OBIMO CHETA
MY LOVE REMEMBER 💕
Tulipoishia
Nisamehe Derila.”Singa alilia akipita pita ndani ya kiijiji chao, kijiji cha Maasai Land,wanajamii wakiendelea na shughuli zao za kijamii, wanawake walionekana wakijenga nyumba, wengine waskikamua maziwa, vijana wadogo wakirejesha mifugo nyumbani kutoka malishoni, wakati wazee wakiketi vikundini wakijadiliana.
***************
Sehemu ya Sita
“Ondoka tu, ondoka kama unavyotaka Mwanaharamu wewe.”Babaye Singa aliongea, ni mwenye hasira, anachukia kwa sababu ya umasikini, anamchukia mwanaye, anamuona msaliti.
“Nenda huko huko unakokuita mjini umeshindwa kuniletea mifugo nyumbani unaniletea majonzi na masikitiko.” Baba aliongea kwa haasira.
“Nitarudi na utajiri safari hii Baba yangu, wala hautalala njaa tena, hautalalamika wala hautanisema kwa ubaya.”Singa akiwa tayari anaondoka kuelekea Arusha mjini.
“Nenda zako mwanaharamu wewe, hufai kitu, wewe ni zigo ndani ya nyumba hii, wenzio wanawaletea faida wazazi wao, wewe unaleta hasara kutoka mjini.” Baba alipiga kelele, Singa hakuwa mtu wa furaha tangu aingie kijijini amekuwa ni mtu wa huzuni, maneno na masimango. Leo hii amebeba kibuyu cha maziwa pamoja na mapande ya nyama ambayo mamaye amemuandalia, anaondoka na kupanda basi la kijiji, basi kuukuuu, japo lina mwendo wa kufika pale Arusha mjini.
~~~~~~~~~~
Singa alikuwa akipeleleza huku na kule akimtafuta mpenzi wake wa zamani Derila apate kumpigia magoti amwombe msamaha, Jua linachomoza, Jua linazama, Singa hajapata kumwona yule amtafutaye, mvua nayo inamsulubu, inamnyima raha na furaha ya kumwona yule amtakaye, siku ya tatu leo anapeleleza peleleza kati kati ya jiji, juu ya pahali anapoishi Derila huyu mwana mama mwenye sauti iliyowateka Watanzania, Wakenya na Waganda, Warwanda na Waburundi, hapati kujua pahali walipo.
Lakini ghafla Singa analiona tangazo, tangazo limebandikwa ukutani nalo linasema:
“Mwanamama mwenye sauti tamu ya kuvutia wengi atakuwepo akitumbuiza Makumira tarehe 25/4/2024..” Waoooh! Singa alirukaruka na kukiondoa kile kibandiko/tangazo, akaibusu ile picha ya mwanamama aliyerembwa akarembeka, Derila ndio jina lake.
***********************************
“Rejea tena, rejea mpenzi,
Rejea, rejea, rejea,
Nayakataa mapenzi yote,
Nawakataa wapenzi wote,
Kwako wewe narejea.
Nipokee, nipokee, nipekee,
Nipokee mpenzi wangu,
Bado ningali ninakupenda.”
Ilikuwa nio sauti tamu ya mwanamama Derila, maelfu ya wale wote waliohudhuria tamasha lile waliburudika, walimpongeza na kumsifu Derila. Walimpigia makofi na kufurahi pamoja naye. Moe-Joe alijivunia kumtoa huyu mrembo ilikuwa ni neema kwake, anapata pesa nyingi zinazotoka kwenye mgongo wa Derila, Derila pia hana shaka, mialiko na matamasha ni mengi, anavuna alichostahili kuvuna, Uche ni mwenye furaha na uzuri wa muziki anaoimba Derila, umefanya apatane na wazazi wake Baba na Mama yake wale waliomfukuza na kumtupilia mbali leo hii wamemsifu na kumwongelea kwa marefu na mapana.
++++++++++++++
Derila akiwa jukwaani anaimba wimbo wake asloupa jina la “Rejetena.” Mara ile alimwona mwanaume kijana amevalia mavazi ya utamaduni wa Kimaasai, ana sime kiunoni, amesuka rasta za Kimaasai, ana shanga nyingi na vito vingi vya Kimaasai miguuni, mikononi na shingoni mwake. Derila alimtambua, sio mgeni machoni kwake, anamjua vizuri sana mtu huyo anayepita katikati ya kundi la watu ili apate kufika pale alipo Derila, Moyo wa Derila ulikuwa ukienda kasi mara ile yule mtu alivyokuwa akija, ni mweusi wa rangi, meno yake ni meupe peee, ana urefu na wembamba wa mwili.
Derila alitamani kuacha kuimba Ili apate kumkimbilia, uvumilivu ulimshinda mara ile alipomwona Singa akija kwa kasi juu ya ule ukumbi, akafurahi sana Derila, furaha iliyoendana na mapigo ya moyo wake, Walinzi waliojiweka tayari kumlinda Derila hawakutaka Singa amsogelee Derila, walidhani anaweza kumletea fujo na kumdhuru, hivyo wakamwamuru kinguvu arejee pale alipotoka.
Derila kuona Singa wake anasumbuliwa, hakufanya ajizi, aliacha kuimba na kumkimbilia yule ampendaye. Oooh! Akamrukia na kumkumbatia, wawili wale walishikana kinguvu, wakitizamana na kulia kama wendawazimu, umati wela watu uliohudhuria burudani ile uliwatizama kwa hisia nyingi sna.
“Nisamehe My Love.” Singa alilia na kuomba radhi.
“Nilikwisha kusamehe siku nyingi mpenzi wangu, bado nakupenda.”Derila alilia, watu walizidi kushangaa.
“Nimekukosea mpenzi.”
“Wala usijari Singa wangu, yaliyopita wacha yapite, sie tuendelee na safari yetu ya kutafuta maisha.”Derila alimbusu Singa kwenye mashavu yake, Derila kwa ule wingi wa Furaha alishindwa kuendelea kuimba, akaondoka pamoja na mpenzi wake wa zamani Singa, watu walifurahi na kuwapigia makofi wale wawili waliopendana, Singa na Derila, wakapanda gari moja nzuri ya fahari ambayo Derila alinunuliwa kama zawadi kutoka kwa produce wake Moe-Joe.
Walihitaji kwenda kwenye nyumba anayoimiliki Derila, amejenga Derila, amejenga maeneo ya Majengo na uzuri wa siku ile Derila alipigiwa simu akiambiwa kwamba Uche mwanaye mpendwa amerejea kutoka kwa Bibi na Babu yake huko Usa River. Derila alifurahi, alifurahi furaha ya kutaka mpenzi wake wa zamani amuone mtoto jinsi wanavyorandana, wanafanana sana, hakuna mfano.
Simulizi hii ya kusisimua inaishia hapa, inaishia pale tulipomwona Derila alivyokuwa na moyo wa msamaha, ajabu mapenzi yake ana machozi ya karibu, ana msamaha na huruma, ana moyo wenye upendo mkuu, alikubali shida zote, tabu na mateso, alikubali kuitwa ombaomba, alipojikita kwenye muziki, akajibidisha, akatoboa na kubomoa, akawa juu, hata pale mafanikio yake yalipozidi kuongezeka Singa akajitokeza na kumpatia msamaha, furaha yao ikaongezeka, raha yao ikarudi tena, tayari wamesameheana, Derila anampenda sana Singa, na uzuri wa Derila hachoki kumpatia pesa mingi huyo mpenzi wake wa moyo wake aitwaye Singa, anampenda sana, pesa anazompatia Singa huzitumia vizuri, Singa huwapelekea Baba na Mama yake waliochekwa kwa umasikini, tizama sasa wamefurahia utajiri unaokuja wasijueni wapi unapotokea.
MWISHO
No comments:
Post a Comment