PAPA J.J
(PAPA SIMBA)
“What!?” Papa J.J alifoka kupitia simu yake ya mkononi,simu ndogo aina ya Mobitel au kwa jina lengine ‘Mkweche wa kichina,’ simu za zamani sana,toleo la kwanza, haziharibiki wala hazichachi ni simu bomba kwa kudumu zipodurable zinadumu
“That’s all my Lord,ndio hivyo bwana raisi,wakurugenzi wote wa serikari wameitisha mgomo,ati wadai kwamba mishahara wapewayo haitoshelezi ni midogo kama mbegu ya haradali”. Waziri domo aliongea kwenye simu
“Ok.its alright,nipo kwenye uwanja wa Ndege ninakuja leo leo,naomba,uitishe kikao pale ukumbi wa kondeni,wapigie simu wakurugenzi wote waambie asikose kufika mtu,kama kuna mtu atakosa basi ajue kibarua chake tayari kimeota nyasi,amemwaga unga yeye mwenyewe sidhani kama nitamuhurumia”. Papa JJ aliongea akitafakari tafakari,wakati wote huo Ndege ilkuwa ikimsubiri ilimhitaji muda ulikua bado ni asubuhi jua ndio linatabasamu.
Papa JJ,ndiye raisi wan chi ya Konde, yeye ndie kiongozi mkuu wa nchi ya Konde, yeye ndiye sauti ya mwanzo na akikataa amekataa na akikubali basi Papa jj amekubali,lazima asikilizwe na lazima aogopwe yeye ndiye mkuu wan chi ya Konde ameshikilia miliki yote,ameshikilia mali na rasilimali zote za nchi ya Konde.
“Ametumia siku yote ya jana kuzindua miradi miradi mbalimbali mikoa ya kusini mwa konde,amezindua viwanda vingi siku ya jana miongoni mwa hivyo kuna kile cha kuzalisha madawa ya konde,kina kile cha kutengeneza unga,kipo kile cha sabuni na mafuta,haki Papa jj ameanza kuyaona maendeleo ndani ya nchini ya Konde juzi kabla ya jana na leo alikuwepo katikati ya nchi ya Konde akizindua miradi miwili mmoja ni ule wa kujenga barabara ya reli mpya itakayotumia nguvu za umeme kuizunguka nchi nzima ya Konde,mradi wa pili ni ule wa ujenzi wa bomba kubwa la mafuta yaliyogundulika kuwepo chini ya aridhi ya Konde haki,Papa jj,anajivunia mafanikio mengi ndani ya utawala wake, ambao amesifika kwa kukomesha rushw,ufisadi na upotevu wa rasilimali nyingi za taifa la Konde.
Aliposhuka juu ya kiwanja cha ndege Konde akitokea mkoa wa kusini mwa Konde,Papa jj hakutaka kuelekea Ikulu,moja kwa moja alienda ndani ya ukumbi mkuu wa mikutano ya kitaifa na kimataifa,ukumbi wa Konde,ukumbi uk umbi uliopewa jina la “fundo lao”naye akiwa na wingi wa hasira iliyojificha moyoni mwake asitake kuonyesha aliingia na kuketi kunako kiti kilichowekwa maalumu kwa ajiri yake ikumbukwe kua hao wakurugenzi wa idara mbalimbali,idara za elimu,idara za mawasiliano,idara za mariasili,idara za ajira idara za afya na kadhalika walikuwepo hapo konde wakimsubiria mheshimiwa raisi aliyeitisha mkutano wa dharura(emergency)
Na dharura yenyewe wasitake kuiacha wakiwa hawajui ae au bee,wamechanganywa na wito wa Papa jj,wanamjua vizuri papa wanamjua kua ni mtu asiyetaka masihara,akinena amenena, akigoma amegoma.
“Kwanini mmeitisha migomo,tena nimesikia migomo yenu mnataka iwe ni migomo ya nchi nzima?”.Papa jj aliwauliza hao wakurugenzi kwa sauti kuuu,pembeni yake yupo waziri domo upande wa kushoto na upande wa kuria hakosekaniki makamu mkuu wa nchi ya bonde.
“Mheshimiwa,mtukufu raisi wetu wan chi ya Konde”Alianza kuongea mkurugenzi mkuu wa idara ya afya.
“Tumeitisha mgomo,yote kwasababu ya maslahi,maslahi yetu ni madogo sana,malipo ya mishahara ni kama punje ya mtama,haya tutosherezi mahitaji mbalimbali ya huduma za maisha yetu,”Mkurugenzi wa afya aliongea kwa papa wakati wote huo papa alitega sikio lake asikilize kwa umakini kilio cha hao wengi
“Bado sijaridhika embu nipeni mfano”.Papa jj alihitaji kuelezwa zaidi mkurugenzi wa elimu alisimama ili atoe mawazo yake,yeye alijitambulisha kwa jina la Bwana kanyau wakati yule wa idara ya Afya alijitambulisha kwa jina la Bwana mapunda.
“Mheshimiwa mtukufu Papa JJ ”.Bwana kanyau aliongea tumbo lake kubwa lilifanya shati yake nyeupe lichomoze kiunoni na kujiachia,haki mkurugenzi huyu anatumbo kubwa kama kontena.
“Tunapozungumzia kuhusu masilahi yetu tunazungumzia pia ongezeko la masilahi yetu,posho zetu na malimbikizo mengine ya mishahara yetu kiduchu haiwezi kuendelea kutuinua kiuchumi ilihali ata wewe mwenyewe Papa unajua namna gani,hali ya maisha inavyobadilika badilika,bei ya bidhaa muhimu inapanda kila uchao,gharama za elimu hazishuki,gharama za matibabu hazishuki,yaani kwa ufupi kile kidogo tupatacho ni kama vile hatukipati yote kwasababu kijapotumiwa uisha hata kabla ya mwisho wa mwezi”.
“Aliongea mkurugenzi wa elimu bwana kapuusi akashangiliwa na mamia ya wakurugenzi”.
“Sawa nimewasikia,Papa aliitikia kwa ufupi kisha akaandika andika kwenye note book yake,mara ile mda si mrefu akafungua tena kinywa chake apate kunena.
“Embu niambie,mishahara yenu inaanza kimo gani cha juu na pia kinaishia kimo gani cha chini?”.Papa alihitaji kujua,ingawaje alijua vema kimo cha mishahara yao”.Alisimama mkurugenzi mkuu wa idara ya fedha Bwana Mwenda kasi naye akafungua kinywa chake apate kunena.
“Mheshimiwa mtukufu raisi wan chi ya Konde,Papa JJ,kila mkurugenzi analo daraja lake la mshahara,yapo madaraja makuu matatu,daraja la kwanza linaitwa daraja”A”,daraja la pili linaitwa daraja “B” na daraja la tatu linaitwa daraja “C”.daraja “A”ni lile daraja ambalo linazingatia na pia linaangalia kama mtumishi amefanya kazi kwa muda wa miaka zaidi ya 30 au 20,basi huyo ulipwa mshahara wa shilingi million saba na nusu,daraja “B”ni lile daraja ambalo linaangalia(linazingatia)elimu ya mkurugenzi iwapo ana degree ya tatu au ya nne basi atalipwa mshahara wa shilingi million tano,daraja “C”ambalo ni daraja la mwisho mkurugenzi ulipwa million tatu na nusu,daraja hili haliangalii muda wa kuwepo kazini(miaka)au kiwango kikubwa cha elimu,yote kwasababu wakurugenzi wengi wanaopokea mshahara wa daraja “C”ni wapya kazini.Hivyo basi mheshimiwa Papa JJ tunaomba nyongeza ya mishahara yetu,ugumu wa maisha unasababisha tusugue sana vichwa ata tushindwe kupata jawabu la wapi na wapi tutapata riziki zetu ikiwa mishahara yenyewe ndio hiyo haba na haba”.
“Ndio!ndio!ndio!ndio!
“Embu tulieni nyinyi mnataka muongezwe nyongeza ya bei gani(shilingi ngapi)kwenye mishahara yenu?Papa alikuwa mtu wa kudadisi siku ya leo,hakika alionekana dhahiri kutokua tayari kutatua changamoto za watu wake pasina kujua nini na nini cha muhimu katika mwafaka wao
“Asante sana mheshimiwa Papa JJ kwa kunipa hii nafasi nzuri ya kueleza hitaji letu,mkurugenzi mkuu wa idara ya Ajira alianza kwa kutoa shukrani,siku ile kila mkurugenzi alikua na haki ya kuongea.
“Tumekaa tumefikiria kwa pamoja kwamba,tuiombe serikali yako tukufu ituongezee kimo cha mishahara yetu,kwa kuzingatia madaraja yetu makuu matatu.kwanza kabisa daraja “A”daraja la wakurugenzi walioitumikia serikali kwa muda mrefu tumekubaliana kwamba baada ya kupokea mshahara wa shilingi million saba na nusu,tunaiomba serikali ituongezee million mbili na nusu ili ziwe million kumi,daraja “B”ambalo mshahara wake ni shilingi million tano,lipandishwe nalo lipokee million saba na nusu,wakati daraja “C”ambalo mshahara wake ni million tatu sio mbaya iwapo kutakua na nyongeza ya shilingi million tano.Haki hapo wakurugenzi wote tutaridhika,na kufanya kazi kwa bidii kwa juhudi na kwa maarifa”no uvivu,no uzembe,no kulalamika na kuwaza hali ngumu ya maisha”.Mkurugenzi huyu aliyejitambulisha kwa jina la bwana Mpori mpori aliongea na kuwaachia vicheko vya furaha wale wakurugenzi wote waliohudhuria wito wa Papa JJ.
Itaendelea
No comments:
Post a Comment