoni na rohoni, mwenye pesa mpishe.

            “Yes, mimi ni Michelle, na huyu hapa ni bwana wangu, mume wangu Barrac Obama, na hawa hapa ni wanangu wawili Sasha na Maria.” Michelle aliongea na kumuachia mshangao mkubwa yule mwenye ile hoteli ndogo, mdomo wazi, bumbuwazi, macho yamemtoka pima kama vile mjusi amebanwa na mlango.

            “Je, wewe ni nani?” Michelle alihitaji kumjua zaidi yule mmwanaume mwenye umri wa miaka 45, umri am,bao unashabihiana na umri wakwake yeye.

            “Oooh!..... Oooh!....Oooh!”Mara kwa ghafla machozi yalianza kumtoka yule mwanaume kijana, alikuwa analia kwa hisia, alikuwa analia kweli, asitake kuamini yale maneno aliyoongea Michelle, ni miaka mingapi sasa hajapata ku,uona wala kumtia machoni pake huyu mwana mama aitwaye First Lady, mwana mama mwenye heshima kubwa duniani.

            “Usilie tafadhali,. Tueleze… wewe ni nani?”Michelle alimpooza yule mwanaume kijana ambaye alitii lile agizo naye akanyamaa kimywa, amejipanga kuongea yale yaliyop moyoni mwake.

            Michelle, mimi ni Alex yule kijana uliyepata kusoma naye pamoja katika chuo kikuu cha Havard miaka 20 iliyopita.” Alex aliongea akiwa bado amesimama akiwa ameshikilia beseni lake atumialo kubebea vinywaji kama vile bia, machozi yanambubujika.

            “What!... It’s you Alex?”(Nini, ni wewe Alex?).Michelle aliongea kwa mshangao

            “Yes, it’s me Michelle.” (Ndio, ni mimi Michelle).Michelle alibaki anamshangaa yule mwanaume kijana, asitake kuamini kama kweli ni yule Alex aliyetokea kumpenda miaka 20 iliyopita, machozi yalitamani kumdondoka Michelle, lakini ilibidi ajizuie asioneshe hisia zake mbele ya watoto na mumewe.

            “Ok, ok, It’s Alright.” (Sawa, sawa yatosha). Michelle aliingiza mkono wake ndani ya mifuko ya mkoba wake alionunua kwa bei poa ya shilingi elfu ishirini, wakati wanawake wengi wanaopenda anasa za dunia hii hawachoki kununua mikoba ya bei gharama, million mbili, million tatu na kadhalika.

“This is my bussness card, take it please.”(Hii ni kadi yangu ya biashara, tafadhali ichukua). Michelle alimpatia Alex card yake ya biashara iliyo na namba za simu za bibie Michelle. Alex aliipokea kwa furaha, wakati huo huo aliona heri awaache wale wapendanao waendelee kufurahia huduma zake.

            Malaji yale manywaji yalikuwa ni matamu ya kuridhisha wale wanafamilia waliofurahia huduma iliyotolewa ndani ya hoteli yake Alex, upendo na ukarimu wake uliwavutia, hawakuacha kumsifu naom wakatoa ahadi ya kuja kumtembelea siku nyingine tena. Walihitaji kuondoka, muda wao wa kuketi pale hotelini ulikwisha. Kwa upendo mkuu walimshukuru sana Alex, nao walimuaga nan kuondoka.

Itaendelea

No comments:

Post a Comment

I promise you

   I PROMISE YOU. (NINAKUAHIDI.) SURA  YA KWANZA. UBAYA WA POMBE. “Umenizingua job, umenizingua kwa muda mrefu sana mpenzi wangu…….kwanini l...