Monday, October 14, 2024

Futures Destroyers... Sehemu ya pili

 


SURA YA PILI   

SIKU SIO NYINGI!

  Huyu kijana mmoja mrefu, mweusi, mzito (mnene kiasi, jina lake anaitwa Vina Visenti, ana umri wa miaka 45 ni mtu mzima. Raia wa Kenya, sio mtanzania  yupo Tanzania kufanya biashara zake. Anafanya biashara kwa nguvu ya East Africa Communuity, biashara huria iso na vikwazo.

                 Uhuru wa kufanya biashara ndani ya jumuia ya Afrika mashariki  ulimfanya Vina  afanye kuhamishia makazi yake kutoka kwao Kenya na kuja kujichimbia Tanzania, akiuza nguo Special, akizitoa Nairobi Kenya na kuzipeleka Dar es saalam Tanzania.

                Basi huyu Vina  Visenti alivyokua akimsumbua bibie Eve looh! Mmmh! Mwenzangu mbona ungelikuwa na huruma ungelimuonea huruma bibie Eve lakini mapenzi bwana ndivyo yalivyo, waswahili wanasema kupenda waweza penda yeyote, mapenzi hayachagui mapenzi hayabagui, kipendacho moyo ni dawa, kipendacho moyo chala nyama mbichi.

                Ni kweli kusema kwamba Vina visenti hamjui vizuri huyu mwanadada aitwaye Eve wala haijui historia ya huyu mwanadada. Amempenda sana, amempenda kwa ghafla, ameupenda urembo, uzuri, haiba na mvuto wa huyu mwana dada, mfupi kiasi, mnene kiasi, mweusi kiasi mzuri kiasi mwenye mwendo wa kuringa na kudengua atembeapo. Vina anafanya kumtokea mara kwa mara huyu mwanamke mwenye watoto wawili.

                Eve amemwoneshea Vina nyodo zake, amempiga kibullshit, amemkataa na kumkatalia, amemwambia hana haja ya kuwa  na mwanaume, anahitaji kuishi yeye na watoto wake, haitaji mapenzi kwa sasa. Lakini Vina alivyo mbishi, hataki kushindwa sababu anafahamu fika kuwa sifa ya mwanaume ni kuto kukata tamaa, mwanaume ni kujipa moyo mwanaume ni kujibidisha. Vina anjiaminisha kuwa mwanmke akimwoneshea Nyodo (maringo) hizo nyodo zina maana yake, hizo nyodo zina sababu zake, hizo nyodo ni matokeo ya kujaribiwa kama kweli Vina ana upendo au la! hana,  je Vina anataka mapenzi ya faster faster? Mapenzi ya nipe nikupe, raha tupate, niache niende  wala usinifate au je anayataka mapenzi ya ujanani hadi  uzeeni? Kazi kwake.

                   Alright Vina anahisi  kwamba Eve anamjaribu, Eve anampima na kuupima upendo wake kwake. Vina ana amini  siku si nyingi Eve ataingia  mkengeni. Basi ikawa hivyo siku sio nyingi Eve akaingia mkengeni, kwa vionjo vile vyenye  vina na mizani, ngonjera, mashairi, nyimbo na tenzi. Usumbufu wa Vina ulikua ni mwingi, Vina alijitahidi kwa kadri alivyoweza, apate kumuweka Eve moyoni mwake, alifanikiwa kwa asilimia mia moja.

 Akamteka Eve kimapenzi, akaingi nyumbani kwa Eve naye akala akanywa, akashiba na kulewa kwa pesa zake yeye mwenyewe, akaingia chumbani kwa Eve akalala pamoja na Eve juu ya kile kitanda alicho kiacha  marehemu Dini, mumewe Eve. Alfajiri jogoo akatangaza siku njema imezaliwa, vina alielekea kazini kwake.

                 Yes, ikawa hivyo sasa, kila alipomhitaji Eve Vina alienda nyumbani kwa Eve akala, akanyawa, akashiba na kulewa na baada ya starehe hizo alihitaji kupumzika, naye akaingia chumbani kwa Eve akalala na kufurahia mapenzi. Kama kawaida majogoo uwaamsha waja na kuwakumbusha kuwa siku njema uonekana asubuhi, asubuhi iliwatawanya hawa wawili kila mmoja alielekea job (kazini) kwake kujitafutia riziki ya kila siku.

                                        ****
                    Vina  Visenti ameiacha familia yake huko nyumbani kwao Kenya ana mke na watoto watatu, wakubwa kidogo, wawili wapo Sekondary na  mmoja yupo primary wanamtegemea baba yao wanategemea awaletee chochote kile ambacho baba kama baba anawajibika  kufanya kwa ajiri ya familia yake. Uzuri wa huyu baba anajari sana familia yake kwa sababu mara zote anaporejea nyumbani Kenya uwafurahisha kwa wingi wa zawadi pamoja na vitu vingine wanavyo vihitaji.

       ##################
Miezi mitatu iliyopita vina alifanya kuhamia moja kwa moja nyumbani kwa mpenzi wake, ua la moyo wake, mzuri ampendaye Eve. Mapenzi yamekolea kweli kweli, yamekolea na kunoga. Vina ni mwanaume na mwanume aliye kamilika kamwe hawezi kuishi upwekeni. Mwanaume hawezi kuridhia upweke, sifa ya mwanaume ni kuwa pamoja na mwanamke pembeni na sifa ya mwanamke ni kuwa na mwanaume pembeni. Mapenzi ndivyo yalivyo, uzuri wa mapenzi ni makubaliano na maridhiano

                     Maya na Mainesi washampata baba,baba mpole mwema kwao na mwingi wa huruma, tena baba huyo sio mchoyo wa huduma anawahudumia awanafamilia kwa kadri ya uwezo wake, anajaribu kumpunguzia mzigo mzito Eve kwa kuwasaidia pesa na mahitaji mengine.

                    Eve akaukamata ujauzito, mimba ya bwana Visenti, lakini kwa bahati mbaya ujauzito ule haukua riziki yake sababu ndani ya miezi minne ya  ule ujauzito mwanamke alikumbwa na mkosi, mkosi mzito sio haba, ni mzito, mzito wa kumuumiza, mzito uliomfanya alazwe hospitali kwa wiki mbili na hata  baada ya kutoka hosptali bado  aliuguza tumbo lake.

                  Sijui ulikua ni mkosi, lakini mmmh! Ni bahati mbaya (bad lucky). Siku ile Eve anapita sebuleni kwake, sebule iliyoezekwa vigae (marumaru)chini ya sakafu, pasina yeye kukumbuka kwamba muda mfupi uliopita mafuta ya kula yalimwagika hapo sakafuni na mwagaji  wa hayo mafuta si mwingine bali ni yeye mwenyewe, aliyamwaga kwa bahati mbaya yalimpokonyoka kutoka kwenye mikono yake na kumwagika chini ya vigae.
Eve  alisahau kama chini ya sakafu kuna mafuta yaliyomwagika, ile anapita tu mara ghafla bila tarajio alijikuta anateleza na kudondoka chini puuuu baya zaidi kudondoka kwake kuliambatana na kulidondokea tumbo ambalo ndio kwanza lina kijusi(kiumbe) chenye miezi minne ndani.

               Msalie mtume! Eve alipiga ukelele wa maumivu, asubuhi ile, aliangukia tumboni, tumbo lilimuuma vibaya sana maumivu hayo makari yaliambatana na utokaji wa damu, damu iliyopita haja ndogo. Laaulah! Ujauzito wake ulikwisha kutenguka, maumivu yake yalikua ni maumivu makari hakuna mfano. Muda si mrefu Eve akazirai na kupoteza fahamu asijue nini kinachoendelea, zaidi ya kujikuta yupo hosptali amelazwa juu ya kitanda akiwa amefunikwa shuka moja jeupe limeandikwa MSD. Kuna dripu ya damu  na dripu ya maji yakipita kwenye mishipa ya mikono yake.

                “Dakta hivi je mgonjwa wangu atapona kweli?” Eve alipozinduka alisikia sauti ya mpenzi wake Vina akiongea na Dakta aliye mhudumia.

                 “Yes, surely atapona lakini pia atahitaji kupumzika kwa muda mrefu maana ameangukia tumbo, mimba yake imechoropoka.

                 “Oooh ! my  God! Have mercy on her.” Vina alipiga kimomboo. Macho ya wawili hawa wapendanao yalipogongana, wakafarijiana kwa machungu na maumivu yale.

                          #################

No comments:

Post a Comment

I promise you

   I PROMISE YOU. (NINAKUAHIDI.) SURA  YA KWANZA. UBAYA WA POMBE. “Umenizingua job, umenizingua kwa muda mrefu sana mpenzi wangu…….kwanini l...