Sunday, October 6, 2024

Madanganyo... (Black mail) Sehemu ya kwanza


 


 

Madanganyo. 

 

 

 

 

SEHEMU YA KWANZA.


KWA SANGOMA.

           “Ati Dakta, umesema tukileta sehemu nyeti za mtoto mwenye tatizo la ngozi mke wangu Cheusi atapona ugonjwa wake wa UKIMWI.” Cheppe aliongea akiwa na huzuni tele juu ya afya ya mkewe Cheusi Mangara. Angali hajui afanye nini ilihali ametangatanga huku na kule kusaka dawa zote za miti shamba, amemaliza mizizi yote inayoota mwituni, akimkorogea na kumpikia mkewe Cheusi, dawa ambazo hata hivyo hazioneshi darili zozote zile za kumponya zaidi ya kumdhoofisha na kumtia uchovu wa mwili.(kukonda na kukondeana)

               “Ndio, dawa ya kuponya ugonjwa wa mkeo ni kuleta sehemu nyeti za mtoto au kijana mwenye ulemavu wa ngozi.  Mizimu inasema mkeo amelaaniwa na wazee wake waliokufa zamani, ana mkosi mzito ndio maana kutwa kuchwa aheshi kuugua magonjwa yasiyo na kikomo na matokeo yake huko hosptali unakompeleka mkeo hao wataalamu wa huko wanadanganya na kunena kuwa mkeo ameambukizwa virusi vyaugonjwa wa UKIMWI. Mganga Mbeleko alinena.

                   Si utani, maneno yote aliyonena mganga Mbeleko yalijaa  uongo, ulubuni na udanganyifu, Cheusi hakurogwa wala Cheusi hakutupiwa laana na mikosi ambayo huyo Sangoma alidai kwamba Cheusi ametupiwa. Ukweli ni kwamba uzinifu, utovu wa uaminifu katika ndoa, usaliti na tamaa yake Cheusi ndio chanzo kikuu cha ugonjwa unaomtesa Cheusi, unamnyima raha na furha.

                 “Leta kiungo ambacho mizimu imekuagiza ulete muda si mrefu mkeo atapona atakuwa ni mwenye afya, nguvu na uzima tele kumbuka usipofanya hivyo duniani hapa kuna kuzaliwa na kufa, nafsi aliyobaki nayo mkeo ni kufa tu, hana nafsi nyingine, Mizimu haitaki masihara, mkeo akiisha kutwaliwa na wewe pia utatwaliwa mwanao James mdogo nayeye pia hana muda wa kupumua duniani atatwaliwa.” Mganga Mbeleko aliongea.

                  Maneno yale yalimtisha sana Bwana Cheppe kufa kwa mkewe kuambatana na  kifo chake kisha kufa kwa mwanaye mdogo Jemsi kulimaanisha  mwisho wao tayali ulikaribia kukamilika, aliogopa Cheppe, aliogopa sana alitetemeka huyu dereva wa maloli makubwa yanayosafilisha bidhaa mbalimbali  zinazouzwa jumla, zikitolewa ndani ya mkoa wa Dare s salam  na kupelekwa mikoa mingine iliyo mbali na Dare s saalam, Mbeya, Iringa, Tabora Arusha na hata Mwanza.

                  Ameajiliwa kuzunguka zunguka mikoa yote ya Tanzania bara akisambaza bidhaa  kutoka kwenye kiwanda cha kibosile mwenye pesa zake nje ya Tanzania

                  “Embu nieleze Bwana Dakta, hivi hiyo laana na huo mkosi uliomkamata mke wangu vinatokana na sababu ipi kubwa haswa mpaka ifikie hatua mkewangu apatwe na ugonjwa huu unaommaliza na kumtesa.”

                 “Kijana haya ni mazito ya ulimwengu, laana hiyo inatokana na ugomvi mkubwa uliotokea miaka ishilini na mitano iliyopita kipindi hicho mkeo akiwa  angali bado mtoto mwenye  umri  wa  mwaka mmoja tu.  Mara baada ya kuzaliwa baba na mama yake walikolofishana, ugomvi uliotokana na usaliti,usaliti aliokuwa nao mama mkwe wako (mama wa mke wako). Mamaye Cheusi alikuwa ni kiruka njia wa kutupwa na kuokotwa, hivyo babaye Cheusi alipoona hali ile haimpendezi ndipo alipofanya shauri kwenda kwa waganga wa kienyeji ili amloge mamaye Cheusi, amloge aachane na tabia yake ya kupenda kula wali mwingi(kufanya ufuska) mganga mbeleko aliongea kwa mafumbo.


                  Aliongea kiubunifu, aliongea uongo mtupu, alidanganya ili mradi kwa vile alikua anjua sana kuongea alitaka tu aonekane kama anaongea ukweli madhubuti. Cheppe alimsikiliza, alimsikiliza kwa umakini, wasi wasi na utulivu mwingi pasina kujua kwamba mwenziwe anamzunguka ubuyu, pasina kujua kwamba yule mganga anamgata kisogo (anamdanganya).


                 “Baba mkwe, babaye Cheusi alipewa sharti moja, sharti la kutafuta sehemu nyeti za mtoto mwenye ulemavu wa ngozi, na alipofanikiwa kuzipata Mizimu ikamfunga mamaye Cheusi, babaye Cheusi aliambiwaa na mizimu hapaswi kuwaambia watu juu ya lile tendo la kumuua yule Albino, alipaswa kuwa msiri na kamwe asithubutu kuwaambia watu juu ya lile tendo alilolifanya, ajabu dunia ya leo, ulevi noma, ulevi umfanya mtu aingie ndani ya majanga asiyo yatarajia.”


                 “Siku moja babaye Cheusi akiwa amevaa miwani(amelewa chakari) haelewi wala hajielewi, alijikuta anawaambia walevi wenziwe namna gani alivyomfunga paka kengere(namna alivvyomthibiti mkewe) si ndo ikawa hivyo walevi wakasambaza habari kijiji chote na hatimaye Mizimu ilipojua juu ya hali halisi kubadirika, haikufanya ajizi ilimuadhibu babaye Cheusi, adhabu ya kifo, ikimlaani mamaye Cheusi pamoja na mwanaye cheusi kwa kuwatupia magonjwa sugu yasiyo na tiba.” Sangoma aliendelea kusimulia.


                “Yuko wapi mamaye Cheusi Mangara, amekufa kama alivyokufa babaye Cheusi, amekufa kwa laana nzito, laana ambayo inaelekea kukutafuna wewe na mwanao James, mara baada ya kufa kwa mkeo Cheusi.” Mganga Mbeleko alitia nanga kunena,akamtaka Cheppe afanye hima hima kumaliza matatizo.


                    *****************************


Itaendelea


No comments:

Post a Comment

I promise you

   I PROMISE YOU. (NINAKUAHIDI.) SURA  YA KWANZA. UBAYA WA POMBE. “Umenizingua job, umenizingua kwa muda mrefu sana mpenzi wangu…….kwanini l...