SURA YA NNE.
ANATENDA UNYAMA.
Cheppe alifanya kuusikiliza moyo wake, moyo ndio ufanyao maamuzi ambayo Cheppe tayari ameyafikiria. Kwamba anapenda kuishi na pia anapenda kuona mkewe yu pamoja nayeye, wakifurahia maisha matamu ya ndoa yao, haijalishi wapo katika hali gani kiuchumi. Je ni mafukara au je wanajiweza? Kitu muhimu ili binadamu aishi ni uhai pumzi na Baraka tele apewazo na Mwenyezi Mungu.
Cheppe alijitahidi kufanya tendo ambalo moyo wake ulimsukuma afanye hivyo, ingawaje ni muoga hajui ataanzaje anzaje unyama wake, hajui afanyeje ili kulitenda tendo analo ogopa kulitenda. Ameambiwa alitende yeye mwenyewe tena wakati wa kulitenda hilo tendo sharti moja asionwe na mtu yeyote akiisha kulitenda hilo tendo.
Cheppe angali bado anaimani kwamba Ushirikina umechukua nafsi kubwa sana kuyadorolesha maisha ya mkewe na hata yake binafsi yangali hayaoneshi matumaini ya kuendelea kuishi duniani. Ndio maana Cheppe anayatafuta hayo matumaini yaliyopotea.
******************************
Tayari amekwisha kuliona windo, windo ambalo ndani ya siku hizi mbili tatu ametanga tanga kwa siri kubwa, akiangaza huku na kule apate kumwona mtu mwenye ulemavu wa ngozi. Bahati haiji mara mbili mbili amekwisha liona windo ndio maana hatulii hapa wala pale, angali anasubiria ufike usiku wa manane ili afanye tendo analodhamiria kulitenda.
***###########
Ni huyu kijana aitwaye joseph ni kijana wa kiume mwenye umri wa miaka kumi na miwili, amezaliwa akiwa na ulemavu wa ngozi (Ualibino) yeye pekee ndiye mwenye tatizo la ulemavu wa ngozi ndani ya familia yao, kaka zake wawili waliomtangulia wangali ni wenye ngozi nyeusi ya kiafrika hata dadaze wawili walionyuma yake ni weusi wa ngozi ya kiafrika.
Wakati huu wakati ambao watu wenye tatizo la ulemavu wa ngozi wanawindwa ili wauwe kwa visingizio vya waganga wa jadi wakidai kuwa ngozi ya Albino ni dili jema mbele ya macho, miguu na mikono ya Mizimu. Ngozi ya watu kama Joseph waganga na washirikina wameweka imani kwamba ina dawa na kinga madhubuti juu ya magonjwa mbali mbali yanayomuandama binadamu,
Ngozi ya Joseph ni chanzo cha utitiri wa utajiri, mtu kama Joseph ana nyota njema inayong’ara si gizani wala si mwangani kote kote ngozi ya Joseph inaleta maendeleo. Ama kweli waganga wa jadi pamoja na washirikina ni waongo wasio tabirika, miezi michache iliyopita waliwadanganya watanzania wengi wakisema ati ngozi ya Albino ni ngozi yenye utajiri mkubwa ndani yake, hiyo ni dawa ya magonjwa sugu kama vile HIVHIV/AIDS, kisukari, pressure, TBna BP.
Makumi ya Albino waliuawa kisiri siri huko vijijini na udhaifu wake matokeo yalikuja kuonesha kwamba waganga wa jadi sio watu wanao ongea ukweli na uaminifu, magonjwa yangali bado yanawatesa watanzania, umasikini ungali bado unawatesa watanzania.
Something wonderfull, inashangaza kuona watanzania wanapumbazwa na kudanganywa kwa kuwatumia watu wasio na utalamu, wasio na elimu jinsi ya kuyatatua matatizo yanayo wakabili.kumuua mlemavu wa ngozi ni moja ya njia zilizo potoka na ni njia potevu, muhimu kupewa elimu ya namna au jinsi ya kuepukana na magonjwa mbali mbali, magonjwa yanayozuka na kulinyanyasa taifa. Je wakifanya kazi kwa bidii hawataweza kuliletea taifa maendeleoau utajiri wanaousaka hadi kwenye mashimo ya panya? Utajiri wanao utafuta kwa waganga wa jadi. Aibu yao wavivu, wazembe, wategemezi, wapenda anasa raha na starehe.
Wakati ambao jamii imezoa sifa mbaya juu ya watu wenye ulemavu wa ngozi, jamii inayo amini kuwa ngozi ya Albino ni dili la utajiri, viungo vyao au ngozi zao ni dawa ya magonjwa sugu. Serikali pia ilikua mbioni kuwalinda au kuwatetea hawa wenzetu wenye tatizo la ngozi.
Sheria mbali mbali zilitungwa ili kuwalinda au kuwtetea hawa wenzetu wenye tatizo la ngozi, adhabu kari zilitolewa kwa wale wote waliowatendea mambo yasiyo ya kibinadamu hawa wenzetu wenye matatizo ya ngozi. Serikali ilikuwa bega kwa bega pamoja na viongozi wa kaya, kata au vijiji ambavyo wenzetu hawa wenye matatizo ya ngozi wangali wakiwindwa na kufanyiwa unyama.
###############****************##########
Usiku wa manane ulingia, Cheppe alijibanza kwenye mti moja mkubwa wa mkorosho, mti uliotazamana na nyumba yao joseph yule Albino ambaye Cheppe alikwisha panga njama ya kumtia mawindoni, alikwisha panga mkakati namna gani akivamie chumba anacholala Joseph. Hakuna mtu aliyemuona Cheppe akiwa amejificha hapo, giza pekee lililozuiliwa na mbalamwezi ndilo lililomuona cheppe akiwa amejificha hapo akijipanga kuufungua mlango wa chumba alalacho Joseph, chumba ambacho kipo uani nje ya nyumba kubwa wanayoishi akina Joseph.
Lakini kabla hajafanya jambo lolote lile, alikuja kuona mlango wa chumba ambacho Joseph analala pamoja na kakaze wakubwa Emma na Eze ukifunguliwa. Cheppe aliliona windo lake, windo lililojijia lenyewe, windo analo lisaka, furaha ilimwingia moyoni mwake.
Mtego unajileta wenyewe.” Cheppe alijisemea moyoni mwake akamuona Joseph anaingia kichakani, akamuona Joseph anafungua Zippu ya suruali yake mara baada ya kufika kichakani, kumbe anataka kuchimba dawa (kukojoa mkojo) Cheppe akammendea yule mtoto, akamnyatia nyatia nyatia nyatia kama pusi anayenyatia panya.
Mara ghafla ngumi nzito ilitua nyuma ya shingo ya yule mtoto aitwaye Joseph. ‘Nduuuuuuuuuuup.’ Joseph alishindwa kupiga ukelele, akaanguka chini akazirai akiwa hajui ae wala bae, Cheppe alikwisha mwingiza mtegoni. Bila kukawiza mambo Cheppe alimzoa zoa Joseph na kumbeba juu ya mgongo wake tayari kwenda kumfanyia unyama na umafia aliodhamiria. Cheppe akatokomea Kichakani.
Kumbe! Kumbe Emma kakaye mkubwa Joseph aligutuka kutoka usingizini mara baada ya kusikia kishindo cha ngumi iliyomfanya Joseph aanguke chini. Mara baada ya Emma kugutuka kutoka usingizini hakutoka nje bali alielekea lilipo dirisha la chumba chao akalifungua pazia la hilo dirisha. Looh! Moyo wa Emma ulidunda ‘ndu ndu ndu ndu,’ kwa kasi mara baada ya kumuona mdogo wake Jose akizolewa mzoe mzoe na kutokomezwa porini
Pasina kupoteza muda Emma alimwamsha Eze akamweleza habari yenyewe kwa ufupi. Haraka haraka Emma na Eze walitoka ndani ya chumba chao, mikononi mwao wameambatana na silaha za jadi, pinde mishare, rungu, mikuki, shoka na mapanga, hofu juu ya usalama wa Joseph ilikua ni hofu kubwa sana wakawamsha wazazi wao wakaenenda ile njia ambayo Emma alimwona mtu aliyempiga Joseph akielekea.
***************************************
Cheppe alimtua Joseph ndani ya kichaka kikubwa alichofikia hakutaka kuupoteza muda mara baada ya kumtua joseph aliyekua tayari amezirai hajielewi hajitambui kwa pigo zito lililotua juu shingoni kwake. Cheppe alikitwaa kisu chake chenye makari kuwili na mara baada ya kukitwaa aliivua suruali aliyoivaa Joseph na baada ya kuiteremsha suruali ya Joseph akaikamata ile sehemu nyeti ya Joseph, kwisha kufanya hivyo roho yake ikamwambia ‘fanya haraka haraka,’ upande mwingine wa roho yake ulimwambia ‘usifanye kitendo hicho, utakuja kujutia hapo baadae, ooh!’. Cheppe alijikuta yupo njia panda, mtihani mzito kwake, maji Keisha yavulia nguo je ayaoge au asiyaoge? Acha ayaoge tu.
Haraka haraka akiwa amezikamata sehemu nyeti za yule mwenzetu mwenye ngozi ya ualibino, akazitia kisu bila huruma, ‘ana moyo wa kinyama,’ alizikata kata nyeti za yule kijana aliyezirai kama mfu kwa sababu ngumi aliyopigwa ilikua ni nzito balaa. Damu zilianza kutoka sehemu ile nyeti ya mtoto Joseph.
‘Paaaaaaa’ Rungu zito lilitua juu ya kichwa cha bwana Cheppe, aliziona nyota nyota kibao zikimcheka ndani ya macho yake, alihisi kizungu zungu kama mtu aliye kunywa bia na kulewa akayumba yumba, yumba yumba na kudondoka chini nduuuu kama gunia la maharagwe. Kile kisu alichofanyia unyama ule kikadondoka kutoka mkononi mwake, kikatua chini, ile sehemu nyeti ya joseph, sehemu aliyoishikilia mkono wa kuume, ilidondoka chini. Emma Eze na wazazi wao tayari walikwisha kufika ile sehemu ambayo Joseph alitendewa unyama. Kwa msaada wa Mbalamwezi wale wanandugu waliona kila kitu kilichotendwa ndani ya dakika kumi zilizopita.
Huruma ziliwajaa kuona ndugu yao na mwana wao akiwa katika hali ile, machozi yaliyoambatana na vilio viliwatoka, wasiamini kama Joseph wao yupo hai au la! Amekufa. Wale ndugu wawili Emma na Eze walijaa hasira kuona mdogo wao ametendwa ukatiri mkubwa kama ule, hasira zao walizimalizia kwenye mwili wa bwana Cheppe walimpiga vibaya mno, walimpiga, piga, piga, piga na kumtwanga kama mihogo inavyotwangwa kwenye kinu , walimponda na kumlainisha firauni yule. Cheppe alipiga kelele za maumivu, kelele zile ziliwaamsha majirani, jamaa na watu wengine wengi walioamka usiku ule, wakipiga kelele na kulaani tendo alililitenda Cheppe.
Itaendelea
No comments:
Post a Comment