Monday, October 14, 2024

4. Ooh! Maskini



 Sehemu ya nje. 

WANATOROKA.

Basi wale vifaranga (watoto), uvumilivu ulipowashinda waliona bora wafanye kutoroka, ukitegemea mateso yao yalizidi, kila ikiwa leo asionekane mtu wa kuwatetea, kuwapigania au kuwasikiliza baba yao mdogo ni kama vile amewasaliti, yupo yupo tu kama sanamu, hawatetei hawapiganii hawasikilizi. Ubaya wa hayo yote baba yao mdogo Beatusi ameungana na mkewe katika kuwatesa na kuwanyanyasa watoto hawa. Ikitokea Neema amewatusi wale mapacha basi Beatusi naye atamuunga mkono mkewe atawatusi watoto wale, ajabu matukano yanavyochoma.


                 Neema akiwapiga hawa mapacha,  Beatusi atashiriki, vipigo vinavyowapasua pasua hawa watoto yatima. Looh! Ishakua ni kukimbizana huku na kule kwenye nyumba ya wenyewe (watoto) hakuna amani ndani ya mioyo ya wale watoto, hakuna furaha kilichobaki ni vilio, machozi njaa huzuni, magonjwa yakuhara na kutapika. Ile fahari waliyo ionja miaka mitano iiliyopita ishageuka shubiri, chungu, chumvi, pilipili, mwiba na mkuki ndani ya mioyo yao.


                  Basi ndugu yangu, wale watoto walipoona hapo wanapoishi hapasomeki (hapaeleweki), hawakua na jinsi bora kuokoa uhai kuliko kufa. Dawa ya mchawi ni kuyahama makazi yake (kidogo inasaidia) watoto wakatoroka Oysterbay. waliona bora nusu shari kuliko shari kamili, Kariakoo yakawa ndio makazi yao mapya, Posta pakawa makazi yao ya kupumzisha vichwa, wakiomba omba kwa wale wapitao njia wakiomba omba kwa kwa wale wenye magari yao, Masikini! Hivi ni kweli kusema hawa ndio wale watoto waliokuwa wakicheza na kufurahi ndani ya magari ya baba na mama yao?


Magari ya raha na fahari, ajabu leo wanawatizama watoto wenziwao, watoto wa matajiri wanafurahi ndani ya hayo magari. Hivi ni kweli hawa ndio watoto wa vibosile? Msubisi yule Mtumishi wa Serikali  pale TRA? Naomi yule Cash madame ndani ya benki ya jumuia ya Afrika Mashariki. Oooh! Jamani, kweli maisha ni wakati wakati wa haya maisha umeshikiliwa na Mwenyezi Mungu Subahana.


Tuseme ukweli hakuna mpita njia au mwendesha boda boda anayewajua hawa watoto katikati ya jiji. Ilala kuna mambo mengi na pia kuna watu wengi ambao sio rahisi kujua ni wapi na wapi wanatokea. Kati kati ya jiji kila mwenye mwili na pumzi yuko bize  kushughurikia  uhai wake, anayejari anajari, asiyejari hajari, anayependa anapenda, asiyependa hapendi anayetoa anatoa, asiyetoa hatoi.


                     Ubaya wa hao wote wasiojari, wasiopenda na wasiotoa ni wabaguzi, wanyanyasaji, wana mioyo migumu ya kusita sita ni mabahiri na ujue tu ujue kwamba wanajipenda wao wenyewe, wanajijari wenyewe, wanajithamini na wanataka wapewe(wapatiwe) wao wenyewe wengi wa hawa watu, shida yao kuu ni mambo ya kimwili, hasara ya roho zao (pesa), matumizi mabaya ya hizo pesa, anasa  na starehe


 inayoitwa ngono tena ngono yenyewewe ni ngono zembe, ajabu wanapenda sifa.

 Mmmh! Kutwa kuchwa kuwabeza wengineo, kuwashusha na kutokuwaona kwamba hao wengineo nao ni watu tena ni watu kama watu wengineo ambao ni hao hao wasojua kesho ikoje, kesho kutwa itakuwaje?


                                      ################

Ni miezi misita sasa tangu Shaabani na Nela watoroke nyumbani kwao hakuna unaafu wa maisha japo kuna amani  mioyoni mwao, si yale matukano, sio yale mapigo na adhabu ziso na idadi yake. Mtu kuadhibiwa pasina kulijua kosa lake? Looh! Watoto washageuka machokoraa na katika wakati huu Beatusi hana mawazo juu ya hawa watoto, hajapata kumuuliza mkewe uwepo wa hawa watoto, tuseme hajawai na pia hajui ni wapi walipo hawa watoto. Duh! Haki ya mungu! Limbwata pumbazo la moyo, limbwata giza la mapenzi, limbwata ondoko la upendo, ni utumwa wa mwili upendao mali na anasa.


Itaendelea

No comments:

Post a Comment

I promise you

   I PROMISE YOU. (NINAKUAHIDI.) SURA  YA KWANZA. UBAYA WA POMBE. “Umenizingua job, umenizingua kwa muda mrefu sana mpenzi wangu…….kwanini l...