NILIICHUKUA GARI YANGU YA FAHARi gari hiyo nilipewa zawadi na mke wangu lupita, pasina kujua kuwa sio bure gari ile alikabidhiwa na Mheshimiwa Antonio, alinipatie kama zawadi leo hii ndio ninaanza kujua kila kitu, ninaanza kujua mambo yote ninaanza kujua gharama zote kubwa kubwa alizogharamian Lupita, ninanza kuujua usaliti wake ambao hapo awali sikuujua.
Nikaelekea Ikulu nimfate mke wangu Lupita moyoni sina raha sina furaha ni huzuni na majonzi pamoja na masikitiko ya kuporwa mke wangu.Kwanini Lupita, kwanini mke wangu kwanini umenifanyia hivyo? Niliongea kwa majonzi na masikitiko
“Rudi mpenzi, rudi lavu nimekusamehe bado ninakupenda hata kama umenisaliti kwanini uniache?” upole ulinizidi, nilihitaji kumsamehe LUPITA. Oh! Masikini, kuachwa na yule umpendaye moyoni niliumia sana, Raisi amenipokonya mke wangu, mke wangu wa ndoa, mke wangu wa ndoa, nifanye nini mimi? Mawazoyalinichanganya mtimani mwangu.
Kutoka nyumbani kwangu hadi maeneo ya Ikulu hakuna umbali mkubwa sana ndani ya dakika kumi na tano tayari nilikwisha fika mbele ya geti la kuingilia Ikulu. Nikajitambulisha mbele ya walinzi walionikuta hapo nami nikawaeleza shida yangu, kwani walinielewa? Hapana, hawakunielewa wale wanajeshi walindao Ikulu,, hawakunielewa kabisa japo nilisistiza na kuomba sana nihurumiwe nipate nafasi ya kumuona mke wangu Lupita maombi yangu kwao hayakusaidia walinikatalia kata kata kungia maeneo ya Ikulu nao walidai kuwa kama ningelikuwa na Appointment na Raisi Antonio hapo ingelikuwa ni rahisi kuingia ndani ya lile jengo kubwa la Ikulu
Niliwashangaa sana kwa jinsi walivyo kadhia neno Appointment, kwao Appointment wanadhani ni rahisi kuipata masikini nikatimuliwa kama Umbwa na tena nikatishiwa vitu vibaya kama ningelileta za kuleta.
Nilirudi nyumbani kwangu nikamkuta mwanangu Maliki amelala juu ya Sofa, nikaridhia kama tayari amekula nami nikamchukua Maliki akalale chumbani kwake. Usiku ule sikupata usingizi nilikuwa nawaza na kuwazua nifanye nini mie Mika? Simu niliyompigia Lupita haikurudi na majibu sababu alikuwa ameizima. Nikafanya kuwataarifu ndugu juu ya kuondoka kwa Lupita pale nyumbani kwangu. Ndugu walibaki wakishangaa, asilimia kubwa walimponda wakidai kuwa walikwisha mgundua kupitia uwepo wa mtoto Seba, Seba hakufanana na mtu yoyote yule katika familia au koo zetu.
Seba alichukulia kila kitu kutoka kwa Rais Antonio na sasa Lupita amempeleka kwa babaye aliyempenda zaidi ya mimi aliyeniacha sababu ahadi tamu za maisha bora zimemchanganya. Usiku ule ulikuwa ni usiku mgumu kwangu, sikuweza kulala zaidi ya kuwaza nifanye nini ili nimrudishe Wangu wa moyoni? Je niende kuripoti kituo cha Polisi? Watanisikiliza kweli? Sio kwamba ati sijiamini, la! Asha, kujiamini na jiamini sana. Tatizo linakuja pale nitakapo weleza hao Polisi kuwa mke wangu amekimbilia nyumbani kwa Raisi Antonio, ingelikua ni kichekesho, kwa ule mtindo wa Wanajeshi walindao Ikulu kunikatalia kuingia Ikulu je hawa polisi watanisaidiaje kwa kweli? Haki, kesi ya Nyani usimpelekee Ngedere.
Nikaukosa usingizi juu ya kitada changu kizito, nikabaki na wingi wa mawazo nikitibuliwa, nikiwa sina usingizi macho yalijaa machozi.
#############################
Ndugu walianza kumiminika nyumbani kwangu, wapate habari juu ya kutoroka kwa mke wangu, rafiki jirani na jamaa walijaa nyumbani kwangu wakinifariji na kunipa pole kwa dhiki iliyonipata, kila mtu niliye mweleza juu ya kutoroka kwa mke wangu alisikitika.
Sina jinsi nimempenda sana mkeo, nina haja naye yeye ni daktari wa Moyo wangu.” Raisi Antonio aliongea, aliongea siku ya leo, siku niliyotembelewa na huyu mkuu wa nchi amekuja moja kwa moja nyumbani kwangu, akiwa pekee hajaongozana na Lupita mke wangu amekuja akiwa na walinzi wamlindao popote pale aendapo yeye.
“Hapana mheshimiwa Raisi, Lupita ni mke wangu wa ndoa please naomba unirudishie ningali bado ninampenda niliongea kwa huzuni, nilijiona kama vile nashindwa kujieleza, ingawaje nilikuwa nikijieleza mbele ya Raisi Antonio.
“Siwezi kumruhusu Lupita arudi mikononi mwako yeye tayari ni mali yangu, ninammiliki, jaribu kumfuta moyoni mwako, tena ujue na utambue kuwa mimi ni mtu mkubwa sana Serikalini ninauwezo wa kukufanyia kitu chochote kile kibaya. Kwahiyo Ujue na ufahamu kuwa Lupita ni mali yangu na pia Lupita yupo mikononi mwangu kamwe hatoweza kurudi mikononoi mwako tena,” Raisi Antonio alinitisha
“Mke wangu wa kwanza alikufa kwa ugonjwa wa Kansa sikuwa na jinsi upweke ulinitafuna sana lakini macho yangu yalitua na kugota kwa yule anayenitibu kimwili na kisaikolojia. Lupita, Dakta anayeutibu moyo wangu, mwanamke mmoja mrefu, mweusi, mwembamba, mzuri wa sura mwenye Elimu ujuzi na maarifa.” Raisi Antonio aliongea.
“Nitakupandisha cheo, nitakutoa kutoka kwenye kazi uipendayo kazi ya ulubani, nawe utakuwa Balozi wa ubalozi wa AUSTRALIA uwe mbali na macho yangu pamoja na macho ya Lupita, umsahau yule umpendaye tena ukumbuke kuwa Lupita kuanzia Sasa ni mali yangu.” Raisi aliongea kwa kunishurutisha
“Sihitaji cheo chochote kile Serikalini, wala sihitaji kutunukiwa jambo lolote lile, mimi sio Mwansiasa na siasa haipo ndani ya damu yangu.” Niliongea kwa ujasiri nimefura kwa chuki na hasira. Wakati huo wote nilikuwa nimeketi na Raisi Antonio aliye nitembelea nyumbani kwangu, amezungukwa na walinzi kibao walioshika mitutu na mabunduki
“Umechelewa bwana Mika, you are too late, hata uende wapi, hata ufanye nini, usitegemee wala usitarajie kuona Lupita arejea tena mikononi mwako, kwa lazima na kwa amri yangu ninakupa cheo, uwe Balozi wangu ukaniwakilishe nje ya nchi yangu, uende mbali na macho ya Lupita,” Antonio aliongea kama mtu mwenye kisasi.
Ile sura yake yenye mikunjo na mikunyato ya uzee ilionekana imemchonga chonga naye alionekana kuwa mbaya zaidi ya wabaya, mbaya kama kinyago cha Mmakonde, mvi nyingi zilizostawi na kumea kama majani mabichi zilionekana kichwani kwake kwa mwonekano ule nilimsikitikia sana mke wangu Lupita, nilijiuliza maswali kichwani mwangu; iweje Lupita aniache mie kijana wa damu yake, mie kijana wa ujana wake naye alikimbilie lile zee zima lililochoka na kuchakaa.
Zee hili linayatumia madaraka yake kupora na kuiba wake wa raia zake, zee hili linatumiia mali, utajiri na fahari zake ili kumteka kimapenzi mke wangu, linawatumia watu na nguvu za watu waliosimama rasimi kumlinda yeye na masilahi yake yeye. (Linatumia Polisi na Wanajeshi) linatutisha na kutuogopesha sie wakina yakhee tusio na mbele wala nyuma
Nilijisikia kulaani kile kitendo cha mke wangu kudanganyika na mali pamoja na fahari alizoshawishiwa na huyu mzee mwenye maradhi ya tamaa. Sawa sikatai kusema kuwaRaisi Antonio ana magari mengi ya fahari, majumba mengi aliyojenga sehemu mbali mbali ndani na nje ya nchi ya BARA mashamba makubwa ya mazao ya viwanda vya biashara, migodi mikubwa ya dhahabu, lulu na ana pesa zake mingi alizo zichota na kuwaibia Wananchi kifisadi. Lupita hajui kuwa nayeye atakuwa mmoja wa watu wanaotumia pesa za majizi wanaoibia Serikali.
Hata hivyo sipendelei kuongelea zaidi na zaidi kuhusu Siasa nimempoteza Lupita, nimempoteza mwanamke wangu, nimempoteza mtu muhimu sana maishani mwangu, nimempoteza mama wa mwanangu Maliki
Mwanamke wangu ambaye hakuchoka kumwagia sifa Raisi Antonio, katika zama zile za mapenzi yetu mie nilikuwa nikichukulia poa pale nikisikia kiongozi wanchi akisifiwa na mke wangu, sikuhisi vibaya, pale nikimsikia mke wangu Mpenzi akimsifu kiongozi hata kama hajatenda jambo zito lenye manufaa kwa taifa
Lupita mke wangu ambye daima hakuchoka kumsifia Antonio kwa kila safari waliyokwea na kurudi pamoja kama nijuavyo Lupita ni Daktari na Daktari huyu ni mtu muhimu kuambatana na Raisi popote pale anako enenda. Zamani zama hizo za mapenzi yetu Lupita hakuchoka kutaja zawadi anazopewa na Raisi Antonio, haku choka kunisimulia vyakula walivyokula pamoja na Antonio kwa kifupi sifa juu ya Raisi Antonio zilijaa ndani ya ubongo wa Mke wangu Lupita na udhaifu wangu mie sikuwa na kijicho wala sikuwa nawivu oyoni mwangu tena sikuwahi kumhisi vibaya mke wangu lupita kuhusu sifa anazomawagia Raisi Antonio
Mimi nilikuwa nikichukulia Poa, nilijivunia sana kuwa na mke anayefanya kazi ndani ya ofisi ya Raisi, ofisi kuubwa yenye hadi na heshima duniani. Leo je? Leo ninajuta mie, ninajuta kwa sababu sikuyajua yote hayo, ndio mana wahenga walisema usilolojua litakusumbua, hakika hili jambo ambalo sikulijua limenisumbua, hakika limeniachia kidonda kati kati ya moyo wangu.
Itaendelea
No comments:
Post a Comment