Mimi ni Baba wa Giza
Lakini sio BABA mbaya
Pale mtu anapohtaji huruma na msaada
Nipo tayari kuitoa roho na nafasi YANGU
Kusaidia
Jioni Moja
Yapata saa kumi na mbili
Si nikamuona
Jibaba mmoja kashika kisu kikali kuwili
Kifuani kwake kamgandamiza mtoto ambaye alikua akilia
Kilio Cha kulitaka Jibaba limuachie
Kilio Cha kutaka arejee mikononi mwa MAMAYE
Ambaye alisimama pembeni amejaa huzuni na kumlilia mtoto wake.
Lilimpigia kelele yule mama mwenye uchungu wa mwana
" Sina pesa hizo, tafadhali nirudishie mwanangu" Mama alilia
" Wewe Mume wako si anauza madini, unashindwa vipi kwenda kumuibia unipe Mimi"
Jibaba lilimshawishi mwanamama akaibe.
" Siwezi kuiba, kuiba ni zambi na ni kosa. Ukitegemea Mimi na mwanangu HATUNA kosa ni wapita NJIA tu"
"Alah! Unanijibu jeuri, Sasa namchinja huyu mtoto"
"Hapana, hapana... Muhurumue mwanangu"
Mwanamama alilia.
Niliyasikiliza maongezi yao
Nikagundua kumbe Jibaba ni Jambazi
Limemteka mtoto makusudi Ili lilipwe
BASI roho YANGU ikaniambia "fanya kitu.. do something"
Nikaivua kofia YANGU
Kofia inayoficha MAOVU
Kofiabinayotenda maovu
Nikalitazama JIbaba
Lile lenye ndevu za Osama
Nilichokifanya Najua MimiMaana Mimi ni SHETANI wa USIKU
Likamuacha mtoto
Mtoto akakimbilia Kwa mama yake
Mimi bado nilikua nafanya kitu
Nadani ya kofia yangu
Limeshikiliankifua
MOYO unaliumaa
Likatapika damu
Kifua, kifua, kifua
Oooh! Kifua kinanibana
Maweee! Nisaidie
Sikujali bado tu nikaendelea kufanya Ushetani wangu
No comments:
Post a Comment