Mm ni POLISI
Mtu mzuri Kwa raia
Mlinzi na mlinda Mali na raia
ππ¦Ί Yaani walinzi
BASI siku Moja
Nilikua Restaurant Moja inaitwa Mac Donald Rest
Nilikua nikipiga kahawa na mabums MDOMONI π©
Mung'unywa mung'unywa nilitafuna
Bila wasi wasi
Maana kawaida YANGU kila ifikapo mida ya jioni
Lazima nipige kahawa na madonats
Bai bwana nikiendelea kumung'unya mung'unywa
Nilishituliwa na masauti ya kilio
Kilio Cha Binti mtu mzima
Upande wa kulia kwangu
Karibu na mlango wa Mc Donald Rest
Nikajisemea mtimani potezea
Lakini bado nilisikia masauti ya kulia
Kama vile mtu alikua ameanguka chini puu!
Raia mwema ametekwa!
Kombe langu la kahawa chini puu
Donati nayo ikanitereza chini puu
Noo! Man life is something precious π
Lazima nifanye kitu
Kuokoa MAISHA ya raia wema
Maana tumewachoka vibaka
WAMEZIDI kuongezeka mitaani
Wanaua
Wanateka
Wanaimba
WanFANYA MAOVU
Wanaweza hata kukupididi... Pidadi
Kamahujielewi hapa mjini
Lift your fuck hand up"
Nilimshurutisha yule haramia aliyemteka binti
Usoni alitisha, Hana macho
Meno yake mawili ta juu marefu
Nywele zimesimama kama majani ya ng'ombe
Shingoni amevaa chuma
Mkono wa mashoto amevaa chuma pia ameshikilia kisu kikali balaa
Mimi Nikajisemea hapana
Ngoja nimlipue kabla hajatenda ubaya
Pyuuuuuu , nikamfyatulia risasi
Bila kupoteza muda
Nyambaaaafu"
Shiti kabisa"
Haifai mijitu hii katika society"
Akaanguka chini
Tayari amezima
Kadedidi
Alikua akitetemeka
Akiogopa
Na kulia sana
Nilimshangaa
Badala ya kunishukuru
Yeye Analiaπ
Nilipigw BUTWAA!!!
Mbona sielewi
Waaandishi???
Mmh!
Wote wananishagaa
Mimi pia nawashangaa
Eeh!
Jesu!!
Waigizaji
Kuna huyu short alievaa miwani
Amebeba ubao umeandikwa
'Cut'
Duh!
Kwaiyo walikua Wana act movie
Au content?
Duh!
Msala,
Nina kesi ya kujibu
Murder case.
Na Jella inanihusu.
No comments:
Post a Comment