SURA YA TATU
HALI SIO SHWARI.Eve aliporejeshwa nyumbani baada ya kukumbwa na balaa lile, hali yake haikua nzuri, homa za mara kwa mara zilianza kumwandama, mara apone mara zimrejee tena, siku nenda siku rudi afya yake ikawa na mgogoro, kutapika, kuhara damu, mafua yanayo pona na kurejea, maralia isiyo tarajiwa uchovu na uvivu wa mwili vyote kwa pamoja vilimwandama.
Hakutaka kwenda kumuona Dakta ili apime kugundua ni tatizo gani linalo msulubu, Eve alikwisha jitambua, Eve alikwisha tambua kwamba maji yamemwagika kamwe yasingezoleka. Alikwisha kijua kile alichopandikiziwa na mumewe mpenzi Dini haba tayari kimekwisha anza kuonesha darili, waswahili wanasema ‘mti ukipandikizwa utaota, usipo ota basi kuna hitilafu.’
Leo hizi Homa za mara kwa mara hazimweshi, Eve anaugua na kuugulia maumivu mazito juu ya kitanda chake. Mpenziwe Eve Vina visenti amekuwa mfariji mkuu katika kipindi hiki cha mapito yenye dhiki.
“Eve kwanini hautaki tumwite Dakta atizame afya yako, apime na kujua ni ugonjwa gani unao kusumbua.” Vina aliongea. Kaendelea kunena.
“Yafaa nini uendelee kumeza madawa ya kila aina, wakati huo huo madawa hayo hayakusaidii yanakuachia mateso na maumivu.” Vina aliongea, amani ilitoweka moyoni mwake akimwona mrembo wake anavyougua.
“Nitapona mpenzi, nitapona hivi karibuni, maombi yako please, maombi yako yatosha kunipa ubukheri, yote haya yanatokana na ile mimba kuji ‘abort’ (kutoka), ujauzito huu umeniletea madhara makubwa sana.” Eve alijitetea akijua fika kuwa maji ndo hayo yashamwagika, darili ya mvua mawingu na darili za ugonjwa wa UKIMWI ndo’ hizo amezishikilia mikononi mwake baya zaidi zinajionesha.
“Sawa mpenzi nitafanya sala kwa ajiri yako, nitakuombea uzima na afya upone ukaponeka.” Vina alipumzika kidogo kuongea. Nukta chache badae akanena tena.
“Kesho nitakwenda nyumbani Nairobi, nakwenda kuitazama familia yangu baada ya muda nitarejea.” Vina alimpatia Eve taarifa.
“Wasalimie Kenya waambie nyumbani Tanzania tunawapenda.” Eve aliongea, Vina akatabasamu.
“Ungelipenda nikuletee nini mpenzi wangu iwapo nitarejea maana nitachukua muda kidogo?” Vina alimwambia Eve achague zawadi yoyote ile aipendayo.
“Chochote kile unachoweza kubeba mpenzi wangu, ila nitafurahi iwapo utaniletea maua yenye rangi nyekundu, hayo ni faraja kwangu.” Eve aliongea.
“Alright! Iwill do so.” Vina aliitikia. Usiku ulipoingia wakala na kulala.
*****************************
Vina alihitaji kupumzika Nairobi nyumbani kwa mkewe kwa kipindi cha miezi mitatu, hiyo ndiyo rikizo anayojipatia yeye binafsi. Huko ana biashara zake, mkewe ndiye msimamizi mkuu wa hizo biashara zake. Tanzania pia ana maroshani (maduka) yake, amewaachia vijakazi waaminifu wapate kusimamia biashara zake yeye akiwa nyumbani Kenya anakula bata na mkewe.
Ana muda mrefu kwenye biashara zake, miaka kumi sasa, anaenda Kenya na kurudi Tanzania, anajibidisha anajituma, ili apate riziki, kama waswahili wanavyo sema riziki popote mola mgawaji. Ana kawaida ya kukaa kwa zaidi ya miezi miwili au mitatu akiwa Tanzania kwenye biashara zake wakati huo huo uikumbuka familia yake iliyopo Kenya, basi atarejea haraka apate kuwa karibu na familia yake.
Itaendelea
No comments:
Post a Comment