Thursday, September 26, 2024

KUKU WA KIZUNGU sehemu ya 9




KUKU WA KIZUNGU

Sehemu ya 9

 ENGLAND

Nyumbani kwa Islama Tino ameketi mezani kuna vyakula vya kila aina juu ya Meza lakini Tino hali chakula machozi yamtoka. Kuna televisheni Screen Moja kubwa imetundikwa kutani, Channel Moja kutoka Afrika Mashariki yaonesha picha za Wanyama wa aina mbali mbali wanaopatikana Tanzania, Milima mirefu iliyopo Tanzania pamoja na watu waishio Vijijini.

Islama aliingia ndani ya Jumba lake la kifahari ameongozana na Davidi mpenziwe wa zamani gari yao ilipaki pahali moja kwa moja Islama na Davidi walipitiliza faranga (Sebuleni) huko walimkuta Tino analia akimwanga machozi.

“Tino!” Islama alimsogelea Tino, akaketi karibu na mwanaye akakitwaa kitamba chake binafsi akamfuta machozi yule Chotara wake.

“Stop crying, usilie mwanangu.” Islama alimfuta machozi Tino David akaketi pembeni ya Tino.

“Hapana Mama I must cry, lazima nilie sababu hautaki kunipeleka kwa Baba yangu Afrika. Kila siku rafiki zangu wanicheka wakinidhihaki kwa kusema sina baba mimi ni yatima, nataka kumuona Baba.” Tino alilia.

“Utamuona Tino, utamuona Babayo Laizer wiki kesho tumepanga kwenda Afrika nimetuma Barua na uzuri wa Barua hiyo Babayo ameahidi kutopokea.” ISLAMA ALIMPOOZA Tino mwanaye maana kila siku Mtoto asumbua amtaka Baba yake wa Kiafrika.

“Its true Mama…… Ni kweli.” Tino alianza kufarijika. Mtoto sasa amekuwa mkubwa ana miaka minane amekopi kila kitu kutoka kwa Laizer BABAYE LABDA Nywele zake ndefu zinazojiviringa hizo amerithi kutoka kwa Mamaye.

“Mama asemayo ni kweli tupu Tino. Tukifika Afrika twaenda kutembelea Mbuga za Wanyama tutapanda Mlima Kilimanjaro na pia tutatembelea maeneo mengi ya Kihistoria David mpenzi wa Islama alichangia hoja.

“Uhakika! Au ni ndoto za mchana.”Tino hakuamini maana amekua akilia kia siku ataka kumuona Babaye Laizer.

“Surely, Uhakika upo.”Islama aliongea tena.

“Chukua hii picha niliificha ajili yako.” Islama aliitoa Mchoro mzuri wa Tembo akampatia mwanaye.

“Umeipata wapi Mama.”Tino alimuuliza Mamaye akaendelea kuitizama ndani ya fremu.

“Babayo alinipa miaka 8 iliyopita lakini sijawai kukuonesha, bahati nzuri unapenda kuchora ukiisha kula nenda ukachore. “Tino alipendezwa na ile zawadi machozi hayakumtoka tena alienda mezani kula akala kwa furaha. Islama na David waliketi mezani wakapakua vyakula vyao wakaanza kula taratibu wakimtizama Tino aliyebadilika kutoka huzuni hadi furaha.

“Tutaketi kwa kipindi cha Mwaka mmoja Maasai Land.” Islama alimwambia David wakaendelea kula.“

" It will be good, ok. Ilimradi Tino apewe ruhusa Shuleni.” Davidi aliongea akauliza.“Vipi kuhusu Pamera Mdogo wako ameipenda Safari ya kwenda Afrika?" 

       "Binafsi nimemshangaa kilio cha Tino kwenda Africa kimekua ni kilio cha Pamera kwenda Africa kwa pamoja wana hamu ya kwenda Maasai land. 

       “Rudi nyuma miaka nane iliyopita ulimsimulia Pamera uzuri wa Tanzania nchi yenye amani, upendo, furaha , raha yenye wema na ukarimu.” Davidi alimkumbusha Islama.   

                “Mazuri haya yamemvuta Pamera kuelekea Afrika.” Islama aliongeza neno.

             “Vema tuachane na hayo tuongee yetu, yetu mapenzi.” David aliketi vizuri pale mezani akaongea.

           “Ni muda mrefu sasa tangu nikuvishe pete  mpenzi kwanini hauniambii ni lini twaweza kufunga ndoa tuishi kama mke na mume.”Davidi alimkumbusha Islama.

“Nitakwambia mpenzi wacha twende Afrika tujapomaliza tour yetu mambo yote yatanoga.” Davidi hakupendezwa na lile jibu lake Islama.

“Wamaanisha harusi yetu itafanyika baada ya kuketi mwaka mmoja Afrika?” David alichukia.

“I dont mean so.Simaanishi hivyo. Lakini Yawezekana tukafunga ndoa tukiwa Afrika.” Islama alibadili nia.

         ‘No, Islama siwezi kuruhusu harusi yetu ifanyike sehemu wanazoishi watu masikini kama Afrika. Ninataka harusi yetu iwe ni harusi ya gharama na fahari. Mimi binafsi sijapenda kwenda Afrika nafanya kukuunga mkono na kiukusindikiza.” 

      “David sijaipenda kauli uliyonena.” Islama aliwacha kula akamtizama David kwa hasira kidogo.

“Mapenzi hayatazamii umasikini au utajiri. Mapenzi yapo popote duniani, kwani waafrika sio watu hata tufikie hatua ya kuyakataa mazingira yao.” Islama alimkosoa Davidi.

“Kama haupendi kwenda Afrika sikulazimishi baki England niache mie na Tino tuenende Afrika,”

       “Aaah! No, David alitweta akainama chini kwa aibu japokuwa alikuwa na maumivu tele moyoni sababu mpenzi wake wa kweli amezaa na mwanaume wa kiafrika. Ni muda mrefu sasa na ubaya wa wa kuletewa motto wa kiafrika anamtia wasi wasi David iwapo Islama atataka kwenda pekee Afrika.

      “Ninakupenda Islama” David mpenzi wa Islama aliongea.

       “Ilove you too David.”Islama alimjibu David waliendelea kula.


..............

(MAASAI LAND- TANZANIA)


Asubuhi Laizer alidamka kimyakimya pasina kumweleza mkewe pahali anapokwea . Swije Mama mwenye watoto wawili bado alikuwa usingizini, Laizer alipotoka chumbani mkuki wake mkononi, sime kiunoni, moja kwa moja akaelekea pahali miaka minane iliyopita, pale penzi lake na Islama lilipozaliwa. Pale Laizer alipokuwa mtumi Maasai,Pale Islama alipomzaa Tino, pale Islama aliishi kwa zaidi ya mwaka mmoja na nusu. Laizer akatabasamu moyoni akajisemea.

         “Uje tena  Mpenzi wangu uje na mwanangu, uje nyumbani.” 

        Nyumba aliyoiacha Islama iliota nyasi ndefu kama kichaka japo milango na madilisha yalikuwa salama, hayakuliwa na mchwa, Laizer alihitaji kuifanyia usafi pamoja na kuikarabati ili iwe bora zaidi lakini je, angeliikarabati kivipi ikiwa idhini lazima itolewe na Balozi, Kibali cha ukarabati kipo mikononi mwa Balozi hata funguo za hiyo nyumba ya wageni wajao kutalii Maasai Land, ili Laizer apewe idhini ya kuingia ndani ya ile nyumba alipaswa kwenda moja kwa moja hadi nyumbani kwa Balozi.

######

      “Wahitaji Ufunguo wa Nyumba ya kulala wageni?” Balozi alimuuliza Laizer moyoni atabasamu ajuafika kuwa kuna mazuri yatafuata pale Masai land.

     “Ndio Balozi ninahitaji kuifanyia ile nyumba usafi.”

    “kawaida ya kuja kuuchukua ufunguo  wa nyumba ya wageni wajao kutalii hapa Maasai land. Embu nidodose kwa ufupi nini kilichokufanya ufanye maamuzi ya kuja kuuchukua ufunguo wa nyumba ya wageni?" Balozi aliuliza.

      “Kuna wageni waja kutembelea Maasai land.”Laizer alijibu kwa ufupi. Balozi alifurahia moyoni uchunguzi wake ni uchunguzi wenye faida kwake.

“Nitakupatia ufunguo utaenda pamoja na Yiaro Mtumi wangu mkasaidiane kufany usafi. BADO UJANIJIBU SWALI LANGU embu nieleze ni nani hao wajao kijijini?” Laizer aliona haina haja ya kuuficha ukweli sababu Wahenga walisem mficha Jipu usaha umuumbua.  Balozi alitabasamu kisha Laizer Akaongea.

“Wamkumbuka Islama?”


Itaendelea

Tuesday, September 24, 2024

MBOSSO.. sehemu ya sita



 MBOSSO

Sehemu ya sita

Lavu aliachwa mikononi mwa babu na bibiye, wakati baba na mamaye wakiwa chini ya mikono ya Polisi. Ubaya wa wazazi wake Diva tayari walikwisha panga mpango wa kumficha  Lavu hadi pale watakaposikia kuwa Diva amelivurugavuruga penzi la yeye na Mbosso. Diva anayavuruga vuruga mawazo na tena Diva anakata tamaa ya kuishi na Mbosso.  Uzuri wa mipango yao walijipa matumaini kwamba Diva angelikubali kuolewa na Msomi mwenzie mwenye kazi nzuri, mwenye maisha mazuri, mwenye cheo na sifa njema katika jamii.            

                        *****        

    Leo ni siku ya tatu, siku  ambayo Diva ametupwa ndani ya Jela ya Segerea, Mbosso naye pia ametupwa Jela, kila mmoja amewekwa ndani ya chumba chake, Diva amewekwa hapo akilalamikiwa kwa kosa la kuwaweka wazazi wake kwenye wakati mgumu mara baada ya kutoroka miaka miwili iliyopita, wakati Mbosso amewekwa hapo akilalamikiwa kwa kosa la kumtorosha Diva akijua kuwa kufanya hivyo ni kuvunja Sheria,  akakumbushwa miaka miwili iliyopita aliiba, alimwibia mkoba mwana mama mmoja Kariakoo. Mkoba ulikuwa na pesa nyingi, vito vya dhahabu pamoja na mavazi ya huyo mwanamama.    

        Itakumbukwa kwamba yule mwana mama alikwenda kuripoti Polisi ndio maana Polisi walipata nguvu ya kumshitaki kwa makosa haya mawili. Kosa la kumuibia mwanamama vito vya thamani na pesa ni kosa ambalo Mbosso aliliona kuwa laweza kutibika haraka, japo yupo hatarini. Ule mkoba wenye mali za bei gharama ulikuwepo bado ungali umehifadhiwa kwenye gari ya mkewe mpenzi bibiye Diva. Pesa walizokwisha kuzitumia hawakuwa na budi kuzirudisha  mara baada ya wao kufanya kazi kwa bidii na maarifa.    

         Kosa la kumtorosha Diva kutoka  Dar es Salaam kwenda Kijijini Lushoto lilikuwa ni mzigo kwa mbosso, japokuwa alijipa matumaini, liwalo na liwe, yote tisa kumi angelijitetea awezavyo. Mawazo juu ya Diva na mwanaye Love yalikiteka kichwa chake, alihuzunika na kusikitika. Kwa upande wa Diva angali yupo sero hataki kula wala kulala, anasikitika moyoni mwake mara baada ya yeye kufanya maamuzi ya kuja Dare es Salaam, anajilaumu na pia anailaumu nafsi yake, afanyeje basi? Hana la kufanya, anakubali kwamba amekosea japo anajipa matumaini  kwamba atatoka tu, yeye na mwanaume wake mpenzi Mbosso. Mawazo yake Diva yanatua kwenye sura ya mwanaye Lavu na mumewe mpenzi Mbosso mara anajikuta akiimba kwa hisia.      

    “Nimekumiss mpenzi wangu,

Nimekupenda mpenzi wangu,

Nitakuwa pamoja nawe, 

wakati sio muda,`      


                 Navumilia,

 matatizo yana muda wake,

Nayo yatakwisha, 

tuvumilie,

Navumilia,

Furaha ina muda wake,

 nayo itakuja,

 tuvumilie.

Kumbe wakati huo, wakati ambao Diva alikuwa bize akiimba kwa huzuni, akiimba taratibu kwa uchungu wa kutenganishwa na Mbosso pamoja na mwanaye mpenzi, ndio wakati ambao Mbosso pia alikuwa akiimba kwa uchungu ndani ya chumba cha gereza.


Nimekumiss Mpenzi wangu,

Nimekupenda penzi langu,

Nitakuwa pamoja nawe,

Wakati sio muda,

Navumilia, 

matatizo yana muda wake,

Nayo yatakwisha, 

tuvumilie,

Furaha ina muda wake,

Nayo itakuja,  

Tuvumilie. 

Kilikuwa ni kipindi kimoja kigumu sana kwao, kipindi cha huzuni ya kutenganishwa, hata wasijue hatima yao.       

                                         *****    

        Zilipita siku saba, Diva na Mbosso  wametupwa Gerezani, Diva hakuhitaji kula, kunywa wala kulala, vivyo hivyo kwa Mbosso aliteswa sana, alipigwa ndani ya lile Gereza, baba na mamaye Diva waliwahonga Polisi wa Gereza wamtese Mbosso, Mbosso akateswa kwa vipigo vikali akihojiwa kwanini alimtorosha binti wa Tajiri? Kwanini amemuondoa nyumbani pasipo ruhusa ya wazazi wake? Mbosso alivumilia mateso ya Gerezani.    

          Diva aliendelea kugoma kula, kunywa na kulala, wazazi wake hawakuchoka kumtembelea Gerezani na kila walipomtembelea, walimshawishi Diva aachane na Mbosso .

 Walisema Mbosso hamfai Diva, Mbosso ni Jizi la Jiji, mtu anayewavunjia heshima na hadhi yao katika jamii. Itakuwaje kwa mfano mtoto wao msomi aolewe na Jizi maarufu ndani ya Jiji? Diva hakuwasikiliza, penzi la mbosso lilimnogea, alibaki na nadhiri yake Moyoni akijisemea; ‘Mapenzi hayachagui, hayabagui, mapenzi ni kumpenda umpendaye, haijalishi ana kasoro gani kiuchumi, kijamii, kisaikolojia na kadhalika. Mapenzi maana yake “Moyo” Moyo ndio hupende, Moyo ndio uchague, Moyo una macho yanayoona mbele kwenye mapenzi ya kweli, moyo una masikio masikizi ya mapenzi yenye udhati, Moyo una Moyo ndani yake na huo Moyo ni Moyo wa wawili wapendanao.  

          “Diva.” Baba alimwita Diva, na siku ya leo mamaye Diva pamoja na Sam  mzuri wamemtembelea Gerezani wapate kumshawishi. Sam mzuri amevalia Suti yake nyeusi pamoja na Tai yake nyekundu, wote kwa pamoja wamekuja kumtembelea Diva.     

       “Abee baba.” Diva aliitika kinyonge sana, amedhoofika, mwili wake umekonda, hatamaniki, yupo chini ya sakafu anawaza, na mawazo yake yote yapo kwa mbosso.       

     “Baba na mama wanahitaji heshima, ukiwaheshimu baba na mama utaishi miaka mingi yenye paradiso, raha na furaha, lakini usipowaheshimu baba na mama utapata laana.” Baba aliendelea kunena.   

         “Diva wewe unatokana na mbegu bora iliyobarikiwa na Mwenyezi Mungu, umeandaliwa maisha bora yenye elimu na maadili. sasa kwanini Diva msomi mzuri kama wewe unafanya kuwasaliti wazazi wakio? Kwanini mwanetu? Kwanini  hautaki kutuonesha heshima kwa uchaguzi na maamuzi yetu yalio sahihi?” Baba alimuuliza Diva, lakini Diva kimya analia kwa uchungu.  

          “Diva mpenzi, maisha ni maandalizi na maandalizi hayo yana nia pamoja na malengo, ukikosea maisha  ni sawa sawa na kuharibu nia na malengo yako yote, sasa tafakari, na baada ya kutafakari fanya maamuzi. Atakupeleka wapi huyo mwanaume mwenye tabia na jina chafu katika jamii? Atakufanyia  ambacho kina heri na afadhari katika maisha yako? Diva mwanangu usikosee wala usithubutu kufanya makosa.” Mamaye Diva aliongea. 

           Samsoni yule mtumishi wa benki akafungua kinywa akanena. “Haijarishi hata kama tayari umezaa na Mbosso, mimi nipo tayari kuishi na wewe. Sikiliza maneno ya wazazi ni busara na hekima ambazo kwako ni maandalizi mema katika maisha, ninakupenda Diva, wewe ni chaguo la moyo wangu unastahili kunikubali, ninastahiri kuwa nawe katika maisha haya yote.” Kelele zote ambazo wazazi wake Diva pamoja na Samsoni walizipiga, Diva alijigeuza bubu asitake kusikia la Ae au la  Bae. 

           “Kwanini kila neno jema tunalonena kwako haulichukulii na kulikubali Diva?” Baba alimuuliza Diva kwa hasira.    

        “Unataka tukupe au tukufanyie nini Diva upate furaha, ukubaliane na kauli zetu?”  Mamaye Diva aliuliza.   

         “Je, unahitaji kuendelea masomo  ‘School of Law’? Tupo tayari kukupeleka Ulaya au Amerika ukasome kipenzi, ilimradi uachane na Mbosso, tupo tayari kukupa nusu ya utajiri wetu ili uachane naye, Diva….. Sikiliza sauti zenye hekima.” Mamaye Diva alimwaga machozi. 

           “Haujibu?” Baba alimuuliza Diva kwa hasira, Diva angali anamwaga machozi, macho yake yamevimba kwa kulia, mashavu yake yamebadilika na kuwa mekundu, yameiva kwa kilio, masikini Diva ukimtazama utamuonea huruma.  

          “Kama hautaki kutupatia jibu sahihi juu ya kuachana na Mbosso, jua fika kuwa lazima tufanye kitu kibaya kwa mwanao  Love  utajuta Diva.” Baba aliropoka ili kumtisha Diva, ajabu Diva hakutishika, alibaki kimya tuli, tulivu.   

         Mara ghafla Diva akaugua Gerezani, akawa hoi taaban sababu ya kukataa kula, kunywa na kulala, Mkuu wa Gereza akawapigia simu mama na babaye Diva, haraka haraka mama na babaye Diva wakamkimbiza Diva Hospitalini, na katika kipindi hicho, Mbosso naye akaugua vibaya sana, akakimbizwa Hospitali aliyolazwa Diva. Hali zao zikawa tete, hawawezi wala hawajiwezi, madripu ya maji mikononi, madripu ya damu mishipani, madawa na masindano tele. Mamaye Diva alikuwa taaban kwa kilio akilalama inatosha sasa, inatosha, watampoteza Diva sababu ya mapenzi, watampoteza Diva sababu ya mwanaume wasiyempenda na yule ambaye wazazi hawampendi. Mama aliendelea kulia na kumsihi babaye Diva alegeze kamba wasije kumpoteza Diva.   

         Kwa shingo upande babaye Diva alikubali Diva atolewe Gerezani, ajabu Diva alipozinduka aligoma kurudi nyumbani kwa wazazi wake akidai anamtaka Mbosso yule aupendezaye mtima wake, la, sivyo atachukua maamuzi mengine magumu zaidi. Hofu ya kumpoteza Diva ilikuwa kubwa mama alimshawishi babaye Diva Mbosso atolewe Jela ili kumnusuru Diva asije akachukua maamuzi magumu. 

           Kwa shingo upande babaye Diva akafanya kumtoa Mbosso Jela akimkanya na kumuonya asijichanganye na Familia yao, asijaribu kuwa karibu na Diva, asichokoze Nyuki asije kupatwa na masahiba asiyoyategemea. Diva akarudi nyumbani kwa baba na mamaye, akala akanywa na kulala, bado aliendelea kupambana na vikwazo vingi kutoka kwa wazazi wake wakimshawishi aolewe na Samsoni.                                    *****

Itaendelea

KUKU WA KIZUNGU ... Sehemu ya nane


Kuku wa kizungu


Sehemu ya nane

 Yiaro alifika nyumbani kwaLaizer, muda ule Laizer alikuwa akimhudumia mbuzi wake aliyetoka kujifungua muda si mrefu, mkewe Laizer Swinje alitoka asubuhi ile yupo Porini kusaka kuni na matunda. Duka lao leo hii sio Duka tena, limefirisiwa kwa hila na kwa chuki zake Balozi ambaye kwa wivu alionao alihakikisha kuwa  Laizer anaugeukia Umasikini aliokuwa nao miaka mingi iliyopita kabla hajawa mtumi wa Islama.

“Karibu Yiaro, karibu Mtumi wa Balozi.”Laizer alimkaribisha Yiaro.

“Asante bwana mkubwa, pole na majukumu yote?  Ninaona mbuzi wako wanazidi kuongezeka.” Yiaro alitania.

“Ah! Wapi waongezeke hawa na njaa hii ya mifugo hapa Maasai land, wafugaji wanapigana na wakulima, mmh! Sidhani kama kwa ukame huu mifugo itaongezeka.” Laizer alimjibu Yiaro Mtumi wa Balozi “Ndivyo ilivyo Maasai Land, Wamaasai  sikuzote hawapendi kujishughulisha na kilimo zaidi ya ufugaji, unajua kama na sisi tungelima tungelikuwa na akiba ya chakula cha Mifugo.” Yiaro aliongea.

“Najua kuhusu hilo.” Laizer alijibu.

“Sio mbaya, kuna barua yako, inasema Imetoka England, hii hapa ikamate.” Yiaro  Mtumi a Balozi alimkabidhi Laizer ile Barua,Laizer aliposikia Barua imetoka England. Moyo wake ukamwenda kasi mapigo. Akaipokea. “Fungua basi, mbona waishangaa.”Yiaro alitaka kujua kilichoandikwa ndani ya Ile Barua.

“Oh! Usijari nitaisoma baadaye, kwa sasa nipo bize,”Laizer aliongea akaelekea ndani, amemuacha Yiaro amechukizwa kwa tendo la kushindwa kuujua umbea ulioandikwa ndani ya ile Barua. Muda si punde Yiaro akaondoka. Laizer akaingia ndani akaiwasha Karabai Faster faster akiwa pekee yake akaifungua ile Barua.

Kitu cha kwanza kukutana nacho ndani ya ule mfuko wa kaki ni Karatasi moja nyeupe imechorezwa Maua na mnuko mzuri wa Marashi ya Pemba na Unguja. Akaifungua ile Barua akaanza kuisoma.


ISLAMA.

ENGLAND.

20/05/2008

ARMOUR WANGU LAIZER.

Laizer wa moyo wangu, baba yake Tino. Tumaini langu  haujambo? Ni miaka saba sasa kipindi kirefu cha muda tangu nimeondoka Afrika, nilikuahidi nitarejea na sasa ninataka kurejea tena.

Love ninajua kuwa nilikuweka katika wakati mgumu sana, mgumu wa kipindi. Ulinimiss Baba Tino, Ulimmiss Tino mwanetu,  anasumbua anataka aje Afrika, aje akuone Baba wa damu yake.

Damu nzito kuliko maji. Love acha mwanao aje Afrika kumuona baba yake. Basi mpenzi katika msafara wetu nitaongozana na DAVIDI Mpenzi wangu wa zamani, PAMERA  Shoga yangu pamoja na TINO mwanetu. Mpenzi utuandalie Makao mema. Hizo million tano zitumie kama mahitaji yako wewe pamoja na mkeo mpenzi Swinje, mie nitakapokuja na Campany yangu gharama zote tuachie nitazigharamia.

Wasaalam akupendayeISLAMA (MAMA TINO).

“Waooo!” Kila mstari wa ile Barua ulimtia Presha na mapigo ya moyo Laizer, moyo mapigo yalimwenda kwa fujo lo! Ujio wa yule aliyempenda zamani. Aki! Milima haikutani binadamu wanakutana. Kweli damu ya mtu haipotei hivi hivi.

Tabasamu pana lahaja  lililipuka mdomoni kwa Laizer akaingiza mkono ndani ya ule mfuko wa kaki, akatoka na mabunda matano ya pesa, kuhesabu haraka haraka ni milioni tano Cash. Furaha, furaha na raha  alijikuta Mori ya furaha imempanda anaruka juu kama mwendawazimu, anaruka ndani ya nyumba yake yenye kofia refu la bati.

###############################

Yiaro alirejea nyumbani kwa bwana wake Balozi, alipofika tu Balozi alimuuliza Yiaro.

“Ile barua ya Laizer ilisomeka kuwa inatoka wapi na wapi hapa Tanzania?”

“Ile barua haikutoka sehemu yoyote Tanzania bali ilisomeka kuwa inatoka England kwa wazungu.” Yiaro alijibu kwa ufasaha.

“What?” Balozi aliuliza macho pima kama mjusi aliyebanwa mlangoni.

“”Ndio Balozi, ile Barua imetoka Euorope.”

“England!?” mmh! Laizer hana ndugu England, atakauwa ni nani aliyemtumia?”

“ Nisijue mie, maana nilipoileta ile barua nilikwambia Customs yetu ni kuifungua barua na kuisoma au kucheki kilichomo ndani, ajabu wewe ulipiga kelele tusiifungue.” Yiaro kijana wa 22 Age  mrefu, mwembanba Keisha baleghe tayari alimjibu Balozi Bwana wake.

“Oh! My GOD!! Ulipofika kwa Laizer ulimwona Laizer akiifungua?” Balozi aliongea amejaa wasi wasi. Bahati nzuri wakati huu hakuwa karibu karibu na eneo  walipo wakeze, alijiketisha mbali na nyumbani, kama angeliketi Nyumbani basi Bi. Mkubwa angelimshambulia kwa maneno ya misuto.

“Ah! No, hakuifungua alidai ataifungua baadaye.”

“ God have Mercy! Una maanisha Laizer hajaifungua ile Barua.” Balozi alitilia mkazo swali lake, Yiaro asijue nini kinamfanya Bwana wake awe mkali namna ile.

“Sure, kitu kama hicho, alikuwa bize akitoa huduma kwa mbuzi wake aliye zaa muda si punde.” 

“Yiaro Mtumi wangu, embu niache nikamsabahi Laizer.” Balozi Ole aliongea, akaingia ndani ametoka na mayai kumi ya kuku wa kienyeji pamoja na buyu la asali  zawadi maalumu kwa ajili ya Laizer adui yake.

###

Balozi alifika nyumbani kwa Laizer kuna umbali kidogo na pahali anapoishi yeye na wakeze wawili. Alipofika akabisha hodi mara mbili tatu lakini bila tarajio hakuna mtu aliyekuja kumfungulia mlango sababu  muda kidogo Laizer alitoka ana kwenda Benk Arusha mjini kutunza Pesa alizopewa na Islama.Amebadilika sana, siku hizi amekuwa mtu aliyeelimika tofauti na miaka saba iliyopita. Ole akaingia ndani ya geti kubwa nyumbani kwa Laizer.

“Ma’ Yoyo!” Balozi aliita asijibiwe. sababu Mama Yoyo mkewe Laizer hakuwepo nyumbani yupo kisimani kuteka maji pia amepita  Porini kukata kuni.

“Laizer!” Balozi alimwita Laizer ajabu Laizer hakuitika sababu hayupo ametoka ni mwenye furaha tele ya kupata bahati nasibu kama ile.

“Wapi tena wenyeji wa nyumba hii? Ukimnya kama Pango la Ibilisi.” Balozi akaufungua mlango na kwa bahati nzuri mlango uliegeshwa ovyo akapata nafasi ya kuingia na kuutafuta ule mfuko wa kaki wenye Barua aliyotumiwa Baba Yoyo.

“Mmmh! Kiza totoro.” Akawasha Karabai iliyotelekezwa juu ya  meza. Iliwaka pasina kupoteza muda Balozi alianza kuinama chini ya Mavungu ya Meza, viti na kuparanganyua masufuria na vyungu akiitafuta Barua iliyotumwa kwa Laizer. Bahati iliyoje akauona mfuko wa kaki, Furaha iliyoje akaketi juu ya Viti vya Laizer tabasamu jingi usoni  akaaanza kusoma nje ya bahasha moyo mapigo yakamwenda kasi alikutana na jina Islama likiwa limeandikwa nyuma ya ule mfuko wa kaki. mbele ya ile Bahasha aliuona muhuri amabao kwa uhakika alijua ni muhuri kutoka England. mapigo ya moyo yakamwenda kasi haraka akachungulia ndani ya ile Bahasha kuona kama kuna Barua ataipata hakuipata zaidi aliambulia kuiona Dollar moja mpya inanukia vizuri, haraka haraka akaichukua ile Dolar moja akaificha ndani ya mfuko wa Serewili yake.

“Iwapi Barua kutoka England?” Alijihoji asipate jibu

“Yamkini imehifadhiwa chumbani.” Alijijibu fikirani. akaeleka chumba alalacho Laizer na Swinje mkewe. akapapasa kitasa cha lango la chumba cha Laizer na mkewe, hakupendezwa maana ulikuwa umekokomewa kwa ufunguo ulipitishwa ndani ya kile kitasa.

“Si haba! Chale zanicheza yawezekana Islama  atakuja Maasai land.” Alijiaminisha.

Teh teh teh teh. Alicheka kidogo.

“Ni furaha kwangu ni amani Moyoni mwangu Islama anakuja na ujio wake lazima nimpokee, lazima niwe karibu nayeye tena.” Furaha ilimjia Balozi.

“Zubaa zubaa mwana umkose! Nimempenda Islama. Je, nimkose? haiwezekani kwa sasa nimekwisha boreka, nimekuwa mzuri zaidi, nimekuwa kijana tofauti na zamani.” Akajitizama tizama mwili wake ulivyo akajiona yeye bado ni mali ya kupendwa na mabinti kisha akaurejea mlango wa kutokea nje akaufunga vizuri ile Bahasha ya kaki akairejesha pahali pake naye akafanya kuondoka kurejea nyumbani kwake mwingi wa furaha na matumaini.


Itaendelea.

Monday, September 23, 2024

DONDA LA WIVU.. sehemu ya tatu



KASHIKWA SHARUBU.

            Mtume! Mungu wangu we! Mzee jamali alishituka mara baada ya kufika ndani ya shamba lake  alilopanda karoti, nyanya  na kabeji. Shamba lilikua limeharibiwa vibaya sana, aliwakuta Ng’ombe wakiwa wameingia ndani ya shamba lake na kuanza kuharibu haribu. Ng’ombe wale walikua wakishambulia mazao yake kama vile nzige ashambuliavyo mara baada ya kuingia kwenye mimea.


Looh! Mama we! Mzee Jamali alichanganyikiwa, asitake kuamini kama tukio lile analoliona machoni kwake ni jambo la kweli ama la! Ni utani, asitake kuamini kuwa lile tukio alishuudialo mbele yake ni sinema au ndoto za mchana, ndoto za kufikirika.


            “Yallah! Hasara gani tena hii mbele ya macho yangu?” Muda ule ule mzee Jamali alianza kuwafukuza wale  Ng’ombe pamoja na kondoo waliokuwa bize wakiharibu mazao  shambani kwake. Hata hivyo kitendo kile cha kuwafukuza wale wanyama hakikusaidia kitu, kwani tayari wale wanyama walikwisha kuharibu haribu shamba lake. Tayari walikwisha kumtia hasara kubwa isiyo weza kuhesabika.


             “Joeli, Joeli, Joeli.” aliita mzee Jamali  aliita kwa sauti kuu.


             “Joeli we!”  Aliita tena lakini asiitikiwe.


 “Amekwenda wapi huyu mtoto mpumbavu Joeli, amewaacha wanyama wa Mzee Shemagendo wakiniharibia shamba langu, hapana, ni lazima niende kwa mzee Shemagendo nikamshitaki huyu kijana, amenitia hasara kubwa kiasi.


  Aliongea pekee  mzee Jamali, amekasirishwa na kitendo cha Joeli, kivulana kilichopewa kazi ya kuchunga na kuwongoza wanyama. Ubaya wa huyu Joeli angali bado ni mtoto mtundu na mtukutu. Wakati wote mtoto huyu hupenda kucheza mpira akiwa pamoja na watoto wenziwe, uwasahau wanyama. Basi utamkuta anapanda juu ya


anapanda juu ya miti na vilima akifukuzana na watoto wenziwe. Joeli bado ni mtoto tena mtoto wa kufurahia michezo.


            “Looh! Masikini jamani! Nilikwisha panga kuvuna mazao yangu  niwauzie wafanya biashara wanaosambaza mboga mboga ndani ya jiji la Arusha na Dar es saalam. Mpuuzi mtoto Joeli amewaacha wanyama wakiharibu haribu shamba langu……. Oooh! Masikini uzembe gani huu?”


  Hasira zilimpanda Mzee Jamali, alitamani angelikua na mbawa za ndege apate kuruka afike pale alipo Joeli. lakini atafanya nini mzee? Amevunjwa moyo,  shamba lake halitamaniki tena, limeachwa nyang’a nya’ga, Ukitegemea wiki ya kesho alitarajia kuvuna na kuwauzia wafanya biashara mazao yake.


“Tokeni!  Tokeni! Tokeni!” Mzee Jamali alijitahidi kuwafukuza wale Ng’ombe, Mbuzi na Kondoo ambao walikua wangali bize wakiharibu haribu shamba lake, shamba lake halikutamanika machoni, lilikua limeharibiwa haribiwa vibaya sana,  ndugu yangu iwapo kama ungelipata nafasi ya kulitazama haki! Ungelimuonea huruma Mzee Jamali. Mzee yule akawa mnyonge wa ghafla, masikitiko makuu moyoni,  akiyatizama tizama mazao yake yalivyoharibiwa, mategemeo yake yalikua ni kukikamata kiasi cha shilingi laki sita mkononi. Pesa ambazo tayari zilikwisha kupotelea ndani ya midomo  na matumbo ya wale wanyama waharibifu.


“Joeli, Joeli, Joeli we!” Mzee Jamali alimwita tena yule mtoto aitwaye Joeli, mtoto mwenye kadirio la umri wa miaka kumi na mitatu, kapewa dhamana ya kuwatunza wale wanyama lakini kwa utoto wake mwingi ndio hivyo sasa kaenda kucheza mpira na kupanda juu ya miti akiwaacha wanyama wale wakifanya uharibifu ndani ya shamba la Mzee Jamali.


                       “Nitamtafuta huko huko kwa mzee  Shemagendo, nipate kumshitaki kwa makosa aliyonifanyia, Mzee Jamali alishika njia  inayokwenda nyumbani kwa Mzee Shemagendo apate kumshitaki mwajiri wake. Alikwisha itambua ile mifugo, aliitambua kuwa ni ya Mzee Shemagendo, anaijua vizuri,  imewekwa alama nyuma ya migongo yao na alama zile sio ngeni machoni kwake. Basi safari yake ikaanza, akipanda Vilima na kushuka Vilima, amejaa hasira hasara anaongea pekee njia yote ni kama vile kageuka na kuwa mwendawazimu fulani aliyepoteza mwelekeo.


             Ndani ya dakika harobaini na tano Mzee Jamali alikwisha kufika nyumbani kwa mzee Shemagendo, alikaribishwa vizuri kama kawaida ya mgeni yeyote yule aendaye ugenini. Uzuri wa siku ile alimkuta Mzee Shemagendo akiwa ametulia tuli, ametulia kama maji  mtungini, anavuta makambo kambo, kiko mdomoni, moshi unafuka na kutoka kwa raha zake zote. Pembeni ya eneo aliloketi  amewekewa pombe ya asili inayotengenezwa kwa kutumia Miwa. Mzee yule alifurahia kuvuta mikenge miwili mitatu pamoja na moshi utokao puani na mdomoni kwake kwa kutumia Kiko yake.


Walisalimiana na baada ya salamu mzee Jamali aliyatoa maumivu yake yaliyotulia moyoni, akayasambaza masikioni kwa Mzee mwenzie aliyejiweka bize akijiburudisha kwa yale matamanio ya pua na mdomo.


               “Ndio hivyo mzee mwenzangu, N’gombe wako wamekula na kuharibu haribu shamba langu, wamenitia hasara kubwa sana hasara ambayo sikuitarajia, sikuitarajia kama ningeliiona, machoni, amini, kama hauamini maneno yangu kuwa ni maneno thabiti wacha tuongozane, tufike shambani kwangu ili ukajionee wewe  mwenyewe uharibifu uliofanywa na mifugo yako.” Mzee Jamali aliihitimisha akiwa na hasira shingoni.


                    “Mmmh! Maneno uyanenayo yana ukweli, ama! Waileta kesi isiyo nihusu mie na mifugo yangu?” Mzee Shemagendo alimuuliza mzee Jamali.


            “Ndio maana nimekwambi itakua vizuri iwapo tutakwenda pamoja ukashuhudie uharibifu uliofanywa na mifugo yako, hapo ndipo utakapo niambia dhariri kama  mifugo tutakayoikuta shambani kwangu ni ya kwako au la!”


             “Nitayaaminije maneno yako mzee Jamali? Ama, wewe utaniaminije iwapo nitakuchukua na kukupeleka ndani ya Zizi la mifugo yangu? Utaiona ilivyo tulia tuli, haijapata kutoka nje siku nzima ya leo.”



              “Tangu asubuhi ya leo hadi mchana huu mifugo yangu imetulia tuli haijapata kutoka, Joel unaye niambia amefanya uzembe wa kuiwacha mifugo yangu ndani ya shamba lako mbona yupo ndani, ametulia tuli siku nzima ya leo, hajapata kwenda malishoni zaidi ya kupumzisha mwili na akili zake.”


             “Umesema?” Mzee jamali aliongea kwa mshituko.


“Umesema ati Joeli hajaenda malishoni? Mzee mwenzangu muda huu ninaoongea na wewe twaweza kwenda chini ya kilima cha Kidundai kutizama mifugo ilivyoharibu haribu Shamba langu nawe utaniambia ukweli wa shuhuda za macho yako, utaniambia kama Joeli anahusika au hausiki katika  uzembe huo.” Mzee Jamali hakuitaji kutoa maelezo mengi juu ya uharibifu uliofanywa na na Joeli mtumishi wa Mzee Shemagendo.


“Hupaswi kuandikia mate wino ungalipo Mzee wangu tizama kundi langu lote la Ng’ombe Mbuzi na Kondoo hawajapata kutoka ndani ya banda, sababu Joeli mtunzaji wa mifugo yangu ni mgonjwa, tangu usiku wa jana amekamatwa na Maralia.” Shemagendo aliongea. Wakati huo huo Jamali tayari wamekwisha kufika ndani ya  Zizi la Mzee Shemagendo kundi lake limetulia tuli kama maji ya mtungini. Kundi limeshiba limetuna tuna na kuwa na afya bora, hali ambayo inazidi kumstaajabisha Mzee Jamali, ni kama vile Mzee Jamali alikuwa ndotoni, ndoto ya mchana, ndoto isiyo mletea picha, picha halisi ya kile anachokiona. Nusu saa iliyopita mifugo ile ile ambayo anaiona   ndani ya banda la Mzee Shemagendo ndio ile ile mifugo iliyolisafisha shamba lake la nyanya, karoti na kabeji. Mifugo hiyo imelisafisha shamba na kulifanya liwe jeupe kama saruji.


                     “Je, ni halali kuileta kesi ya visingizio nyumbani kwangu? Joeli unayedai kuwa ameiwacha mifugo yangu shambani kwako ndie huyu huyu unayemwona amelala ndani ya kijumba nyasi changu, yu mgonjwa wa Maralia iliyomkamata usiku wa kuamkia jana.” Shemagendo aliongea pasina hofu wala wasi wasi, wakati huo tayari amekwisha kumvuta Mzee  Jamali ndani ya kijumba nyasi alicholala mtumishi wake Joeli.


                    “Wallah! Hii ni miujiza sasa, ninashindwa kuelewa vizuri, mbona mifugo niliyoiona ikilitafuna shamba langu, ndio hii  mbele ya macho yangu, ajabu! Imetulia tuli kama vile sio hii niliyoiacha muda si mrefu ndani ya shamba langu.” Mzee Jamali aliongea kwa kuchanganyikiwa.


                   “kama una ushahidi wa kutosha, ni vema ungeliileta hiyo kesi nyumbani kwangu, lakini sio kufanya maamuzi yasiyo na vithibitisho. Utaushangaza sana ulimwengu Mzee mwenzangu pale unaposhindwa kuwa na vithibitisho kamili. Kwanini usiikamate mifugo iliyotafuna mazao yako? Kwanini usimkamate Joeli ambaye wewe binafsi unadai kuwa anahusika katika uharibifu wa mazao yako?”


                      Mzee Shemagendo  alinena, amemwacha mzee Jamali hana neno la kunena, ni mwingi wa wa hisia anahisi labda amechezewa akili zake sababu jambo kama hili linaupumbaza  moyo na akili zake, asitake kuamini au kuelewa kama huu mchezo ni wa sihiri au ni madanganyo, yeye anazidi kujiuliza kichwani kwake, kwanini iwe hivyo?  Basi  Mzee Jamali akarejea Shambani kwake apate kutazama tazama hali halisi aliyoachana nayo.


                                     ########################


Allah! Kumbe Mzee Jamali alizidiwa kete, kazidiwa nguvu, kazidiwa ujanja, tena kazidiwa na mtoto mdogo aitwaye Joeli, kapigwa chenga. Kapigwa changa la machokalamba jokerkapitishwa njia za panya. Joeli kaiswaga swaga ile mifugo  aliyoachiwa aitunze ile ishibe, inywe  itosheke. Wakati Joeli  alikwisha kumuona Mzee Jamali , alimwona  akija, akija Shambani kwake akajificha pahali pembezoni mwa miti mingi iliyopo pale shambani kwa Mzee Jamali. Alijua ile ishakua kesi, alijua ile ishakua balaa, maji shingoni na iwapo ile kesi ingelimfikia Mzee Shemagendo basi Joeli ategemee kibarua chake kuota Unyasi. Ategemee  mshahara wake wote, ule mshahara anao tunziwa na Mzee Shemagendo  ungelitumika kulipia uzembe alioufanya.


            Joeli     hakukubali, Presha ilimpanda, akamwona Mzee Jamali akipanda juu ya kilima cha Kidundai, akielekea nyumbani kwa Mzee Shemagendo moyo ulizidi kumdunda ‘ndu ndu ndu ndu!’  Pasina kuchelewa alihakikisha kuwa  anawaondoa 


wale wanyama katika eneo lile akawaswaga faster faster akaelekea nyumbani kwa Mzee Shemagendo kwa kupitia njia nyingine, njia za panya.


Mara baada ya Joeli kuwafikisha nyumbani wale wanyama  akawaingiza Zizini, akawalazimisha kulala nao wakamtii kwa lazima,kama wanavyomtii siku zote. Akamwendea Mzee wake Mzee Shemagendo, akamkuta akiwa bize anavuta vuta makambo, akiwa bize anavuta vuta mikenge kwenye mtungi wake wenye pombe ya asili. Joeli akamsimulia Mzee Shemagendo, akamsimulia juu ya kesi inayomkabili. Ujanja ujanja  pekee ulitosha kwa Mzee Shemagendo kulinusuru lile jahazi ambalo muda si mrefu lingelizama. Tayari alikwisha kumuelewa mtumishi wake Joeli, tayari alikwisha elewa hasara ambayo mzee Shemagendo angeli gharamia.


        Shilingi laki sita sio pesa ndogo ni pesa mingi sana, kuzitafuta hizo pesa na kuziweka kibindoni yataka moyo, ni kazi nzito na ngumu sana. Yataka moyo, yataka moyo wa kuzitafuta, la sivyo mambo yangelikua mshike mshike  mambo yangelikua mabaya iwapo ile kesi ingelifika Barazani kwa wazee.


              “Jifanye kuwa unaumwa, jifanye hujui chochote kinachoendelea, mimi nitafanya juu chini  kuhakikisha kuwa mambo yanakua sawa, wala usitie shaka, enenda ukalale umefanya vema kuwakimbiza hawa wendawazimu ndani ya mabanda yao, hawana uelewa, hawatambui chochote kile wanachoambiwa, daima hawa ukiwakokota wankokoteka, ukiwafukuza wanafukuzika ni wajinga wenda wazimu.” Alionga Mzee Shemagendo, akiikosoa na kuizodoa ile mifugo yake.


 

Itaendelea









Sunday, September 22, 2024

JUTO sehemu ya tatu


 

JUTO

Tulipoishia

Kumbe! Kumbe binti hakujua kuwa wenzie wapo kazini, pale wanamchota akili, kilichofunikwa binti anaona kimefunuliwa na kilicho funuliwa anaona bora kifunikwe ni kama Mazingaombwe, yeye mwenyewe haelewi nia na malengo ya hawa Mashosti, Mabesti na Mashoga zake.

Hakushtuka wala hakushtukia kuwa hao wenziwe anaowaona kuwa ni wafariji wake kimawazo wamemtamani Mumewe Denis, maana Denis mwenyewe hatulii nyumbani ni kiguu na njia, yupo bize kusaka pesa, kutwa kuchwa yupo ndani ya Coster anasaka hella ya Bosi ili apate kidogo dogo ambacho ni haki kwake. Au labda hawa Mashosti walimuonaDenisi hapo Malapa? Labda, maana Denis ni Dereva na Dereva lazima akutane na makumi ya watu kila siku iitwayo leo. Jamani hisi na hisia hazitoshi, tusilolijua litatusumbua, tusilolijua lipo kizani.


Endelea hapa

“Hembu tuwekewazi Shoga yetu, Mumeo kakuachia kiasi gani cha Pesa ili zikuwezeshe kupata mboga mboga na viungo vingine?” Leo Elizabeth alimuuliza Lily, wamekuwa wakimuuliza maswali kibao yanayomhusu yeye na Mumewe hata asijue kuwa hao Shagaze ni wajanja tena ni wajanja wa Jiji.

“Yeye huacha kila siku Elfu Ishirini juu ya Meza, hizo zatosha kununulia vitu vidogo vidogo ilihali nyumbani kwangu hapakosekani mboga, viungo, mchele, unga, mafuta nakadhalika.” Lily aliwajibu wale rafikize.

“Mmmh! Shosti huoni kwamba Mumeo hakutendei haki? Yaani uachiwe Shilingi elfu Ishirini? Jamani Dereva huyu anakutesa sie wenzio waume zetu huacha Mezani Shilingi laki moja na nusu kwa ajili ya matumizi ya mboga mboga na pengine zinapobaki ni kwa matumizi yetu binafsi, si unajua tena kila mtu ana Mume wake, kila mtu Mumewe anamjali Mkewe.” Anjelina alitia neno. Lily aliachia domo wazi akishangaa.

“Jamani kweli au utani? Siamini, pesa yote hiyo ya kazi gani kwangu wakati kila kitu kipo nyumbani hata hiyo Elfu ishirini ni kama zawadi anipayo Mume wangu maana kuna sikuhiyo pesa haitumiki yote sababu nina kila kitu ndani.” Lily alijitetea. “Shoga sio hivyo, tusikilize sisi Mumeo hakupendi, kama angelikuwa anakupenda angelikudekeza kama Mtoto mchanga. Ajabu anakutendea kama sio Mtoto mchanga, alipaswa kukuachia Pesa nyingi kila siku kuanziaShilingi laki moja na kuendelea.”Mashosti walitia neno, neno ambalo liliuchanganya sana Mtima wake Lily akijiuliza Mumewe ambaye mwisho wa mwezi hupokea Shilingi laki tatu, ataweza kweli kumpatia shilingi laki moja kila siku? Mmmh!  Vigumu, haiwezekani, hiyo Elfu ishirini pekee Mumewe hupewa na Bosi ili imtoshe kwa  mahitaji ya nyumbani. Je, hiyo laki moja au laki mbili Mumewe atapewa na nani? 

“Tena Shogangu keshokutwa unikopeshe Shilingi Elfu hamsini nina shida nayo, nina shida kweli kweli nitakapopewa na Mfalme wa moyo wangu sitachelewesha nitakulipa, si unajua tena ukame ni kitu cha lazima? Acha basi chako kula na wenzako” Lisa ambaye ndiye aliyemsuta Lily kwa kumwambia Mumewe hamtendei haki anapompatia pesa ndogo ya mahitaji ya nyumbani ajabu ndiye aliyekuwa akiazima pesa akidai atairudisha pale Mumewe akimgea.

“Kweli Shoga zangu au ni utani haya maneno yawatokayo vinywani?” Lily alitia neno.

“Uongo ushindwe, uongo hauna nafasi kwetu, sababu msema kweli ni Mpenzi wa Mungu, Shosti umewekwa hapa kama Sanamu, huelewi wala hujielewi, tunakushangaa sana yaani Mwaka mmoja wa kuishi na Mumeo hajawahi kukutoa Out ukapate Dinner au kukupeleka Sinema mkacheki Muvi, Mwaya ujisikie kuwa hupo kwenye ndoa ujisikie kupedwa, jamani lo! Masikini.” Mashosti waliongea zaidi na zaidi.

“Kinachotuumiza sie ni kitendo cha Mumeo kushindwa kukujali, anajifanya anajali sana kazi kuliko kumjali mkewe, adamke alfajiri mapema arejee usiku wa manane, hajui unavyoendelea, hajui unavyommiss, hajui unavyotamani awe karibu karibu nawe. Hivi je, ukipatwa na tatizo lolote lile linalohitaji Emergence utafanyaje Shosti? Masikini tunakuonea huruma.”

“Shosti, mnenacho chaniingia moyoni japo sijui nifanye nini mie mwenzenu mwaniacha njia panda.” Lily aliongea, akiamini maneno ya Mashosti ni ya kweli.

“Shosti, sie tunakupenda, pendo la kupendeka, utambue na pia ujue kwamba rafiki mzuri ni yule anayekushauri.  Hatujakukataza kuwa na Mumeo, hatujakushauri uachane na Mumeo lakini sie tunakushauri…..umtafute mwanaume kijana wa umri wako, huyo awe karibu karibu na wewe, akupooze mawazo yanayoendelea kulindimaa, akuondolee upweke wa kutokuongea na Mwanaume japo awe mfariji wako.” Elizabeth alimshtua Lily kwa yale maneno.

“Itakuwa siri yetu Mwaya, hatutamweleza mtu, kikubwa ni kuona mwenzetu hauteseki, umesikia wapi na wapi kwamba binadamu tuliumbwa kuteseka? Hata vitabu vya Dini vinapinga kuhusu hilo, hata vitabu vya Dini vinasisitiza kusema kuwa binadamu tuliumbwa tuishi kwa raha mustarehe.” Anjelina alinena.

“Mmmh! Shoga zangu nimsaliti Denis nitoke nje ya ndoa wakati nimefundwa uvumilivu na ustahilivu, wakati nimefundwa upendo usio na kikomo.” Lily aliongea.

“Mwaya, kama hautaki kutusikiliza basi ni bora tukuachie huo ‘Upunda na Ukondoo wako, wenzio tumeona jinsi unavyoteseka, tunakuhurumia wewe mwenyewe lakini wewe hautusikilizi wala haujali mashauri yetu.” Elizabeth aliongea, Safari hii hana furaha, amenuna, domo halimpendezi, kumbe anafanya makusudi ili kumteka yule binti.

“Wenzio tunapoona waume zetu waenda njia tusozitaka tunawaonya na tujapoona hawaonyeki tunawaacha na kufuata Uhuru wetu wewe pia unapaswa kuwa huru pale unapoona Mumeo haendani sawa na wewe mkalie kimya wala usijivute vute kwake, jitafutie njia zako.”Aliongea Anjelina, muda sio mrefu walihitaji kuondoka wakamuacha Lily yu ndani ya dimbwi la mawazo

********************

Lily alikubaliana na mawazo ya wale Shosti zake mara baada ya kutafakari kwa kina pasipo kupata jawabu sahihi. Alihisi kama Mumewe hamtendei haki, japokuwa sio kweli kusema ati Mumewe hamtendei haki, uwezo wake finyu wa kukaa na kufikiri ulimfanya anasishwe kwa kijana mmoja mitaa ya Buguruni Malapa, Geofrey, ndio jinale labda hupenda aitwe Geo, ambalo ni kifupisho cha jina Geofrey.

Mapendo yakawa ni ya siri sana pasipo Mumewe Lily kugundua wakati huu pendo la Lily na Geo mbona lilinoga, Geo alimfanyia Lily mambo mengi ambayo Mumewe mpenzi Bwana Denis hajapata kumfanyia. Kumtoa Outing kula Dinner, kwenda Beach, kwenda Shopping, kumtembeza tembeza kwenye kumbi za raha na starehe, kumfanyia suprisment za mara kwa mara. Hayo ni baadhi ya mambo ambayo Denis hajawahi pata kumfanyia Lily, Lily akakolea naye, akazidiwa kwenye Pendo la huyu kijana aitwaye Geo.

“Safari hii Mtoto alianza kujilaumu kwanini aliolewa na Mwanaume asiyemjali?  Kwanini anaishi na Mwanaume asiyempa raha na starehe za Duniani? Ooh! Jamani dharau alianzisha, binti akawa anadai matumizi makubwa ya Pesa, na akinyimwa hana furaha, binti akawa mkali mwenye hasira kwa Mumewe. Mume arudipo makaripio ndio salamu kwake. Akamuona Mumewe kama bwege lisojitambua, hakukumbuka kwamba ndiye Mumewe aliyemtoa Kijijini, hakukumbuka kwamba ndiye Mumewe aliyemtafutia Kungwi ili amfunde kazi za nyumbani, matumizi ya zana zinazotumia Umeme nakadhalika. Alisahau kuwa sio yeye yule mwenye ngozi ya asili, nywele za asili na mwili wa asili.

Alichokumbuka sasa ni kuvaa mavazi ya bei gharama, kununua mawigi ya kila rangi, kujipodoa ili mtoto apodoke. Loh! Walisema wahenga Kuku mgeni asikose kamba mguuni, mwacha asili si mjasili. Matukano, malalamiko, mabezo na maneno mengine makali yalimtoka mdomoni, sijui ni nani alimfunda kuwa na mdomo mchafu? Au hao Shogaze? Mmmh! Tizama Mumewe akishindwa kumtimizia yale ayapendayo basi asitegemee kupata upendo wa Mke na mume.

Masikini Denisi alisumbuka, alitaabika na kuchanganyikiwa. Kama ni kumpenda Mkewe jamani alimpenda, alimpenda kuliko kitu chochote kile.

*********************

Basi wale Mashosti walipoona huko nyumbani kwao Lily moto unawaka, furaha iliwajaa wakaona sasa mambo yapo smart, Dawa ya Lily bado kidogo kuchemka, ameyataka yeye mwenyewe sasa wacha wamtengenezee, wamlipue kabla hajalipuka. Unajua walichofanya Mabeduni hawa? Unajua walichofanya hawa mabaradhuri, hujui eeh! Ndio hujui, basi wakamtengenezea Bomu, Lily alipuke na akiishalipuka ndio uwe mwisho wake.

Fumanizi halikugonga mwamba, si walishamtonya Mumewe Lily kwamba ‘Mkeo anachepuka’ tena anachepuka na kijana mdogo wa umri wake, ni kijana mdogo lakini kwa maujanja ni mtu mzima. Bomu lililotegwa likalipuka, fumanizi likazua Talaka tatu, tena Talaka kama tujuavyo hazimtaki mtu kurejea tena kwa Mtaliki wake.

Loh! Masikini Jamani kilio, majonzi na huzuni, Lily akawa hana pahali pakwenda zaidi ya kukimbilia kwa Geo, Geo naye akamtimua akamwambia hataki Mwanamke wa kuishi naye, anahitaji kuwa Singo boi. Geo kwa ubaya wake akahama Mji hata asijulikane ni wapi alikohamia. Lily akawakumbuka wale Mashostize Elizabeth, Lisa na Anjelina, kutwa kuchwa ikawa ni kuwatafuta hapa na pale Buguruni hata asiwapate, masikini. Majuto mjukuu, msaliti hujuta. Lily  akajuta na kuumia.

Siku sio nyingi alikuja kupata fununu ati huyo Shogaye mkubwa aitwaye Elizabeth, amewekwa kinyumba na Mumewe, mtoto anakula raha na starehe. Nyie! Masikini roho ilimuuma sana yule binti, kumbe porojo zote zile ni utapeli, ametapeliwa Mume, ameibiwa mchana kweupe, machozi na majuto yalimjaa Lily. Amekosea yeye mwenyewe, amekosea mara baada ya kuruhusu rafiki zake waingize machombezo yao, ajabu machombezo hayo yamefanya aachwe na kisha mwenziwe aingie ndani.

“Ushamba umemponza, alifundwa awe mvumilivu, alifundwa awe mstahimilivu, alifundwa awe na upendo kwa Mumewe, tizama marafiki wamemharibia, tizama marafiki wamempotosha, amelijisahau kama yeye tayari yupo ndani ya ndoa. Sasa amevuliwa nguo, amepokonywa tonge mdomoni , amedanganywa na hao waliodai ati wanaishi maisha bora wakati sio kweli ni waongo wapandikiza chuki, migogoro na uvunjifu wa ndoa za wengine.

Aliyachukulia yale maneno ya Mashosti kama  kweli tupu kumbe Bibie hakutafakari kwa kutumia elimu, pupa zimemponza, ameachwa na Mwanaume mwenye pesa zake, ameachwa na Mwanaume mwenye nia na malengo, Mwanaume mwenye muonekano(Handsome) Mume amekamilika, yaani kwa kifupi ni Mwanaume wa nguvu, sijui vijana wa kileo wangelimwita ‘Dume la Mbegu’, Ajabu alipotoshwa na kuingizwa Mjini, leo hana mbele, hana nyuma, maji yamemwagika hawezi kuyazoa, anajuta juto juu ya juto na majuto mjukuu, msaliti lazima atajuta tu.


Mwisho

KIGUU NA NJIA.. sehemu ya nne



 KIGUU NA NJIA

#

Nyumbani


MAMAYE AMINA: Eeh! Na hii barua nayo inahusu nini tena, au ndio umesamehewa na hao walimu wako? (Anaifungua barua mara baada ya kuweka vifuko vya karanga pembeni).

AMINA: Hata sijui inahusu nini, yanini kuandikia mate wino ukiwepo, hembu funua wewe mwenyewe nawe uridhie kilichoandikwa humo.

MAMAYE AMINA: (Anayakodolea macho yale maandishi). Mmh! Hembu muamshe babayo aje atusomee hii barua, mie mwenyewe sijui kusoma, nakodolea hii barua macho kama mwenda wazimu vile, ni heri na mwenzangu yeye amesoma soma hadi darasa la sita kuliko h mimi ambaye hata darasa la kwanza silijui vizuri.

AMINA: (Anamwamsha Babaye aliyelala usingizi wa fofofo kama samaki aina ya pono). Baba, Baba, Babaeeeh! (Anamtingisha). 

MZEE KIPUTA: Nini nawe mwana, usimwamshe aliyelala, ukimwamsha utalala wewe (Anaamka pale kwenye mkeka alolalia fofofo). Shida nini haswa. (Ananyanyua chupa ya matapu tapu na kuimiminia mdomoni mwake mafunda mawili matatu).

AMINA: Kuna barua kutoka Shuleni mama anakuomba uisome (Anamkabidhi ile Barua).

MZEE KIPUTA: Mimi mwenyewe nina matatizo ya macho siwezi kusoma vizuri. Tafadhali soma mwenyewe. (Anajitupa juu ya keka lake na kufunga macho yake).

AMINA: (Anaisoma ile barua aliyopewa Shuleni). Jamani baba na mama, Barua inasema kuwa nimefukuzwa Shule kwa sababu nina…”

MZEE KIPUTA: (Anagutuka). Nini? Umefukuzwa shule kwa sababu gani?

AMINA: (Analia na kushindwa kuisoma ile Barua, anakimbilia chumbani na anajifungia huko analia kilio cha Kwi! Kwi!

MAMAYE AMINA: Mtoto amefukuzwa shule kwa sababu ya ujauzito aliopewa na wanafunzi wenzake. (Anaongea kwa masikitiko).

MZEE KIPUTA: What!? Wala siwezi kuamini hayo maneno. Hiyo mimba ni nani amempatia na kwanini ameipata akiwa shuleni? Nakuuliza ewe mwanamke.

MAMAYE AMINA: Mume wangu, nitajibu nini mie daima nilijisemea moyoni mwangu kuwa Amina atakuja kutukomboa katika umasikini na ujinga, lakini jambo la kushangaza yaliyozuka ndio hayo  yanayoumiza mioyo na kutukatisha tamaa.

MZEE KIPUTA: Lawama zote nakutupia wewe mke wangu, wewe ndiye unayemharibu mtoto, kutwa kuchwa kumfanyisha kazi za kuuza ubuyu na karanga, anajikuta hana muda wa kujisomea zaidi ya kufanya biashara inayomkutanisah na wanaume waharibifu. (Anaongea kwa hasira).

MAMAYE AMINA: (Anaongea kwa hisia na uchungu) Usiseme hivyo mume wangu, kumbuka kuwa huyu ni mwanetu, na jukumu la kumlea kimaadili sio la kwangu mimi pekee bali ni la kwetu sote. Tulipaswa kukumbuka usemi wa wahenga waliposema, Samaki mkunje angali mbichi. Hata hivyo mume wangu na wewe umezidi haujali maendeleo ya mtoto kielimu, hautaki kusikia kama anaendelea vizuri, haujui kama anadaiwa ada, sare mpya za shule, michango mbali mbali ya shule, nauli, na hata pesa kidogo za kula shule. Vyote hivyo ninagharamia mimi, wewe kutwa kucha unashinda virabuni, kunywa na kupiga kelele za wendawazimu.

MZEE KIPUTA: Hilo halinihusu, ninachotazama ni kama mwanangu  anasoma na kufaulu  mitihani yake tu. Ajabu umemharibu mwanangu, na sasa utetezi wako unanitupia kombora ati sigharamii huduma zake..

MAMA AMINA: Usimlaumu dobi, kaniki ndio rangi yake, maji tayari yamemwagika, wala hayazoleki, hatujuii hatima ya mwenetu.

MZEE KIPUTA: (Anacharuka kama mvuta bangi). Nasema hivi muondoke haraka sana hapa nyumbani kwangu, siwezi nikawa nawalinda binadamu kumbe nawalinda mapaka na majibwa yasiyo na faida, mmenitia hasara isiyohesabika.

MAMAYE AMINA: Tuondoke twende wapi? Labda uondoke wewe na hiyo hasara ni wewe unayetutia hapa nyumbani, kutwa kuchwa kushinda virabuni na ukirudi unabweka kama Jimbwa ati nikuwekee chakula, unadhani chakula hicho kinaokotwa?! Kinatafutwa babu we! Elewa wajibu wako kama Baba katika familia, elewa unapaswa kufanya nini wewe kama kichwa cha familia.

MZEE KIPUTA: (Ananyanyuka ili kwenbda kukabiliana na mkewe). Nadhani umekwisha iamsha mizimu ya akili zangu. Sasa chokoza nyuki ulambe asali. (Wakati huo mamaye Amina anakimbilia ndani  alikojificha mwanaye).

****************

AMINA ANAMTEMBELEA ZEE LA PUTAPUTA.

Amina amekutana nna Zee la Putaputa pale pale wanapokutanaga siku zote. Amina hakumficha zee la PutaPuta, alimweleza kinagaubaga juu ya suala la yeye kugundulika kuwa na ujauzito na kufukuzwa shule lakini jambo la kushangaza zee la putaputa hakutaka kabisa kusikia kilio cha Amina.

ZEE LA PUTAPUTA: Huo ni uzembe wako wewe mwenyewe Amina, unajua kuwa wewe ni mwanafunzi tena mwanafunzi wa Sekondari, unaamua kujiingiza katika suala la mapenzi kwenye umri huu mdogo ulionao. (Anaendelea kumfokea) Na huo ujauzito sio wangu, kawapelekee hao hao wahuni wenzako, sio mimi. Sipendi kesi za kubambikiziwa, mimi ninayo familia yangu, nina mke na watoto wengi tu, isitoshe kunipakazia ujauziuto huo siwezi kukubaliana na wewe.

AMINA: Lakini Zee la PutaPuta wewe ndiye uliyenisonga twende kufanya zinaa huko kwenye magest na mahoteli, kumbuka wewe ndiye uliyenizoesha tabia hiyo.

ZEE LA PUTA PUTA: Nimekwambia nisingelipenda kuendelea kusikiliza kero zako, Mbwa wewe, na ukiendelea kunifuatilia nitatumia pesa zangu kukutia matatani. Kama sio kwenda jela basi ni ahera, Pusi wewe! Mbwa kabisa. (Zee la Putaputa, akawasha gari yake na kuondoka). Ndio ujue kuwa mimi ndio Zee la PutaPuta, sitaki  michezo ya kitoto na vitoto kama nyie, pesa kwangu zinaongea na kuogelea.

Amina alilia siku ile, alilia akijua kuwa yule mzee aliyemchezea mwili wake na kumuachia kidonda chenye hasara. Amina akajishauri  labda aende Buguruni kumwona Ben ampakazie ile kesi, kwa bahati nzuri, Ben siku ile alikuwa ameketi kwenye Geto lake, yeye pamoja na rafiki zake Kijiko na Kichungu wanapiga stori mbili tatu juu ya matatizo yaliyomkumba Bwana Ben.

KIJIKO: (Ameketi juu ya kitanda chake Ben). Hembu tustorishe mshikaji wetu,. Ilikuwaje hata ticha Mbigi akataka kukurostisha Skuli.

BEN: Mmmh! Kweli mapenzi na elimu ni sumu moja kali sana, tena sumu inayoua haraka sana, yaani wazee nilipoitwa pale Ofisini kwa Master nikasomewa shitaka la kumpa mimba Amina yule Demu aliyenipenda balaa.

KICHUNGU: Eeeh! Ikawaje? Ulikubali hilo shitaka au ulikataa? ( Kichungu ameketi kwenye kiti kilicho karibu karibu na meza ambayo Ben anaitumia kwa ajili ya kujisomea.

BEN: Ningekubalije ikiwa habari hizo ni mpya kwangu na tena ni za kushitukiza, ilibidi nikatae, hapo ndipo panga kali la maneno ya Headmaster lilianza kunirarua mwili wangu wote.

KIJIKO: Duh! Hatari.

BEN: Headmaster alinisema mbele ya Madam Grace, alinisema vibaya mno, alisema ati nimechoka kusoma ndio maana nimeona nijihusishe na mapenzi katika umri mdogo wa miaka kumi na minane, maneno…Maneno…Maneno… yalimtoka Headmaster, mwisho si aliafiki kuwa ni lazima nifukuzwe Shuleni.

KICHUNGU:Mbona hatari!

BEN: Nililia kama mtoto mdogo, nililia kweli. Nililia kama vile nimefiwa na mtu wangu wa karibu. Hatimaye nikapewa leta ya  kuwaita wazazi wangu waje skonga. (Ben alipumzika kunena).

BEN: Faza na Maza walikuja skuli,  wakasomewa shitaka langu, maongezi marefu yakashika Pahali pake, baba na mama walikesha wakiniombea msamaha ukitegemea imebaki miezi miwili tu ili nimalize kidato cha nne, hata hivyo roho ya mkuu wa shule ilikuwa ngumu kama jiwe. (Ben akaendelea kusimulia). Korapsheni  ndio iliyosovu tatizo lile, bila corruption  basi bandugu leo hii msingeliniona nikija skuli kuendelea na makamuzi.

KICHUNGU: Lakini hata hivyo tulikuambia unapotaka kugongana na yule demu ungelitumia Salama, Kwanini sasa haukufanya hivyo?

BEN: Duh! Unajua mwanangu nilikuwa new comer kitandani, Hivyo mambo yote nilimuachia yule Demu ayashughulikie,  hata suala la kukumbuka matumizi ya mpira wa salama nilikwisha yasahau kitambo.

KIJIKO: Huo ndio uzembe lakini ushukuru hongo limetumika, bila hongo leo hii hicho cheti cha form four ungelikisikia tu  midomoni mwa watu. (Mara walisikia mlango ukigongwa, alikuwa ni Amina, naye akakaribishwa, mara baada ya kukaribishwa, Ben aliwaomba Kijiko na Kichugnu wawapishe wapate kunena yao ya moyoni).

AMINA: Pole sana kwa yote yaliyokukuta mpenzi wangu. (Anamtizama Ben kwa masikitiko makubwa).

BEN: Pole nyingi zikuendee wewe mwenzangu, mimi mwenyewe nimenusurika kidogo tu mara baada ya wazazi wangu kutoa rushwa iliyoniwezesha kupita hivyo hivyo kwa taabu na mashaka. (Ben yungali mwenye sononeko na huzuniko).

...... Sorry karatasi  Moja ilipotea hapa๐Ÿ‘‡....

AMINA: (Analishika shika tumbo lake). Usiniche Ben, hata kama mie nimefukuzwa shule mpenzi bado ninakupenda, tena bado nakutegemea sana mpenzi, nipe nafasi niendelee kuwa wa kwako moyoni.

BEN: Lakini  nikuulize swali Amina, Hivi huo ujauzito wako ni mimi niliyekupa au una mwingine pembeni.

AMINA: (Anasita sita kulijibu lile swali lakini anaona heri nusu shari kuliko shari kamili). Kwanini uwe wa mwingine Ben wangu? Mie ndiye nitakayekuzalia mtoto mzuri, sijui atakuwa wa kike? Sijui atakuwa wa kiume? (Akawaza kimoyo moyo). Lakini nitashukuru mwenyezi Mungu kama huyu Mtoto atakuwa wa kike aliyechukulia kila kitu kutoka kwangu. Kikubwa ni kwamba soma sana  ili hapo baadaye tuje tumtunze mwanetu.

AMINA: Ben, niamini mpenzi, tazama baba amenifukuza nyumbani, sina pahali pa kwenda, hapa nilipo nimekuja kuomb hifadhi kwako, tafadhali Ben, please.

BEN: Sina neno, waweza kwenda popote pale unapoona panafaa kwenda. (Ben alijiandaa kutoka ndani ya chumba chake).

AMINA: Tafadhali Ben, Please Ben!!! (Amina alilia kilio cha Kwi! Kwi! Kwi!).


Mwisho


OMBI:  kurasa mbili zilipotea, Mola Jalia nitaandika tena.

KUKU WA KIZUNGU.. sehemu ya Saba.


 KUKU WA KIZUNGU

Sehemu ya Saba



BARUA KUTOKA ENGLAND.

Baada ya miaka Saba kupita


Ni siku nyingine tena, Miaka saba kipindi kirefu tangu Islama aondoke Maasai Land na kurudi ENGLAND, siku ya leo Balozi Ole ameketi  kwenye Kijumba nyasi chake, yupo yeye na wakeze wawili, wamemwandalia Nyama ya mbuzi aliye chomwa, kuna maziwa mengi ndani ya kibuyu kikubwa kama mkongojo wa tembo. Anakula na kunywa taratibu, siku hizi hana mawazo mengi kama kipindi kile English figure alivyomkondesha kwa kumpenda Laizer, kupungua kwa mawazo yake kumemfanya Balozi Ole anenepe  vizuri sana, Mvi juu ya kichwa chake zimeanza kumtamania. Mkewe mkubwa alikuwa akiwajibika kazi ya kujenga Nyumba yao. Balozi anataka awe na nyumba mpya pale Maasai Land, sababu ya wivu na kijicho chake kwa Laizer mwenye nyumba ya Bati na milango saafi ya mbao na chuma kisichoshika kutu wala kisicho liwa na mchwa. Anamwonea wivu Laizer sababu amependelewa, amejengewa nyumba bomba pale kijijini, amejengewa kwa pesa za English figure, amefanyiwa mazuri ya mengi kipindi kile. Ndo’ sababu Balozi ameona heri ajichange change kidogo haba na haba akauza mbuzi na ng’ombe wake wengi pale kijijini akanunua sementi, tofali na mabati ya kuekeza Kofia ya nyumba. Basi kazi ya kujenga ile nyumba akawaachia wakeze wawili wajenge kama mila za wamaasai zinavyowataka wanawake wajenge nyumba. Lakini leo mkewe mkubwa amechukua jukumu la kujenga akiwa pekee, mke mdogo ambaye bado ni kijana kijana anafanya kukamua maziwa ya ng’ombe na mbuzi akiisha kumaliza kazi hizo budi aende Kisimani kuteka maji au Porini kuokota kuni.

“Hodi hod hodi Mheshimiwa Balozi.” Ilikuuwa ni sauti ya YIARO Mtumi wake Balozi Ole, alitumwa aende Posta, Arusha mjini kuchukua Barua Za wanakijiji , kijiji cha Maasai Land. Leo amepokea Barua moja tu, siku zingine huja na barua tatu au tano, leo amekuja na Barua moja tu.

“Ingia Yiaro Mtumi wangu.” Yiaro aliingia Mkuki wake mkononi, sime yake kiunoni, vumbi miguuni kama ugolo wa kimaasai. Alimsabahi Balozi na baada ya Kumsabahi Yiaro  alinena.

“Leo Posta nimeikuta Barua moja tu, hii barua ni maalumu kwa Ole Laizer, Yiaro aliongea akitegemea Balozi angeli ichukua ile Barua aifungue  apate kusoma nini kiklichoandikwa ndani. Ndio kawaida ya Balozi siku zote Barua za wanakijiji zikiwasili uzifungua na kusoma soma nini kilichoandikwa ndani na kwa sababu Balozi ni Mbea tena ni Mwizi siku hizi, Barua za wanakijiji zikiwasili lazima aibe pesa kidogo zilizotumwa ndani ya hizo Barua, iwapo tu hizo Barua zimeambatanishwa na Fedha.

‘Mfyuuuuuuuu,’ Balozi aliachia mfyonyo wa nguvu, uliomshitua hadi Bi. mkubwa, mkewe wa kwanza aliyekuwa bize akichanganya changanya mchanga na sementi  ili aendelee kuijenga nyumba yao.

“Embu mpelekee mjinga huyo barua nyumbani kwake, sitaki hata kusikia habari za Laizer.” Balozi alinena mara baada ya kusikia kuwa ile ni barua ya Laizer adui yake.

“Balozi kwa hiyo leo hatuifungui Barua ya Laizer kama tunavyozifunguaga Barua za watu wengine, ili tuusome umbea ulioandikwa ndani.”

“Bull shit! Yiaro usitake nipandishe Mori sasa hivi, embu mpelekee Laizer mali yake, sipendi kabisa kusikia habari za Laizer.” Balozi aliongea Yiaro alitii amri ya mkubwa wake moyoni mwake Yiaro amesikitika sana sababu mfuko wa ile Barua ya kaki ulituna balaa, kama sio pesa zile basi ni vitu vya bei gharama.Yiaro aliondoka, Balozi maneno yanamtoka balaa, anamchukia na kumlaani adui yake.

“Miaka misaba iliyopita Laizer alikulaga kuku wa Kizungu pekee yake na ubaya wa yeye kumla Kuku wa kizungu amesababisha kuku wengine wasije hapa maasai Land, huu ni mkosi, tena huu mkosi ufagiliwe mbali.” Balozi aliongea maneno ambayo wakeze hawakumwelewa neno baada ya neno.

“Jamani oneni wazungu walikuwa wakimiminika hapa Maasai Land kama mvua ya gharika, ajabu kama maajabu miaka hii saba ya mkosi hajaonekana Mzungu au chotara wa kizungu hapa Maasi Land.” Balozi alikuwa ndani ya mawazo.

“Eeh!” Mara akashituka.

“Hivi ile Barua ya Laizer imetoka wapi? Mungu na Miungu ya Maasai Land nilisahau kumuuliza Yiaro, au nimkimbilie ili nijue ile Barua imetoka wapi?........ mmmh! Ngoja arudi.” Wasi wasi na shaka kidogo vilimwingia Balozi.

“We mume, kula nyama, kunywa maziwa hayo, acha kuongea vitu usivyovijua, ujue muda unakimbia, vikao vya wazee vinakungoja.” Bi. Mkubwa alimpigia kelele Balozi ambaye mawazo yalianza kumtinga na kumsumbua kichwani.

“Alafu mume wangu tabia uifanyayo siku hizi sio nzuri na tena haipendezi katika jamii.” Bi. Mkubwa aliacha kujenga nyumba  yao  akiwa amesimama hapo anapojenga aliongea.

“Tabia gani we mwanamke? Unaacha kufanya kazi zako unaingilia mambo ya wanaume, haipendezi katika Maasai Land.”

“Hata kama haipendezi katika Maasai Land mume wangu sio vizuri kufungua barua za wanakijiji, unavunja heshima zao unaharibu siri zao, unaiba pesa zao.”

“ Achana na mimi wewe, wewe ni mwanamke tu, hupaswi kujua siri za wanaume, mambo haya hayakuhusu, kwanza wajibu wako wewe ni kuzaa na kulea watoto tu.”

“Sababu hujaelimika ndio maana unanijibu hovyo, lakini ipo siku utakuja kulifungua Jini ndani ya hizo barua za wanakijiji.” Bi. Mkubwa alilalama. 

“Kweli kabisa, kweli usemalo Bi. Mkubwa.” Bi . Mdogo aliaacha kukamua ng’ombe maziwa akamuunga mkono  Bi. Mkubwa.

“Wanawake nyie mna nini ? mbona mna umoja wa kunishutumu, mimi ni kiongozi na kiongozi lazima ajue mienendo ya wanakijiji wake, je iwapo watu wabaya wamepanga njama ya kufanya ugaidi hapa Maasai Land? Itakuwaje sasa?”

“Ugaidi kwa kupitia barua.”Bi. mkubwa na Bi. Mmdogo walimjibu Balozi kwa pamoja. Balozi hakuendelea kuongea aliuchunia maana alitambua kuwa tayari ameaibika.      

          ##########

Itaendelea.

Saturday, September 21, 2024

CELIN DlON (ILOVE YOU) ๐Ÿ’ž

 

I MUST BE CRAZY NOW
MAYBE I DREAM TOO MUCH
BUT WHEN I THINK OF YOU
I LONG  FEEL YOUR TOUCH


TO WHISPER IN YOUR EAR
WORDS THAT ARE OLD AS TIME
WORDS ONLY YOU WOULD HEAR
IF ONL YOU WERE MINE.

I WISH I COULD GO BACK TO THE VERY FIRST DAY
SHOULD I HAVE MADE MY MOVE WHEN YOU LOOKED IN MY EYES
CAUSE BY NOW I KNOW THAT YOU WOULD FEEL THE WAY THAT I DO
AND I WHISPER THESE WORDS AS YOU WOULD LIE HERE BY MY SIDE

I LOVE YOU PLEASE SAYS
YOU LOVES ME TOO, THESE THREE WORDS
THEY COULD CHANGE OUR LIVES FOREVER
AND I PROMISE YOU THAT WE WILL ALWAYS BE TOGETHER
TILL THE END OF TIME

SO TODAY I FINALY FIND THE COURAGES DEEP INSIDE
JUST TO WALKS RIGHT UP TO YOUR DOOR
BUT MY BODY CANT MOVE WHEN I FINALY GET TO IT
JUST LIKE A THOUSAND TIME BEFORE

THEN WITHOUT A WORD YOU HANDED ME THIS LETTER
READ I HOPE IT FIND THE WAYS INTO YOUR HEART
IT SAYS

I LOVE YOU
PLEASE SAYS YOU LOVE ME TOO, THESE THREE WORDS
THEY COULD CHANGES OUR LIVE FOREVER
AND I PROMISE YOU THAT WE WILL ALWAYS BE TOGETHER
TILL THE END OF TIME

WELL MAYBE I, NEED A LITTLE LOVE YEAH 
AND MAYBE I NEED A LITTLE CARE 
AND MAY BE I, MAY BE YOU , MAYBE YOU, MAY BE  YOU,
OH, YOU NEED SOME BODY JUST TO HOLD YOU,
IF YOU DO, I JUST REACH OUT AND I WILL BE THERE

I LOVE YOU PLEASE SAY
YOU LOVE ME TOO
TILL THE END OF TIME
THESE THREE WORDS
THEY COULD CHANGES OUR LIVE FOREVER
AND I PROMISE YOU THAT WE WILL ALWAYS BE TOGETHER

Oh, l love you
Please say you love me too
Please, please say you love me too
Till the end of time
My baby
TOGETHER TOGETHER FOREVER 
TILL THE END OF TIME 
I LOVE YOU
I WILL BE YOUR RIGHT
SHINING BRIGHT
SHINING THROUGH YOUR EYES
MY BABY

I promise you

   I PROMISE YOU. (NINAKUAHIDI.) SURA  YA KWANZA. UBAYA WA POMBE. “Umenizingua job, umenizingua kwa muda mrefu sana mpenzi wangu…….kwanini l...