CHUPI YA BIBI KIZEE ILIVYOMPA HASARA MUME WANGU.
'Trip...trip trip' Nilisikia sauti ya vijisenti vilivyodundulizwa ndani ya chungu kikubwa yaani kibubu kilichohifadhiwa chini ya kitanda chetu mie na Mume wangu Bidozi. Mume wangu alikua akidunduliza pesa zake ndani ya kile kibubu. Ni kawaida yake kila aliporejea kutoka shuhulini alidunduliza 'ndo ndo ndo si chururu, haba na haba itajaza Jibaba.'
"Pam my Dear umeamkaje?" Alinisogelea kitandani akanipiga kiss shavuni๐ mie nikiwa macho Usiku ule,
"Nililala kukuota na kukumiss Daring, ninakupenda ." Nikampiga kiss ๐ juu ya komwe lake.
"Asante kunipenda nami ninakupenda pia." Bidozi alinifanya nitabasamu, nikafarijika na kujisikia.
"Pole na shuhuli." Nilimfariji nikichezea chezea tundevu twake twa ujanani na uzee majaliwa..
"Niko poa, SEMA bado nasumbuliwa na zile ndoto zenye tamaa ya kuwa na nyumba yetu, Biashara yetu kubwa pamoja na Usafiri wetu." Aliongea mawazo yamziguayo,
"Hilo Mola atafanya my Love tukaze kuomba na kufanya bidii, maana bidii itazaa matumaini," Nilimfariji Tena.
"Asante, alinitzama Kwa mahaba mazito Kisha akagandamiza lips zake kwenye komwe langu ๐ kiss, kiss.
"Lakini Bidozi Mume wangu Mimi naona haunitendei haki" Akawa atensheni kunisikiliza, nikayatoa ya moyoni mwangu.
"Hautaki Mkeo nifanye kazi hata ya kuuza nyanya, vitunguu bamia na ngogwe. Mkeo nizoe zoe vijisenti vya kununulia mahitaji YANGU muhimu: Sabuni, mafuta, viatu au nguo." Niliongea Kwa hisia
"Mwanamke mzuri kama wewe kamwe sintakuruhusu miguu YAKO ikamate vumbi na nywele zako zikaushwe Juani. NATAKA uishi kama Malkia." Kauri hizi Bidozi hutamka kila siku.
"Malkia ๐คฉ" Nilijichekesha, " Malkia mwenye nguo kuukuu, viatu vikuukuu, nywele tipwa tipwa hata kusuka twende kilioni naona shida. Sielewi Wala sijielewi bado tu hata sabuni ya kuogea siipati." Niliumia kimoyo.
" Ipo siku yote uyatakayo Mamie utayapata..... Embu tuliza MOYO Mtima tutimize malengo yetu, ona Hadi Sasa tumedunduliza Millioni 30 bado kidogo tufikishe millioni hamsini"
" Mmh! Sawa mwenzangu nimekuelewa" Nilikubali Kwa shingo upande,
" Aya Sasa Mke wangu, rafiki wangu na mama YANGU mpenzi nenda kanifanyie MAJI moto ya kuoga Rafiki YAKO NIWE safi niondoe Shombo la viazi chips." Alinitaka nikamwandalie maji moto.
"Hilo umepata omba jingine." Nikadamka pale tandani nikaeleka Mekoni kumwandalia Bidozi maji moto ya kukoga.
.................
Nusu saa kupita nilirejea gettoni kutoka Mekoni nilikoenda kuandaa MAJI moto ajiri ya mume, rafiki na Baba wangu MPENZI Bidozi. Kitandani nilimtazama alivyolala fofofo akiunguruma kama Simba Dume 'Ngrooo....ngroooo.ngroooo' Mpika chips wangu lazima achoke yaani atoke Alfajiri mapema aelekee Kariakoo kuuza chips Kisha arejee usiku saa SITA, Lazima achoke Tena akiamka kutoka usingizini akiisha Toka kukoga lazima nimuombe mambo mazito kitandani, akigoma Kwa kisingizio Cha: 'ooh! Nipo ovyo, nimechoka' lazima nimforce Kwa nguvu na akijifanya kuninunia na Mimi namnunia Nikimuuliza:
' Umenichoka eeh!?'
'Umepata Malaya huko unakokaanga chips'
'Haunitaki Tena? SEMA niamue kimoja'
Aloo! ๐๐ Mambo nzito nzito.
'Driiip' Nilishituliwa na mlio wa simu yake Bidozi. Ishara kwamba Simu yake inakata chaji, nikajidamsha kivivu pale nilipoketi na kueleka kuichukua Ili nimuwekee chaja akiamka Rafiki MPENZI aikute ishajaa chaji, yaani Fuluuu Mia Moja asilimia.
'Driiip Ziiip' Nilipoigusa ile simu ikaniashiria kuwa chaji inakaribia kukata, ghafla mwanga wa ile simu ukaniashiria kuwa Kuna meseji zinaigia Kwa mfuatano. Bahati nzuri Leo Mume wangu aliiacha simu yake ikiwa 'on,' ameiondoa Password. Hana kawaida ya kuiwacha SIM yake Wazi lazima atailock kuninyima nafasi ya kusoma jumbe au kuangalia video za huko Fb, Twitter au YouTube.
Nikaipeleka ile simu Chaji, ningali naikodolea mimacho, roho ikaniambia 'Embu Leo ifungue' Roho nyingine ikanionya ikaniambia 'Wacha ukorofi wako ' Basi ile Roho ya kiupelelezi na umbea wa kike kike ikashinda Pamera mie nikafungua simu ya Bidozi wangu ๐, nikache kicheki Statasi za Wasap na meseji zinazoingia na kubisha hodi kwa hasira zikipokezana ndani ya group la WASAP.
Mbea mie nikaingia ndani ya group la Wasap, Wasap ya Bidozi wangu, Group lilikuwa na marafiki wapatao Miatano...Duh! Mwenzangu ana marafiki Mjini
'Teh teh teh ๐
๐๐' Kilianza kiicheko kilichosindikizwa na kiimoji kinachocheka kwa raha Hadi machozi kububujika.
'Amekosa nguo huyo au tupitishe bakuli la kuomba msaada wa pesa na mali' Mmoja wa marafiki wa Bidozi alichangia hoja.
'Astaghafirurah! Mie nitamuibia CHUPI ya mke wangu avae tu.'
Jesu! Nilishituka nikaiona comment ya Mume wangu Bidozi.
' Aibu jamani! Mie nilijua nimeoa Kigori kumbe nimeoa Mbibi na hii CHUPI yake chafuu ina MIAKA mitatu hajaibadilisha, yaani ni mwendo wa kauka nikuvae. Macho YANGU yaligota kwenye picha ya CHUPI iliyopostiwa kwenye group Tena ajabu CHUPI ile yenye madoa madoa meupe na meusi nimevaa MIAKA mitatu Sasa, nimevaa Hadi imenikataa Kwa mwendo wa kauka nikuvae. Nikaendelea kusoma jumbe na kuangalia viemoji vya dharau.
'Umeo mbibi, umeoa kikongwe asiyetaka mabadiliko' Rafiki mwingine wa Bidozi alichangia hoja. Nikaendelea soma zile Jumbe.
'Babu we si umnunulie Chupi mpya Bana.' Rafiki mwingine alichangia hoja.
"Sina muda huo." Bidozi alimjibu yule Rafiki akaweka na kiimoji Cha kucheka Kwa sauti๐. Sikutaka kuendelea kusoma au kuangalia vile viemoji vyenye dharau nikamuangalia Bidozi pale alipolala Kwa HASIRA nikatamani niondoke chumbani nirejee Mekoni niyatengue Yale MAJI yaliyokua yakichemka mafigani nije nimwagie yule mpuuzi aliyelala fofofo pale Tandani lakini we! Hasira hasara Acheni tu, ndoa zataka uvumilivu
Bidozi anachukua Chupi zangu za zamani Kisha anapiga picha na kuzisambaza kwenye magroup ya Wasap sehemu ambazo Rafiki zake wasio na stara wakinicheka na kunidharau, Mume Hana adabu huyu ๐ฅถ๐ก.
Anajua fika kuwa kila siku ninalia kumuomba aninunulie nguo mpya, viatu vipya, sabuni na mapodozi, hajali maombi YANGU, hathamini kilio CHANGU Tena haeshi kunipooza Kwa maneno yake ya kiuchumi '
'Tusichezee mapesa Dear, pesa hizi kibubuni ni Kwa ajili ya kusaka maendeleo.' Ananipooza hivyo.
'Tutajenga nyumba KUPITIA pesa hizi tunazoweka kibubuni'
'Tutanunua viwanja na kujenga maduka'
'Tutanunua magari na mashamba ya mpunga'
BASI mie Pam nikilia kidogo tu 'Mume nifanyie huruma nifanye kazi itakayonipatia pesa nikasuke twende kilioni, nivae mitumba na Yebo yebo.' Bidozi anawaka kama fuu la nazi hataki kusikia kelele zangu.
'Mh! Mazito ya Dunia. Mwanaume ana mambo huyu' Nikajikasirisha Kisha nikapanda Tandani nijilaze nikampea mgongo Bwanagu aliyelala Fofofo kama maiti ya kimakonde.
' MAJI ya kukoga yakaukie motoni' Nikabwata Kwa sauti kama Nina wazimu.
'Sipiki chakula, wakakupikie hao hao marafikizo wapuuzi wanaokomenti na kuunga mkono ujinga wako.'
'Mume huna adabu wewe! Sawa, tuone nitakukomesha Ili ujue mke ataka matunzo Babu we!' HASIRA zilifura kifuani kwangu.
'Machache yamekushinda, mengi mengine utayaweza? ' Bado mwanamke nililalamika.
'Kesho nafanya mambo mazito Babu' Nilipunguza makasiriko.Nikajitandaza miguu pale kitandani nikimsukuma sukuma Bidozi Nikitaka adondoke kutoka tandani 'Puu' kama gunia la mbaazi๐๐๐.
----------------
"Usiniambie Pamera au watania" Mama mkwe aliziba kinywa na kushangaa. Leo nimempigia simu Mama mkwe wangu amekuja fasta ndani ya Getto nilalalo na Bidozi Mume wangu nimemweleza na kumuonesha mapicha na makomenti ya hao marafikize Bidozi wakiiponda CHUPI YANGU yenye madoa meupe na meusi, komavu yenye michano na michubuko.
"Ndo hivyo Mama mkwe, Mume wangu Bidozi ananiaibisha mitandaoni, ananichafua akijua fika kwamba hanisaidii machache nimwombayo' Nilimweleza Mama mkwe machozi yakinibunujika.
"Acha kulia Pam, wewe sio mtoto mjinga, wewe ni mwanamke ambaye unapaswa kufanya jambo la kumuonesha mume kwamba haujazuba unaweza kufanya jambo la kimaendeleo na mabadiliko'." Mama Mkwe aliongea nikayafuta machozi YANGU Kisha nikamwazima masikio nimsikilize.
"Jambo Gani Mama?" Pam mie mnyonge niliuliza.
"Mwanaume hawezi kukutawala milele" Nilimsikiliaza Mama Mkwe.
"Akikutawala kihisia na kimwonekano wewe mtawale Kwa akili na vitendo zaidi." Alinipa somo
"Hivi tunavyoongea ungelikuwa mbali sana kimaendeleo, sema hauna uthubutu pia haujataka kuthubutu ndio maana Bidozi ร mekukalia Hadi anakutawala kwenye Chupi." Somo alinikosoa mie mwanagenzi nilikaa mkao wa KULA nishibe.
"Uliwai kuniambia Bidozi arejeapo kutoka Gengeni kuuza Viepe urejea na mashilingi anayoyahifadhi kibubuni chini ya mavungu ya kitanda, Mwanamke ni wakati wako Sasa wakati wa kumuonesha kwamba haukuolewa Bure umkalie Mekoni ukichambua tembele na kutolewa machozi kwa hivyo vitunguu MAJI na moshi wa kuni. Huu ni wakati wa kumuonesha kwamba lazima azisikilize hisia na matamanio YAKO." Mama Mkwe alinipa somo.
"Kuingia ndoani sio kufurahia tendo la ndoa tu, ndoa sio ati kumpikia, kumfulia au kumtengea MAJI moto na kumuogesha Babu, ndoa ina maana Pana sababu hayo MATENDO tajwa hapo juu hata Sokwe aweza kuyafanya. BASI Bibi huu ni wakati wa Babu kukusikiliza kuheshimu, kujali na kuthamini hisia na matamanio YAKO. Somo YANGU alinipa somo.
"Ingia uvunguni, chukua chungu icho pasua kibubu chukua kiasi Cha pesa uzitakazo Kisha tutoke Outing tukauoneshe Ulimwengu wa wanaume kwamba sisi sio tegemezi tunaweza hata tusipowezeshwa." Mama Mkwe aliongea mie niliyekua na hofu na woga kushika kibubu Cha Bidozi Mume wangu nikaanza kuregea taratibu, nikaenda uvunguni nikachukua chungu chenyewe nikapeleka mbele ya mama Mkwe tukavunja Kibubu chenye Mahella ya kutosha kututamanisha.
.................
Katika zile Millioni therathini zilizohifadhiwa kibubuni nilichukua Million kumi tu. Safari yetu ya kwanza ilikua ni kukaribishwa ndani ya maduka ya pale Kariakoo, Maduka ya nguo special, mikoba na viatu. Nilihitaji kufanya Shopping pamoja na mama Mkwe . Nikajichagulia kila aina ya vazi na vao la mwanamke, mikoba mizuri, Viatu vya kutosha na Ili kumkomoa yule Bidozi aliyenidhihakia Chupi YANGU mtandaoni nilifanya kununua yapata Chupi na bikini ๐ Mia Moja na ishirini. Wacha we!๐คฃ๐คฃUtajiri wa vyupi ulinivamia.
"Shuhuli ya kwanza ishaisha, Mama Mkwe alinambia.
"Shuhuli inayofuata ni kujitengenezea uchumi wako mwanamke" Somo YANGU Mama mkwe aliongea wakati huo twatoka Saluni tumependeza wee! Had basii.
"Leo tunampigia simu Darali atusaidie kupata fremu (Chumba Cha biashara) lazima mwanamke uchangaamke Ili mume apate akili na akupende zaidi. Frem YAKO itakua kubwa na Pana Ili wewe Mwanamke utulie ukiuza mapodozi, nguo, viatu na urembo mwingine. Nakwambia hao hao wanao kudhihaki mitandaoni watakuja kuwanunulia wake zao bidhaa kutoka KWAKO." Somo Yangu Mama Mkwe alinipa wazo la kiuchumi.
"Si Bidozi anawaza kujenga nyumba basi Bibi mtajenga wote KUPITIA faida ya biashara. Anataka kununua Magari nakwambia mtanunua wote Kwa faida ya biashara. Anataka kuendeleza biashara basi wote mtaendeleza Kwa faida ya biashara" Somo Yangu Mama mkwe aliniambia tukaondoka Saluni tukaelekea Getto huko Mama Mkwe akanitaka nikoge na kujipodoa Kisha nivae viwalo vipya. Baada ya hapo alimpigia simu Bidozi Mahabuba wangu afanye hima kuja Getto anishangae.
"Hapa mnapoishi mhame Kwa HESHIMA ya pesa mlizonazo, mtafute Apartment yenye vyumba viwili, seble, jiko stoo na choo ndani... PESA haikai tu, nguvu ya pesa ukienda soko ni kujaza makapu Hadi pesa iseme basi." Somo alijua kunisomesha, nilimwelewa.
Ndani ya dakika therathini Bidozi aliwasili akanikuta mie na Mama Mkwe tumejaa tele twajimiminia Chupa ya Mzabibu kama vile tupo kwenye harusi ya Kana, ile harusi ambayo Yesu alifanya muujiza wa kutengeneza divai kutoka Mbinguni.
"Embu nipe Simu YAKO." Kabla hajatoa salamu niliikwaapua simu yake Bidozi nikaanza kujiselfisha na kutengeneza content video ambazo nilizirusha kwenye magroup yake ya Wasap kule alikonidhihaki yeye na rafikize.
'Haya Sasa Jamani yule Chimama aliyekua akisepa na vichupi vya vibibi vikongwe Sasa kawa Malkia bin MALAIKA.Keisha fungua Boutique yake Makumbusho maneno ya Mwananyamala. Karibuni bei ya kiwandani.'
Niliandika na kuposti picha ndani ya magroup ambayo Bidozi alikua ananidharilisha
"Waoo Malkia Boutique imechangamka lazima nije ninunue." Marafiki walikomenti.
"Niwekee Chupi Mia ila siziwekomavu kama Mbibi." Mwingine alitania Bidozi alishangaa tu
"So gorgeous and lovery ๐ฅฐ" Comment zilizidi kumiminika zikashindana kuingia na kufukuzana.
"Kesho nitapita Mwananyamala na mie wangu aje ajichagulie" comment zilimaliza data. Mie na Mama mkwe tulitabasamu.
TCHAO ..........
'
No comments:
Post a Comment