MICHELLE OBAMA’S PRAYERS.
(Maombi ya Michelle.)
Waswahili wanao usemi wao, mara ile watakwambia lisemwalo lipo lingoje. Ndivyo Michelle Obama alivyoyaweka ndani ya moyo wake hayamaneno mawili matatu ambayo hatimaye kwa imani yalikuja kutimia na kuwa kweli isiyopingika kusema kuwa umwombapo Mwenyezi Mungu yupo papo naye atakusikiliza maombi yako naye atakutimizia kwa muda na kwa kipindi mwafaka yawezekana timizo la hayo maombi yako likawa ni leo hii na muda huu ama timizo hilo likawa kesho, kesho kutwa, mwakani au mbele miaka ijayo.
Muhimu kumwomba Mwenyezi Mungu, muhimu kuiweka imani yako mbele na wewe utakuwa ni mwingi wa raha na furaha. leo hii Michelle Obama ni mwenye furaha na tena furaha yake ni bonge la furaha, furaha kubwa furaha ambayo kamwe haimtoki moyoni mwake bali furaha hiyo umwachia tabasamu moja nono zito lenye wingi wa furaha. Michelle ni miongoni mwa wanawake (wale) wachache wenye majina makubwa sana duniani, ni miongoni mwa wanawake wachache waliobahatika kupata heshima ndani na nje ya Amerika, sio Amerika tu bali hata huko Asia, Europe, Australia, Afrika pmoja na visiwa vinginevyo vingi duniani.
Kuitwa ‘First lady’ sio jambo dogo ni jambo kubwa tena zito na tena linaloshangaza, ile mwanamke mweusi mwenye asili ya kiafrika kuingia ndani ya ‘White house’ kila mtu ni lazima ashangae sio tu kushangaa bali pia kumshangaa Michelle mwanamke mweusi mwenye asili ya Afro Amerika kuingia ndani ya jumba hilo kubwa lenye heshima duniani. Hakuingia bure bali aliingia kwa imani na maombi yake yeye kwa mwenyezi Mungu. Uzuri wa imani pamoja na maombi Mwenyenzi Mungu aliyasikiliza tena akamsaidia Michelle kutimiza matamanio ya moyo wake.
“Nilimwomba Mwenyenzi Mungu, nilimwomba kwa imani, nilimwomba pasina kuchoka, niliamini na pia niliweka imaniyangu iniongoze sikufa moyo nilijua itakua tu…….itakuja kuwa kama niombavyo” Michelle alikua akiongea na maelfu ya wanafunzi wa chuo kikuu cha Havard, siku moja alipo pata wasaa wa kuwatembelea.
“Kwa imani nilikua nikiongozwa na Malaika, Malaika aliyenipiga mwiko kukata tamaa, Malaika aliyenifunda kuendelea kuamini, yote kwa sababu imani pekee ilitosha kunifanya niamini kuwa mafanikio yangu mimi na familia yangu yatakuja.” Michelle alipigiwa makofi na hawa wanafunzi wengi pomoni wakati huo huo vyombo vya usalama vilitulia tuli vikimlinda asipatwe na kadhia yoyote ile vyombo vya habari navyo viliendelea kuchukua habari njema kama ile.
“Mungu ndiye mpaji wa vingi kwa mwanadamu, Mungu ndiye mgawaji wa vipawa na vipaji, Mungu ndiye mtoaji, mpokeaji na yeye ndiye baba mkuu wa imani. Kamwe Mwenyenzi Mungu hawezi kumwacha mtu mwenye imani,bali Mungu atamsaidia,kutimiza imani,mapenzi na mapendeleo ya mtu huyo” Michelle aliongea kwa ujasiri na haiba yake ilionekana wazi mbele ya kadamnasi ile.
Michelle ni mwanamama ambaye daima uambatana na mumewe Barack Obama popote pale aendapo hawezi kuwaacha pembeni wanawe wapenzi, Sasha na Maria lakini leo ilimbidi awe pekee katika hili kongamano kubwa lililoandaliwa na wanafunzi wa chuo kikuu cha Havard, sababu kuu iliyomfanya Michelle awepo pekee siku ya leo pasina uwepo wa mumewe au wanawe ni kwamba ubize ndio uliowafanya wawe na umbali huo, muda pia uliwafanya wagawane majukumu yao. wakati mumewe akiwa ndani ya white house akishughurika shughurika na mikutno ama kutia saini mikatataba muhimu ya kulinufaisha taifa hilo kiuchumi kisiasa na kidplomasia ama akitembelewa na wageni mbali mbali kutoka nje na ndani ya Amerika.
Sasha na Maria walihitaji kuwepo darasani kupata elimu ambayo kwayo ni ufunguo mkuu wa maisha yao. Kwayo ndiyo njia pekee ya kuishi kwa furaha, elimu ni kila kitu kwao, walihitaji kuudhuria darasani walihitaji kujifunza mengi wafundishwayo na walimu wabobevu katika taaluma wajuzi na wenye madegree yao.
Ndio maana siku ya leo Michelle hakuwa budi kuudhuria kongamano kongamano hili akiwa pekee ndani ya chuo kikuu cha kimataifa chuo cha Havard moja ya vyuo vikuu vitukufu ndani na nje ya Amerika chuo kinachozalisha maelfu ya viongozi wa dunia yetu, ukitegemea hata mumewe michelle bwana Barrack Obama amesoma hapo amesomea masomo ya sheria leo hii kwa nguvu ya maombi ya bibi michelle Barrack ni kiongozi mkuu wa taifa kubwa la Marekani naye anashika nafsi ya 44 mara baada ya viongozi wengine wa Marekani kustaafu, kuachia ngazi au kupatwa na umauti
Michelle aliendelea kuongea kwa imani,
“kumwomba mwenyenzi mungu ni tendo la milele na milele kumwomba mungu ni mkazo na msukumo ambao mkazaji na huyo huyo msukumaji anapaswa kuto kukata tamaa yote kwa sababu mungu umwombaye yupo papo naye anakusikiliza naye anakutimizia na iwapo timizo hilo halijatimia leo basi litatimia kesho au kesho kutwa ama siku yoyote ile ambayo mwenyenzi mungu anaijua yeye,”
“haijalishi ni lini yote umwombayo mwenyenzi mungu utafanikiwa hata ipite miaka elfu mia utafanikiwa.” Makofi furaha na vifijo vilisikika ndani ya Hall ( ukumbi) kubwa la kile chuo kikuu cha Havard.
Inaendelea
No comments:
Post a Comment