SURA YA SITA
TUZO.
Shughuli nzito ya kutambikia lile zoezi ilianza, shughuri nzito ya kuomba Mizimu ilianza, ilikua ni shughuli nzito kweli kweli, yalikua ni maombi makuu, ngoma za jadi zilichezwa, watambikaji wakala nyama ya hilo tambiko wakanywa pia vileo vilivyo andaliwa kwenye lile tambiko, tena wakaimba na kucheza.
“Mwenye makosa aonekane,
Watambaji waalimba nyimbo zao, wakiiomba Miungu itende haki, pale haki inapotakiwa kutendwa pamoja na kuiomba Miungu itoe adhabu pale uvunjifu wa haki ulipoonekana kushika nafasi yake, maombi yaliendelea kuombwa. Mizimu iliombwa itende haki ili apate kuonekana ni nani aliye na makosa ama ni nani asiye na makosa? Ni upande gani ulio stahiri kupewa adhabu ama ni upande gani ulistahiri kutunukiwa tuzo ya heshima? Kwa sababu ya ukweli na uwepo wa haki isiyo na kasoro.
Wazee wa mila walikua na kibarua cha kupiga manyanga, walipiga manyanga, walipiga manyanga, walipiga manyanga, walipiga manyanga weee! Walipiga manyanga kama wendawazimu masaa nenda masaa rudi waliendelea kupiga manyanga wala wasichoke kupiga manyanga, kelele za mayoe pamoja na nyimbo, makofi vifijo na nderemo kwa pamoja vilisikika mbele ya hadhira kubwa iliyo hudhuria.
Mwisho ngoma ilifikia tamati, Mizimu pamoja na roho wengine waovu wakajibu sala za wazee wa mila.
Matokeo ya maombi yao yalionekana mbele ya hadhira, kila mwenye macho mawili aliyaona matokeo ya lile tambiko, masikini mzee Jamali yaliyo mkuta yasiwe ya kuadithiana yaliyomkuta ni mazito ya dunia, yaliyomkuta yanatisha na kuogopesha.
Kumbe ni yeye binafsi aliyekutwa na hatia kumbe ni yeye ndiye mkosaji, kumbe ni yeye binafsi ndiye….. loh! Waswahili walisema umdhaniaye kuwa ndiye kumbe sie. Waswahili walisema hisia hazijengi, wengine walisema fikiria kabla ya kutenda, heri nusu shari kuliko shari kamili. Looh! Masikini mzee Jamali alibadirika na kuwa na umbo la mnyama wa kufugwa.
Kila aliyepata kumuona mzee Jamali akiwa katik a umbo lile alisikitika na kuogopa pia. Tizama haraka haraka imemnyima baraka, tizama kuficha ficha kwake mambo kumemfanya apungukiwe heshima mbele ya jamii iliyomzunguka, aibu ya karne aibu kuu. Mzee Jamali alikimbilia nyumbani kwake, alikimbia kama vile Ng’ombe akimbiavyo akajificha ndani ya nyumba yake, huko akalia machozi, akalia kilio cha kwi! Kwi! Kwi!
Itaendelea
No comments:
Post a Comment