SEHEMU YA PILI
HOSPITALI.
Cheppe alichanganywa, alichanganywa kwa yale mneno aliyoyasikia kutoka kwenye kinywa cha yule sangoma(mganga wa kienyeji). Mjadi yule hakutaka kumwambia ukweli na bwana Cheppe aliporejea nyumbani hakutaka kumwambia mkewe ukweli juu ya kauri alizonena yule Dakta wa jadi, bwana Mbeleko.
Cheusi alikonda na kudhoofika, hakua na afya wala uzima tele, ukimtazama huwezi kuamini kama cheusi ndiye yule binti mweusi ambaye hapo awali alikuwa ni mrembo mzuri wa kuvutia ameshiba amenawili na kutakata, anapendeza na kuvutia.
Leo hii Cheusi hana tofauti na kipande cha karatasi inayochanika, amechoka, amedhoofu, ameharibika, hatamani wala hatamaniki. Hatamani kuishi wala hatamaniki tena mbele ya kundi kubwa la wanaume walevi, wakulima madereva wa maroli makubwa na watu wengine wengi waliomtamani kimwili.
Baya zaidi mumewe Cheusi bwana Cheppe hakuwa ni mtu wa kuketi nyumbani. Siku mbilii alizoonekana nyumbani zilikua ni siku tosha, siku nyingi kwake kuketi nyumbani pamoja na mkewe Cheusi. Siku ya tatu angeli safiri pamoja na roli lake ambalo moja kwa moja angeli elekea mikoani kusambaza bidhaa kutoka kwenye kiwanda alicho ajiriwa afikapo mikoani jamaa ukaa na kupumzika wiki mbili tatu au nne ndipo ufanya kurudi nyumbani kwa mkewe amfurahishe kimahaba na kumpatia uzima wa ndoa.
Itakumbuka kwamba Cheusi alikwisha jenga mazoea, tabia ya kuwakusanya wanaume ndani ya nyumba ya mumewe, akiisha kuwakaribisha utenda nao zinaa pasina mumewe kujua, tizama sasa aibu imelipuka na kumkamata, tamaa mbele mauti nyuma asiyefunzwa na mamae dunia itamfunza, hakuwa mwaminifu ndani ya ndoa yake, alikua akilala na kila mwanaume mwenye pesa zake na matokeo yake amezoa UKIMWI anajuta na kulia kwa uchungu.
******************************
“Vipi bwana Dakta mke wangu anaendeleaje?” Cheppe alimuuliza Dakta John, wakiwa ndani ya hospitali kubwa ya kijiji cha mkuranga (pwani). Ndani ya chumba cha hospitali hiyo Cheusi amelala juu ya kitanda kikubwa, chupa mbili za damu zingali zinatembea ndani ya mishipa yake, chupa mbili za maji zingali zinamsubiria huyu binti mwenye umri wa miaka ishirini na mitano umri sawa na mumewe.
“Hali ya mkeo kidogo hajambo.” Dakta john aliongea maneno ya kufariji ili asimvunje matumaini bwana Cheppe yeye binafsi alijua na pia alifahamu fika kuwa hali ya Cheusi haitamaniki.
“Dakta hivi ni kweli kusema kuwa mke wangu ni mgonjwa wa HIV/AIDS au labda vipimo vinazingua, vinaonesha tofauti na matarajio?” Cheppe aliongea, pembeni yake yupo mwanaye James mtoto mwenye umri wa miaka mitano bado anahitaji malezi ya baba na mama.
“Kabla sijakujibu swali lako embu bwana Cheppe niambie, mpaka sasa wewe na mkeo mmerudia mara ya ngapi kupima damu zenu?” Dakta aliuliza.
“Ni mara ya tano sasa.”
“Na vipimo vimeonesha nini?”
“vipimo vimeonesha kwamba mimi na mke wangu, tumeathirika kwa ugonjwa wa UKIMWI.”
“Hilo ndilo jibu bwana Cheppe hata ukienda kupima afya yako nje ya Tanzania vipimo vitabaki kuwa ni vile vile, tayari mmenasa juu ya UMEME. Dakta aliongea wakati huo Cheusi alikuwa katika usingizi mzito kama vile tayari amegeuka maiti.
“Duh! Embu niambie Dakta, hivi je huna imani kusema kwamba ugonwa huu wa HIV/AIDS kuna nguvu fulani za kishirikina ambazo mke wangu ametupiwa? Nina maanisha kuwa mke wangu ametupiwa jini ili limuue taratibu taaratibu na kisha baada ya jini kumuua mke wangu liniue na mimi au mwanetu James.” Cheppe alirejea mawazo feki aliyopandikizwa na Mganga Mbeleko.
“Idont trust about majini, siamini kuhusu ushirikina, mie nina amini kwamba ugonjwa huu wa UKIMWI una sababu zinazopelekea uwepo na kusambaa, miongoni mwa sababu hizo ni mtu au watu kufanya ngono zembe (pasina kutumia kinga), kuchangiana zana zenye ncha kari kama vile nyembe sindano na mikasi, Kutoka kwa mtu aliye athirika kwenda kwa yule aliye salama. Pia kuna kuongezeana damu, yaani mwathirika kumchangia damu yule ambaye hajaathirika na hii mara nyingi ufanywa na madakta wa vichochoroni, madakta feki waso na taaluma ya udaktari.” Dakta aliendelea kunena.
“Mama aliye athirika ajapo mnyonyesha maziwa mwanaye, maziwa hayo yajapokuwa na vimelea vyaugonjwa wa UKIMWI hilo nalo ni tatizo. Basi fahamu kwamba hizi ni baadhi ya sababu, zipo nyingi nyinginezo. Unapoongea kuhusu ushirikina mie binafsi siweki imani na nafsi timilifu.” Dakta John aliongea.
“Mmmmh! Nipo katika wakati mgumu sana bwana Dakta, sijui ni sababu ipi iliyompelekea mke wangu kuugua ugonjwa huu wa aibu na hatimaye kuniambukiza mimi nisiye na hatia.” Cheppe aliongea kwa huzuni.
“Embu niambie bwana Cheppe unalevo gani ya kisomo chako?” Dakta alimuuliza Cheppe.
“Mimi ni wa Standard seven.” Cheppe alijieleza.
“It’s good, embu niambie unajishughurisha na shughuri gani kuyaboresha maisha yako naya familia yako?”
“Mimi ni dereva wa maroli yanayotoa mizigo Dar es saalam na kuyasambaza mikoani.”
“Alirght, unampenda sana mkeo?”
“Yes, Dakta nampenda sana mke wangu.”
“Ok. Sasa unapaswa kumuuliza sababu kuu iliyo pelekea ugonjwa aliokuambukiza, yanini umkalie kimya wakati unayo haki ya kujua?” Dakta aliongea.
“Dakta watu wengi wanasema kwamba matatizo sio kushindwa bali ni kutafutia mbinu ya kuyatatua, sikatai kusema kwamba nimejitahidi sana kumuuliza mke wangu nini haswa kilichomsababishia ugonjwa huu wa bahati mbaya.”
“Hajakujibu?”
“Ndio, nashindwa kumuelewa bwana Dakta,”
“Duh! Ok! Usife moyo endelea kumuliza pamoja na kupeleleza njia zake, njia alizo pitia pindi haupo naye karibu, waweza kufanikiwa kupata jawabu nini haswa kimesababisha apatwe na ugonjwa wa UKIMWI?”
“Njia……… Mbona nimezunguka kila njia nimefika kwa waganga wa jadi walioniambia kwamba mke wangu alirogwa, ametupiwa laana na mikosi.”
“Usiamini sana mambo ya jadi, mimi ni msomi, ndio maana ninajaribu kukusaidia, endelea kupeleleza njia alizopitia mkeo.”Dakta aliongea wakati huo huo alihitaji kuendelea na shughuri zake za kuhudumia wagonjwa wengne.
Itaendelea
No comments:
Post a Comment