Tuesday, October 22, 2024

FAKE DEATH

 






MWANANGU NA BOYFRIEND WAKE WALIFEKI VIFO LAKINI KILICHOMKUTA MWANANGU MBONA ALIJUTA.

     'Ajali?" Niliuliza Kwa Mshangao mkuu siku ile nilipoletewa taarifa zilizoushitua MOYO wangu.

     "Ajali mbaya sana mama, ajali imetokea Buguruni Malapa Lisa bintiyo na Dani Boyfriend wake wamekufa VIFO visivyotamanisha kuona MACHONI,"Mleta taarifa alifanya MOYO wangu uende mapigo na Kasi ya ajabu.

     "Lisa amekufa, Dani pia? Siamini."Macho yaliniwasha na kunitoa machozi.

      "Mama Lisa ina maana hata taarifa ya habari ndani ta TBC hujaiona sembuse kuisikia. Ninaposema hawatamaniki Nina maanisha hawatamaniki kabisa, Miguu Imekatika, mikono imekatika, viwili wili vimetupwa kule, sura zao hazitambuliki zaidi ya vitambulisho vyao na nguo walizovaa siku ya Leo."Mleta habari alinidodosa habari iliyonifanya nitoke machozi na kulia kilio kikuu

      "Lisa mwanangu Lisa ndoto zako za kwenda University zimemezwa na ajali iliyotoa uhai wako na WA boyfrendi wako Dani "Nililia Kwa uchungu.

       "Pole sana ama Lisa."Mtoa habari alinifariji wakati huo huo marafiki, majirani na watu wengine walimiminika nyumbani  kwangu kuja kunipa pole na KUFANYA matanga. Masikini mie Selina mamaye Lisa nilikuwa katikati ya maumivu kusikia habari hizi za kuumiza MOYO. Kupoteza yule nimpendaye yule niliyemtoa tumboni kwangu. Walahi! Mbona niliumia. Sijui upande wa Dani Boyfriend wa Mwanangu Lisa ninajua na wao pia waliumia.

******
Tulianika matanga, miili ile ambayo tulishindwa kuitambua zaidi ya vitambulisho na mavazi ya Lisa na Boyfriend wake ilizikwa makaburi ya Kisutu, sie tuliewapoteza tuwapendao tulilia usiku na mchana, tukaomboleza juu ya VIFO vya vijana wetu tuliowapenda.

        Siku sio nyingi mara baada ya kuanua matanga nikavamiwa na kampuni iliyojiita KAUSHA DAMU kampuni hii iliniletea madai kwamba Lisa Binti yangu pamoja na Boyfriend wake Dani walikopa mamilioni ya fedha za kampuni Kwa lengo la kwenda kuzitumia waendapo Chuo. Baya zaidi upumbavu wa marehemu Binti yangu Lisa aliwekeza nyumba yangu kama dhamahana.

     Uwii! Mbona nilichanganyikiwa, kichwa kiliwaka mfano wa kifuu Cha nazi. Nilipagawa na kuvurugwa. Siku chache zilizopita nilimpoteza wangu nimpenaye Leo hii naletewa habari nyingine ya kupoteza nyumba yangu. Hapana nitapigana kijike jike. Nilijiambia.

Haraka nikakimbilia mahakamani lakini huko Nako nilidodakea pua, nilibaki rojorojo, dikodiko, mlenda mtupu.Tena Kwa Aibu nzito nilishindwa na nyumba yangu ikapigwa mnada nikiingalia inavyonitoka PASINA kupenda. Nililaani, Nikabwata kwanini Dunia Haina huruma?



###########

MIAKA SITA BAADAE

Serina mie ni Mwalimu yaani mwajiriwa wa Serikali. Basi siku Moja nikapewa barua iliyonitaka niende Arusha  kwenye Semina na mafunzo Fulani ya kunijenga kitaaluma. Siku ya siku Safari yangu ilipamba moto hata Lile tukio la kuuza nyumba yangu MIAKA misita iliyopita nilikwisha aanza kulisahau ingawaje moyoni nilibaki na maumivu ya Lile tukio la kufiwa na Binti yangu.🥲😥😪

      Nilifika Arusha mjini salama salimini nikalipia HOTELI Moja ya kifahari maana mshiko wa nguvu niliukamata kibindoni. Nikiwa mapokezi kulipia gharama za HOTELI ghafra Kwa mbali  kidogo macho yangu yasiyo na pazia yaliona  vijana wawili mmoja wa kiume na mwingine wa kike wakiwa wanakula Raha za ujanani, wakilishana yakula vinono na vinywaji vya bei gharama.

       Chale Fulani zilinicheza machoni  niliwatazama wale vijana hisia zangu zikaniambia mmoja wa wale vijana ninamfahamu  au nilimwona pahali! Lakini wapi hapo? Sikupata jawabu. Nikajishauri niwache mizigo yangu mapokezi nikawaone wale wawili waliokuwa wakiyashambulia manono na manonozi. Nikawasogelea

          Jesu!  Nilishituka niliogopa pia nilihisi ni jambo la kutisha machoni . Bado niliwatizama wale vijana wawili mwanaume na mwanamke macho hayakunidanganya na MOYO pia haukunidanganya niliwafahamu vizuri wale vijana wawili

         "Lisa" Niliita yule Binti aliyekua akilishwa na mwanaume chakula. Aligeuka na kunitazama. Hofu ilimuingia  Lisa ghafla akadondosha kijiko alichokua anakitumia kula chakula akantazama Kwa woga Dani pia alinitazama Kwa woga.

        "Lisa its you, ni wewe!?" Nilihoji kwa mshangao.

         "Dani naomba tuondoke."Lisa alimwambia Boyfriend wake ambaye bila kupoteza muda alisimama ili waondoke

         "Tafadhali msiondoke nisije nikaita POLISI." Niliwpigia kelele wakasimama wanaangaliana Kwa hofu na kutetemeka.

         "Hapana Mama usiite POLISI tutaeleza." Lisa Binti yangu aliyetangazwa ameaga Dunia MIAKA SITA iliyopita aliongea.

       "Si nyie mliaga Dunia MIAKA SITA iliyopita?" Nilihoji.

        "Nyie ndio mliotangazwa kwenye Radio, Television na mitandao ya kijamii kwamba mmekufa? Leo naota ndoto au?' Nilikua na maswali chungu nzima.

       "Mama tupo tayari kueleza."Lisa aliongea akitetemeka, Dani aliitamani kukimbia mbali na uso wangu lakini angelikimbilia wapi?"

        "Kueleza Nini? Kueleza juu ya ufufuo wenu?"Maswali yalinitoka.

      "Tafadhali keti mama keti chini tukueleze, "Lisa Binti yangu alinitaka niketi kitini lakini nilikataa kuketi akaanza kueleza kisa na Mkasa,

        "Tulifeki VIFO Mama, yote uliyoyaona au kuyasikia kwenye Television na mitandao ya kijamii sio ya KWELI Bali ni feki."Nilimsikiliza.

     "Sababu kubwa ya kufeki juu ya VIFO VYETU ilitokana na  Siri nzito ya mafanikio tuliyoyapata." Niliendelea kumsikiliza.

       "Mafanikio yetu yalitufanya tuisi Dunia na watu wetu wa karibu wangelitusumbua sana kwahiyo tuliogopa usumbufu. "Nilimsikiliaza Binti yangu.

        "Mama tulishinda Bahati nasibu ya Taifa shilingi billioni Moja na nusu kwahiyo hatukutaka watu wajue mafanikio yetu maana tuliona wangelitusumbua,"Binti yangu alipumzika kussimulia.

      "Kwa Sasa sisi ni matajiri wa kutupwa. Tunapata kila kitu muhimu kitupacho raha na starehe za maisha, "Dani alimpokea Lisa kunena.

     "Kwasababu ya pesa, Raha na starehe ndio mfikie hatua ya kufeki VIFO,?"Nilihoji Kwa kisirani. Walishindwa kujibu.

      " Hivi Lisa na Dani mnajua jinsi Gani mlivyotuweka katika wakati magumu? Mnajua jinsi Gani tulivyoumia na kupatwa na mishituko juu ya vifo vyenu feki?" Walishindwa kujibu..   

       "Pesa uondoa utu na ubinadamu. Pesa umpa mtu kiburi na kumuongoza vibaya, nimepoteza nyumba yangu sababu tu ya made ni uliyoyaazima Lisa."Machozi yalinibubujika.

      Silii ati Kwa sababu ya Numba yangu ilizyopigwa mnada na KAUSHA DAMU mlikoazima pesa Kwa Siri na kuiwekeza nyumba yangu kama Dhamana. Nalia Kwa sababu mmetuweka katika majonzi na huzuni alafu Leo tuambiwe waliokufa kwenye ajali ya gari wamefufuka?" Niliongea.

     "Mama utusamehe'Waliniomba msamaha"

     "Kama mnataka msamaha wangu tafadhali Lisa twendeni nyumbani tukaongea na kuyamaliza'Niliwapa mtihani. Lisa alionesha darili za kukubali kurejea nyumbani lakini Dani Alimzuia

      "Lisa UNATAKA kuniacha mpenzi? UNATAKA kuniacha na kumfuata mama yako? Haunipendi Lisa? Dani aliushikiria mkono wa Lisa Binti yangu aliyeonekna kunenepa na kupendeza. Nguo alizovaa zilikua ni nguo za bei gharama. Vidani vyake masikioni na puani vilikua Dhahabu tupu achana na Uzuri wa nywele zake zilizopamba Vito vya lulu na almasi hakika Binti yangu alipendeza."

          "Niruhisu Dani niruhusu nirejee Kwa mama."Lisa alionesha Darili za kunifuata.

"Hapana Lisa, hapana siwezi kukuruhusu. Je, tumepungukiwa Nini? Hatuli vizuri? Hatuvai au kufanya starehe za gharama? hatuizunguki Dunia? Lisa MPENZI tumepungukiwa Nini? Kama pesa tunazo ni pesa za kutulisha MIAKA zaidi ya ishirini bado tu zitabaki nyingi. Tafadhali Lisa, Tafadhali nifuate Mimi ninayekupenda."Dani alimshawishi Lisa nikawaona wanaondoka pale chakulani wakiwa mwameshikana mikono na kukumbatiana viunoni. Niliumia, niliumia sababu damu ni nzito kuliko MAJI. Lisa bado ni Binti yangu ni Binti madogo kuyajua MAISHA. Pesa isiwe sababu ya kunitenganisha na Binti yangu Lisa.

        "Lisa Binti yangu MPENZI tafadhali nifuate."Nilimwita Lisa ambaye alikua akitoweka taratibu huku akiwa anaigeuza Shingoye kuniangalia.Hakika MAPENZI yalimtawala Lisa hata afikie HATUNA ya kukataa kunifuata mamaye mzazi. Chozi lilinibubujika

##########

Semina iliisha nikiwa ningali katika dimbwi la mawazo, nilimuwaza Binti yangu Lisa niliwaza alivyoniweka katika Dimbwi zito la wasiwasii, nikaruhusu YAPITE na MAISHA yaaendelee ingekuwa vema niende POLISI kuripoti lakini niliona  hapana Wacha nimpe Lisa nafasi nyingine milango yote ya kuingilia nyumbani kwangu ipo Wazi akiona yafaa atarejea.

     MIAKA mitatu mingine ilikatika bado tu sikuiona sura ya Lisa Binti yangu, sikuenda POLISI kuripoti Nilimpa nafasi, nafasi ya kurejea, na KWELI siku Moja mvua kubwa ilikua ikinyesha nikafanya hima kwenda kumfungulia mgomgaji aliyekua akigonga mlango wangu.
    
       Eeh! Nilishangaa  nilishangaa mara baada ya kuiona sura ya Binti yangu Lisa amesimsma barazani, nguo zake zikiwa zimeloa MAJI, nywele zake nywele zile nzuri zenye afya tele zilikua zimekatika tena zipo ovyo zinanuka. Nguo zake chafuu zimeoza na kuharibika, alidhoofu sana Kwa kifupi alikua kama mwenda wazimu asiyetamanika. Nilimshangaa.

        "Tafadhali mama naomba niruhisu niingie ndani,"Aliomba

        "Ok. ingia'Nilimfungulia mlango na kmruhsu aingie.

 Nikalichukua taulo zito na kumpatia ajifute MAJI yaliyojaa mwilini

        "Utakunywa kahawa au tangawizi? Nilimuuliza

        "Asante Kwa kunijali mama nitakunywa kahawa."Alinijibu nikaingia jikoni kuandaa kahawa ajili ya Binti yangu Lisa. Baada ya dakika chache nilirejea na birika la kahawa na vikombe viwili.

       'Nisamehe mama."Aliongea mara Bada ya kugida fundo zito la kahawa.

      "Pole "Nilimfariji chozi zito lilimtoka

      "Nisamehe Leo nimeamini asiyesikia la mkuu uvunjika miguu, mtoto mleavyo ndivyo akuavyo na mdharau mwiba umchoma."Nilimfuta chozi nikaendelea kumsikiliza.

     "Tuliposhinda bahati nasibu Dani alinidanganya tufeki VIFO Ili jamii isitusumbue maana tulikua na mabillioni ya pesa...... Aah! Jamani Leo hii Dani amenikimbia niponipo tu kama Tajiri aliyefilisika." Aliongea.

     'Tatizo Nini Lisa? Nilimuuliza

      "Bora ningelikusikiliza mama, Bora ningelisikiliza sauti YAKO uliposema nirejee nyumbani pamoja na wewe... Ona mama, ona nimerejea mpweke."Aliongea Kwa hisia

      "Dani amenikimbia pia amekimbia na mapesa yote tuliyoshinda kwenye Bahati nasibu yaani sijui niwapi alipokimbilia?" Aliendelea mkusimulia.

      "Kwasababu tulikuwa na pesa nyingi Dani alinishawishi tuanze kuchezea kamari.Nilikubali Mimi na Dani tukaanza kuchezea kamari kwenye makasino na makumbi makubwa ya Kamari. Kamari ilipomtawala Dani akaanza kuweka dau kubwa kubwa la pesa kumbe ndio HATUA ya yeye kufilisika. Alifeli mara nyingi na alipoona pesa zinakimbilia ukingoni akaend Benki kuzichota pesa zote Kisha akakimbilia pahali nisipofahamu. Dani ameniacha mikono mitupu yaani Sina hata mia mfukoni."Nilimsikiliaza, Lisa mwanangu aiyetoa chozi lenye kamasi.

        "Pole sana marehemu uliyefufuka."Nilimkebehi Binti yangu,

         "Sasa Binti yangu UNATAKA nikusaidiaje maana pesa zilizokupa furaraha na kiburi zimekukimbia?

         "Nisamehe mama ninataka kuishi na wewe Tena." Aliomba uso wake ukiwa tumejaa huruma.

          "Sawa, suala la kuishi na Mimi sio mzigo tunaweza kuishi wote iwapo utalifuata jambo Moja tu.?Nilimwambia     
   
           "Jambo gani hilo mama?'Aliniuliza.

            "Nenda kajisalimishe POLISI pahali salama kwako"

            " POLISI tena mama.?Alishangaa.  

           "Ndio mwanangu POLISI ndio pahali salama ukienda kujisalimisha utakuwa na amani ila usipojisalimisha utaandamwa na wengi na hao wengi watakukata tamaa.'Nilimpa matumaini.

        "Nisaidie mama"Aliogopa

         "Usiogope Binti yangu bado unayonafasi ya kuishi na mmi na Ili uishi na Mimi sharti uwe na amani." Nilimshauri, aliketi Kimya zaidi ya dakika ishirini Kisha akanena.

       "Sawa mama nitaenda lakini si utanisindikiza.

       "Ndio Lisa nitakusindikiza kwanini nisikusindikize? Nashukuru Mungu upo hai, bado ninakupenda Binti yangu,' Niliingia chumbani kwangu nikatoka na nguo mpya safi, nikamtaka Lisa avae tutoke twende POLISI.







######


TCHAO







  

No comments:

Post a Comment

I promise you

   I PROMISE YOU. (NINAKUAHIDI.) SURA  YA KWANZA. UBAYA WA POMBE. “Umenizingua job, umenizingua kwa muda mrefu sana mpenzi wangu…….kwanini l...