.. 2
Ndoto ya kutisha
Sehemu ya pili
SEHEMU YA PILI
Kishindo changu aridhini kilimshitua Joka kubwa Iililolojikunja pembeni ya njia tuliyokuwa tunapita. Fysaa Joka lilijichanua likaziba njia yote. Mimi niliyekuwa upande wa mkia nilipigwa naule mkia ulioniusogeza ukanisogeza umbali wa miguu kumi na mitano wale wawili waliokuwa upande wa kichwa wakangaliana uso kwa uso na lile joka.
Nilipokuwa nnanyanyuka nilipodondoshwa na Joka ili nianze kukata mbuga sikuwaona wale wangunjwasi wawili waliokuwa wakiangaliana na Jokai la niligundua vishindo vya mate na Joka lilipotua aridhini nilikimbia eneo la tukio kwa mwendo wa mwanga huku nikikubaliana na maeno ya wahenga waliposema mambo mazuri hutokana na mabaya
Baada yam bio za mwendo mfupi katika eneo refu nilianza kuhisi maumivu mgongoni, ndipo niligundua kuwa ninabubujikwa na damu nyingi sana pale nilipopigwa na Joka nilipogeuka nyuma nilikuwa nimezitiririsha njia nzima na kuacha michirizi ya damu. Michirizi ambayo iliwasaidia wale aWangunjwasi wengine wanifatilie kwa urahisi kwani kabla sijaugulia kidonda changu cha mgongoni niliwaona kwa mbali wakinijia kwa hasira wakiongozwa na yule kiongozi wao niliye bahatika kumuona paji la uso na macho akiruka kwani walikuwa wanatokea kwenye kajibonde.
Nilipoangalia huku na huko hamna pa kutokea, Mungu si athumani, nikaliona shimo. Haraka nikakata shauri la kujificha humo. Lakini kadri walivyozidi kuja hofu ilinizidi, ilinibidi nitoke ndani ya shimo kwani nilijihisi siko salama mule nilipogeuka nizianze mbio nililiona shimo lingine nikalifata. Hili lilikuwa kubwazaidi
Ndiposa niliingia kwenye lile shimo nijifiche ila sasa ndo’ nagundua sauti ya vuu! Lilikuwa ni jiwe kubwa lililotupwa ndani ya shimo nililo jificha, nami nisijue nikakimbia sasa nimejikuta nina vidonda utosini na maeneo mengine ambayo siyahisi uso wangu umepambwa na michirizi miyekundu mingi inayoendelea kushuka kama maporomoko ya maji ya Udizungwa.
Sasa turudikwa yule Mkwiranyinza aliyekuwa akinihoji maswali ya hapa na pale kiukali sana. Huku akinilaumu mimi kuwa sababu ya yeye kupoteza vijana wawili wachapakazi tena akidai kwamba kumezwa na Joka kwenye jamii yao ni ishara mbaya kwani Joka lile umeza watu wa jinsia mbili tofauti. Hivyo basi kama Joka amewameza wale vijana wa kiume ni ishara kwamba atawatafuta hata wake zao apate kuwameza.
Mwili wangu ulikuwa umefadhaika sana mambo yote niliyasikia lakini nilishindwa hata kutingisha kope cha zaidi niliangalia mbele tu ambapo macho yangu yaligongana na kifua cha Mkwiranyiza ambacho kilikuwa na makovu ya mishale mingi iliyoingia pale. Mkwiranyizwa alivyokuwa anaongea kwa ghadhabu kuu juu yangu , asijue jambo baya la kunipa kama adhabu itakayonipasa. Ghafla yule kiongozi mfupi wa porini alinisogelea mkononi akiwa ameshika chuma kilichochongoka mbele, ambacho kimewekwa motoni mpaka kimekuwa cha rangi ya machungwa. Chenye kutoa moshi, Kisha akajaribu kunichoma nacho machoni asifanikiwe kutokana na kimo chake.
Baada ya miruko kadhaa akilihusudu jicho langu Mkwiranyinza alimbeba na kumleta usawa wa kifua chake akimwangalizia kwangu. Kisha eneo zima la wangunjwasi lilisimama na kushitushwa kwa kelele niilizozitoa kwa maumivu ya kutolewa jicho langu la kulia kwachuma chenye moto. Nikapoteza fahamu.
No comments:
Post a Comment