Mume wangu mie ni mjamzito,” Lupita alinishitua siku moja, siku hiyo tukiwa tumeketi mezani tunakula mlo wetu wa jioni (Dinner.)
“What? My God Jesus! Unasema kweli mpenzi mke wangu?” Niliongea kwa furaha kuu nikimtizama mke wangu Lupita, habari zile za furaha zilinishitua mtima wangu, damu ilinichemka na kwenda kwa kasi mithili ya Tetemeko.“ Ndio mpenzi mume wangu mie nina mimba ya miezi miwili sasa, tutarajie kumkaribisha mwanetu nyumbani sasa.” Lupita aliongea maneno matamu yaliyoufurahisha mtima wangu.
“Asante sana my love nimefurahia sana kusikia habari hizo ni habari njema za kufurahisha moyo, wacha mdogo wake Maliki- shua aje aungane na Maliki upweke umtoweke Mwanetu Maliki.”Niliongea kwa furaha wakati huo huo nikamkumbatia mke wangu Lupita kwa furaha, nikampiga mabusu mawili matatu kwa furaha.
“Asante sana mume wangu tuombe Mungu mtoto atakaye zaliwa awe ni mtoto wa kike mzuri mwenye furaha.” Lupita alitamani mtoto wa kike.
“Ni sawa, sawa mke wangu, mawazo yako yapo sahihi, wacha mtoto atakaye zaliwa awe ni wa kike ili aje akusaidie kazi za hapa nyumbani.” Nilimuunga mkono Lupita kwa pamoja tukiwa ni wenye Furaha.
##############################
Upendo wa mke wangu Lupita haukuwa mkubwa sana kama zile zama za kufurahia ndoa yetu, Sikujua kwanini Lupita hakuwa na furaha siku zote awapo pamoja na mimi, Sikujua kwanini Lupita hakuhitaji kuwa karibu karibu na mimi kama zile zama zetu za mapenzi moto moto
Wakati huu alijiweka bize zaidi kwenye kazi za kiofisi, wakati huu hakuhitaji kunipa nafasi ya kufurahi pamoja nayeye aliporejea kazini aliupitisha usingizi wake moja kwa moja hadi asubuhi siku iliyofuata, haki yangu ya ndoa hakunipa tena hakutaka kusikia usumbufu juu ya kuomba haki yangu ya ndoa nilijaribu kumbembeleza lakini wapi? Madai yake ya kuchoka kutokana na shughuri za kiofisini hayakumkauka Lupita.
Sikupendezwa na mabadiriko ya Ghafla ndani ya ndoa yetu nikajipa kazi kubwa ya kutaka kufahamu sababu zinazo mfanya mke wangu Lupita abadirike ghafla namna ile. Sababu zinazomfanya mke wangu Lupita asiwe na furaha awapo pamoja na mimi, sababu zinazomfanya mke wangu Lupita awe mkali mwenye wingi wa hasira hasara Nikaanza kumchunguza njia zake zote anazopitia lakini yote tisa kumi sikuweza kubahatika kujua nini haswa kinachomfanya Lupita wangu abadirike kiasi namna ile. Kila nilipomuuliza mke wangu Lupita kinachomfanya abadirike namna ile, niliambulia ukali kutoka kwake. Alikuwa mkali wa pilipili.
Nikachukulia labda ni sababu ya ujauzito wake, lakini hapana mbona Lupita alipokuwa na ujauzito wa mwanetu Maliki-Shua hakuwa na ukali wa namna ile,hakuwa na hasira pamoja na matukano, hakuushusha upendo wake kwangu, alinithamini na kuniona mie ni mtu muhimu kwake. Hapana Lupita amebadirika na tena amebadirika mbadiriko makubwa yamkini kuna jambo linamkwaza lakini hataki kuniambia.
Basi miezi mitisa ilipita , uchungu ulimkamata Lupita haraka haraka nikamkimbiza Hosptalini, kufika Hosptalini Madakta wakamhudumia Lupita. Haraka haraka akajifungua mtoto wa kiume, furaha ilinijia mtimani mwangu mara bada ya kuambiwa kuwa mke wangu mpenzi amejifungua mtoto wa kiume, furaha ilinijia mtimani mwangu mara bada ya kuambiwa kuwa mke wangu mpenzi amejifungua mtoto wa kiume, haki ya mungu nilimsifu sana Mwenyezi Mungu kwa wema na upendo wake kwangu
Lakini kuna jambo moja ambalo lilinikwaza, lakini pia sio kunikwaza mimi bali ndugu wa ukoo wangu walikwazika pia, kwa sababu ya sura aliyonayo mtoto aliyezaliwa masaa machache yaliyopita.Mtoto hakufanana na mimi wala mtoto hakufanana na Lupita. Mtoto hakuchukulia sura ya ndugu au jamaa yoyote yule aliyetoka katika ukoo wangu au ukoo wa Lupita. Jambo hilo liliamsha maswali mengi kutoka kwa wanandugu, jamaa na marafiki wetu
“Mbona mtoto hafanani na baba yake mzazi?” Baba yangu mpenzi alimuuliza Lupita ambaye hakulijibu lile swali, alitizama chini kwa aibu. Hatukupenda kumchosha Lupita kwa wingi wa maswali ambayo tulihisi yanaweza kumchanganya na kumvuruga amani ndani ya moyo wake basi tuliona ni vema kama atapata muda mwingi wa kupumzika sababu ametoka kwenye uchungu wa uzazi
Ghafla furaha na raha ya Lupita ilipotea, kwanini Lupita hakuwa na furaha? yawezekana ni kutokana na Uchungu wa uzazi aliotoka kujifungua. Lakini yote tisa kumi hatukujua ni nini haswa kinachomkwaza Lupita
Ilipita miezi mitatu mara baada ya Lupita kujifungua, yule mtoto akaibu Gubu ndani ya Nyumba yetu, akaninyima raha na furaha kwa sababu……..
Ilipita miezi mitatu mara baada ya Lupita mke wangu kujifungua, mtoto aliyezaliwa aliibua gubu ndani ya nyumba yetu, yule mtoto alininyima raha nafuraha kwa sababu ndugu wa upande wangu hawakutaka kumtambua yule mtoto ndugu wa upande wangu walidai kwamba mtoto yule hajafanana na mtu yoyote yule katika familia au ukoo wangu sembuse iwe kwenye ukoo wao Lupita.
Nilimuuliza Lupita nilimuuliza mara kwa mara anieleze juu ya tuhuma na gubu la ndugu kulalamika kuwa mtoto aliyezaliwa hafanani kabisa na mtu katika ukoo wangu au ukoo wake.
Lupita alinijibu kwa kuniambia mtoto yule ni mtoto wa ukoo wetu sipaswi kuwa na wingi wa mashaka juu yake. Mimi sio mume bwege moyo wangu uliniambia sipaswi kuwa mume bwege kama rangi iliyo mbele yangu ni rangi nyeusi kwanini niite rangi hiyo nyeupe na kama rangi iliyo mbele yangu ni nyeupe kwanini niite nyeusi? . hapana macho hayana pazia nilimwona vizuri yule mtoto nilimtizama kwa macho yangu mawili nikagundua kuwa hana ufanano na mtu yeyote yule katika ukoo au familia yetu. Jambo hilo lilinivunja moyo.
Siku moja ndani ya miezi hii michache mara baada ya mke wangu Lupita kujifungua mtoto aliyeleta gubu ndani yanyumba yetu nilimwita mke wangu Lupita nilimwita ili tuongee na pia tujadiliane kwa mapana na marefu zaidi juu ya mtoto huyu anaye tuletea Gubu.
“Mke wangu mpenzi tizama kila mtu aingiaye na atokaye ndani ya nyumba yetu hawachi kusema ati mtoto uliyezaa hafanani na mtu yeyote yule katika koo zetu au familia, embu nieleze mke wangu mpenzi unayachukuliaje hayo maneno yanayo nenwa na ndugu zetu?” Nilimuulza Lupita ingawaje hata mimi binafsi nilijua kwamba mtoto yule hafanani kabisa na mtu katika koo au familia yetu.
“Mika mume wangu mpenzi, ya nini kusikiliza maneno ya watu? Je haujui fika kuwa kitanda hakizai haramu? Je haujui fika kuwa uchungu wa mwana anaujua mzazi? Wewe ni Mume wangu na mimi ni mke wako mpenzi tunajuana vema na pia tunapendana sana. Basi weka moyoni mwako kwamba mtoto huyu ni wetu mie na wewe, wewe ndiye baba yake na mie ndiye mama yake.” Lupita aliongea.
“Mke wangu ukweli ndio unaoweza kulidumisha pendo letu likadumu na kudumika, ukweli ndio unaoweza kutufanya tuweze kuishi maisha yenye wingi wa aha na starehe, maisha marefu na Baraka tele, kwanini wanificha? Kwa nini hautaki kuniweka wazi tizama mtoto huyu hafanani kabisa na mie.
“Mume wangu kwanini unanivunja moyo? Je ni kosa langu kukuzalia mtoto? Furaha yetu ya ndoa. Je nisingelizaa huyu mtoto ungelisema hivyo?”
“Lupita usiongee upuuzi mke wangu,Mtoto upangwa na Mwenyezi Mungu, tafadhari niweke wazi, ni nani haswa baba wa mtoto huyu?” Nilimuuliza Lupita ambaye hakunijibu zaidi ya kunikalia kibubu. Sikupendezwa na hali ile lakini nifanyaje, upole nao umezidi kipimo.
Itaendelea
No comments:
Post a Comment