DONT TRY TO MESS WITH SINGLE MAMA.
Miaka miwili iliyopita mie Belinda nilitengana na James Mume wangu wa ndoa niliomba talaka kinguvu maana hakuwa tayari kutengana na mimi. Sababu kuu ya kutengana na James mwanaume awezaye kuniridhisha kitandani (Nilimpendea sana kwenye tendo.) alikua ni mlevi na mvivu, mlevi yaani mlevi nyoko akiaanza kunywa pombe asubuhi na kumaliza atamalizia jioni, ukimuona huwezi kumtambua kama ni yeye maana ujigaragaza topeni sio kwa aibu na fedhea ile.
Alikua ni mvivu hataki kufanya kazi yoyote ile, mwanaume kutwa kuchwa alijifungia chumbani akikiroma 'ngrooo ngrooo ngruuu' ๐ด๐ชkwake usingizi ulikuwa kama chakula na aliupenda sana usingizi kuliko Binti zake wawili wadogo Jena na Mariamu. Mwanaume alifanya kazi ya kulala tu, pesa ya chakula hakumbuki ni lini mwisho aliitoa zaidi ya kuitoa mie mwanamke. Haya Sasa ninaitoa kutoka wapi!? Shuhuli na vibarua vidogo vidogo nilivyojishuhulisha.
Ila ni jambo la kumshukuru Labuka maana baada ya James kufukuzwa kwangu akapunguza sana ile tabia yake ya kunywa pombe akapunguza ulevi nyoko akajikita kazini angarau apate pesa ya kula, ubaya wake hakuleta pesa za matumizi ya watoto nyumbani. Basi mwanamke nikapata akili ya kujbidisha Mimi mwenyewe kufanya vibarua vidogo vidogo vilivyonipa vijisenti vya kuwanunulia watoto mahitaji yao ya kila siku.
Mara Leo niitwe kulima au kupalilia shamba, mara niitwe kupika au kusafisha vyombo maharusini na kwenye shuhuli mbalimbali, siku zingine nilipigwa Simu na mabosi wakubwa nikasafishe Ofisi, nyumba au kuwafulia nguo lukuki. Belinda mie nilikua kiguu na njia ilimradi nipate tonge la ugali na jinsi watoto wanavyosumbua, du! Kuwa Singo Mama yataka moyo.
"Mama Leo twaweza kwenda Kigamboni Beach."Jesu! Huko Kigamboni Beach kwani mtu anaingia Bure!? Mwendo wa pesa, tulienda angarau Beach za Bure.
"Mama Leo pika Pizza na Baga." Toba! Watoto Hawa wanalilia vinono na vitamu. Lakini singo mama mie nilijitahidi kufanya watakacho.
**********
Basi mie Singo Mama nilikua najiandaa kutoka nyumbani kwangu, October ya tarehe kumi nilipigwa Simu na kibosile fulani huko Gogolamboto kwenye birthday ya mwanaye. Mie nikapike na kupakua mahanjumanti, manono na manonozi. Tajiri aliniahidi kitita cha shilingi laki Moja kama malipo ya shuhuli nzima ya kupika na kupakua.
"Belinda Jirani wa mie." Sauti ya mwanamama iliniita niligeuka na kuacha kutembea mtaa wetu wa Segerea
"Abee dada" Nilimwitikia MAISHA, Maisha ni Jirani wangu mgeni na mpya katika mtaa wetu amehamia hapo yapata miezi SITA iliyopita na tushamzoea. MAisha kama watu wengi wanavyomwita MASHA P. DIDY (nicheke mie๐คฃ๐คฃ๐) nisijue hilo jina wenyewe wamelizoa wapi? Anapenda starehe kila siku, kila wiki, na kila mwisho wa mwezi. Kwenye nyumba aliyohamia utasikia mapigiti ya Muziki mnene wenye sauti ya juu. Huyo Masha anafanya sherehe za kula na kunywa kila mara ndani ya mtaa wetu wa Segerea
"Nakuona una haraka Dear Kuna jambo naomba tuongee" Mh! Niliguna nikasimama nimsikilize au anataka kunialika kwenye hizo party za kula kunywa na kumwaga pesa.
"Sina haraka Dear Nashukuru kama Kuna jambo nono unahitaji kuniambia." Nilijishebedua hamu na shauku ya kujua.
"Dear, Nyumba yangu ipo chafuu chafukoge haitamaniki. Jana tumethrew part la nguvu, watu wamekula, kunywa na kufanya vurugu"Aliongea huyu Jirani ambaye nimesikia tetesi zake watu wengi wananiambia: 'Shuhuli yake ni kuomba omba misaada kwenye mashirika ya Dunia akisingizia ati anaipeleka hiyo misaada kwenye vituo vya watoto Yatima na wale wanaoishi kwenye mazingira magumu.' Teh teh teh๐ค๐น nacheka kama mazuri. Sijui hao wanaokula, kunywa na kufanya vurugu ndio Yatima na watoto wanaoishia kwenye mazingira magumu? Mh! I don't know,
"Ndio Dear hapa umefika lazima nikusikilize" nilisimama kumsikiliza.
"Naomba Leo uachane na shuhuli yoyote uliyonayo ninahitaji mtu wa kunifanyia usafi nyumbani kwangu nipo tayari kukupa shilingi laki tano mara baada ya kazi kukamilika' Kabla sijakubali au kulikataa Lile donge nono Masha alichomoa funguo za nyumba yake anayoangushia Party kila wiki.
"Oh! Dear kwanini tusifanye kesho maana Leo nina shuhuli ambayo sipaswi kuikosa." Niliongea lakini moyoni nikizitamani zile laki tano mashallah!
"Jirani, nyumba yangu itaoza na kuharibika ukitegemea siku mbili zijazo ninategemea kuwapokea wageni kutoka Ulaya Kuna mambo fulani ya Documentary nahitajika kujaza na kuita Saini yangu"MASHA P. DIDY alinibembeleza.
"Ok Haina tabu nipo tayari kukusaidia.Vipi kuhusu malipo, ingekuwa vizuri uniachie Advance"
"Usijali wewe fanya usafi Kwa siku mbili tu Kisha suala la malipo nitakupatia ukimaliza kuwajibika. Uzuri ni kwamba ndani ya siku hizi mbili sintakuwepo nyumbani basi fanya kuitawala nyumba yangu iwe kama yako." Aliniambia nikapokea funguo ya nyumba yake na kuahirisha Safari yangu yenye faida kiduchu nikakimbilia ile yenye donge nono.
*******
Mmh! Mazingira niliyokutana nayo ndani ya nyumba ya Masha P DIDY Mama ya starehe mbona niliyaogopa Tena ninaogopa hata kusimulia kila sehemu ya ile nyumba ilikua chafu tena chafu zaidi ya chafu. Sebule nzuri ilibadirika na kuwa pambo la mabakuri machafu. Mabirauli machafu, makopo na chupa zilizotumika usiku wa Jan. Vyakula vilimwagwa kila Kona ya ile nyumba kuanzia kwenye Masofa, kutani jikoni huwezi kuamini hata ndani ya choo kulitisha Kwa matapiko na vinyesi vya hao watu waliokuwa wakafanya starehe ambazo hata sikuzijua zaidi ya furaha ya kula pesa za Mashirika, Makampuni na Wadhamini,
Pombe pamoja na mabaki ya chupa za pombe zilinitibua. Nilijiuliza naanzia wapi kufanya usafi? Tisa kumi sikufahamu zaidi ya ya kufagia sebule iliyoharibiwa Kwa chupa zenye kilevi, nilipomaliza kuishuhulikia ile sebule nikaanza kukusnya vyombo na mabaki ya vyakula kisha nikaanza kuvikosha vyombo vingi sana, yamkini watu Mia walifanya Party ndani ya lile lijumba likubwa. Sikuchoka tu bado nilifahamu Kuna kukosha masofa, vitanda, mashuka n mablanket mazito. Kazi ile nzito ilinichukua zaidi ya siku mbili kuimaliza
ilikua ni kazi nzito kidogo nilipoa baada ya kubeba manyaji na vyakula ambayo havikuharibika nikawapelekea wanangu. Baada ya siku mbili za kazi mwenye mali alirejea kimya kma MAJI mtungini, hakunitafuta wala hakutuma mtu aje aniite sembuse anifate. Kwa ustaarabu wa kudai CHANGU nikamwendea Ili kumkumbusha kuwa ahadi ni deni na deni lazima lilipwe.
"Nini?" Unanidai shilingi laki tano Kwa kazi Gani haswa?" Eh! Masha huyu vipi!?" Maswali Gani Tena haya au ametumia dawa za kulevya zilizompu,mbaza?
"MAISHA au umelisahahu donge nono uliloniahidi kunipa baada ya shuhuli hii nzito inayochosha na kuumiza mikono, mgongo na mwili wangu? Kumbuka ndani ya siku mbili hizi mie nimekosa usingizi" Nilimkumbusha
"Belinda wewe ni mtu mzima Tena mwenye akili na kumbukumbu, nilipokuja kwako nilikuja kuomba unisaidie kufanya ile shuhuli 'FREE' bila malipo. Sasa ilo donge nono la shilingi laki tano umelitoa wapi?" Makubwa! Masha huyu huyu aliyenibembeleza nimfanyie usafi Leo hii anakuja kuniambia aliniomba nimfanyie ile kazi free huo muda wa kumifanyia kazi free nitautoa wapi mie Singo mama ninaye waangaikia wanangu waupate ugali na tembele?
"MAISHA naomba usijitoe akili na ufahamu yaani ile kazi nzito ya kuchomwa na chupa zilizovunjika, kuzoa matapiko na makombo ya walaji, kusafisha vinyesi vilivyotapakaa hadi jikoni utafikiri wanyao hivyo vinyesi ni Kuku na nguruwe. Nimekuoshea Masofa yote, Mablanketi, Mashuka, Vitanda yaani hadi kuisugua Dari ya nyumba yako Leo hii unakuja na Motion inayoitwa FREE ." Nililalamika,`
MWANAMKE UNAPASWA KUWA NA HURUMA JUU YA MWANAMKE MWENZIO ANAYEJITOA KUKUSAIDIA. NImeumia sana Masha, kichwa changu kilichoka kujitwika maji ya kisimani, hadi Leo hii bado ninaumwa kichwa na mgongo alafu wewe unakuja na Mada inayoitwa Free,"Huruma hizo siziwezi. Niliongea
"Bwana we fanya mambo yako, embu nipishe nipite na uniachie niende." Masha aliingia ndani ya Gari yake Kisha akaikoki na kuondoka kwa Kasi huku nyuma akiacha sauti kubwa ya kiicheko chake . Teh teh teh ๐น๐น๐น. Nilifura Kwa hasira. nikaona hizi sasa hii ni dharau na dhuruma. Singo mama mie sipaswi kucheka na Binti ambaye anapaswa kuniita Dada. Je, alipanga dhuruma hizi tangu awali? Je, ndio mchezo wake mchezo wa dhuruma? Ndivyo anavyowafanyia hao Wadhamini wenye Mashirika na Makampuni anayoomba misaada ya kuwasaidia watoto yatima na wale wanoishi katika mazingira magumu? Kwa hiyo hayo mazingira magumu ndo' yale ya kurusha part za kunywa na kula kisha kuchafua nyumba? Hapana, kama ni kumharibia issue zake sipo tayari lakini ngoja Sasa ngoja tuone nitakavyomfanyia kitu kibaya. Atanikoma na kunikumbuka, atakumbuka neno Moja la kizungu "DONT MESS WITH SINGO MAMA"
"Yes!" Nilitabasamu.
"Si funguo za nyumba yake kaniachia! Ah! No kazisahahu. Nilipata akili ya kuzaliwa.
"Haya tuone Sasa si yeye SINGO Dada, tapeli mpenda starehe na Mimi ni ni SINGO mama mpambanaji na mpenda haki. Nilitamani kufanya sherehe hata kabla sijatimiza biashara yangu.
Nikafanya hima kwenda Sokoni kununua Viroba karibia kumi na Tano Kisha nikakodisha Gutta baada ya kupata vitu hivi muhimu kwangu nikakimbilia Dampo la Tabatha huko nikaanza kuchimba na kuchimbua kila aina ya taka taka, uchafu na ujinga.
Maganda ya ndizi zilizooza, maparachichi yaliyooza, maembe yaliyooza. Pedi zenye vinyesi vya watoto. Mifuko iliyooza na ile yenye vyakula vilivyooza tena Uzuri hata zile chupa na sahani zilizovunjika nilizoziondoa nyumbani kwake bado zilikuwepo Jalalani. Sikusahau vinyesi vya wanyama pusi na umbwa ng'ombe na nguruwe. Usiniulize nilivitoa wapi maana SINGO mama mpambanaji ninalijua vizuri Jiji na vijiji.
Kwisha kukamilisha zoezi la zoa zoa nilihakikisha ninapita NJIA ambayo hakuna mtu angeliniona. Napita vinjia na vichochoro vya kuelekea nyumbani Kwa MAISHA. Nilipofika nyumbani Kwa MAISHA nilianza kazi ya kurenew kile kilichopotea. Teh teh teh๐คฃ๐คฃUfunguo nilikua nao basi nikajifungia ndani Mimi na Viroba vyangu na magunia mazito yenye uchafu, kilichofuatia sidhani kama kuna haja ya kusimulia.
Nilipakaza vinyesi vya wanyama kila chombo kilicho kabatini mwake, nilipakaza vinyesi vya wanyama Jiko lake lote. Kuta za Jiko na Kuta za choo chake cha ndani nilipakaza matunda yaliyooza na kutoa wadudu Nilipakaza mashuka yake yote meupe pee. Nilipakaza kwenye masofa, mapazia vitambaa hata juu ya Dari. Sikuchoka bado tu nilisambaza yale mabakuri na shahani chafu juu ya meza yake. Pedi za watoto, chupa na takataka kibao nilisambaza sakafuni kwake. Nyumba yake ilitisha mfano wa HALF HELL nusu Jahanamu. Kwisha kumalizia ile shuhuli nikaufunga mlango mkuu wa kuingilia SEBULENI, Ufunguo nikaupachika chini ya kapeti dogo la kuingilia ndani likiwa limeandikwa Wellcome Guest.
Ingawaje mtimani niliumia kumfanyia Jirani yangu UBAYA UBWELA lakini nilipaswa kujipongeza sababu yeye binafsi amenidharau. Mie huyo nikarejea nyumbani kwangu kukoga na kuwapikia wanangu vinono nilivyobeba kutoka Kwa Tapeli wangu MASHA P DIDY. Vilikua vinono kweli, Kuku wawili wakuba, debe moja la mpunga, lita tano za mafuta bila kuhesabia unga na spices mbalimbali za mboga
**********
'Ngo ngo ngo' Wanangu walishituka na mie pia nilishituka
"Belinda tafadhali naomba Ufungue mlango" Sauti ya MAISHA iiliunguruma Kwa hasira NILIENDA KUUFUNGUA MLANGO WANGU.
"Gonga Kwa ustaarabu tafadhali. Hii ni nyumba yangu Wala sio choo"Nilimkaripia MAISHA ambaye alitibuka akafura Kwa hasira hasara, hasira za mbogo alojeruhiwa.
" Ndio Nini ulichonifanyia Belinda?" Aliniuliza
"Kwamba nimekufanyie Nini?"Nilirudisha swali.
"Ina maana huelewi jinsi gani umenichafulia nyumba yangu na kuniharibia"Alinipigia kelele.
"Una uhakika kwamba ni Mimi ndiye niliyekuchafulia nyumba yako?"Nilimtupia swali.
"Kwanini nisiwe na uhakika ikiwa wewe ndiye uliyenifanyia usafi na wewe ndiye ulierejesha uchafu ndani" Aliongea mate na povu likimtoka mdomoni. Mie sikutetereka nilimjibu na kumuuliza kadri alivyoniuliza,
"Tafadhali naomba uondoke nyumbani kwangu mambo ya hisi na hisia za kufikirika siziamini wala sizikaribishi nyumbani kwangu" Nilimtaka asepe.
"Belinda I will call Police, nitaita police"
"Ita Bibi ita hata Sasa chukua simu yangu ita" Nilimpa simu yangu.
"Ita Tena waambie Belinda amenihujumu. Wakikuuliza aliingiaje nyumbani kwako utajua jinsi ya kuwajibu maana mie hata Ufunguo wa Nyumba yako sina tena siujui "Niliongea maneno yaliyomfanya MAISHA aondoke Kwa hasira.
Teh teh teh ๐คฃ ๐คฃ ๐คฃ ๐ Sikuogopa wala sikutishika. Unadhani hao POLISI waliitwa? Waitwe wapi? MAISHA alipata funzo. Siku ile nililala salama salimini mie na wanangu. Nina Imani hawezi tena kuja kuniita nimfanyie kazi Free ya bure bin utapeli.
************
DONT MESS WITH SINGO MAMA WEWE ๐ซ
..................
TCHAO