Tuesday, July 8, 2025

I PROMISE YOU.

I PROMISE YOU 

(NINAKUAHIDI)

Sehemu ya  Nne.

SAFARI YA SOUTH.

Ndege ya British Air wings ilitua ndani ya uwanja mkubwa wa kimataifa ndani ya jiji la Pretoria Afrika ya kusini, nilikuwa tayari kuteremka ndani ya kile kiwanja, ilikuwa ni mara ya kwanza mie kupanda ndege. Bosi wangu Steven Biko aliniambia kwamba nikiisha kanyaga mguu wangu ndani ya uwanja wa ndege, angelikuja mzungu mmoja mwenye jina la Dos santos, huyu aliwekwa maalumu kunipokea ndani ya uwanja mkubwa wa kimataifa.
                Lakini ajabu hadi zinatimia dakika 45 nikiwa ningali ndani ya kiwanja cha ndege sikuweza kumtia machoni mwangu huyu jamaa ambaye tayari picha yake nalikuwa nayo mikononi mwangu. Nilitegemea kama angeliniona  au mie ningelimuona basi safari yetu ingelipamba moto. Nilianza kuingiwa na wasi wasi, hofu ilinipamba usoni na ushamba  wote ule mbona sikuwa na amani.
              Nalimpigia simu bosi wangu, ili nipate kujua kwanini mwenyeji wangu  hapatikani, ajabu iliyoje hadi linatimia li saa limoja bosi hakupokea simu, simu yangu iliita iliita iliita iliita lakini hata hivyo haikupokelewa, hofu ilinimeza na kunitia wasi wasi juu ya usalama wangu.
              “Hallow can you follow my step?” Ilikua ni sauti ya mtu mwenye lafudhi ya kizungu , sauti hiyo ilipita masikioni mwangu, wakati huo huo nimetetemeshwa mwili wangu kiwa kuguswa bega la upande wa mashoto na huyu mtu  aliye nyuma ya mgongo wangu.
              “Yes I can do so.’ Nilimjibu yule Mzungu ambaye mara baada ya kuigeuza sura yangu, nilikuja kugundua kumbe hakuwa bwana Dos Santosi aliyewekwa maalumu kuja kunipokea ndani ya kiwanja kile cha kimatifa. Mikononi mwangu Brief ase  ilitulia tuli isipate kuyumba yumba au kutikisika kwa sababu ndani ya ile brief case kulikua na vitu nilivyopaswa kuvileta  South Africa.
                  “But Sir where are you taking me to?” Nilimuuliza yule mzungu ambaye nilimfuata kama alivyo nielekeza nimfuate.
                 “Don’t worry, you are going to know every thing after we reach out there.”  Aliongea yule bwana mweupe, mie nikiwa sijui ae wala bae nilimfuata yule Bwana mweupe kama  Umbwa amfuataye bwana wake,    nilijivuta vuta kama Ng’ombe apelekwaye machinjioni. Japo ndani ya moyo, hofu na wasi wasi vilimiminika.
                #############################
                   Looh! Yaliyonikuta hayafai kuadithia, yaliyonikuta ni mazito ya dunia, wacha nifupishe kwa kusema huu ni mwaka wangu wa tatu bado nipo ndani ya Gereza la Pretoria  kama sio mapenzi ya mungu, haki leo hii mie ningelikuwa mfu na mgonjwa wa majanaba yaliyo ndani ya hilo Gereza la Pretoria. Nina haki ya kusema asante sana bwana yesu, asante mungu maana juma tatu ya leo safari yangu, safari ya kurejea nyumbani Tanzania imewadia. Nimekitumikia kifungo cha miaka mitatu ndani ya gereza la pretoria mara bada ya mie kukutwa na hatia ya kuingi Afrika ya kusini nikiwa na dawa za kulevya.
               Mwe! Jamani mwe! Kama sio Mungu leo mie ningelikuwa tayari maiti, sababu msongo wa mawazo niliokuwa nao haukuwa msongo wa kawaida, jera kubaya,  jera ni kama kuzimu, jera ni jahanamu ya kutisha. Masikini mie Job? Kwanini nilifanya pupa? Kwanini sikuyakumbuka maneno ya wahenga pale waliponena fikiria kabla ya kutenda, haraka haraka haina Baraka, tamaa ni hasara.           
 Mwe! Masikini machozi yananibubujika, ninalia kama mtoto mdogo, ninalia nikiwa ndani ya treni linalonirejesha nyumbani Tanzania, treni ile inapita Zambia kisha inakomea mkoa wa Mbeya, nikaichukua gari iliyonipeleka Iringa nyumbani, moja kwa moja hadi nyumbani kwa bibi na babu yangu.
                Sijui  nianzeje kusimulia, sijui  nianzie wapi kueleza juu ya mkosi  ulionipata pindi nikiwa Pretoria, pindi ile nimepokewa na yule mtu mweupe. Labda niseme kwa ufupi Steven Biko alinishika sharubu, alinitaiti, alinipiga chenga, alinizidi kete pasina mimi kujua ule ulikuwa ni mpango wake, mpango wa kunihujumu mke wangu mtarajiwa. Sikujua na tena sikujua kuhusu suala hilo, jambo nisilolijua limenisumbua, jambo nisilolijua kama usiku wa giza nene, jambo nisilolijua limenichoma na kuniumiza.
                  Leo hii mara bada ya mimi kufika Iringa, nilipatiwa fununu mbaya, tena mbaya zaidi, waswahili wanasema chelewa chelewa mwana sio wako, ndio hivyo tena sio kwamba nimechelewa pekee bali nimekwisha ibiwa mke wangu mtarajiwa na yule aliyeniibia  si mwingine zaidi ya bosi na rafiki yangu mkubwa Bwana Steven Biko. (Adui yangu rafiki yangu)
                 Sijui alimshawishi namna gani mpenzi wangu Brenda, ushawishi wake ndio uliopelekea Brenda aingie mkenge, akayavulia maji nguo naye akayaoga, yamemwgika hayazoleki, nimeachwa mpweke kama mti ulioota jangwani tena mti huo umeota kwa bahati mbaya, nimeachwa mpweke kama kinda aliyetelekezwa na mamaye.
                Biko Keisha nizidi kete, Biko Keisha muweka ndani yule niliyempenda sana maishani mwangu, Biko Keisha mlainisha Brenda wangu kwa maneno matamu kuliko nyama ya ulimi, matamu kuliko asali na uzuri wa hayo maneno Biko ni mtekelezaji wa haraka haraka hitaji la yule aliye mikononi mwake. Hapo ndipo Brenda aliingia kingi, kwanini akatae, ukitegemea baada ya mie kuondoka alikuwa mpweke ndani ya nyumba aliyonikabidhi bosi wangu, nyumba iliyopo  kinyerezi. kipindi chote hicho mie nalikuwa bado natumikia Gereza la Pretoria Afrika ya Kusini.

No comments:

Post a Comment

OBIMO CHETA

  OBIMO CHETA REMEMBER MY LOVE 💕  Sehemu ya nne Hakuwa na pahali pazuri pa kulala, hakuwa na maji, hakuwa na chakula, alilala kwenye majeng...