Sunday, October 13, 2024

Michelle Obama prayers (Maombi ya Michelle) 2



 Sehemu ya pili

"Kuna mshairi mmoja duniani, nimelisahau jinale(jina lake limenitoka kidogo) aliwahi imba shairi lake, shairi ilo linaitwa nitaimba wimbo, naye akasema ;" Michelle alianza kughani wimbo wa mshairi huyu wa dunia ambaye yeye binafsi alidaikuwa kuwa jinale limemtoka kidogo. 


          “Nimepitia makwazo,

njia yangu ina miiba

Vigumu sana kupita,

kupita, 

vigumu sana kupita,

Lakini najipa matumaini,

 naamini, 

Ipo siku moja taamu,

taamuu, 

nitaimba wimbo


Makofi vifijo pamoja na vicheko vya furaha vilimiminika miongoni mwa wale hadhira.Michelle aliendelea kughani kwa furha.


“ipo siku moja taamu nitasimama,

Ipo siku moja nitaimba wimboo,
Ipo siku moja tamu,nitaonesha 
Kipaji changu majaliwa, 
Ipo siku moja taamu nitaimba wimbooo.


“hata ipite miaka mia,

 nitasimama,
Hata ipite miaka mia,

 nitaimba wimbo,
Hata ipite miaka mia,

sitakufa moyo,
Hata ipite elfu mia,

nitaimba wimbo.


Nderemo shangwe pamoja na vifijo zilimiminika kutoka kwa wale wamarekani weupe na weusi walipendezwa na jinsi gani first lady Michelle alivyokua akilighani lile shairi tamu linalotoa matumaini ya kutokuvunjika moyo, ata kama itachukua muda mrefu maishani mwa mwanadamu asikate tamaa bali ajipe matumaini ushindi ni wake ilihali anajua na pia anatambua kuwa mwenyenzi mungu yupo


“Michelle( au labda tungelimwita kwa jina la maichelli kama linavyotamkwa na hao hao wenye rafudhi zaki Afro Amerika na zile za kizungu) ni miongoni mwa wanawake wachache sana duniani wenye bahati, sifa zake kuu ni kujichanganya changanya pamoja na watu wote duniani pasina kubagua rangi jinsia, udini au utaifa, yeye uwasikiliza watu wote tizama hapendi na tena hapendelei makuu haijalishi hata kama mumewe bwana Barrack Obama anazo pesa mingi kiasi gani yeye ni mwanamke anayejari anaye thamini na pia ni mwanamke anaye thubutu.


Vaa yake ni mfano wa kuigwa na kupigiwa debe, havai mavazi ya bei kubwa sana duniani,kama wanavyo vaa wanawake wengine popote pale duniani, wanawake wa viongozi, matajiri, mabillionea na wenye fedha zao,ajabu yeye uvaa mavazi ya bei poa, magauni skafu sketi au brauzi za bei ambazo mtu fukara hawezi kushindwa kununua,hata viatu vyake ni viatu vya bei poa si kicheko iwapo mpenzi msomaji utaambiwa kwamba kiatu chake yeye ukifanyia shopingya shilling elfu hamsini tu, na pungufu ya hapo ni shilling elf 35, wakati wale wanawake wote walio olewa na matajiri wa dunia hii upendelea kuvaa viatu vya bei gharama si chini ya shilling million tano, sita au saba ata kumi inafika, kulingana tu na kampuni inayotengeneza hizo bidhaa, lengo likiwa ni kujionesha mbele ya jamii ya kwamba wao wana uwezo mkubwa duniani.


Ooooh!! Ajabu inashangaza tena inatia moyo wenye furaha duniani, kusikia kuwa familia ya bwana Barrack Obama ni familia inayojari na pia inathamini sana vitu vya nyumbani, ndio maana waswahili wanasema wahindi ni wamoja na kwao ni kumoja inapendeza sana kuona na kusikia kwamba familia ya raisi Obama mara nyingi tena kwa siri hujumuika pamoja na kula mapocho pocho madiko diko na malaji mengine pamoja na watu wa daraja la chini( lower class) tena uzuri wake familia hii ufurahi pamoja kwenye hayo mabanda ya vyakula vinavyopikwa na wakina mama nitilie…oooh! Inapendeza.


“hivi huyu Michelle(maichelli) Obama ni nani haswa ata sisi tutake kumjua zaidi na zaidi; maichelli ni mwana mama mwenye mabinti wawili Sasha na maria mabinti wazuri wenye mvuto duniani, warembo walio rembeka si kwa mafuta ya bei gharama au kwa mapambo ya bei gharama bali ni kwa matunzo, malezi bora utii na usikivu, maichelli ni mwanamke menye asili ya Afro Amerika, kama alivyo mumewe bwana Barrack Obama, ambaye babaye mzazi bwana Hussein Obama ni mwafrika wa Kenya ya afrika mashariki wakati huo huo mamaye ni mzungu wa huko ulaya. Hivyo basi Obama ni chotara wa kia frika na kizungu.


Barrack Obama ni raisi wa 44 wa A merika(2008-2015) hakuingia bure ndani ya ikulu ya white house balia iingia kwa nguvu na kwa msaada wa mkewe mpenzi bibie Michelle Obama wanawe wawili Sasha na Maria pamoja na wa Marekani wote wenye umoja, hapo ndipo ule usemi unao sema alipo mwanaume mwanamke yupo hakosekaniki wanawake sio tu kusema wana mvuto, ni wazuri na warembo bali pia wanawake wana ushawishi mkubwa sana kwa mwanaume au kwa jamii husika ili kuleta maendeleo.


            Jinsi Mabillionea wa dunia hii, hupendelea kuvaa viatu ‘Sendo’ za bei gharama, si chini ya hilingi millioni tano, sita, saba, hata kumi kulingana tu na kampuni inayotengeneza hizo bidhaa.


            Oooh! Ajabu inashangaza, tena inatia moyo wenye furaha duniani kusikia kama familia ya Barrack Obama ni familia inayojari, na pia ni familia inayothamini vitu vya nyumbani ndio maana Waswahili wanasema ‘Wahindi ni wamoja, na kwao ni kumoja.’ Inapendeza kusikia na kuona habari inayosema kwamba ‘Familia ya Raisi Obama, mara nyingi tena kwa siri, hujumuika pamoja kula mapocho pocho, madiko diko, na malaji mengine pamoja na watu wa daraja la chini (Lower class) Tena uzuri wa familia hii, hufurahi pamoja kwenye hayo mabanda ya vyakula vinavyopikwa na wakina mama Ntilie na kina Baba Ntilie’ Oooh! Inapendeza.


            

            Obama hakuingia ndani ya White House hivi hivi, bali aliingia kwa nguvu mojawapo ya Michelle, ulitosha kumsukumiza Obama ndani ya Ikulu ya White House, yote kwa sababu Michelle alikuwa bega kwa bega yeye na wanawe wawili Sasha na Maria kuhakikisha kwamba Obama anaingia ndani ya White House,. Si kwa Kampeni pekee, bali pia kwa ushawishi ili Wamarekani waamini kwamba Obama ataleta mabadiriko.


            Uzuri wa matokeo yake, Obama aliingia ndani ya Ikulu ya White House kwa kishindo mara baada ya kuwaangusha wapinzani wake wote, mara baada ya mamilioni ya Waamerika kumwamini mtu mweusi wa kwanza kuingia ndani ya White House. Haikuwa jambo rahisi, hata hivyo Wamarekani hao walijikuta wanazizika tofauti zao, itikadi zao na mapungufu yao, wakampaka mafuta Barrack Obama awe Raisi wao wa 44.


Alright, Tusiandikie Mate wino ukiwepo, mdogo mdogo ndio mwendo, tutafika, tena tutafika kwa furaha, kitu kikubwa hapa ni kushiriki imani na kumtanguliza mwenyezi Mungu wetu kwa kila jambo, yote kwas sababu Mungu wetu yupo tumwombapo, yu papo, naye atatujibu kwa wakati na kwa muda wake. Jina la bwana libarikiwe sana.


            Michele Obama anaanza kutusimulia simulizi yake tamu, iliyojaa hisia za mapenzi, japo kwa upande mwingine aliumia, pia aliumizwa mapenzini, hakufa moyo wake, alijitahidi kuzionesha hisia zake yeye kama mwanamke wa Afro-Anerika, kabla hajawa First Lady, kabla hajaonana na Barrac Obama, alizionesha hisia zake kwa huyu kijana aitwaye Alex, kipindi kile akiwa angali bado binti wa chuo kikuu cha Havard.


            Anaongelea, na pia anasimulia hadithi moja tamu ya mapenzi, anataka kuwaonesha hawa wanachuo kwamba mwanamke na yeye anazo hisia, hisia za mapenzi, na hisia zake ni muhimu ziheshimiwe. Michele anajua na pia anatambua kuwa mwanaume pia anazo hisia zake,na hisia za mwanaume siku zote ni za hali ya juu, mhemko mkuu, tam,aa na matamanio. Michelle anasimulia, kipindi hicho alikuwa yungali ni binti mbichi katika mapenzi, nayeye aliona mmmh! Hapana, kuna kijana mmoja mzuri sana pale chuoni, amemvuta na kumvutia, sio kwamba aliogopa kumwambia, hapana, hisia zinapozidi, mapenzi huwa juu ya kichwa cha mhusika, mapema huwa zigo linalohitaji kushushwa, iwe au isiwe na hata kwa gharama.


            Alex anaonekana kuutibua moyo wa Michelle, kwani Michelle hakuweza kula, kunywa na hata kusoma, mara zile fikra zake zilipomsogeza na kumkumbusha mbele ya picha ya mwanaume kijana aliyempenda ajabu. Alex ndani ya mtima wa Michelle alikuwa ni kama Barafu iliyoupooza moyo ulioganda na kugandana. Alex aliutibua moyo wa Michelle, hata Michelle hakuweza wala hakujiweza, balim alikuwa hoi kimawazo juu ya yule ampendaye wa moyo wake.


            Kipindi hiki kilionekana kuwa ni kipindi kigumu sana kwa Michelle mwanadada mmoja mrefu, mweusi wa Asili, mwembamba mwenye tabasamu lisilo chuja, ni mwenye malengo, matarajio, nia na mengi katika maisha yake.Hembu atueleze kwa undani zaidi nini kilichoendelea, hatutaki kuandikia mate wino ungalipo.


                                                ********************************


Itaendelea



No comments:

Post a Comment

I promise you

   I PROMISE YOU. (NINAKUAHIDI.) SURA  YA KWANZA. UBAYA WA POMBE. “Umenizingua job, umenizingua kwa muda mrefu sana mpenzi wangu…….kwanini l...