Monday, October 14, 2024

3. Ooh! Maskini!!



 Sehemu ya tatu 

USHIRIKINA

             Nilisahau kukwambia, nilisahau kukwambia mpenzi msomaji, nilisahau kukwambia jambo moja ovu alilolitenda Neema kwa huyu  mumewe Beatusi nilisahau kukuambia kuwa tendo la Beatusi kuuza zile nyumba mbili na horofa moja pamoja na yale magari mawili matatu yaliyoachwa maalumu kwa ajiri ya watoto wa Msubisi na Naomi kama urithi, sio bure bali ni kwa nguvu za ushawishi wa Nema ambaye alikwisha kupata solution ya taizo hili dogo linalo msumbua. Ufumbuzi juu ya kilio chake, chuki zake na mawazo yake

                 Hizo pesa zilizoachwa Benki kwa ajiri ya watoto Shaabani na Nela, zilichezewa ovyo,  kwa nguvu ya ushawishi wa  Neema binti aliyeanza kufurahia  raha na tabasamu la maisha manono ya jiji la Dar es saalam.

                Keisha mfunga mumewe, Keisha mchawia mumewe, mwanamke anataka asikilizwe na kutekelezewa yale yote anayoyataka yeye, anayo yaamuru ama kuyatamka mbele za mumewe, mbona waganga wapo, tena wale waganga wenye kutumia Majini, Mashetani, Pepo, Maruhani na viumbe visivyo onekana. Mwanamama keisha enenda huko Unguja kumtafutia mumewe dawa ya komesho. Keisha enenda hata akafika Pemba kutafuta Jini litakalo mfunga mumewe ili jambo lolote lile aongealo, atakalo, awazalo, apendalo, asikilizwe, afanyiwe hima hima.

              Ndio hapo sasa mume keisha fungwa, hafunguki, yu kama zezeta fulani, limbukeni, zuzu na chizi. Ndio maana ya limbwatamume ogopa tena usijaribu, ukumbuke kuwa sio kila mwanamke umwonaye hapa duniani ni mzuri wa moyo, japo umbo, sura sauti na mwendo umejaa mavuto, mavutio na matamanio.

               Wakati huu ndio wakati mzuri kwa Neema kuachia tabasamu nono lililonononoka, jini linafanya kazi, dawa zinafanya kazi, kila amwambialo mumewe mume atafanya kama alivyo ambiwa, akimkataza mume anakatazika.  Beatusi Keisha geuzwa ndondocha, mtumwa msikivu, mtiifu, aso mbele aso nyuma anaperekeshwa kama Ng’ombe aendae chinjioni, mwe! Wanawake kama Neema ni shidaah!

               Mateso wanayoteswa watoto wa Msubisi pamoja na Naomi, mwenzangu usiombe tena nisikwambie tu, ni mateso juu ya mateso ni manyanyaso juu ya manyanyaso kupigwa pigwa ovyo kama ngoma ya Masangwila, ile ngoma ya mpwita, kunyimwa mahitaji muhimu ya kibinadamu, chakula, maji dawa, mahali pazuri pa kulala, elimu, uhuru na kadharika.

                   Watoto wamekuwa wakilia na kusikitika, weisha komaa kwa vipigo, weisha vunjwa meno yao ya mbele na nyuma kwa bakora, mboko na stick, haki! Looh! Mwanamama Neema si mchezo ni katiri aliyesomea  chuo cha ukatiri  na ubaya wake Neema atakuwa na degree za ukatiri sijui mbili sijui tatu, anajua yeye mwenyewe sie twapita tu, twapita njia ile tunayowaonea huruma watoto wa Msubisi na Naomi, wawili hawa tayari washatangulia mbele za haki, Bwana azilaze roho zao mahali pema peponi. “Amina.

 “Embu tokeni ndani ya sebule yangu, tokeni haraka kalaleni nje!” Maneno haya sio haba ni makaripio ya Neema, anawafukuza Shaabani na Nela waondoke pale sebuleni walipokuwa wakitizama Televisheni. Mara baada ya kuchoshwa na zile kazi za kijungu jiko, kazi za kufua, kuosha vyombo, kupika kunyoosha nguo kwa kutumia pasi, kufyeka, kuosha magari, kutumwa tumwa hapa na pale.


                  “Wajinga wakubwa nyie, mavi yenu, niliwakataza kuoga maji ya moto lakini nyie mwanifanyia ukaidi, sawa, sasa mtanikoma.” Neema aliwavuta masikio wale watoto aliwavuta na kuwapeleka mekoni, mumewe hana hili wala lile anatizama jinsi watoto wanavyonyanyaswa, wanavyoteswa pia, anawatizama kama vile mtizamaji wa wa filamua anavyotizama filamu husika.


    ‘chwaaa….chwaaa..chwaaaa’ hiyo ni milio ya bakora, tena ni bakora nzito ajabu, sijui wangapi wanaijua ile miiko ya kusongea ugali? Shaabash! Wale wote wanayoijua hiyo miiko ya kusongea ugali basi wajue kuwa watoto wa Shaabani na Nela walikuwa wakikong’otewa kwa kutumia hiyo miiko. Neema hakuridhia hapo basi angelichukua visu vikari vyenye makari kuwili angeliwafinya hao watoto kila sehemu za miili yao, damu zingeliwatoka na michubuko pamoja na makovu yaso na idadi yangelionekana,


                Vilio vyao havisaidii, ni nani wa kuwahurumia? Ni nani wa kuwasikiliza? wakati huo huo maji yenye baridi kari kutoka ndani ya jokofu (fridge) yame kwisha andaliwa tayari maalumu kwa ajiri ya hawa watoto kuosha miili yao, kwasababu Neema hataki kusikia ati watoto hawa wanafurahia joto la maji yenye ujoto


 Itaendelea

No comments:

Post a Comment

ZEE LA ZAMANI

  SEHEMU YA KWANZA. HOTELINI Ndani ya Hoteli Paradiso katikati ya Jiji la Mzizima (Dar es salaam) ZEE LAZAMANI akiwa na Mwanagenzi wake JAN...